Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

John W. Mlacha

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
3,504
1,341
attachment.php

Katibu wa Kamati ya Wabunge wa Chama cha Mapinduzi, Jenista Mhagama, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao ambacho kimewashauri mawaziri wanane kujiuzulu.
MOTO uliowashwa bungeni na wabunge kuibana serikali baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG), sasa umewalazimu mawaziri wanane kutakiwa kupima uzito wa makosa yao na kufanya maamuzi ikiwa ni pamoja na kutakiwa kung’oka.

Alhamisi usiku, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alitoa wito kwa wabunge wote kujiorodhesha kwa nia ya kupata saini za wabunge 71 ambao wangewasilisha kutimiza matakwa ya kisheria kupata asilimia 20 ya wabunge kwa ajili ya kumuondoa Waziri Mkuu.

Mawaziri ambao usiku huu tayari wamejipinda kumuandikia barua Rais Jakaya Kikwete, kwa ushauri wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuikoa serikali ya chama hicho isianguke kutokana na mpango wa wabunge kujirodhesha kutaka kumuondoa Waziri Mkuu,Mizengo Pinda.

Wanaotakiwa kuondoka ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika Jumanne Maghembe na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

Hata hivyo, baadhi ya Mawaziri hao, wameelezea kuwa wataandika barua kwa Rais Kikwete kuelezea uozo wote uliosababisha kusakamwa kwao, baadhi wakidai kwamba hawahusiki kwa lolote na mambo wanayotuhumiwa nayo, huku baadhi wakiona mambo ni mazito na kuamua kujiondoa usiku huu.


CHANZO: Mawaziri wanane watakiwa kung’oka, wamuandikia barua Kikwete | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

Waziri Mkuu anaondoka katika Mazingira Tatanishi licha ya kuwaita kwa nguvu waandishi wa vyombo mbalimbali ambao walitegemea angetoa Tamko kuhusiana na maamuzi mazito ambayo tayari yamekwishazungumzwa hapa JF, Bahati mbaya sasa anatoka yeye kupitia mlango wa uani na muda mfupi kidogo anatoka Jenista Mhagama na yeye anapotakiwa kutoa Tamko kama ilivyoagizwa awali anasema maelezo yote atayatoa mwenyekiti wao Waziri Mkuu ambaye kisha chepuka kama dk 15 zilizopita.

  1. Kimejiri Nini hakuna anayejua
  2. Atatangaza kesho asubuhi katika Bunge, Inaelekea hii ndo plan ili wasipre-empty kikao cha Bunge
  3. Au wanasubiri baraka za Vasco Da Gama, hakuna anayejua
Ila kwa kauli ya Jenista Mhagama Mawaziri saba wameamuriwa Kujiuzuru mara moja nyadhifa zao....Nakamata detail za mwisho kabla sijaondoka niwajuze wanajamvi

Kwa sasa hayo ndo yanajiri kutoka viwanja vya Bunge

Adios

Kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa leo Mawaziri wanne wa CCM wamejiuzulu kwenye kikao cha kamati ya uongozi ya CCM kilichofanyika na hata katibu mkuu kiongozi alishiriki na sasa ndio wanaenda kuwatangazia wabunge wa CCM kwenye kikao cha ndani.

CONFRIMED!!!!!!! BY BLACK BAT......kutoka DODOMA.


Field Marshall ES said:
- Mawaziri Wanne wamejiuzulu tayari ndani ya CCM, sasa wanajitayarisha kulifahamisha taifa rasmi, Wabunge wa CCM wako kwenye kikao chao cha chama kabla ya kuja kwenye bunge ili itangazwe rasmi.


- The dataz toka kwenye kokus CCM ni Mawaziri SABA, wanaojiuzulu stay tuned!, KOKUS HAIJAISHA!

- Waliitwa kwenye kamati ya Uongozi chini ya Waziri Mkuu, wakaambiwa wajiondoe wenyewe, wakajifanya kulia lia kwamba inaonekana vibaya, lakini msimamo ni ule ule lazima waondoke na wamekubali, wanajaribu kulia lia huko kokus waonewe huruma lakini hakuna!, stay tuned!

ES!
 

Attachments

  • jenister.jpg
    jenister.jpg
    31.3 KB · Views: 10,223
[h=6]Kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa leo Mawaziri wanne wa CCM wamejiuzulu kwenye kikao cha kamati ya uongozi ya CCM kilichofanyika na hata katibu mkuu kiongozi alishiriki na sasa ndio wanaenda kuwatangazia wabunge wa CCM kwenye kikao cha ndani.[/h]

mlikuja na mambo ya sita mchana oh sibuka fm
 
Welcome to the 21st century:
Phones-wireless.
Cooking-fireless.
Cars-keyless.
Food-fatless.
Youth-jobless.
Leaders-shameless.
Relationships-meaningless.Attitude-careless.
Feelings-heartless.
Education-valueless.
Am just speechless.
Everything has become LESS but still our hopes are endless!! good 9tless.
 
Back
Top Bottom