Matukio ya kutengenezwa ya kujiteka

Masajihisho ya kichwa cha habari: Alijiteka. T226 DJQ
 
Hata kama huyu kajiteka ila haiondoi ukweli kwamba hayo matukio yapo
 
Simple tu!! kwanini serikali isifuatilie ili kujua wanaotengeneza hayo matukio ili wanaotengeneza hayo matukio wachukuliwe hatua zakisheria hali yakuwa uwezo huo serikali wanao kuliko kuendelea kutupiwa lawama hali yakuwa uwezo wakujitoa kwenye hizo lawama wanao?
 
Ok kuniteke wenyewe tumekusoma nyani. Lkn ulitakiwa umalizie kujipiga mabomu wenyewe,kujitwanga risasi za moto wenyewe nk nadhani andiko lako lingekua poa
 
Azory Gwanda!
 
Ni kweli waliowengi kwa sasa wanataka KIKI tu na kumchafua rais wetu kipenzi mrekebisha tabia mbovu za watu kutaka kuonekana miungu watu yaani mabwana na watwana, watashindwa na kidume JPM atawarekebisha wote, Bwana asifiwe!!
 
UNAPAFAHAMU HAPO KWA MJOMBA WAKE, ULIENDA UKAMKUTA HUKO? BAADA YA HAPO ALIENDA WAPI.
 
Taarifa hizi ni muhimu sana kwani zitasaidia kupata wapi vyombo vyetu vianzie ili kupata ukweli na suluhu ya haya matukio yanayoogofya kwa sasa.
Ofisi za kampuni ya basi hilo zipo,hivyo zitasaidia kupata taarifa za hawa abiria wawili wenye seat no.G3 na G4. Wote kati yao wakiwa muhimu zaidi ingawa mmoja wao ni rahisi kutumia taarifa za uongo pia au hata kukatiwa ticket na mtu mwingine. Lakini ushirikiano ukiwepo kuna jambo litafanyika.

Ikithibitika taarifa hizi ni kweli basi Sheria zifuate mkondo wake na Watanzania watakuwa wamejua aina ya vijana tulionao,wanasiasa tulionao,taifa tulilonalo pamoja na chuki tulizonazo.

Ikithibitika huuvni uzushi,sijui utakuwa unafanya mambo haya kwa faida ya nani. Nadhani hutastahili hata mbele ya shetani.

Lakini wito wangu kama taifa.....mambo yote haya yanaepukika. Tusikubali kutumika na wala mamlaka zisiwaingize vijana wetu katika dhambi mbaya eti kwa sababu wapo kwa ajili ya kutii kila AMRI inayotoka kwao.

TAARIFA HIZI NI MUHIMU KWA VYOMBO VYETU VYA USALAMA
 
Hata kama huyu kajiteka ila haiondoi ukweli kwamba hayo matukio yapo
Blackmailed, like, panda gari fika sehem flani Tupo nandugu yako. Usimwambie mtu. Concipiracy
 
wanataka umaarufu kupitia marehemu
 
Yaonekana ulihusika na huo utekaji. Na hadithi yako yatia mashaka.
Kinyume chake nenda katoe taarifa polisi ili "UCHUNGUZI" ufanyike ili kama itathibitika alijiteka akamatwe.
 
Inawezekana maana hata matukio ya kuokota wafu kwenye maji kwa idadi kubwa hayakuwa miongoni mwa mazoea yetu...
 

Na wengine wanajikata mapanga.....wanajipiga risasi.....dah hizi movie hizi
 

Hakuna haja ya kusubiri mpaka 2020. Jeshi la polisi na Usalama wa Taifa unapaswa kufanya kazi yake.

Watoe majibu hawa watu wapo wapi? Kama ni kwa mjomba ni rahisi sana kwa sababu huyo mjomba tayari ni alibi.

Kama hawajui hawa watu wapo wapi basi Jeshi liombe msaada nje lisaidiwe.

Serikali haitaki msaada. Serikali haitoi majibu ya uchunguzi wake kwenye haya mambo.

Lakini lawama Serikali haipaswi kutupiwa? Hili si suala si la imani kwani kila mtu anaweza kuamini chochote anachotaka.

Swali ni kwa nini hakuna majibu? Kama ni wapinzani wa Serikali wanateka watu, Jeshi la polisi halijui?

Magufuli kakemea haya mambo ya utekaji mara ngapi?
 
Nadhani polisi watakuwa wamepata clue kwa kwenda NEW FORCE na kuangalia majina ya wasafiri waliotumia siti namba G4 na G3 ila kwa sasa ngoja naye ahojiwe usiusemee moyo wake na kututoa kwenye reli.
 
Hawa watu wataendelea kucheza hii michezo ya kuigiza mpaka lini. Eti oh nimetekwa, huku bado unatumia simu. Kutekwa gani huko?
Usaniii ule ule ule wa akina Ben Saanane Roma mwandishi wa habari kujiteka,ni ule ule wa Lissu kujifyatulia risasi 38 na wengine kujikata mapanga mpaka kufa ,Watanzania tuko juu sana kwa usanii.
 
Tuondolee upuuzi wako hapa. Umekula maparachichi huko unakuja kutapika hapa? Hujiulizi kwanini kila anayeikosoa Serikali anapotea au kupigwa risasi?
 
Jamani mchina ni level nyingune lile bus T226DJQ lina gps tracker na kuna camera za siri, haya ngoja wadogo waumbuke sasa. Naomba sirro awachukue maelezo wafanyakazi wa hilo bus ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya huyu dogo mshenzi.
 
Nilisema tusubiri 2020 kama kuna haja ya kumuwajibisha Magufuli.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…