Matumizi ya Neno Mkuu JF

Matumizi ya Neno Mkuu JF

Neno Mkuu limetumika na magwiji wa hoja ili kupoza mzuka.
Jf ya zamani ilikuwa uwanja wa hoja, unatoa hoja inajibiwa kwa hoja.
Sasa mjadala unakuwa mkali na hoja huwa za moto, likatumika neno  Mkuu ili kujenga urafiki na mahaba na yule unayejadiliana naye ili kupunguza munkali.

Ni kama vile mawakili walivyochagua Kuitana 'Wakili msomi' wakiwa kwenye kurushiana vifungu vya sheria mahakamani.
Nia ni moja tu, kujenga undugu na urafiki na kupunguza uhasama unaotokana na vichapo vya hoja.
 
Nachochukia ni kwamba akina dada wa humu nao wanatumia neno Mkuu, mpaka mtu unahisi ni mwanaume kumbe ni mwanamke.
Itisha kikao mtafute neno la kuwatambulisha jinsia ya ke.

Mnialike kama mjumbe.

Ingawa matumizi ya neno mkuu ilikuwa ni kuleta usawa kwa jinsia zote.
 
Back
Top Bottom