Mawasiliano na Mahusiano

Mawasiliano na Mahusiano

Mkuu ndo umesha'cheat' hivyo...ila inasolvika kwa sababu hakun a ndo hapo bado....lol

Wee acha tu...kuna mtu alikuwa anapima elasticity limit ya Babu hapa hadi nikanyanganya madesa (simbi)....Bahati nzuri nimestuliwa na kuyaona mapema kabla sijazidi kuvuruga majiografia!
 
aha!? ....very interesting!....

nilishaambiwa, "yaani darling najuta ...mwanaume mwenyewe si lolote si chochote ...kwanza alikuwa ananichafua tu!"

khaaa?
mbu nikabakia nimelegeza kidevu nikiwaza nakuwazua yanayowakumba wake zetu huko kwenye maliwazo,
au alikuwa ananipiga changa la uso tu! mnh, ndoa hizi!

Bado naamini kuna serial cheaters ambao hawaangalii makunyanzi...Hao wanaokaa na kupiga tafakuri ni madenti wa hiyo business...Ma haluatani huwa wanapiga kwa kwenda mbele na wanaona ni sifa sana!
 
Bado naamini kuna serial cheaters ambao hawaangalii makunyanzi...Hao wanaokaa na kupiga tafakuri ni madenti wa hiyo business...Ma haluatani huwa wanapiga kwa kwenda mbele na wanaona ni sifa sana!

umeona ee? ....kuna thread ilikuwapo hapa takribana wiki mbili zilizopita, nikasikia kina dada wanasema aheri ya wale hit and runners, kuliko wanaofanywa nyumba ndogo....dahhhh....

sasa hapo ndio kuna kuliwazwa vipi yarabi?...kwa tafsiri ya kawaida naona nyumba ndogo ni yule asiye na mume/bwana wa kudumu...hawa wanaotetea hit and runners ndio wale wanaojiliwaza kwa kuchafuliwa, ama?....

aisee....ni bora kuufungua mdomo na kuongea na mumeo/mkeo kuliko kwenda kuchafuliwa nje bana!
kwa udadisi wangu, hizi hit and run mara nyingi hufanyika sehemu za ajabu ajabu sana, mfano chooni huko maofisini, ndani ya gari, na wengine kidogo hujitahidi kujisevia kwenye vi semina hivi vya uongo na kweli....mnh!

aisee ngojeni kwanza nistahmili haya mambo...yanauma kukumbukia ati alikuwa anajiliwaza chooni, au kwenye gari pembezoni mwa barabara...mke wangu huyo!...duuuuuhhhh! heshima ipo wapi hapo?...si ni sawa na kufanywa kama changudoa tu wa jolly club ama?
 
Hahahaha AshaDii umewaza mbali mpenz but ni ukweli mtupu! Laiti ingekuwa hivyo. Mimi nilishashuhudia mahusiano ambayo mmoja wa wanandoa alijikuta kwenye wakati mgumu,ambao mwenzie alikuwa anamfanyia visa vya kila aina yaani ile ya mashati kurudi na milipstick, handkerchiefs za kike n.k lakini Mdada yule hakurevenge may be kwa sababu alikuwa na guts za kuquit. But kwa yule ambaye hana guts hizo, kuna mbinu yoyote ya kumsaidia akamketisha mumewena kuongea nae?
Maana ni wazi hali ikiendelea vile bila matuimaini huyu mdada atakuwa vunerable na yeyote atakayempa attention na kuonyesha kumjali anaweza akamshawishi naye akashawoishika.

The same kwa mwanaume anayedharauliwa na mkewe na hana uwezo wa kumwacha pengine naye watoto au jamii inamzuia



MJ1 Your discussion inahitaji kichwa na akili kutulia, as much as i was jamvini sikuweza jibu earlier wala post yoyote ulokua inahitaji utulivu wangu... Hivo basi B2T naomba nizungumzie on behalf of my fellow woman, for with men ni rare kujikuta hana uwezo wa kureact kwa Mwanamke other wise awe amejitakia...

Wanawake bado tunasafari ndefu saana katika kila nyanya ya maisha... Kujikomboa, kujitambua, kujiendeleza na most importantly kua independent, hayo mambo yanachangia saana response ya mwanamke towards an abusive husband. Wanaume mara nyingi hata yule mpole ana kaelement fulani hivi ka majigambo kwa mwanamke - yaweza pishana level from one man to the next but it is there...

Hivo basi kujibu swali lako la kusema afanyeje.... Mara nyingi huyo mwanamke waweza mshauri mengi i.e achana na huyo mwanaume, mshitaki, revenge and the likes BUT Ukweli unabaki MJ1 kua such a woman hashauriki ila tu the best thing about it ni kwamba hua mara nyingi aweza mchenjia mwanaume mpaka huyo mwanaume ahisi kakosea njia.. pale tu roho yake itaposema "baaas sasa yatosha!"
 
Mamii kwahiyo unataka kuniambia huwa WANALAZIMIKA???
Sitaki kuamini kwamba wapo watu wanaoona/amini walil/wanazimika kucheat ,whatever the reason (or rather the excuse) behind it.
I mean naelewa kwamba hao watu nao wanamahitaji kama wengine ila kama ya umuhimu sana na imeshindikana kuyapata toka kwa wenzi wao hawawezi kwenda huko wanakoyapata moja kwa moja???Maana mtu mpaka afikie kutoka nje ya mahusiano yake na kujisikia huru kufanya hivyo mara kwa mara anakua ameyachoka hayo mahusiano..amemchoka mwenzi wake, haheshimu hayo mahusiano..hamhesimu mwenzake, hajali hatma ya hayo mahusiano..hajali hatma ya mwenzake...sasa kwanini aendelee kuwepo kwenye mahusiano ya aina hiyo na mtu ambae kamchoka/hamheshimu na wala hamjali???
Kama kweli wangekua wanaona wana haki (wanayojaribu kuonyesha kwa kupitia lawama na visingizio vihusuvyo watu wengine) ya kufanya wafanyayo kwanini wasifanye kwa uwazi??Kwanini wasiwajulishe na wenzi wao kabisa??
Pamoja na kwamba wakikamatwa wanaishia kulalamika na kulaumu bado wanajua wanachofanya sio sahihi na ndio maana wanaficha.



Lizzy dear hii post uloeleza... ni ya msingi na ndo inatakiwa iwe hivo.. na ndo inatakiwa wanandoa wawe na msimamo huo... Na huu msimamo hapo juu, nilou-qoute hapa ndo msimamo wangu ulikua hivo hivo hapo nyuma..... BUT I have changed, maisha, experiences zangu na za watu walonizunguka zimenibadilisha bila kupenda na kuniambia there is no black and white in everything..... hasa katika ndoa.... Naomba nitoke nje ya mada ili labda walau upate where it is coming from tunaposema kua spouse aweza changia mwenza wake a-cheat....

Natolea Mfano....

Jamaa ana mtoto wake ambae anaumwa saana, anajali familia yake, anampenda mkewe na watoto pia - na siku zoote hujitahidi kwa kila namna kutimiza majukumu yake ndani ya familia kwa uwezo wake mdogo alo nao. Bahati mbaya hata hio kazi ambayo anapokea mshahara mdogo bahati mbaya nayo anaipoteza just because tu wamepunguza wafanya kazi.. Mtoto ghafla anaumwa na yupo in a critical condition (na waelewa hospitali zetu bila pesa hujatibiwa) hana pesa kabisaa!! Anaenda kwa kila anaemfaham wa karibu akope hio pesa but hapewi, for waswahili wakijua huna kazi wala jinsi ya kulipa; basi hukopeshwi in most cases.... The wewe rafiki ambae amekutembelea na ni wazi kabisa una uwezo wa kumsaidia but umemfanyia tu roho mbaya, unanyanyuka labda kuingia chumbani na kumuacha hapo sebuleni (but while doing that umeangusha wallet bila utambuzi wako)

What do you expect hapo itakua?? Jamaa hajawahi iba na ni mpingaji wa wizi ile mbaya na hata ni namba moja kwa kuadhibu wezi... BUT then mtoto kazidiwa na inatiwa aende hospitali lasivo aweza mpoteza.... I am telling you as a parent the only logic hapo ni kuiba hio wallet uage na ukaokoe maisha ya mtoto wako. Haijalishi ameiba kwa ajili gani huyo tayari ni MWIZI... Nani hapo alaumiwe?? Mtoto aloumwa?? Walo mfukuza kazi?? Walomnyima msaada?? aloangusha wallet?? yeye mwenyewe??

IMO Haijalishi nani wa kulaumiwa, inachojalisha ni kwamba KAIBA, BUT ukweli unabaki kaiba kwa kusukumwa.... Dah! Sijui kama nimeeleweka. One thing is for sure.... Nakuombea uzima na maisha marefu na ndoa pia. Lakini what you are thinking saizi kua it is black and white will surely change one day.... Na take note; ninapozungumza haya si kwamba na condone ila tu napenda niangalie pande zoote za shillingi na ndo maana post yangu nikasema hii topic ni ngumu.....
 
MJ1,

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa "Mawasiliano" ndo shida kubwa katika ndoa/mahusiano.

Maana sababu nyingi sana huwa ni kutowasiliana na mwenzi wako, mf. kama unaona mimi nina matatizo si uniambie tu au wewe mwanaume kama naona una matatizo si nikwambie tu kuliko kutafuta sababu eti oohh wewe sababu uko hivi ndo maana niliamua "Kucheat" ki msingi hakuna sababu yoyote ni "Uzinzi" tu, na mara nyingi sana "Kucheat" kwa wanawake huwa ni visasi unakuta unamkamata mwenzako mara nyingi sababu anazokuapa hazina kichwa wala miguu, unapandwa na hasira na wewe unafanya yale anayofanya.

Niliwahi kumuuliza rafiki yangu (Wa kike) siku moja tulikuwa tunafanya nae kazi, nikamuuliza kwanini unacheat na umeolewa tena ndoa yenyewe ina miaka mitatu tu..........alikuwa anacheat na our boss tena waziwazi unajua alichonijibu " Nilipokuwa nimesafiri..................nilipandwa na hasira nikaamua kucheat baada ya kumpigia mzee nyumbani simu saa tano usiku nikasikia sauti ya mwanamke na yeye hayuko nyumbani" Nikajikuta nimekosa jibu kabisa.


Kuna mwingine alinambia kuwa amegundua mumewe anacheat na alimkata zaidi ya mara tano na sms na zingine kukosea kutuma kwake badala ya kwa mpango wa kando na yeye akacheat live mumewe alipoona hivyo akapunguza yeye akadai eti ngoma droo mmhh haya bana.


Tuelezane ukweli ndani ya mahusiano kama mwanaume mlevi, hajali familia na sababu nyinginezo tukae chini na kuzungumza na kuweza kusaidiana "No one is perfect" na huwezi kumbadili mtu tabia hata siku moja zaidi ya yeye mwenyewe ajibadilishe.

Lakini kuna hii kitu moja hapa niliipenda sana, kuna jamaa mmoja alikuwa anacheat sana na mkewe akagundua kumuuliza jamaa akaruka futi 1000 hajawahi kucheat mkewe akasema kweli eehhh sawa, akaweka uchunguzi wake wa karibu kwa kuwalipa watu kufanya hivyo, jamaa bila kujua akamwambia huyo mpango wa kando kuwa ahame mahali alipokuwa anaishi ahamie sehemu ya hali ya juu kidogo msichana akasema sawa lakini hiyo nyumba unayotaka nihamie mie sina vitu vya kuweza kutosha hiyo nyumba jamaa akamwambia no problem Jumamosi tutakwenda Nakumat ununue kila kitu hata hivyo ulivyonavyo uviuze vyote hutahamia navyo, kweli J1 ikafika hao Nakumat Style Supermarket, shoppping ya nguvu, friji, masofa, kitanda, jiko la gas, na vitu vingiii vya jikoni ilimcost kama 1,000,000 Kshs. jamaa yuko analipa kwa visa card amekuwa cleared kila kitu mkewe akatokea kachukua hiyo receipt akaenda akawaambia nipatieni hivi vitu mkewe hata nyumbani hana jiko la gasi wala hata friji, jamaa alizimia hapo hapo mpango wa kando ukajiondoa taaratibuu maana watu walijaa na ilikuwa story, na huyo mama baada ya kama miezi miwili hivi kama sikosei alikwenda radioni akasema tangu siku hiyo mumewe hajawahi "Kucheat" kamwe na amekuwa anamuheshimu kuliko mwanzo" (Nilitamani ningekuwa mimi siku hiyo kha!)

Jamani tuache kucheat kwa visingizio nawatakia siku njema wapendwa
 
MJ1,

Hakuna cha mapungufu ya mke au mume katika suala hili. Mtu anaamua mwenyewe halafu anajipeleka mwenyewe na kudai amefurahia kuzini halafu anakuja kusema eti kasababishiwa na mwenzi wake!! Ni ajabu sana kusikia haya maneno!

Unajua, binadamu kaumbwa na magunia zaidi ya milioni moja ya tamaa! Na mbaya zaidi tumezidiana. Kuna wengine wana mafuso kibao yamejaa hizo tamaa zao wakati wengine wanaweza kujaza ka-bajaj kamoja tu!! Sasa huyo mwenye mafuso yake ya tamaa, hata mke au mume angekuwa malaika bado angeeda kuzini! Upo hapo.

Mengine ni mazungumzo baada ya habari!!

Nitarudi baadaye kidogo!

Babu nimekuelewa vizuri sana hapa. Ninaomba tu nijuze kitu kimoja...............katika maisha ya ndoa, kwenye ndoa ambayo kimahusiano iko normal, mwanamke na mwanaume wanaweza kustahmili muda gani pasipo kupeana haki ya ndoa!? Woote wapo pamoja, hakuna ugonjwa wala sababu ya kuzuia tendo hilo lisifanyike.
 

....mwj1 mahbouba....tatizo ninaloliona hapa tayari kuna fitna ya kutafutwa sababu ya kutoka nje kwa hali yoyote...
mosi,
hivi hakuna solution nyingine yeyote ya mwanandoa kustahmili ndani ya hiyo ndoa bila ku cheat aka kutoka nje???

pili, una guarantee gani huko nje ndio itakuwa maliwazo tosha kufariji moyo, na uhakika atatoka na wangapi
akidhi kiu ya kupata kitu roho inapenda???

Hapana sweetie najua unanifahamu vema jinsi nsivyojua kujielezea. Hii tafsiri haikuwa niloikusudia, si kuwa kuna mtu anataka kutoka la hasha, najaribu kufikiria extremes za wanandoa ambao kwa namna moja au nyingine wananyimwa hakizao za msingi ndani ya ndoa hiyo na kwa bahati mbaya hana uwezo wa kujitambua na kurebuke hiyo abusive relationship (Hapa nitazungumzia zaidi wanawake wale ambao hawana uwezo wa kutoka au kudai haki zao- wanawake ambao kama yanavyosema nukuu hizo kuwa wanalazimika kutoka ili kupata liwazo.

And ofcoz mwenye uwezo wa kusema kama analiwazika kweli au lah ni mtokaji, nikirejea ile thread ya MADAM T kuna wadada waliokiri kucheat na wakaonyesha kuwa wanafurahia and they do not regret darling , je huyu utasema hapati liwazo??
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kweli mkuu,
Hakuna liwazo lolote linaweza kupatikana kwa njia hii. Kama mtu kakwazika basi hakuna ujanja...Ajaribu kutimiza wajibu wake, but within limits!! i.e amkalishe mwenzake na kumweleza feelings zake jinsi asivyoridhika na hali inayoendelea..(ingawa najua watu wengi huwa na kiburi na hudharau vitu vya namna hiyo) na kama hali haipati suluhisho basi kila mtu aanze maisha yake!

Umenena vema Babu , lakini ulishajiuliza kuwa itakuwaje iwapo ule upande unaoonekana kumpunja mwenzie ukajenga kiburi, dharau na jeuri kiasi cha kutotoa nafasi ya mwenzake kufikisha malalamiko yake.??? Na kwa bahati mbaya upande unaonyanyasika ukashindwa kuwa strong enough wa kuamua kuanza maisha yake kama unavyodhania? Ni mara ngapi tunasikia ndoa zinashikiliwa na kamba nyembamba iitwayo watoto, au jamii au umasikini??

Binafsi siamini kabisa katika ndoa ya hadi kifo...Samahani kama kuna mtu nimemkwaza......Freedom ya mtu na utu wake anayo mwenyewe. Hakuna sababu yoyote au uhalali wa aina yoyote unaweza kupatikana kwa kuumiza feelings zako eti unalipiza kisasi au kumkomoa mtu mwingine!!

Cheating ni tamaa tu na hakuna maelezo mengine!

Babu funguka zaidi. Msome AshaDii, Gaga, DA na I wish muhanga angekuja akalielezea vema post yake. Nadhani mngeelewa.

Nilitegemea kabisa reactions zenu kama wanaume na reaction za wamama kama wanawake. Ninajifunza somo muhimu sana hapa.
 
Jamani asanteni kwa mamichango yenu...................... nimejifinza sana. MJ1, keep it up dear........
 
Hapana sweetie najua unanifahamu vema jinsi nsivyojua kujielezea. Hii tafsiri haikuwa niloikusudia, si kuwa kuna mtu anataka kutoka la hasha, najaribu kufikiria extremes za wanandoa ambao kwa namna moja au nyingine wananyimwa hakizao za msingi ndani ya ndoa hiyo na kwa bahati mbaya hana uwezo wa kujitambua na kurebuke hiyo abusive relationship (Hapa nitazungumzia zaidi wanawake wale ambao hawana uwezo wa kutoka au kudai haki zao- wanawake ambao kama yanavyosema nukuu hizo kuwa wanalazimika kutoka ili kupata liwazo.

And ofcoz mwenye uwezo wa kusema kama analiwazika kweli au lah ni mtokaji, nikirejea ile thread ya MADAM T kuna wadada waliokiri kucheat na wakaonyesha kuwa wanafurahia and they do not regret darling , je huyu utasema hapati liwazo??

...usinikumbushe uchungu, pamoja na kuombwa msamaha zaidi ya mara saba na serial cheater wangu,
ipo siku nilimsikia kwa masikio yangu akijigamba hajutii!...aiseee....

...anyway, nikisemacho hapa ni kila tunapochimba kutafuta sababu iliyopelekea mtu ku cheat nje, naona kama
tunatafuta tu kuhalalisha matendo haya ambayo yamekatazwa kwenye mafunzo ya kiimani na hata kidunia.

Kwa mtazamo na msimamo wangu, na kwakuwa nilishawahi kuishi kwenye mazingira ya kujifanya mume *****
mwenye uwezo wa kuyafikiria yote yanayoweza justify cheating...mwishowe niligundua ONCE A CHEATER ALWAYS A CHEATER!

...mwenzio akisha cheat mwanzo kwa sababu yeyote ile hataacha, bora kuachana tu!
hakuna mawasiliano aina yeyote yatayojenga na kurudisha trust iliyokwisha vunjika...

wakatabahu!
 
Kwa mtazamo na msimamo wangu, na kwakuwa nilishawahi kuishi kwenye mazingira ya kujifanya mume *****
mwenye uwezo wa kuyafikiria yote yanayoweza justify cheating...mwishowe niligundua ONCE A CHEATER ALWAYS A CHEATER!

...mwenzio akisha cheat mwanzo kwa sababu yeyote ile hataacha, bora kuachana tu!
hakuna mawasiliano aina yeyote yatayojenga na kurudisha trust iliyokwisha vunjika...

wakatabahu!

Cheating is way too easy.....we should try something very challenging ; being Faithful !
 
huyo kwa vile ulimgundua tu, ila wanawake huwaa tuna mapenzi ya kweli, na ikitokea umetoka ujue mambo ni mazito pamoja na kwamba jamii haiwezi kukuelewa ila ndio hali halisi inavokuwa, unavumilia mpaka unaona huwezi tena, na hapo kama ukipata washauri wabaya ni rahisi sana kuanguka dhambini aisee, huyo wako alikwambia kweli unachafulwa tu, sababu tendo lile kwa mwanamke linahitaji akili itulie na ujione uko safe, wasiwasi haukufikishi hata kimara kwa safari ya arusha, wakati wa tendo akili yake inazongwa na mambo mengi na mawazo......

Mie nawaambia wanaume wawapende wake zao na kuwahakikishia wako safe na kuwapa mapenzi yooote waone kama kuna mke atakayetoka, mpe mkeo muda wa kutosha, imagine kila siku mtu saa saba nane, kalewa, mara masimu yanaanza kuingia, msg ..maneno yote mazuri anaambiwa hawala

Hilo lingewezekana kama wanawake wangekuwa malaika. Lakini Ooooo, wanawake nao wana matatizo kibao tu. Hakuna justification ya kuwa eti hujapendwa! Ilikuwaje mkaingia kwenye ndoa???? Wanawake wana tamaa mara mbili zaidi ya wanaume (tamaa za vitu vingi). Tamaa hizi huwaingiza wanawake mtegoni, akishaingia, lazima atatafuta wa kumrushia zigo la lawama; na hakuna mwingine zaidi ya mme wake!
 
Uko sawa KipimaPembe natamani wengi wangekuwa na mawazo ya aina hii hasa wanaume wale ambao wanakuwa na nyumba ndogo kwa kisingizio cha mke hamjali, au wanaotembea na wasichana wa kazi kwa kuwa tu mke yuko buzy.

Mnachonishangaza ni pale mnaposhauriana kuwa mke akikudharau, akijifanya buzy huna haja ya kupigizana nae kelele,tafuta wa pembeni maisha yaendelee !! Ila linapokuja kwa mke akiwa ndie victim yeye hatakiwi kabisa kutafuta wa pembeni!! Hili hatulipingi na ndio maana nikaomba sasa tusaidiane namna ya kumsaidia victim wa hali hii ili asitoke nje, si mwanaume, si mwanamke.

Tusikushangaze hakuna common agreement ya wanaume kuwa eti mke akifanyiwa hivyo asitoke nje!! Mhhhh, kwanza akitoka nje huenda kuliwazwa na mwanaume mwingine na probably atayamwaga mauzi yake kwa huyo anayempa relief!! So what? Haya yote ni upuuzi na ubatili wa binadam; ndo maana wengine wanafikia hatua ya kusema sisi wenyewe hatuwezi; tunahitaji nguvu iliyo juuu yetu zaidi - ingawa nguvu hiyo haijawahi kuonekana kuifanya kazi hiyo either!
 
Mjukuu haunitendei haki kabisa au macho yangu ndiyo mabovu hii mada kwanini imenipita fasta hivi
 
Lizzy Baby, natamani hii ndio ingekuwa reality. Am telling you kuwa katika wanawake wanaocheat ndoa zao ni wachache sana ambao wanacheat kwa kupenda au pesa. But wengi wao hucheat kwa kutafuta faraja, ambayo imekosekana ndani ya ndoa zao. Ni kweli kabisa akikamatwa hata kama alicheat kwa kuwa alinyimwa unyumba na mumewe kwa miaka miwili mfululizo bado kosa litakuwa kwake ninakubali kabisa ndio maana ninauliza mbinu ya kurekebisha mambo. Ukiisoma vizuri nukuu ya muhanga utagundua kuwa ni needs za kibinadamu ambazo sometimes zinapelekea hiyo cheating sasa tunafanyaje kuzikizi hizi needs pale ambapo mawasiliano kati ya wanandoa hayapo kwa kuwa tu mmoja wao ameona hakuna haja ya kusikilizana na mwenzi wake. Mf. tuseme mwanamke kila akirudi analalamika kichwa kinauma, amechoka au leo nina hacra siwezi'toa huduma' bosi amemuudhi n.k kwa miezi mitatu mfululizo na bado hayuko tayari kuketi kitako na kusilikiza feelings za mwenzi wake. Huyu victim afanyeje ili asitoke nje??

The same lame excuse, sikubali!!! Faraja haitoki kwa mtu mwingine, faraja inatoka ndani yako mwenyewe kwa kujua thamani yako, full stop. Mwanamke akikosa faraja ndani ya ndoa, amechangia kukosekana kwa hiyo faraja. Hakuna kosa la ndani ya ndoa linaloletwa na mtu mmoja, wote mnachangia. Katika kutafuta solution, kila mmoja anajiona yeye yuko right, ndo chanzo cha misemo hiyo.

Kama huyo mme alikuwa ni mtu mbaya wa kihivyo, msingefunga ndoa!! something has changed somewhere, ndo maana watu wanaanza ku-behave wierdly. Siri ni wote kujua kuwa mna makosa na muwe tayari kuyafanyia kazi.
 
Yah!Wa kwanza kulaumiwa ni mume kwa upande mmoja na upande mwingine ni mke mwenyewe!Ila kama ilivyo ada hakuna justifcation ya huu ujinga!

Ukiangalia matatizo kwa makengeza namna hiyo hutapata solution asilani!! Hakuna wa kwanza kulaumiwa, lawama inakuwa shared equally! Wote wanachangia 50% 50%. Hakuna wa kwanza wala wa mwisho, full stop!
 
There aint no reason for cheatin, just excuses...People say oh he/she did it first.. well i do believe 2 wrongs make a right in some cases but not with relationships... not only are you risking your life but putting youself in the way of diseases but affairs of the heart should be taken more seriously than playing tit for tat games...

Other people say he/she was not there for me when i needed and the other person provided what i needed... Well you shoulda been honest with the partner and let them know the deal and if you felt it was time to find what you need from some other shorty, be like yo, you aint there for me and i gotta move on...But all that said, we are all human and make mistakes...
 
MJ1, kichwa cha habari yako kimebeba yote. Mawasiliano kwenye relationship. Through my experience, hii kitu haipo katika nyumba nyingi. Nimeona nyumba nyingi zinavunjika sababu ya kukosa kuwasiliana. Mwambie mwenzio unataka nini, what you feel, kipi bora kwako, kipi hakifai. Hii yote inatokana kuwa mmekua baba fulani na mama fulani, kaheshima kakipuuzi mnakajenga wenyewe. Unajikuta ukidhani kua nikimwambia baba fulani nataka aniguse hapa, sijui atanionaje. lakini nikikutana na wa pembeni, yule vile ni sweetheart, namwambie vile ninavyojisikia bila uoga. baba fulani nae nyumbani, he's too busy, mikutano the whole day, akirudi kabeba ma file kuna kazi za kufanya maana ana presentation first thing in the morning na mengine mengi. sasa hata tunda likiliwa ni ile style ya "kubali yaishe" hakuna mahanjam, ni bora liende. nikienda pembeni, tumeipainga, kila mmoja ana hamu na mwenzie mapenzi motomoto ananiridhisha. cheating itaisha kweli kwa maisha yetu haya ya kiafrika... watu wata cheat hadi mwisho wa dunia, unless mabadiliko yatokee.

Kumwambia tu ingekuwa inatosha, matatizo yasingekuwa mengi kama ilivyo. Umwambie, awe tayari kusikiliza na kuona mambo vile unayaona wewe! Hapo ndo changamoto kubwa!

Utamwambia vile unafeel, kipi bora kwako na kipi hakifai; ila yeye anaona vinginevyo; yaani kile we unaona bora, yeye anaona si bora. Hapo ndo changamoto ilivyo, si rahisi!
 
Back
Top Bottom