Lizzy dear hii post uloeleza... ni ya msingi na ndo inatakiwa iwe hivo.. na ndo inatakiwa wanandoa wawe na msimamo huo... Na huu msimamo hapo juu, nilou-qoute hapa ndo msimamo wangu ulikua hivo hivo hapo nyuma..... BUT I have changed, maisha, experiences zangu na za watu walonizunguka zimenibadilisha bila kupenda na kuniambia there is no black and white in everything..... hasa katika ndoa.... Naomba nitoke nje ya mada ili labda walau upate where it is coming from tunaposema kua spouse aweza changia mwenza wake a-cheat....
Natolea Mfano....
Jamaa ana mtoto wake ambae anaumwa saana, anajali familia yake, anampenda mkewe na watoto pia - na siku zoote hujitahidi kwa kila namna kutimiza majukumu yake ndani ya familia kwa uwezo wake mdogo alo nao. Bahati mbaya hata hio kazi ambayo anapokea mshahara mdogo bahati mbaya nayo anaipoteza just because tu wamepunguza wafanya kazi.. Mtoto ghafla anaumwa na yupo in a critical condition (na waelewa hospitali zetu bila pesa hujatibiwa) hana pesa kabisaa!! Anaenda kwa kila anaemfaham wa karibu akope hio pesa but hapewi, for waswahili wakijua huna kazi wala jinsi ya kulipa; basi hukopeshwi in most cases.... The wewe rafiki ambae amekutembelea na ni wazi kabisa una uwezo wa kumsaidia but umemfanyia tu roho mbaya, unanyanyuka labda kuingia chumbani na kumuacha hapo sebuleni (but while doing that umeangusha wallet bila utambuzi wako)
What do you expect hapo itakua?? Jamaa hajawahi iba na ni mpingaji wa wizi ile mbaya na hata ni namba moja kwa kuadhibu wezi... BUT then mtoto kazidiwa na inatiwa aende hospitali lasivo aweza mpoteza.... I am telling you as a parent the only logic hapo ni kuiba hio wallet uage na ukaokoe maisha ya mtoto wako. Haijalishi ameiba kwa ajili gani huyo tayari ni MWIZI... Nani hapo alaumiwe?? Mtoto aloumwa?? Walo mfukuza kazi?? Walomnyima msaada?? aloangusha wallet?? yeye mwenyewe??
IMO Haijalishi nani wa kulaumiwa, inachojalisha ni kwamba KAIBA, BUT ukweli unabaki kaiba kwa kusukumwa.... Dah! Sijui kama nimeeleweka. One thing is for sure.... Nakuombea uzima na maisha marefu na ndoa pia. Lakini what you are thinking saizi kua it is black and white will surely change one day.... Na take note; ninapozungumza haya si kwamba na condone ila tu napenda niangalie pande zoote za shillingi na ndo maana post yangu nikasema hii topic ni ngumu.....