Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

Mola anasikia kilio cha wabongo sasa. Enyi ndugu zetu wabunge endeleeni kukaza buti. Na huyo Pinda kwa nini asijiiweke kwenye hiyo list?
 
hpo bdo wakurugenzi na makatibu wakuu wao. . . .!
 
Huu ni upuuzi hii inaonyesha serikali jinsi gani ilivyojaa upendeleo kwenye matumbo yao naomba niweke wazi laiti raisi kikwete angesikia mawazo ya watu na hao wabunge mwaka jana mwaka huu tusingekuwa na wizi waa kiasi kwa hiyo soln sio tu hao waliojizulu pamoja na huyu bwana na naamini hata anaoenda kuwachagua nao wanakauja kula na kuwaumiza kichwa tena mnaomba wajiuzulu why????na baada ya kujiuzulu what next??
 
Bwana ametoa na bwana amechukuwa RIP Mkulo, Chami, Mponda, Magembe, Ngeleja a.ka. Mr.Giza, Malima a.k.a Wamoro, Maige. Bwana amechukua next target ni Vasco Da Gama Pori
 
Watanzania tuweke nani bado anatakiwa kujiuzulu pengine mpaka jumatatu wakisoma watakuwa wameongezeka humu kujiuzulu
 
Kamanda mi sijalala nilikuwa nasubiria hii habari hebu weka nyama kidogo eleza kwa kina kilichojiri dodoma kwenye cocus ya ccm

Nayatazama haya maamuzi kama ya kulinda masilahi binafsi zaidi kuliko masilahi ya Umma. Kuna naibu waziri mmoja anatajwa kuwa huenda akawa kundini nachelea kumuandika kwa kuwa ni kama bado palikuwa na sintofahamu na nini waazimie kama hatima yake.

Shinikizo lilikuwa kubwa na jamaa walimhakikishia mtoto wa Peasant kuwa '' kama hutawawajibisha vijana wako tuliowataja bila kuuma maneno kesho wote tunaanguka sahihi katika fomu ya ZITTO ZUBERI KABWE na kikosi cha CDM''

hapakuwa na Ujanja tena, kilichonistua ni mbwembwe zote za kualika MEDIA kisha wapashaji habari kuishia kutorokwa na zigo kutwishwa Mhagama ambaye alikuwa kama kameza kanda kwa kutoa jibu hilo hilo moja ati mambo yote kesho, mwenyekiti ataongea, Nani huyo....Si Waziri Mkuu.

Huku alikwisha ondoka kama dk 10 zilizopita. MBIVU na MBICHI kesho Asubuhi Mjengoni

GR Ntasimama LIVE kulikabili jukumu nililoliIntroduce JAMVINI


ADIOS
 
Outcome ya M4c ni hii! Hoja ilianza kwa Mdee, Lisu akapigilia msumari, Zitto akawaingiza mtegoni wakajaa! Now they r fighting...well planned! I hope by kesho cabinet nzima itakuwa chalii.
 
Huu ni upuuzi hii inaonyesha serikali jinsi gani ilivyojaa upendeleo kwenye matumbo yao naomba niweke wazi laiti raisi kikwete angesikia mawazo ya watu na hao wabunge mwaka jana mwaka huu tusingekuwa na wizi waa kiasi kwa hiyo soln sio tu hao waliojizulu pamoja na huyu bwana na naamini hata anaoenda kuwachagua nao wanakauja kula na kuwaumiza kichwa tena mnaomba wajiuzulu why????na baada ya kujiuzulu what next??
mahakama ya umma ndiyo eventually itaamua thru ballot papers
 
FULL LIST
Mkulo
Mponda
Nkya
Magembe
Nundu
Mkuchika
Chami
Maige
Ngeleja

KWA HISANI YA
https://www.jamiiforums.com/members/ghost-ryder.html

Du hapo sawa kumbe yule jamaa aliyeibiwa pale Morogoro, akishughulikia madini ya Mahenge hayumo? au hajikusanyii mali
kumbe bora kushughulikia mabibi kama mwenzake aliyekuwa Mkuu wa Dsm sasa waziri wao wamepona
tusubiri kukuche
 
Wanamjua mkuu wa kaya anaweza kuwageuzia kibao, haeleweki huyu na pasi zake za kusakizia.

Wabunge wote wa CCM ni wavivu wa kufikiri.....nitafafanua....!!

Naamini wote wanajua kuwa tatizo kubwa katika nchi hii siyo mawaziri wala PM....The problem is JK mwenyewe. Na wanajua kuwa JK keshawafanyizia mara kibao, na kuwasababishia matatizo makubwa kwa wapiga kura wao. Kwa nini hawataki kujivika mask na kumaliza kazi once and for ever??



Pamoja na hao mawaziri kuondoka hoja ha kutokuwa na imani na Waziri Mkuu iwepo pale pale.
Sijawahi kuona Waziri Mkuu wa aina hii. Alitakiwa yeye aweza wa kwanza kuondoka.
Waziri Mkuu amepewa madaraka lakini anashindwa kufanya maamuzi magumu. Hatufai huyu.

Wabunge wa CCM hawana ujasiri kufanya tukio la kihistoria kama hilo ndugu yangu...ndiyo maana wanakimbizana na kuziba matundu kwenye paa ambalo limeshatoboka kila mahali...!!

I wish they had something in their heads and some courage in their hearts!!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
tunaomba waharakishe mambo kwani hata sitaki kuwasikia wananiboa sana
 
CCM inajimaliza kwa kila upenyo inaopata, na kuongeza maadui kila ikiamka usingizini.

Nakubaliana na wewe Mkuu 100%!
Kila wanalofanya wakifikiri ni jema kwao, kumbe ndio linaongeza mwanga kwa UOZO wao.

Mie si mwanachama wa chama chochote, lakini kiukweli nafarijika sana na CDM wanavyoipigania nchi yetu. Mungu awabariki sana katika jitihada zao hizo na kujitoa kwao, pamoja na safari ndefu ya KUBEZWA walioipitia, hawajakata tamaa, wameendelea na wanaendelea kupambana na sasa tunaona dalili zote za kufanikiwa kwa juhudi zao.

Nakumbuka hapo nyuma Dr. Slaa akiwa bungeni, alikua akiigombania nchi hii na kuonekana kama mwehu au kituko lakini hakurudi nyuma.

Zitto Kabwe! Namkumbuka sana alipoingia bungeni, alipambana sana na Spika (Mzee Sitta) kuhusu kanuni za bunge, namshukuru Mzee Sitta alikua kwa kweli anamchallenge kama mtoto wake, lakini kufanya vile alikua anamjenga. Sitta wakati mwingine alikutwa anabanwa na kijana Zitto baada ya kukesha usiku akipitia kanuni ktk maktaba ya Bunge na Mzee Sitta aliona ukweli japo wakati mwingine aliziua hoja za Zitto kwa njia za utani na Zitto alikua mpole, nakumbuka siku moja Sitta alimtishia Zitto kwamba yeye ni Chifu huko kwao hivyo zkubliane na anachomwambia.

Kiukweli Mzee Sitta alijitahidi kutumia busara sana japo chama na serikali yake vilikua havibebeki.

Wamefanya kosa la mwaka la kumtoa Mzee yule na kumkabidhi bibi kiroboto na lukuvi matokeo yake ndio hayo wanaumbuka kila uchao. Makinda namsikitikia maana hajafaham kuwa Zitto sio level yake kabisa, yuko makini na hatua mia mbele kabla hata Makinda hajatoa mwongozo wake, kinachotokea Zitto huwa anahifadhi silaha za kummaliza kama yanayomkuta Mkullo leo hii, nimesikilia hoja za Lissu na Mnyika jioni ya leo, wale jamaa hawajaomba muongozo kama bibikiroboto na wengine wanavyofikiria, pale wameweka kumbukumbu kwy hansard, zitakuja kuwamaliza baadae labda wazipoteze.

Hoja ya mtoto makamba ni nyepesi sana ktk kuomba muongozo, ule ni mpango uliopangwa ili bikiroboto apate nafasi ya kujianika upeo wake mdogo wa kutetea maovu ya serikali badala ya kutetea wabunge wake pasipo kujali itikadi. Jinsi alivyokua anaeleza msimamo wa Spika bikiroboto (body language) yake ilikua ni wazi kabisa anafunika hiyo hoja kwa ukari usio na sababu japo alijitahidi asijulikane lakini kwa wabunge makini wa CDM wamejifunza kitu na nina Imani watafanyia kazi kila walichoonyeshwa!

Mungu wabariki CDM wamalize kazi ndogo iliyobakia ya kuikomboa Nchi yetu ya ahadi yenye Mikate na Asali ulizotujalia wanao ambao leo hii tunazulumiwa na wachache tulio wapa majukumu ya kutuandalia lakini wameamua kula wao na kutuachia makapi na ukoko tugawane tulio wengi.
Na imani Mungu wetu hutaacha udhalimu huu uendelee, walinde CDM baba Mungu nakulilia Mwanao. Amin!
 
List ndiyo hiyo hapo juu
Pinda kawaambia yeye sio jambio waondoke
yeye amalize salama ahamie cdm
 
Jk akirudi atapinga kujiuzulu kwao kwenye kikao cha wazee wa Dar es salaam na kuwalaani walioanzisha chokochoko. Bonge la presid! Saa hizi anapanga ratiba ya mazishi kule Malawi na anaandaa b/fast na Maximo

....Nimeipenda hii
 
Infact huu ndio mzizi wenyewe. Sidhani kama JK anaweza kuapisha mawaziri safi, wasio na scandal yeyote kutokana na sababu zifuatazo 1)kupata uwaziri lazima uwe mshkaji wa Kikwete au mtu wa ndio mzee 2) Kikwete anapenda watu ambao hawajamzidi kumfikiri (not very smart) 3) wanachama wa CCM walio safi/wazalendo wengi wao hawajapewa nafasi zozote za uongozi, so mpaka kuja kutambulika una-exist ni kazi saana etc. Kwa uwezo wakufikiri wa rais wetu lazima atafanya recycling tu. Akienda mbali sana atachukua wale wa awamu zilizopita akina Meghji.Lakini bado naamini kuwajibika kwa mawaziri ni hatua nzuri whether wamekuwa-pressured or not.

mzungu anakuambia VERY WELL SPOKEN. . .dah . .Nime LiKE mara laki nane. . .
Huyo jamaa pichani sub average thinking capability yake ipo very below low standard
 
Nadhani analysis yao ili-focus zaidi kwenye hii report ya CAG, lakini ukweli ni kwamba Baraza la Mawaziri la JK limejaa vimeo, wana kashfa za kufa mtu na wengi wao ni mzigo

Mkuu,

Tatizo siyo baraza la mawaziri. Hata likiundwa jipya litatakiwa kuvunjwa ndani ya mwaka mmoja...

These guys are not heating the nail on its head...Why not boot out the root cause???
 
Kweli Tanzania raha sana. Unaiba mali ya umma unapewa ushauri u-step down au ujipime. Tena kizuri zaidi hulazimishwi kurudisha ulichochukua so una options nyingi tu. Argh!:A S angry:

Hapa Mh.Zito na Mh. Deo wakiwaacha hawa jamaa waendelee kutumbua maisha kwa jasho la watanzania, ni taamini nao (Deo na Zitto) wamepewa mgao wa wizi huo.

Nitawaelewa (Zitto & Deo-maana wanaushahidi muhimu dhidi ya 'waezi'),kama, kwa kushurikiana na watu wa sheria hawa "waeizi"wakifikishwa mahakamani na kuhakikisha mahakama inatenda haki kwa kuwaamuru warudishe shilingi yoyote ile 'waliyowaibia' watanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom