Matumizi ya Neno Mkuu JF.

Matumizi ya Neno Mkuu JF.

Kuna verified members tunawajua kwa sura na kazi wanazofanya hasa hawa wanaotumia majina yao halisi still tunaendelea kuwaita mkuu. Mfano ni huyu member maarufu anayepaita humu jamvini na nyuzi huziita bandiko
Matumizi ya neno mkuu bado hayajapoteza maana ;

Kufahamu mtu sura na kazi haimaanishi unafahamu pia na kipato chake halisi.
 
Papai hilo linataka kujitongozesha,kaa nalo mbali mkuu,ndio tabia yake hiyo kushobokea wanaume hapa JF,

Usije kusema hukuambiwa mkuu.
Ukitaka kuuliz swali you go straight to the questioning, nikapata wasiwasi anaomba kuniuliza swali...
 
Ukiona umeitwa mkuu ni heshima, wengine wametuzidi umri, elimu, ujuzi, maarifa na uchumi still wanatuita mkuu, ni utamaduni mzuri wa kuheshimiana bila kujali jinsia wala wajihi, imani za dini, siasa na itikadi zingine za mirengo mbalimbali, ni bora kuitana mkuu kuliko kuitana status za matusi, kudhalilishana, kebehi, dharau, kejeli, dhihaka, kushushiana heshima eti kwa sababu ya kutofautiana maoni, itikadi za kisiasa na imani za kidini
 
Matumizi ya neno mkuu bado hayajapoteza maana ;

Kufahamu mtu sura na kazi haimaanishi unafahamu pia na kipato chake halisi.
kujua kipato cha mtu ni siri, hata uone salary slip yake still hutajua kazi zake za pembeni zinamuingizia hela kiasi gani
 
Kuna members huniita mkuu Loth tunapojadiliana humu, inaonesha wanaheshimu watu na wana maadili. Mojawapo ya malengo ya elimu ni kuheshimiana, watu wenye elimu wanaheshimu watu wengine bila kujali status zao. Neno mkuu kama linavyotumika humu lina mawanda mapana zaidi, hasa ni ku appreciate maoni ya mtu bila kujali mnatofautiana, na like unapewa!
 
Back
Top Bottom