Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

Watanzania wameshindwa kuichukua nafasi hii kudai kile wanachokita.
Sidhani kama wanachokita Watanzania ni kujiuzulu kwa mawaziri nane.
Lakini habari ya kujiuzulu kwa mawaziri nane inawafanya Watanzania so excited mpaka wamesahau kila kitu.
Ni kama vile hao mawaziri wapya nane watakaokuja wata solve kila kitu.
Huwezi kusema gari bovu sana liko fit kwa kubadilisha taa za mbele.

Mkuu EMT, Hapo kwenye nyekundu, Watanzania wamebadilika wengi wetu tunaangalia matokeo ya kila jambo, tukishrikiana na viongozi wetu waadilifu wenye kuona mbele (Dr Slaa, Mh, Mbowe na Vijana wao) mapambano yataendelea. Hii si ngoma ya watoto isiyokesha ni ya kubwa itakesha Haki ipatikane!
 
Ila kama opportunity imejitokeza kwa nini tunaitosa?

Unadhani wakisimama na ku-hold the bull by its horns watashindwa??
Ni kweli Mkuu opportunity ikiwepo inawezekana, Ila kwa mfumo uliopo mjengoni wana CDM/wanaukombozi kufanya hivyo itakuwa ngumu, Idadi yao pale inayanya mapinduzi yasiwepo haraka. Kwani Magamba ni ndumilakuwili wakibanwa na wanene wanafuta kauli, Ndiyo maana nasema kila jambo na nyakati zake UMMA umeamka tunawapa suport Makamanda tunasonga mbele. Tutashinda!!
 
ni vyema sana kupeana taarifa za kweli sio kutunga tunga uharo kama huu hapa
 
HATIMAYE mawaziri saba kati ya nane wakiwemo wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, wamekubali kuandika barua za kujiuzulu wenyewe kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukinusuru Chama cha Mapinduzi (CCM).

Habari za kuaminika kutoka mjini Dodoma zimesema kuwa mawaziri hao, walilazimishwa kujiuzulu katika kikao cha dharura kilichokuwa chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kilichofanyika mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge.

Taarifa zimewataja waliokubali kujiuzulu kuwa ni pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika; Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu; na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.
Wengine wanaodaiwa kujiuzulu ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; Naibu Waziri wa Afya, Lucy Nkya; na Naibu Waziri wa Viwanda, Lazaro Nyarandu.

Hata hivyo, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye alishambuliwa vikali kwa kuitwa kinara wa ufujaji, hakuwepo katika kikao hicho kwa madai kuwa yuko nje ya nchi, anasubiriwa aungane na wenzake kuachia ngazi.

Kujiuzulu kwa mawaziri hao kumekuja baada ya kuzuka kwa mjadala mzito ndani ya Bunge kwa siku mbili mfululizo kuhusiana na tuhuma za ufujaji wa kutisha wa fedha za umma, kiasi cha kusababisha kuwepo kwa azimio la kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

chanzo: Tanzania Daima
 
Hivi wakishajiuzulu hawa mtaridhika? au mtasema "angalau tumeanza mahali" na hivyo kuonesha kuwa mmesahau kabisayaliyiotokea 2008 au ya kina Kiula miaka kadhaa nyuma?

Ndiyo maana binafsi ninafikiria namna hii:

Hapa Mh.Zito na Mh. Deo wakiwaacha hawa jamaa waendelee kutumbua maisha kwa jasho la watanzania, ni taamini nao (Deo na Zitto) wamepewa mgao wa wizi huo.

Nitawaelewa (Zitto & Deo-maana wanaushahidi muhimu dhidi ya 'waezi'),kama, kwa kushurikiana na watu wa sheria hawa "waeizi"wakifikishwa mahakamani na kuhakikisha mahakama inatenda haki kwa kuwaamuru warudishe shilingi yoyote ile 'waliyowaibia' watanzania.
 
Ni kweli Mkuu opportunity ikiwepo inawezekana, Ila kwa mfumo uliopo mjengoni wana CDM/wanaukombozi kufanya hivyo itakuwa ngumu, Idadi yao pale inayanya mapinduzi yasiwepo haraka. Kwani Magamba ni ndumilakuwili wakibanwa na wanene wanafuta kauli, Ndiyo maana nasema kila jambo na nyakati zake UMMA umeamka tunawapa suport Makamanda tunasonga mbele. Tutashinda!!

Kama hao CCM hawawezi kusoma alama za nyakati na kuona fursa mbele yao basi wasubiri maumivu...

Kama wangejua, cost ya kutofanya maamuzi sasa hawakuja kuilipa kamwe!!
 
ukitazama sura zao kwa makini zimekaa kifisadi fisadi na ujanja ujanja
tena wakamatwe mara moja na kushtakiwa kwa uzembe na wizi kama Mramba na Yona
ikiwezekana mahakama zitoe amri mara moja ya wao kufilisiwa
ile sheria ya kunyonga mafisadi nayo ipitishwe mara moja kazi ianze
i wish ningekuwa osama hawa wate ningejitoa nao mhanga nchi ipone
Breaking News mawaziri nane waachia ngazi

thumbnail.aspx
thumbnail.aspx
thumbnail.aspx
thumbnail.aspx
thumbnail.aspx
thumbnail.aspx
thumbnail.aspx
thumbnail.aspx

Habari tulizopokea toka kwa ripota wetu toka Dodoma ni kwamba Tanzania imeanza kukomaa ambapo mawaziri nane wameachia ngazi baada ya wabunge kuwatolea uvivu. Ingawa habari hii hajathibitika toka serikalini, wanaotajwa ni Omar Nundu (Uchukuzi), William Ngeleja (Nishati na Madini) , Dk. Haji Mponda (Afya), Jumanne Maghembe ( Kilimo Chakula na Ushurika) , George Mkuchika (Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Cyril Chami (Viwanda na Biashara), Mustafa Mkulo (Fedha) na Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii).

Hii ndo raha ya upinzani....
watu wanakimbilia majumbani kuangalia bunge sio tamthiliya.
 
Watanzania wameshindwa kuichukua nafasi hii kudai kile wanachokita.
Sidhani kama wanachokita Watanzania ni kujiuzulu kwa mawaziri nane.
Lakini habari ya kujiuzulu kwa mawaziri nane inawafanya Watanzania so excited mpaka wamesahau kila kitu.
Ni kama vile hao mawaziri wapya nane watakaokuja wata solve kila kitu.
Huwezi kusema gari bovu sana liko fit kwa kubadilisha taa za mbele.

Heshima nyingi kwako Mzazi EMT!
Nilidhani mwenye mawazo haya nipo peke yangu,
asubuhi ya siku hii itakuwa ni siku ya kero sana kwa watu wenye mawazo makubwa sana juu ya nchi yetu, sababu siku itaanza kwa kelele za kwenye maredio na magazeti yetu....
Mbaya zaidi kelele hzi zitakuwa ni za ushabiki na hisia.
Sijui kama kuna atakayehoji juu ya hasara na majereha ambayo nchi imeyapata kutokana na hao "nane".....
Hivi ndio kweli tulichohitaji kwa wakati huu?
Naona mashabiki wa serikali na ccm watakavyojitokeza kwa kuipongeza serikali sikivu kwa kuchukua "maamuzi magumu" na pia kukipongeza chama tawala na wabunge wake kwa "kuisimamia serikali vizuri", ni unafiki juu ya unafiki ....
Ndio tunachokitaka hichi kweli?
Hivi kuna atakayeuliza juu ya wanyama waliondoka kwenda uarabuni na hujuma zingine katika wizara ya Maige??
Huyo waziri "mpya" atawezaje?
Tutapata jibu juu ya gesi, nishati na madini yetu? Vipi kuhusu hasara na hujuma tulizozipata kipindi chote cha Ngeleja! Nani anazilipa??

Tukifanya mapitio ya maswali ya namna hii katika wizara zote tutakubaliana kuwa kinachohitajika katika taifa letu sio "wizara nane tu" .....

Lakini ninachosikitika ni kwamba, sio hicho tutakacho kijadili asubuhi...
Tuamke watanzania, twendeni mbele zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Something is better than nothing!
Safari moja huanzisha nyingine!

Heshima nyingi kwako Mzazi EMT!
Nilidhani mwenye mawazo haya nipo peke yangu,
asubuhi ya siku hii itakuwa ni siku ya kero sana kwa watu wenye mawazo makubwa sana juu ya nchi yetu, sababu siku itaanza kwa kelele za kwenye maredio na magazeti yetu....
Mbaya zaidi kelele hzi zitakuwa ni za ushabiki na hisia.
Sijui kama kuna atakayehoji juu ya hasara na majereha ambayo nchi imeyapata kutokana na hao "nane".....
Hivi ndio kweli tulichohitaji kwa wakati huu?
Naona mashabiki wa serikali na ccm watakavyojitokeza kwa kuipongeza serikali sikivu kwa kuchukua "maamuzi magumu" na pia kukipongeza chama tawala na wabunge wake kwa "kuisimamia serikali vizuri", ni unafiki juu ya unafiki ....
Ndio tunachokitaka hichi kweli?
Hivi kuna atakayeuliza juu ya wanyama waliondoka kwenda uarabuni na hujuma zingine katika wizara ya Maige??
Huyo waziri "mpya" atawezaje?
Tutapata jibu juu ya gesi, nishati na madini yetu? Vipi kuhusu hasara na hujuma tulizozipata kipindi chote cha Ngeleja! Nani anazilipa??

Tukifanya mapitio ya maswali ya namna hii katika wizara zote tutakubaliana kuwa kinachohitajika katika taifa letu sio "wizara nane tu" .....

Lakini ninachosikitika ni kwamba, sio hicho tutakacho kijadili asubuhi...
Tuamke watanzania, twendeni mbele zaidi.
 
HATIMAYE mawaziri saba kati ya nane wakiwemo wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, wamekubali kuandika barua za kujiuzulu wenyewe kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukinusuru Chama cha Mapinduzi (CCM).

Habari za kuaminika kutoka mjini Dodoma zimesema kuwa mawaziri hao, walilazimishwa kujiuzulu katika kikao cha dharura kilichokuwa chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kilichofanyika mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge.

Taarifa zimewataja waliokubali kujiuzulu kuwa ni pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika; Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu; na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

Wengine wanaodaiwa kujiuzulu ni: Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; Naibu Waziri wa Afya, Lucy Nkya; na Naibu Waziri wa Viwanda, Lazaro Nyarandu.

Hata hivyo, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye alishambuliwa vikali kwa kuitwa kinara wa ufujaji, hakuwepo katika kikao hicho kwa madai kuwa yuko nje ya nchi, anasubiriwa aungane na wenzake kuachia ngazi.
 
ni vyema sana kupeana taarifa za kweli sio kutunga tunga uharo kama huu hapa
we bwana inauma, kompyuta zako kariakoo soko lake linaendaje? sasa mbona unaropoka hapa, nawewe ulikuwa unafaidika na mianya ya kukwepa kodi yetu, eeh?
 
HATIMAYE mawaziri saba kati ya nane wakiwemo wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, wamekubali kuandika barua za kujiuzulu wenyewe kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukinusuru Chama cha Mapinduzi (CCM).

Habari za kuaminika kutoka mjini Dodoma zimesema kuwa mawaziri hao, walilazimishwa kujiuzulu katika kikao cha dharura kilichokuwa chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kilichofanyika mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge.

Taarifa zimewataja waliokubali kujiuzulu kuwa ni pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika; Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu; na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.
Wengine wanaodaiwa kujiuzulu ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; Naibu Waziri wa Afya, Lucy Nkya; na Naibu Waziri wa Viwanda, Lazaro Nyarandu.

Hata hivyo, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye alishambuliwa vikali kwa kuitwa kinara wa ufujaji, hakuwepo katika kikao hicho kwa madai kuwa yuko nje ya nchi, anasubiriwa aungane na wenzake kuachia ngazi.

Kujiuzulu kwa mawaziri hao kumekuja baada ya kuzuka kwa mjadala mzito ndani ya Bunge kwa siku mbili mfululizo kuhusiana na tuhuma za ufujaji wa kutisha wa fedha za umma, kiasi cha kusababisha kuwepo kwa azimio la kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

chanzo: Tanzania Daima
mkuu, kama habari hii ni yakweli, basi kesho nitashinda niki-MALIMA siku nzima
 
Baada ya kujiuzulu, washitakiwe kwa kutumia madaraka yao vibaya na kuliingizia taifa hasara, na ikiwezekana wafungwe kwa muda mrefu sana gerezani. Kujiuzulu tu halafu wakaenda kutumbua mali waliyotuibia hakutoshi; ningetegemea watoa hoja waongeze kipengele hicho kwenye hoja hiyo.

Raisi naye awajibishwe kwa kushindwa kuwasimamia watu aliowapa madaraka hadi wakaliingizia taifa hasara kubwa kiwango hicho; naye ashitakiwe (ingawa najua sheria hiyo haipo).
 
View attachment 52275

Wakuu lakini huyu si Daudi balali mwenyewe au amekufa ame twit kasema

Wanasiasa waongo, wasio na dira na wanafiki ndani ya jamii iliyojaa wananchi wasio na ufahamu wa kutosha. Okoeni Tanzania. Amkeni.
 
Back
Top Bottom