Matumizi ya Magufuli, tuyajadili

Matumizi ya Magufuli, tuyajadili

Vyo
- Daraja la kigamboni bilioni 200
- Daraja la furahisha mwanza bilioni 200 (nakaribisha masahisho)
- Daraja la Coco Beach-bilioni 200 zimetengwa
- Barabara ya Dar-Chalinze-zaidi ya trilioni 1.3(dollar milioni 500)
- Mabasi yaendayo kasi -zaidi ya bilioni 200
- Flyover ya Ubungo bilioni 100

Iwapo serikali ingeamua kujenga treni za umeme badala ya mabasi yaendayo kasi ingetumia dollar milion 430 kwa km 32...yaani karibu Dar yote ingekuwa unapanda treni dakika 10 uko popote pale hata Kigamboni treni ingefika kupitia Mbagala.

Hii ni link ya Ethiopia inaelezea gharama za treni hizo na tayari wenzetu wanatumia..

Ethiopia gets first sub-Saharan Africa metro - CNN.com

Na kama hizo bilioni zingetumika kujenga vyuo vikuu UDOM gharama zake ilikuwa kiasi cha bilioni 25.
Barabara, train na mabasi yaendayo kasi vyote tunavihitaji but tuanze na kimojawapo
 
- Daraja la kigamboni bilioni 200
- Daraja la furahisha mwanza bilioni 200 (nakaribisha masahisho)
- Daraja la Coco Beach-bilioni 200 zimetengwa
- Barabara ya Dar-Chalinze-zaidi ya trilioni 1.3(dollar milioni 500)
- Mabasi yaendayo kasi -zaidi ya bilioni 200
- Flyover ya Ubungo bilioni 100

Iwapo serikali ingeamua kujenga treni za umeme badala ya mabasi yaendayo kasi ingetumia dollar milion 430 kwa km 32...yaani karibu Dar yote ingekuwa unapanda treni dakika 10 uko popote pale hata Kigamboni treni ingefika kupitia Mbagala.

Hii ni link ya Ethiopia inaelezea gharama za treni hizo na tayari wenzetu wanatumia..

Ethiopia gets first sub-Saharan Africa metro - CNN.com

Na kama hizo bilioni zingetumika kujenga vyuo vikuu UDOM gharama zake ilikuwa kiasi cha bilioni 25.
Mkuu mimi binafsi sihitaji dira wala mapendekezo, wala mikakati wala vision wala etc..... Nahitaji barabara, maji, dawa hospital nk....... Nahitaji kuziona live dira wapelekee marubani
 
The Boss nafikiri huwezi kuwa Rais free style lazima ujipangie, ufuate, mikakati thabiti. Tanzania vipaumbele ni kila kitu na hivyo katika kila kitu basi pangilia kwa vipaumbele ndani ya vipaumbele. Mfano ni dhahiri Tanzania vipaumbele rahisi na muhimu kweli kweli kuliko madaraja na flyovers - maji safi na salama kwa kila mtanzania hiki ni kipaumbele cha kwanza ndani ya vipaumbele, then umeme kwa kila mtanzania, na ikibidi mabarabara basi kwa vipaumbele mfano mikoa yenye uzalishaji mazao ya chakula na biashara ipewe vipaumbele vya barabara na madaraja. Flyovers ni madoido ikiwa hata maji safi na salama serikali haiwezi kutoa kwa raia wake, na ikiwa maji haya hutoka au kutiririka bure ardhini. Aibu!!!

Lakini ukiangalia kwa makini utaona mwisho kuanzia mwanzo. Yule wa wizara ya nje alifanya sana nje na huyu wa ujenzi atafanya sana ujenzi. In a nutshell huo ndio mwisho wake na utakuwa mzuri sana kwetu watanzania kwa kuwa tutakuwa na chochote.
 
Huu mfuatano utashuka mpaka 0.85Trillion then utaanza kupanda taratibu ila kwa uhakika. Asitegemee mapato kuongezeka ilihali huku akipunguza sana matumizi ya kawaida ya Serikali ambayo ndo chachu kuu ya mzunguko wa pesa katika uchumi.

Watu wachache sana wamekuelewa...
 
Wengi Wa wachangiaji wana elimu ya hapa na pale. Kupitia michango yao isiyo na chembe ya utafiti hata Wa kujua hela zinatoka wapi, basi utaelewa hawa ni vilaza Wa kufa mtu. Hata hili jukwaa la GT's haliwafai.

Queen Esther
Naona Unatafuta Bwana Kwa Nguvu?
 
Na sehemu kubwa ya hizi gharama ni 'overpriced'
mfano amekuwa waziri wa ujenzi almost miaka 20
lakini haoni kuwa kuagiza lami kutoka nje kunasababisha gharama ziwe mara tatu zaidi
za ujenzi wa barabara....
Unataka kuniambia hii lami inayobanduka baada ya siku mbili tatu inatoka nje,,,,
 
Unataka kuniambia hii lami inayobanduka baada ya siku mbili tatu inatoka nje,,,,

yap huwezi amini but ndo ukweli
halafu ni ghali mno
tunanunua mara tatu ya Africa Kusini..
tungetengeneza wenyewe lami tungekuwa na lami bora na nafuu
 
sawa hata angeamua kufanya hayo pia ungekuja hapa na wazo tofauti na hayo ,sijui unatakaje mkuu ili nafsi yako iridhike,ifike hatua wandugu tuone kuwa kuna haja ya kuacha kwanza yafanyike alafu ndiyo tuje na mapendekezo,kuliko hii ya kujifanya kila mtu anamaono
Mawazo ni kitu cha bure wala sio sheria. Kwamfano hili wazo la huyu jamaa kwasasa haliwezi kusaidia kwani umeme wa majumbani tu ni shida. Msichukulie mawazo ya watu kwenye negative way
 
Mawazo ni kitu cha bure wala sio sheria. Kwamfano hili wazo la huyu jamaa kwasasa haliwezi kusaidia kwani umeme wa majumbani tu ni shida. Msichukulie mawazo ya watu kwenye negative way
umeme shida?kivipi embu fafanua kidogo kwani mimi ninavyojua mradi wa rea unasambaza umeme karibu vijiji vyote hivi sasa nchini
 
Mpaka sasa tunajiuliza nini kipaumbele cha serikali hii ya awamu ya Tano? Jibu "Hapa ni papala tu..."
...kipaumbele ni fukuzafuza.
Wananchi ndo wanafurahia hicho.
Kati ya kazi walizofanikiwa mawaziri ni hiyo.
Hakuna ubunifu wa mipango na namna ya utekelezaji
Hata strategic plans za hizo taasis sidhani km mawazir wamezipitia
 
Back
Top Bottom