Matumizi ya Magufuli, tuyajadili

Matumizi ya Magufuli, tuyajadili

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,654
- Daraja la kigamboni bilioni 200
- Daraja la furahisha mwanza bilioni 200 (nakaribisha masahisho)
- Daraja la Coco Beach-bilioni 200 zimetengwa
- Barabara ya Dar-Chalinze-zaidi ya trilioni 1.3(dollar milioni 500)
- Mabasi yaendayo kasi -zaidi ya bilioni 200
- Flyover ya Ubungo bilioni 100

Iwapo serikali ingeamua kujenga treni za umeme badala ya mabasi yaendayo kasi ingetumia dollar milion 430 kwa km 32...yaani karibu Dar yote ingekuwa unapanda treni dakika 10 uko popote pale hata Kigamboni treni ingefika kupitia Mbagala.

Hii ni link ya Ethiopia inaelezea gharama za treni hizo na tayari wenzetu wanatumia..

Ethiopia gets first sub-Saharan Africa metro - CNN.com

Na kama hizo bilioni zingetumika kujenga vyuo vikuu UDOM gharama zake ilikuwa kiasi cha bilioni 25.
 
sawa hata angeamua kufanya hayo pia ungekuja hapa na wazo tofauti na hayo ,sijui unatakaje mkuu ili nafsi yako iridhike,ifike hatua wandugu tuone kuwa kuna haja ya kuacha kwanza yafanyike alafu ndiyo tuje na mapendekezo,kuliko hii ya kujifanya kila mtu anamaono
 
Ni huyu aliyekua akishinikiza kwenye vikao vya bajeti wizara yake ipewe hela nyjngi kwani nyingine hazina umuhimu!!!

Watu wenye akili wameshaanza kuchoka na huyu bwana....

Rais sio nyapara ndio maana hadi Leo tusio mashabiki hatujui ni ipi vision ya serikali yake....
 
mimi naona angeachana na madaraja yasiyo na tija hasa lile la coco ambalo naona kama anasa na urembo. Sioni element za kumsaidia masikini kwenye huu mradi.

Kwanza nchi lazima ikue holistically sio dsm tu. Priority ingekuwa ni kuunganisha mikoa yote na wilaya zote kwa rami.Hapo kutahamasisha maendeleo ya kweli.
Ahame na serikali yake yote pamoja na Ikulu wahamie dodoma.

Badala ya barabara SITA za Dar Challinze, Ingetengenezwa reli na treni express DSM moro, ninauhakika asilimia zaidi ya 40 ya wakazi wa dsm wangehamia Moro.
sina uhakika ila naona hizo barabara sita zitasababisha bottleneck effect.
 
sawa hata angeamua kufanya hayo pia ungekuja hapa na wazo tofauti na hayo ,sijui unatakaje mkuu ili nafsi yako iridhike,ifike hatua wandugu tuone kuwa kuna haja ya kuacha kwanza yafanyike alafu ndiyo tuje na mapendekezo,kuliko hii ya kujifanya kila mtu anamaono

Soma vizuri utajua sijapinga chochote
mimi naonesha tu matumizi yake
na nalinganisha na kwingine...
 
huyo ni mfalme juha ajiona ni mungu mtu kila kitu kinawezekana atakacho yy bila ushauri
 
mimi naona angeachana na madaraja yasiyo na tija hasa lile la coco ambalo naona kama anasa na urembo.

Kwanza nchi lazima ikue holistically sio dsm tu. Priority ingekuwa ni kuunganisha mikoa yote na wilaya zote kwa rami.
Hapo kutahamasisha maendeleo ua kweli.

Ahame na serikali yake yote pamoja na Ikulu wahamie dodoma.

Badala ya barabara SITA za Dar Challinze, Ingetengenezwa reli na treni express DSM moro, ninauhakika asilimia zaidi ya 40 ya wakazi wa dsm wangehamia Moro.
Nina uhakika ila naona hizo barabara sita zitasababisha bottleneck effect.

Na sehemu kubwa ya hizi gharama ni 'overpriced'
mfano amekuwa waziri wa ujenzi almost miaka 20
lakini haoni kuwa kuagiza lami kutoka nje kunasababisha gharama ziwe mara tatu zaidi
za ujenzi wa barabara....
 
Alipoanza Makusanyo yalikuwa Trilioni 1.3, Mwenzi uliyofuatia yalifika Trilioni 1.5 na yakafika Trilioni 1.0.. Swali la msingi mfuatano huu (trend) una maanisha nini?

Ni aibu hata kusema hadharani
sijui why haoni umuhimu wa ku stick na written speech
sasa hapo ni mapato yameongezeka au yameshuka?
si aliambiwa kila mwisho wa mwaka mapato huongezeka..
sio makusanyo stable ya kila mwezi
 
mimi naona angeachana na madaraja yasiyo na tija hasa lile la coco ambalo naona kama anasa na urembo.

Kwanza nchi lazima ikue holistically sio dsm tu. Priority ingekuwa ni kuunganisha mikoa yote na wilaya zote kwa rami.
Hapo kutahamasisha maendeleo ua kweli.

Ahame na serikali yake yote pamoja na Ikulu wahamie dodoma.

Badala ya barabara SITA za Dar Challinze, Ingetengenezwa reli na treni express DSM moro, ninauhakika asilimia zaidi ya 40 ya wakazi wa dsm wangehamia Moro.
Nina uhakika ila naona hizo barabara sita zitasababisha bottleneck effect.
Mkuu, umesema kitu kimenigusa. Kwa kweli express railway to Morogoro ingepunguza sana jam ya Dar. In fact, JPJM anatakiwa kuweka vipaumbele kwa mujibu wa mipango iliyopo. Vinginevyo tunaengelea kuthibitisha kuwa ni mkurupukaji.
 
Daraja la kigamboni bilioni 200
daraja la furahisha mwanza bilioni 200 (nakaribisha masahisho)
daraja la coco beach-bilioni 200 zimetengwa
barabara ya dar-chalinze-zaidi ya bilioni 200
mabasi yaendayo kasi -zaidi ya bilioni 200
flyover ya ubungo bilioni 100

Iwapo serikali ingeamua kujenga treni za umeme
badala ya mabasi yaendayo kasi ingetumia dollar milion 430
kwa km 32...yaani karibu Dar yote ingekuwa unapanda treni dakika 10
uko popote pale hata kigamboni treni ingefika kupitia Mbagala..
hii ni link ya Ethiopia inaelezea gharama za treni hizo na tayari wenzetu wanatumia..
Ethiopia gets first sub-Saharan Africa metro - CNN.com

na kama hizo bilioni zingetumika kujenga vyuo vikuu
UDOM gharama zake ilikuwa kiasi cha bilioni 25....
Watanzania wanajua mambo sasa hivi usipime! Mimi naona baada ya miaka 10 Tanzania itakuwa zaidi ya USA kwa sababu kila Mtz atakuwa anamiliki mijengo ya adabu kwa bajeti hizi ambazo wanazokichwani. Nahisi wabongo wana mikampuni ya hatari!!!
 
Kumuelewa Magufuli Na Utawala Wake Kwa UJUMLA Unahitaji Kutulia Na Wala Usiwe Na Papara! Soon Mtamuelewa TU
 
Back
Top Bottom