Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

nadhan kunahtajika msimamo fulani bungen juu la hli sakata hata kama wamejiuzuru lazima serikal itoe msimamo juu ya hatua za kuchukua , tatzo mlengwa pinda lazma aseme kwa niaba ya serikal hapo ndo tatzo
 
Hii habari ni kweli au ni uzushi tu!?...Maana Magamba hawana utamaduni wa kujiuzulu hata wakivurunda kwa kiwango cha juu kabisa vinginevyo Ngeleja, Mkullo, Maghembe, Hussein Mwinyi na wengineo wengi wangekuwa ni history miaka mingi iliyopita...Ahsante Mkuu Mzizimkavu kwa kunitag.
 
dosama, una faidi nini kuwatetea mafisadi?
Unapaswa kutoa heko kwa chama cha chadema na mh. zitto kwa kuwa fedha za umma hazitaibiwa tena na hawa mafisadi

zitto huyu ambaye akiutakaga urais mnasema anatumiwa na ccm, leo mnamuona chadema safi,sio kibaraka wa ccm tena,haya bwana siye yetu macho,lakini kijana anatumia jasho lake jingi sana kuibeba chadema ila linapokuja suala la dini yake na mkoa atokao,anatengwa na kuwekwa mbali na mafanikio ya chama
 
Vuvuzela Nape hupo?
Je, hawa mawazili ni magamba?
Je, hawa mawazili ni wezi na majambazi wa mali za umma. AU
Je, wamepoteza mvuto ndani ya ccm na kwa wananchi kwa ujumla.
Je, ndo utekelezaji wa sera ya kujivua magamba?
Funguka vuvuzela...


Kumbe Nape ni Vuvuzela la wazee wa CCM? Basi utashangaa anaona ujiko!
 
Watanzania wameshindwa kuichukua nafasi hii kudai kile wanachokita.
Sidhani kama wanachokita Watanzania ni kujiuzulu kwa mawaziri nane.
Lakini habari ya kujiuzulu kwa mawaziri nane inawafanya Watanzania so excited mpaka wamesahau kila kitu.
Ni kama vile hao mawaziri wapya nane watakaokuja wata solve kila kitu.
Huwezi kusema gari bovu sana liko fit kwa kubadilisha taa za mbele.


Naam Mkuu anayetakiwa ajiuzulu pamoja na Serikali yake yote ni Kikwete kisha kukaundwa Serikali ya mpito ambayo itakuwa ni ya mseto kujiandaa kwa uchaguzi mpya katika miezi 12 au 15 ijayo na pia kuharakisha zoezi la kupata Katiba mpya ili itumike katika uchaguzi huo. Nchi inayumba sana kutokana na kukosekana kwa uongozi makini nchini. Njemba pale Ikulu inakenuakenua tu na kusafiri huku na kule kila kukicha wakati kiwango cha maisha ya Watanzania walio wengi kinazidi kudidimia.
 
Kwa namna moja ama nyingine lazima Kikwete atakuwa kaumia bcs wale watu ni wake na aliwapa ulaji kwa kumlindia maozo yake katika wizara husika. Haiwezekani waziri anaiba wewe rais unachekelea tu na kudanganya wananchi wako kila kukicha eti tufunge mikanda wakati nchi inaibiwa. Hapa lazima Kikwete naye aachie ngazi au la apinduliwe tu. We've had enough misery na hii administration yake. It's time for a change hatutaki kucheka tena maana ni muda mrefu nyuso zetu zimekunjana kwa huzuni juu ya utawala mbovu wa Jakaya. Leave now!
 
Baada ya kujiuzulu, washitakiwe kwa kutumia madaraka yao vibaya na kuliingizia taifa hasara, na ikiwezekana wafungwe kwa muda mrefu sana gerezani. Kujiuzulu tu halafu wakaenda kutumbua mali waliyotuibia hakutoshi; ningetegemea watoa hoja waongeze kipengele hicho kwenye hoja hiyo.

Raisi naye awajibishwe kwa kushindwa kuwasimamia watu aliowapa madaraka hadi wakaliingizia taifa hasara kubwa kiwango hicho; naye ashitakiwe (ingawa najua sheria hiyo haipo).

Yeah, hicho ndio nilichokuwa nakifikiria na mm! Wawajibishwe
 
Wameanza kujihukumu wenyewe kabla ya kuhukumiwa na wananchi, hizi ni rasharasha kabla ya 2015.
 
PINDA nadhani ni Mr. Yes boss! Hamsaidii bosi wake katika kuweka mambo shwari. Malima yumo pia? Na kama hayumo nashauri Zitto aendeleze movement yetu ya no confidence na PM.
 
Bora.....lakini na waliobaki eg Mkulo, wafuate nyayo. Na isiishie hapo tu wawajibike pia watendaji wengine wa wizara amabo wanalalamikiwa.
 
mwisho wa siku JK anaacha maswali mengi hivi urafiki atauendekeza hadi lini?......maana uteuzi wake kila siku ni noma tu.....
 
Tumshukuru mungu kwa hao walio jiuzuru kula pesa za wa tz' wa tz tufunge na kuomba ili wakamatwa nakufugwa jela maisha iwefundisho na kwa wengine.
Tumwombe God Bless Lema afunge tena siku saba kwa ajili ya hawa mawaziri halafu tuone kitakachotokea. Itakuwa ni kupukutisha serikali yote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom