SoC02 Matumizi ya madawa ya kulevya; Sababu, madhara na namna ya kuzuia

Stories of Change - 2022 Competition

JAKA35853

New Member
Jul 19, 2022
3
1
Ilikuwa asubuhi na mapema baada ya hali yake kubadilika, alisikika akitoa kauli za matusi na vitisho vya kutaka kuua ndugu zake, ilikua ni takribani wiki mbilitu baada ya kufeli jaribio la kujiua. Ni mgonjwa wa akili ambaye amekua na historia ya matumizi ya madawa ya kulevya kwa kipindi kirefu.

Yeye binafsi anakiri kua ameeanza matumizi ya bangi tokea alipokua kidato cha kwanza alipokutana na marafiki wanafunzi wenzake waliomshawishi. Lakini sasa anasema wazi kua anatamania aache kutumia lakini anadai kua kwake imekuWa ngumu sana kuacha. Lakini ni kwa vipi amefikia hali aliyonayo kwa sasa?

Anakiri ushawishi kutoka kwa marafiki wapya aliokutana nao pindi tu alipojiunga kidato cha kwanza, hata hivyo hakua tayari lakini ushawishi ulipozidi aliona ili aweze endana na marafiki wake hao wapya ni kua mtumiaji wa bangi kama wao.

Je malezi ya wazazi walimu na jamii kwa ujumla ina madhaifu gani katika kukabili matumizi ya madawa ya kulevya? Kijana huyu ambaye alishakua mraibu wa marijuana anadai kua pamoja na kuanza kutumia marijuana(bangi) tokea akiwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza tu wazazi wake hawakua wanafahamu mpaka aliposhindwa kumaliza masomo yake ya chuo sababu ya kudorora kwa afya yake ya akili ikiwa ni matokeo ya matumizi ya madawa ya kulevya.

“Nikiwa sekondari walimu walifahamu na wamekua wakiwaadhibu wanafunzi wanaotumia marijuana kwa viboko na wakati mwingine walitupa adhabu kama kulima, kungoa visiki na kufanya usafi wa madarasa”

Je, inawezekana kuzuia matumizi ya madawa ya kulevya? Jibu ni ndio. ELIMU ni silaha muhimu katika kuzuia matumizi ya madawa ya kulevya. Elimu hii ya matumizi ya madawa ya kulevya haipaswi tu kutolewa mashuleni bali katika ngazi ya familia na jamii kwa ujumla juu ya sababu, madhara na namna ya kuzuia au kukabiliana na matumizi ya madawa ya kulevya. Kupitia elimu kutakua na ongezeka juu ya ufahamu kuhusu matumizi mabaya ya madawa hivyo kupunuza wagonjwa wa afya ya akili wanaotokana na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya.

Vidokezo vya kuzuia matumizi mabaya ya madawa kulevya na uraibu Usijaribu kutumia dawa ya kulevya hata mara moja. Baadhi ya watu wengi wakiwemo ni vijana hupenda kujaribu vitu. Na madawa ya kulevya ni moja ya vitu ambavyo vijana wengi hujaribu kutaka kujua ni nini haswa kinachowavutia watumiaji. Katika kujaribu ndiko kunakokua mwanzo wa matumizi ya madawa ya kulevya.
Kwa matumizi yoyote ya dawa zingatia maelekezo ya daktari.

Usitumie Zaidi ya dozi au mda kadri ya maelekezo ya daktari. Mfano kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi uraibu wa opioids(dawa za kupunguza maumivu) unaanza siku tano tu baada ya matumizi yake kuanza. Hivyo ni vyema kufuata ushauri wa daktari.

Katika kuzuia matumizi ya madawa ya kulevya ni vyema kutoa elimu juu ya madhara ya madawa ya kulevya kimwili, kisaikolojia, kiuchumi na kwa jamii kwa ujumla.

Madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya katika afya ya mwili ni pamoja na kukohoa, kuongezeka kwa hatari ya maambukizi katika mapafu, magonjwa ya moyo na kudorora kwa afya ya mwili kwa ujumla. Pia inawaweka watumiaji katika hatari ya magonjwa ya kuambukiza kama UKIMWI kwa wale wanaojidunga madawa ya kulevya.

Matumizi ya madawa ya kulevya katika saikolojia ni pamoja na kuongeza hatari ya magonjwa ya akili.
Madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya kiuchumi na kijamii ni pamoja kupotea kwa nguvu kazi, kuongezeka kwa watoto wa mitaani, kuvunjika kwa ndoa na kushiriki katika matukio ya kihalifu kama wizi na ubakaji.

Jambo la muhimu vya kuzingatia ni ushiriki wa wazazi, waalimu mashuleni, viongozi wa kidini, serikali na jamii kwa ujumla kushiriki katika kutokomeza matumizi mabaya ya kulevya. Nafasi kwa mtumiaji wa madawa ya kulevya vile vile ya kupewa elimu, ushauri, kumuonesha upendo na hata kumsaidia kuwaona wataalamu wa afya lengo likiwa ni kumsaidia. Jamii nyingi zimekua zikiwatenga, kuwasema vibaya au kuwaona vijana wasiofaa katika jamii na adhabu kama vibokoi hatua ambazo hazitoi ufumbuzi katika matumizi ya madawa ya kulevya.

Je, ni namna gani watu wote waliotajwa hapo juu wanaweza kushiriki katika kuzuia matumizi ya madawa ya kulevya?

WAJIBU WA WAZAZI: Wazazi ni watu muhimu na wa kwaza katika malezi ya watoto. Mzazi ana nafasi kubwa zaidi ya kujenga tabia za mwanae katika kukabiliana na changamoto za mfumo wa sasa wa maisha ya dunia ya leo. Wazazi tuanze kuwafundisha watoto kuhusu uhalisia wa maisha vitu vya kuwafundisha ni pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya madhara na namna ya kuyaepuka. Tuwalee watoto wetu katika misingi ya kiimani na misingi hii ianzie nyumbani tangu mtoto akiwa mdogo. Waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi. Tuna nafasi kubwa zaidi ya kuwajenga watoto wetu wawe na tabia chanya wakiwa wadogo kwa kuwafundisha na kuwaonesha upendo.

WAJIBU WA WAALIMU MASHULENI: Waalimu mashuleni ni watu ambao hukaa na watoto/wanafunzi kwa mda mrefu zaidi. Hii inafanya waalimu kugundua madhaifu katika tabia ya wanafunzi mapema na kua na idadi kubwa ya wanafunzi ukilinganisha na idadi ya waalimu. Waalimu tuwekeze zaidi kuwafundisha hawa wanafunzi juu ya madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya na kuwasaidia namna ya kuepuka. Tuwasaidie pia wale ambao tayari ni watumiaji kutafuta suluhisho la kitabibu badala ya adhabu ya viboko au adhabu nyingine kama kazi ngumu.

WAJIBU WA VIONGOZI WA KIDINI: Viongozi wa kidini wana nafasi kubwa sana katika malezi ya kiimani. Viongozi wa kidini tuweke nguvu na msisitizo katika matumizi ya madawa ya kulevya. Waumini wetu wafahamu madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya inavyoathiri Imani yao na pia itakua ni sehemu ya kuwalinda waumini wetu katika hatari za kudorora kwa afya zao.

WAJIBU WA SERIKALI: Ni pamoja na kutengeneza mazingira bora ya ajira kwa vijana na kujiajiri ili kuondoa tatizo la ajira na umaskini unaochangia kwa kiasi kikubwa tatizo la matumizi ya madawa ya kulevya.

Jambo la kuzingatia ni ikiwa wewe ni mtumiaji wa madawa ya kulevya na unataka kuacha ni vyema uzungumze na marafiki, ndugu unaowaamini na ni vyema zaidi kumuona mtaalamu wa afya kwa ushauri zaidi.

Unaweza pia kutushirikisha uzoefu wako juu ya matumizi ya madawa ya kulevya kama shuhuda katika jamii unayoishi au kama una historia ya matumizi ya madawa ya kulevya au kama wewe ni mtumiaji wa madawa ya kulevya kwa sasa.

ASANTE
 
Kunipigia kura bonyeza sehemu iliyo na alama kama hii ^
Hapo utakua umenipigia kura
 
Back
Top Bottom