Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

Tunashukuru sana wadau wenzetu, tutendeeni kama wana dar es salaam tulivyowatendeeni. Hatukuwaangusha ila tunaonesha makamanda tunajari.tumuombee dada yetu regia apumzike kwa amani, moro endeleeni kutupa curent newz
 
Bila shaka kamanda Regia ameonyesha na kufungua njia kwa wanamorogoro, hasa kwa huo ukanda wa kusini Kilombero-Ulanga.

Natarajia huko mbele ya safari mkoa wa morogoro utakuwa mbele katika kuchagua mabadiliko ya kweli na ya kujiletea maendeleo.

Kamanda Regia ama kwa hakika amewaunganisha wana moro na watanzania wote katika kipindi hiki kifupi.

Kinachotakiwa baada ya mazishi, mkoa na taifa wasilale kuendeleza mapambano na kushughulikia mzozo wa hapo wilayani
 
Mvua ni kubwa kweli,

watu wanasema aondoki mtu.
 
Mvua inanyesha,na watu wengi wamesimama kwenye mvua.

Wengi wanakiri REGIA alikuwa na neema,
Ibada na shughuli zote zimesitishwa.
Mvua ni ishara ya upendo aliokuwa nao marehemu kwetu, .. kweli alitenda anayomaanisha rohoni kwake, changamoto wa wanasiasa waongo na wanaosaini mikataba usiku wa manane kuuza nchi bila aibu - tena wengine wapo hapo hapo makaburini macho makavu...
 
attachment.php

attachment.php
 
Pembeni mwote mwa uwanja ni magari. magari. magari!. Hakuna parking hivyo inakubidi uliache mbali gari na kutembea kwa miguu mpaka uwanjani.

Wana Ifakara nao wamejitokeza kwa wingi, uwanja umezungukwa na pikipiki na baiskeli.

Halafu watu wa Ifakara ni mashujaa, hawaogopi mvua, mvua inanyesha wageni wamejibanza viambazani mwa nyumba za jirani, wenyeji wamejisimamia, mvua inawanyeeshea!.
 
R.I.P Regia Mtema!!! There is no good word to express how we will miss your presence.
 
Regia please please,mummy naomba uamke tazama watoto,wazee ,wakina mama walivyo loona kwa mvua,

zaidi wanaizungumzia barabara uliyozoea kupita na kusema nani ataendelea kuisemea?

Regia sema basi na watu wako hata kama umekuwa kimya kwangu.
 
M-mbabe, don't take me seriously because I'm not a serious person. I just say what I see, hear and feel!.

If you think that democratic channels are not being exercised now, why did'nt you speak out what you truely see ? I know that you are acustomed to pathological lies but that is where you get your bread. I dont want to spill the water anyway, go ahead !
 
regia tunakusindikiza kwa mara ya mwisho leo,
moyoni nabubujikwa machozi,kumbuka mama yale tuliyozungumza na kuyawekea mikakati.

Regia nani atanisaidia kuyasimamia yale tuliyoyaongea,nisaidie mama,nitafanya,lakini wewe ndiye yalikuwa maono yako,nisaidie huko uliko.

Dr anakulilia,watoto wangu nyumbani wanakulilia,hata dada aliyekuwa anakuhudumia anakulilia.

Tulikupenda.
umenifanya nitokwe na machozi dada josephine! Mungu atutie nguvu....
 
Kwa jinsi nilivyosoma post kwenye hii thread,nahic na mimi nimehudhuli safari ya mwisho ya mpendwa wetu Mh.Regia Mtema(RIP).Nawashukuru wote walio2pa update na wanaondelea ku2pa update,Mungu awabariki sana
 
Ukiondoa chakula cha msiba Migagawa yote ya karibu hakuna chochote!. Soda zote zimenunuliwa, maji yote yamenunuliwa, chakula chote kimenunuliwa!.

Nadhani waheshimiwa walloandamana na JK watakuwa wamepitishwa kwanza kupata ndipo waje!. Wale wenzangu na mimi ambao asubuhi hatukuiona na huu mchana ndio huu unapita, leo tutashiriki swaumu ya hiari kwa heshima ya shujaa wetu Regia!.
 
Waombolezaji wa kweli na uhakika wako msibani leo. Hapa Dar nilijionea waombolezaji feki wengi tu. Wapo waliotaka waonekane kwenye Tv, wapo waliotaka umaarufu wa kisiasa tu, wapo waliotaka kuonesha mavazi na magari yao ya bei mbaya, wapo waliolazimika kuwepo kwa sababu ya nyadhifa zao, wapo waliokwenda kuwaona na kuwashangaa "wakubwa" wetu, wapo waliofuata mapochopocho tu, wapo waliokwenda kutengeneza pesa pia.
 
Regia please please,mummy naomba uamke tazama watoto,wazee ,wakina mama walivyo loona kwa mvua,

zaidi wanaizungumzia barabara uliyozoea kupita na kusema nani ataendelea kuisemea?

Regia sema basi na watu wako hata kama umekuwa kimya kwangu.

Pole sana mama, maneno mazito sana haya hata mimi nimesisimkwa naamini watu walioko hapo uwanjani pamoja na mvua inayonyesha inatoa somo kwa kila mmoja wetu kujitathmini na kujiweka tayari muda wowote.

Naamini kwamba Mungu atawainulia wana kilombero Regia mwingine atakayewakilisha matakwa yao na kuyasimamia.
 
Regia please please,mummy naomba uamke tazama watoto,wazee ,wakina mama walivyo loona kwa mvua,

zaidi wanaizungumzia barabara uliyozoea kupita na kusema nani ataendelea kuisemea?

Regia sema basi na watu wako hata kama umekuwa kimya kwangu.

aaaah uwiiiii daaah aaah
 
Waombolezaji wa kweli na uhakika wako msibani leo. Hapa Dar nilijionea waombolezaji feki wengi tu. Wapo waliotaka waonekane kwenye Tv, wapo waliotaka umaarufu wa kisiasa tu, wapo waliotaka kuonesha mavazi na magari yao ya bei mbaya, wapo waliolazimika kuwepo kwa sababu ya nyadhifa zao, wapo waliokwenda kuwaona na kuwashangaa "wakubwa" wetu, wapo waliofuata mapochopocho tu, wapo waliokwenda kutengeneza pesa pia.

Na huo ndio mchanganyiko wa watu tulio nao katika jamii yetu. haiwezekani wote tukawa na tabia za kufanana mkuu.
 
Regia please please,mummy naomba uamke tazama watoto,wazee ,wakina mama walivyo loona kwa mvua,

zaidi wanaizungumzia barabara uliyozoea kupita na kusema nani ataendelea kuisemea?

Regia sema basi na watu wako hata kama umekuwa kimya kwangu.
pole sana mama, inauma sana kwa kweli.
 
Back
Top Bottom