Matumizi ya Neno Mkuu JF

Matumizi ya Neno Mkuu JF

Neno Mkuu limetumika na magwiji wa hoja ili kupoza mzuka.
Jf ya zamani ilikuwa uwanja wa hoja, unatoa hoja inajibiwa kwa hoja.
Sasa mjadala unakuwa mkali na hoja huwa za moto, likatumika neno  Mkuu ili kujenga urafiki na mahaba na yule unayejadiliana naye ili kupunguza munkali.

Ni kama vile mawakili walivyochagua Kuitana 'Wakili msomi' wakiwa kwenye kurushiana vifungu vya sheria mahakamani.
Nia ni moja tu, kujenga undugu na urafiki na kupunguza uhasama unaotokana na vichapo vya hoja.
Sure!

Ufafanuzi murua kabisa,ni hali pia mimi hupitia pale ninapokuwa na mjadala mkali na mtu then nikaona ni kama ameshani-knock out so natumia hii kauli kumpunguza spidi halafu napotea mazima.
 
Back
Top Bottom