Matumizi ya Magufuli, tuyajadili

Matumizi ya Magufuli, tuyajadili

Busara asingelisifia hilo gazeti moja kwa moja
angechukua taarifa na kuzifanyia utafiti
Tayari hilo gazeti limeshagomba na JK na familia yake waziwazi
ni kama analitetea kiaina....mtu mwingine anaweza kudhani hilo gazeti
linapewa taarifa na TeamMagufuli....limdhalilishe JK kusudi...
anazidi kutengeneza maadui wasio na lazima
mambo yasipo nyooka atamhitaji JK kwenye uchaguzi ujao
wa fix matokeo...
lengo si taarifa bali alitaka magazeti yawe na uzalendo. Gazeti kama Tanzania Daima kila siku kinaandika fitna tuu. kwanini lisifanye uchunguzi wa mambo.yenye faida kwa jamii.
 
Mpaka sasa tunajiuliza nini kipaumbele cha serikali hii ya awamu ya Tano? Jibu "Hapa ni papala tu..."
Nadhani kuna jambo kubwa linatakiwa lifanyike kubadili mind set za vijana wetu ambao wengi wao wapo opposition.Muda mwingi tunapoteza kumjadili Magufuli na serikali yake badala ya kuelekeza nguvu na maarifa tuliyo nayo kuendesha Halmashauri tulizo shinda ili baada ya muda mfupi watanzania waone tofauti kati ya Halmashauri zilizo chini ya wapinzani na zile zinazo ongozwa na CCM! Nionvyo mimi, Magufuli watu wanamkubali sasa kuliko wakati mwingine wowote! nilishuhudia siku moja pale Msamvu Morogoro jinsi watu walivyo jaa ghafla kumsikiliza kwa shauku kubwa na kwa hakika walimpokea kwa dhati ya mioyo yao.siasa ni kukubalika miongoni mwa watu.
 
Simple calculation isiyohitaji kwenda chuo kikuu cha UDOM, Nyerere alishawaambia hamieni Dodoma mkamuona mjinga leo hii mnatumia billions of money kujenga vidarajadaraja mshenzi na vijibarabara vya hapa na pale visivyomsaidia huyu mtanzania mwenye hali ya chini.

Nenda Dodoma au mkoa jirani piga master plan ya mkoa mzima, forecast 50-100 yrs mbele weka vitu pale hizo jam za dar mnabaki nazo wazaramo hapo
Dar huwezi ikataa..hata ukihamia dodoma bado dar inatakiwa kujengwa vizuri. Dar ndio tZ na tz ni dar.
 
......kwa aina ya kuwa na wabunge kama lusinde na musukuma huwezi kupa watu sahihi wa kumshauri raisi hasa kwenye mambo ya kuinua uchumi wa nchi......
 
Hawa wanaochangia hii thread ni watanzania au wanyarwanda? Too negative
UKAWA hawa sifa nzuri kwa serikali ya JPM, wao wanaangalia hasara tu badala ya kuangalia upande wa pili ambao ni tija kwa watz waliowengi haswa wanyonge
 
JAMANI NYUMBA ZENU MLIZIJENGA KWA SIKU 100? MPAKA MTAKE RAIS A FANYENI MAMBO YOTE SIKU 100. HUYO ZITO ACT ALIIJENGA KWA SIKU 100? MAGUFULI ANA ACTION PLAN YAKE IKIFIKA SIKU ATAYOFANYA LITALOKUGUSA UTAFURAHI KAMA BADO SUBIRI.
 
- Daraja la kigamboni bilioni 200
- Daraja la furahisha mwanza bilioni 200 (nakaribisha masahisho)
- Daraja la Coco Beach-bilioni 200 zimetengwa
- Barabara ya Dar-Chalinze-zaidi ya trilioni 1.3(dollar milioni 500)
- Mabasi yaendayo kasi -zaidi ya bilioni 200
- Flyover ya Ubungo bilioni 100

Iwapo serikali ingeamua kujenga treni za umeme badala ya mabasi yaendayo kasi ingetumia dollar milion 430 kwa km 32...yaani karibu Dar yote ingekuwa unapanda treni dakika 10 uko popote pale hata Kigamboni treni ingefika kupitia Mbagala.

Hii ni link ya Ethiopia inaelezea gharama za treni hizo na tayari wenzetu wanatumia..

Ethiopia gets first sub-Saharan Africa metro - CNN.com


Na kama hizo bilioni zingetumika kujenga vyuo vikuu UDOM gharama zake ilikuwa kiasi cha bilioni 25.
Pengine husomi magazeti. Sehemu kubwa ya pesa hizo ni misaada toka Japan ambayo iko tied na specific projects. TZ inatakiwa kuchangia 10-20% za gharama hizo na hivyo haiwezekani ku-divert pesa hizo kwa kitu kingine.
 
Mpendwa, usisahau kulikuwa na makusanyo mengi ambayo yalikuwa ni arrears, sasa ulitegemea nini???? Mbona hufikirishi ubongo wako???? Mimi Ma great thinker wa hivi wananitatiza sana.

Queen Esther

Alipoanza Makusanyo yalikuwa Trilioni 1.3, Mwenzi uliyofuatia yalifika Trilioni 1.5 na yakafika Trilioni 1.0.. Swali la msingi mfuatano huu (trend) una maanisha nini?
 
Wengi Wa wachangiaji wana elimu ya hapa na pale. Kupitia michango yao isiyo na chembe ya utafiti hata Wa kujua hela zinatoka wapi, basi utaelewa hawa ni vilaza Wa kufa mtu. Hata hili jukwaa la GT's haliwafai.

Queen Esther

Kumuelewa Magufuli Na Utawala Wake Kwa UJUMLA Unahitaji Kutulia Na Wala Usiwe Na Papara! Soon Mtamuelewa TU
 
We dont have a stable power supply,we must stabilize it and think to invest on Electrical Train
 
Mpendwa, usisahau kulikuwa na makusanyo mengi ambayo yalikuwa ni arrears, sasa ulitegemea nini???? Mbona hufikirishi ubongo wako???? Mimi Ma great thinker wa hivi wananitatiza sana.

Queen Esther
Wewe ndiyo ushirikishi ubongo wako. Aliposema makusanyo yameongezeka ni kutokana na udhibiti wake, na wapambe wake wakakosoa kama vile kodi ilikuwa inakusanywa kwa chini ya kiwango. Ndiyo maana The Boss amesema yeye hakujua kwamba makusanyo hayathaminishwi kwa mwezi badala yake huthaminishwa kwa mwaka mzima wa makusanyo ya Kodi? Soma elewa kwanza kabla ya kurukia kujibu.
 
sera yao nikutumbua majipu ila mrejesho kama majipu yameacha makovu au vidonda hakuna zaidi ya kuambia tirion zimeokolewa!!what next hata mchanganuo haueleweki wa hizo tirioni tukisema hawakujiandaa kutawala wanakuwa wakali..! kwa kikwete alipoishia angekuja raisi mwenye vision angeona njia kwenye ukungu uliotandazwa na serikali ya kikwete..!! we have platform from there ilikuwa nikubadili hatua moja baada ya nyingine,escrow,meremeta,epa,uda,mtwara gas,zilikuwa na majibu yakutosha
 
Hiyo miradi kaikuta, si kwamba amebuni yeye km rais, mfano kigamboni, mnataka asitishi mradi? Au mwendo kasi, tusubiri hii aliyoikuta ikamilike, then tuone ipi mipya atakayoianzisha.
 

Vitu kama hivi vinahitaji kuwa na takwimu au uhakika fulani ili kutoa maoni yenye maana. Nimesoma kwenye thtread moja humu JP kuhusu daraja la Kigamboni. Madai ni kwamba mradi ulianza wakati wa Magufuli lakini aliondolewa Wizara ya Ujenzi wakati huo baada ya kutokea "mjadala" kuhusu gharama halisi za mradi huo.

Tunajua baadaye sana alirudi katika wizara hiyo lakini mikataba yote muhimu ilikuwa tayari. Kwa hali hiyo, sina uhakika nafasi yake katika gharama kubwa kama hiyo inakuwa wapi.

Huenda ikafanyika audit ya gharama za mradi huo na hapo kila kitu kitakuwa wazi.
 
Iwapo serikali ingeamua kujenga treni za umeme badala ya mabasi yaendayo kasi ingetumia dollar milion 430 kwa km 32...yaani karibu Dar yote ingekuwa unapanda treni dakika 10 uko popote pale hata Kigamboni treni ingefika kupitia Mbagala.
.

Hii hoja yako ina mapungufu mengi.

Kwanza unaongelea kujenga kwa kilomita kama vile hiyo reli itapita maeneo pori.Ujue kuna kulipa fidia majumba kibao kabla ya kutandika hizo reli.Kwa hiyo hiyo gharama yako kwa kilomita lazima uangalie na mambo kama hayo

Pili huongelei gharama za uendeshaji ukishajenga.Ukijenga reli gharama za uendeshaji za kila siku unalipia mwenyewe milele wakati ukijenga barabara sekta binafsi ndio inagharimia matengenezo ya magari yao tofauti na treni ambazo wewe mwenyewe serikali ndio utakuwa unagharimia.

Dar es salaam si mji wenye abiria wengi kama unavyodhani.Abiria wanapatikana wengi Asubuhi wanapoenda mjini na jioni tu wanaporudi.Masaa ya katikati hata wenye mabasi ya daladala wengine utakuta wamelala kwenye daladala.Kukuta daladala ina watu robo tu ni kitu cha kawaida.Ukiweka Treni wakati muda mwingine haliwezi jaza hata behewa moja ni hasara kubwa kibiashara.Teni zinafaa zaidi kwenye maeneo yenye heavy trafic muda wote.Mfano ukiwa na viwanda vingi vyenye shift mfano tatu kwa siku na kila kiwanda kina wafanyakazi 4,000 Unaweza fikiria jenga reli kwenda huko
 
Back
Top Bottom