Matokeo ya Uchaguzi Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya Uchaguzi Mbeya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jan 24, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mkurugenzi wa _Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Rajabu Kiravu, alisema inawezekana majina ya waliokufa yakawa bado yapo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa sababu limeboreshwa.

  Alisema ni kosa lake kwa sababu alipoteza kitambulisho kwa hiyo wakati anakwenda kujiandikisha kwa mara ya pili akakosea jina kwa hiyo `system` ikajua ni mtu mwingine tofauti.

  ``Huyo mwenyekiti wa CCM alipoteza kadi yake ya kupigia kura ambayo ilikuwa na jina la Willim Sisala Simwali, alipokwenda kujiandikisha ili apewe kadi nyingine akaandika jina la William Sisala Simwali kwa hiyo alikosea herufi,`` alisema Kiravu.
  __________________________
  Nina wasiwasi na Kiravu hivi anaelewa maana ya kuboreshwa ? Watu 388 walikwisha kufa ,sasa kama kuboresha watu hao ilikuwa wasiwemo,hapa pana wizi wa kushirikiana na huyu Kirova.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Lakini wafu hawapigi kura. Hata kama majina yao yamo kwenye orodha ya wapiga kura.
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Whats up? sielewi nini kinaongelewa hapa!
   
 4. M

  Mama JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Heading yako inatuambia matokea ya uchaguzi Mbeya, hayo matokeo yako wapi?
   
 5. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,966
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Wasiwasi upi daftari liliboreshwa march 2008.sasa january2009.Katika kipindi chote cha miezi takriban tisa watu wangapi wameshakufa.kumbuka huko ni vijijini.After all vitambulisho vyote vinapicha kama mtu atatumia kitambulisho cha mtu mwingine atajulukana.Wasiwasi wa CUF mawakala wote wametoka aidha Pemba,Zanzibar.na DSM ,badala ya kuteua wa kutoka kijiji husika hivyo wanawasiwasi kwa sababu eti hawawamini wale wanaowaomba kura.
   
 6. K

  Kwaminchi Senior Member

  #6
  Jan 25, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Narudia tena kusema, "tatizo la Tanzania ni TANU/CCM na sisi Watanzania wenyewe." Huyu Kiravu kama si kada, basi atakuwa pandikizi.

  Mtu aliyekufa, hata kama jina lake lingalimo katika daftari la wapiga kura, ukweli ni kuwa hatapiga kura. Pana mushkeli gani hapo?

  Na kama mtu amepoteza kadi yake na anaomba kupewa kadi nyingine, huwezi kumwambia jina lake halikuandikishwa sawasawa. Yeye haandiki jina lake katika daftari. Ni kosa la nani kama jina lake ni WILLIAM na katika daftari pameandikwa WILLIM?

  Bwana Kiravu, anahakikishaje kuwa huyo anayeomba kadi nyingine, amepoteza kweli kadi yake ya awali? Na kwamba haendi kupiga kura mara ya pili?

  Kama yeye kazi yake ni kuhakikisha daftari la wapiga kura liko sawa, nivi sasa anamlalamikia nani?
   
 7. K

  Kwaminchi Senior Member

  #7
  Jan 25, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Narudia tena kusema, "tatizo la Tanzania ni TANU/CCM na sisi Watanzania wenyewe." Huyu Kiravu kama si kada, basi atakuwa pandikizi.

  Mtu aliyekufa, hata kama jina lake lingalimo katika daftari la wapiga kura, ukweli ni kuwa hatapiga kura. Pana mushkeli gani hapo?

  Na kama mtu amepoteza kadi yake na anaomba kupewa kadi nyingine, huwezi kumwambia jina lake halikuandikishwa sawasawa. Yeye haandiki jina lake katika daftari. Ni kosa la nani kama jina lake ni WILLIAM na katika daftari pameandikwa WILLIM?

  Bwana Kiravu, anahakikishaje kuwa huyo anayeomba kadi nyingine, amepoteza kweli kadi yake ya awali? Na kwamba haendi kupiga kura mara ya pili?

  Kama yeye kazi yake ni kuhakikisha daftari la wapiga kura liko sawa, hivi sasa anamlalamikia nani?
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,543
  Likes Received: 18,172
  Trophy Points: 280
  Matokeo gani wanayasubiri wakati uchaguzi bado hajafanyika!. By the way Mbeya sio Tarime. Mbeya ni maji mara moja. Ni CCM inapeta kwa ulaini kama kumsukumiza mlevi.
   
 9. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mwenye kujua yanayojiri huko Mbeya atuhabarishe, hata kama CCM watashinda, mwaka kesho si mbali!!
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hawapigi kura sawa ila hupigiwa na watu wengine kwa niaba yao tena wote humchagua yule anayetakiwa na Tume/Usalama wa Taifa na Polisi ashinde
   
 11. f

  faustin sungura New Member

  #11
  Jan 25, 2009
  Joined: Jan 16, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chadema mlisema wafuasi wenu wasimpigie kura mgombea wa cuf,leo ndio siku ya uchaguzi, je agizo lenu mmelifuatilia huko mbeya vijijini?
   
 12. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mpambanaji Sungura, karibu sana JF naona ndio post yako ya kwanza. Nilipenda msimamo wako hapa kuhusu unafiki wa CUF na CHADEMA.


  Chama cha NCCR-Mageuzi kutosimamisha mgombea

  2008-12-27 15:03:16
  Na Muhibu Said


  Ikiwa leo ni siku ya uteuzi wa wagombea katika uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Mbeya Vijijini, Chama cha NCCR-Mageuzi, kimetangaza rasmi kutosimamisha mgombea na kuvilaumu vyama vya CUF na Chadema kwa kusimamisha wagombea katika uchaguzi huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya NCCR-Mageuzi, jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Organaizesheni na Uchaguzi ya chama hicho, Faustin Sungura, alisema wamefikia uamuzi huo kwa maslahi ya upinzani na taifa.

  Sungura alisema CUF tayari ina wabunge 30 na Chadema ina wabunge 11 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo havikustahili kuweka tena wagombea katika uchaguzi wa Mbeya Vijijini.

  ``Vyama vya NCCR-Mageuzi na TLP hatuna wabunge. Katika akili ya kawaida ilitegemewa vyama visivyo na wabunge ndivyo vingestahili kupewa nafasi ya kuweka mgombea,`` alisema Sungura na kuongeza:

  ``NCCR-Mageuzi kwa maslahi ya upinzani na taifa kwa ujumla wake, tumeamua kutoshiriki katika uchaguzi wa jimbo la Mbeya Vijijini kwa kuweka mgombea, bali tutashiriki kwa kuwaelekeza wanachama, wapenzi na mashabiki wetu kukipigia kura chama kilicho katika ushirikiano na chama chetu``.

  Alisema katika kuheshimu ushirikiano wa kisiasa kati ya NCCR-Mageuzi na vyama vya CUF, Chadema na TLP, NCCR-Mageuzi iliiunga mkono CUF katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Tunduru mwaka 2007 na Chadema katika uchaguzi mdogo wa Kiteto, mwaka huu.

  ``Hata hivyo, katika uchaguzi wa Tarime mwaka 2008, mbali na vyama vyetu kutoa ahadi ya kumuunga mkono mgombea ubunge atakayeteuliwa na vyama ngazi ya jimbo la Tarime.

  Vyama vya CUF na Chadema vilikataa kuheshimu maamuzi ya kumuunga mkono mgombea wetu, Enock Haroun Marwa aliyeteuliwa na vyama vyetu kuwakilisha kambi ya upinzani,`` alisema Sungura.

  Hata hivyo, alivitaka vyama vya CUF na Chadema vikubali kukaa pamoja na kushirikiana wao wamteue mgombea mmoja dhidi ya mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  SOURCE: Nipashe
   
 13. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Upinzani una nafasi nyembamba kushinda Mbeya Vijijini Jumapili

  2009-01-21 10:48:36
  Na Theodatus Muchunguzi


  Mwelekeo mzima wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Mbeya Vijijini, mkoani Mbeya sasa ni dhahiri kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina nafasi kubwa na kitaibuka na ushindi katika uchaguzi huo utakaofanyika Jumapili ya wiki hii Januari 25.

  Katika uchaguzi huo ambao CCM kimemsimamisha Mchungaji Jackson Mwanjale; Chama Cha Wananchi (CUF) kimemsimamisha Daudi mponzi wakati Chama Cha Sauti ya Umma (Sau) kimemsimamisha Subira Mwakipiki, Mchungaji Mwanjale anapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi.

  Dalili za ushindi wa Mchungaji Mwanjale na CCM zinatokana na mwenendo mzima wa kampeni hizo zilizoanza Januari 4, ambazo kwa kiasi kikubwa zimebainisha kuwa CCM na mgombea wake wamefanya mikutano mingi ya kuomba kura.

  Ni jambo lisilo na ubishi kuwa kampeni za vyama vya CUF na Sau zimekuwa ni za kusuasua kwa kipindi chote.

  Hata hivyo, CCM kimepata bahati ya kukosa upinzani kutokana na kutoshiriki kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambacho aliyekuwa mgombea wake, Sambwee Shitambala, kumeenguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika orodha ya wagombea wakati wa uteuzi kwa maelezo kuwa alikiuka sheria ya viapo.

  Shitambala ambaye kugombea kwake kulikuwa kumeshaanza kuonyesha dalili kuwa kungesababisha ushindani mkali na kuzichangamsha kampeni hizo, baada ya kuenguliwa kampeni hizo zikadorora na CCM kukosa upinzani.

  Ilitarajiwa kuwa wanasiasa machachari wa Chadema wangekwenda Mbeya Vijijini kuchuana na timu ya kampeni ya CCM inayowajumuisha vijana wa chama hicho pamoja na wazee hususan mwanasiasa mkongwe ambaye ana rekodi ya kukibeba chama tawala katika uchaguzi mdogo, John Samwel Malecela maarufu kwa jina la ``Tingatinga``.

  Wanasiasa kama Mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrood Slaa; Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe; Mkurugenzi wa Vijana, John Mnyika; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu, ni miongoni mwa wanasiasa hao ambao wangeongoza kampeni hizo na kuzungumzia mambo mbalimbali mazito ya kitaifa.

  Ingawa hakuna utafiti rasmi uliokwishafanywa kubainisha nguvu za vyama vya upinzani nchini, lakini mwenendo wa hali ya kisiasa nchini hivi sasa unaonyesha kuwa Chadema kinaongoza kwa kuungwa mkono Tanzania bara wakati kwa upande wa Visiwani kama kawaida CUF kinaendelea kuongoza.

  Chadema kimepanda chati kutokana na uwezo wa kuibua ajenda mbalimbali za kuikosoa serikali na ujasiri wa kuzieleza kwa umma baada ya kuzifanyia utafiti.

  Miongoni mwa hoja hizo ni pamoja na kashfa kadhaa za ufisadi.

  Kwa upande wake, CUF kimeendelea kuwa na mvuto upande wa Visiwani pengine kutokana na chama hicho kujikita zaidi katika harakati za kushindana na CCM kutaka kushika dola ya Zanzibar. Kwa upande wa Tanzania bara hivi sasa CUF hakina hata mbunge mmoja wa jimbo.

  Udhaifu huo umekifanya chama hicho kukosa timu imara ya kukitangaza kwa ``kushikia bango`` ajendamuhimu za kitaifa ukimwondoa mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba na Naibu Katibu Mkuu, Wilfred Lwakatare.

  NCCR-Mageuzi kwa sasa hakina hata mbunge mmoja na hakijaibua mambo mazito ya kuikosoa serikali hasa kashfa za ufisadi na utendaji mbovu kiasi cha kuwavuta watu wengi zaidi.

  Chama hicho kilipata umaarufu mkubwa kuanzia mwaka 1995 baada ya Augustino Mrema kujiunga nacho akitokea CCM.

  Tanzania Labour (TLP) nacho kimepoteza nguvu kilichokuwa nazo kuanzia mwaka 1999 baada ya kumpokea Mrema kutokea NCCR-Mageuzi.

  Kujiondoa ama kuondolewa kwa timu ya wanachama na viongozi waliohamia katika chama hicho wakiwa na Mrema, kumekipunguzia nguvu kiasi kwamba hivi sasa hakina hata mbunge mmoja.

  Kwa maana hiyo, Chadema kinazidi kuwa na nguvu kila kukicha.

  Matokeo yaliyokipa ushindi katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Tarime na wa udiwani kata ya Tarime mkoani Mara Oktoba, mwaka jana, ni ushahidi tosha kuwa kina nguvu kubwa hasa kutokana na kuchuana na CCM pamoja na vyama vingine vya upinzani vya NCCR-Mageuzi na Democratic (DP).

  Kipimo rahisi cha kujua umaarufu wa chama cha siasa hapa nchini ni kuitisha mkutano wa hadhara na kuona idadi ya ya watu watakaojitokeza.

  Kipimo kizuri ni kuitisha mkutano katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.

  Hivi sasa chama cha upinzani kinachoweza kuitisha mkutanokatika viwanja hivyo na kuvijaza ni Chadem na kwa viwanja vya Zanzibar ni CUF.

  Kutokana na kupanda chati kwa Chadema ndiyo maana wananchi kadhaa walikuwa na shaukukubwa ya kufuatilia kwa karibu kampeni za Mbeya Vijijini kabla mgombea wa chama hicho kuenguliwa.

  Jambo linaloshangaza ni kuwasikia baadhi ya viongozi wa upinzani wakielekeza mashambulizi yao kwa Chadema wakati wa kampeni zinazoendelea Mbeya Vijijini badala ya kuyaelekeza kwa mshindani wao CCM.

  Hatua hiyo inaonekana wazi kudhihirisha kuwa ushirikiano wa vyama vinne vya TLP, Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi umekufa rasmi.

  Sababu kubwa ya viongozi wa upinzani walioko katika majukwaa ya kampeni jimboni Mbeya Vijijini kukishambulia Chadema ni kubaini kuwa CUF walichokwenda kukipigia debe hakina ubavu wa kuikabili CCM katika uchaguzi huo.

  Kauli zinazotolewa kuwa Chadema kimekiukamakubaliano ya kwapinzani kushirikiana hayana ukweli kwa kuwa katika uchaguzi wa Tarime hakuna chama kilichokiunga mkono licha ya kujulikana wazi kuwa ndicho kilichokuwa kinaungwa mkono na kukubalika kwa wananchi wengi wa Tarime.

  Madai kuwa CUF ilikiunga mkono Chadema Tarime siyo ya kweli.

  Hakuna agizo au kauli yoyote iliyotolewa na viongozi wa Taifa wa CUF kuwaeleza viongozi wa Mkoa wa Mara na Wilaya ya Tarime waiunge mkono Chadema, isipokuwa viongozi wachache wa mkoa na wilaya kama Mwenyekiti wa CUF Mkoa, Mustafa Wandwi walioonyesha nia ya kuiunga mkono Chadema kama watu binafsi, ambao hawakupata maelekezo ya viongozi wa taifa.

  Kama Profesa Lipumba na timu ya uongozi wa taifa ingetoa tamko na vile vile kufunga safari ya kwenda Tarime na kusimama majukwaani kuwanadi Charles Mwera,aliyekuwa mgombea ubunge na mgombea udiwani wa tarime Mjini, John Heche, hapo tusingesita kuwaita Chadema kuwa ni wasaliti wa upinzani.

  Katika kuonyesha kusikitishwa na uamuzi wa NEC kumwondoa Shitambala kugombea Mbeya vijijini kwa tiketi ya Chadema, kuna mtu mmoja aliyediriki kusema kwa utani kuwa ``wananchi wa Mbeya Vijijini watakosa uhondo wa kuiona Chopper na Mbowe`` akimaanisha kuwa hawataiona helkopta na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

  Licha ya watu kadhaa kusikitishwa na kuondolewa jina la mgombea wa Chadema, lakini wapo wanaounga mkono uamuzi huo wa NEC baada ya vyama vya CCM na CUF kuweka pingamizi.

  Kwa mfano, Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema, alisema mwishoni mwa wiki katika mkutano wa kampeni wa CUF wilayaniMbeya kuwa kuwekewa pingamizi kwa Chadema, Sambwee Shitambala katika uchaguzi huo na vyama vya upinzani siyo kosa kwa sababu alikiuka taratibu na sheria za uchaguzi.

  Katika mkutano huo wa hadhara wa kampeni uliofanyika
  katika mji mdogo wa Mbalizi kumnadi mgombea wa CUF ,Daudi Mponzi , Mrema alisema sio kosa mgombea kuwekewa pingamizi anapokiuka taratibu za kisheria zilizowekwa na NEC..

  Mrema alikwenda mbali zaidi kwa kuwataka wananchi kupuuza propaganda za viongozi wa Chadema wanaodai kuwa vipo vyama vya siasa ambavyo vinashirikiana na CCM kuhujumu demokrasia nchini na kukishutumu kuwa kimeshindwa kutimiza masharti na kwamba hiyo siyo mara ya kwanza kwa chama hicho kukiuka makubaliano ya ushirikiano.

  Lakini Mrema alilitumia jukwaa hilo kwa kukisifu CUF kuwa ni chama cha kiungwana kwa maelezo kuwa pamoja na kusalitiwa na Chadema katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Tunduru ilipofika uchaguzi wa Tarime walikiunga mkono Chadema.

  Mrema alisema chama chake kimeamua kukiunga mkono CUF katika uchaguzi wa Mbeya Vijijini kwa sababu chama hicho kiko mstari wa mbele kupigania demokrasia nchini.

  Kwa upande , Mwenyekiti wa Taifa wa PPT Maendeleo, Peter Mziray, akihutubia katika mkutano huo wa kuipigia debe CUF, aliwataka viongozi wa Chadema kutoa tamko haraka la kuwaunga mkono CUF katika uchaguzi huo.

  Katika kampeni hizo, zimetolewa kauli nyingi za kukishutumu Chadema kwa kutokiunga mkono CUF.

  Licha ya vyama vingine vinavyokiunga mkono CUF nacho kimetumia muda mwingi wa kampeni kuelezea jinsi Chadema kilivyokisaliti kwa kukaidi kukiunga mkono kutokana na kukubalika zaidi katika jimbo hilo kuliko Chadema.

  Kimsingi, kambi ya upinzani imeshiriki katika uchaguzi wa Mbeya Vijijini bila kuwa na ajenda za maana za kuwaeleza wapiga kura na wananchi wa Mbeya Vijini kwa ujumla kuhusu mambo yanayowapa kero na namna ya kuyashughulikia.

  Badala yake wametumia kampeni hizo kushambuliana wenyewe hasa Chadema na kusahau kuwa mpinzani wao mkuu ni CCM.

  Mwenendo mzima wa kampeni za upinzani unaondoa matumaini ya kushinda katika uchaguzi wa Jumapili na kutoa nafasi kubwa kwa CCM kulitetea jimbo hilo lililoachwa wazi na aliyekuwa mjumbe wake, marehemu Richard Said Nyaulawa, Novemba mwaka jana.

  SOURCE: Nipashe
   
 14. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkuu, sidhani kama hii ilihitaji kuwa katika thread mpya. Kuna thread ambayo inahusu matokeo ya uchaguzi huko Mbeya, ungeweza kuiweka hii yako kama post. Ile thread iko hapa:
  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/23420-matokeo-ya-uchaguzi-mbeya.html

  Anyway, new member karibu sana JF !!


   
 15. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sijasoma popote kuwa CHADEMA kwamba wanachama wake wasipigie kura mgombea wa CUF. Nilichosoma ni kauli ya Dr Slaa kwamba CHADEMA haiungi mkono chama chochote katika uchaguzi huo. Na kauli ya Mbowe kuwa CHADEMA haihusiki katika uchaguzi huo inaendelea na operesheni Sangara. Na kauli ya Zitto kuwa wananchi wawe huru kufanya uchaguzi huko Mbeya Vijijini. Hiyo ya kwamba wamesema CUF isipigiwe kura iko wapi?

  Asha
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - CUF na Chadema acheni utoto, mnajiabisha bure tu mbele yetu wananchi na mnazidi kutukatisha tamaa ni bora mnyamaze, maana mkizidi kuzozana inakuwa vigumu kwetu kuchagua yupi anayemfukuza mwenziwe ambaye ni mwendawazimu akiwa uchi,

  - Kama ya Mbeya yamewashinda, basi subirni majimbo mengine lakini acheni huu utoto wa siasa. Mkuu Kitila niliwahi kusema hapa kuwa Lipumba alinunuliwa kwa shillingi millioni 70 kutoka Oman kuwa bendera ya CUF bara, baada ya kuzikataa millioni 50 za CCM, ukamtetea sana kuwa ni mwalimu mwenzako na ana dignity na heshima sana na watu wengi sana hapa wakakuunga mkono, sasa unayaona haya ya CUF na Lipumba?
   
 17. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkuu Habarindiyohiyo, una uhakika kwamba huyu new JF member ndio yule mpambanaji? Isije ikawa ni majina tu yamefanana !!
   
 18. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona bado yuko hapa, yeye mwenyewe ndiye atuambie kama ni yeye au ni mtu mwingine ambae wamefanana majina.

  .....ndiyohiyo
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Na Maregesi Paul

  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeendelea kukishambulia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikisema chama hicho hakina nia ya dhati ya kuwakomboa wananchi kwa vile viongozi wake hawana historia nzuri ya kutetea wananchi.

  Akihutubia mkutano wa hadhara Manzese jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jusa, alisema ingawa viongozi wa Chadema wanawaambia Watanzania, kwamba chama chao ndicho kinachowajali zaidi, kauli hizo siyo sahihi kwa vile viongozi hao hawana historia ya kitaifa.

  “Chadema walikuwa hapa jana, Mbowe alisema mengi sana katika mkutano wake huo, lakini ukweli ni kwamba, chama hicho hakina jipya kwa sababu viongozi wake hawana cha maana ukilinganisha na viongozi wa CUF,” alisema Jusa.

  Alisema wakati CUF kinaanzishwa mwaka 1992, viongozi wa chama hicho walidhani wangeweza kushirkiana na vyama vingine vya upinzani kuiondoa CCM madarakani, lakini kutokana na sababu ambazo haziko wazi, chama hicho cha upinzani kimegeuka na kukidharau CUF ingawa CUF kina wanachama wengi katika maeneo yote ya nchi.

  Kutokana na hali hiyo, alisema njama za kuihujumu CUF zinazofanywa na viongozi wa Chadema hazitafanikiwa kwa vile chama hicho kinaheshimika kutokana na kazi nzuri zinazofanywa na viongozi wa chama hicho.

  “Chadema wanataka kutumaliza bila sababu za msingi kwa sababu siku hizi kila wanapopanda majukwaani, ajenda yao kubwa ni kutusema vibaya kadiri wanavyoweza. Lakini, ukweli ni kwamba, hawatatuweza na kama wanataka kujua nguvu tuliyonayo, basi wakawaulize CCM kwani ndiyo wanaotujua vizuri kuliko chama kingine chochote hapa nchini,” alisema.

  Akizungumzia majigambo ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, kwamba viongozi wa Chadema ndiyo vinara wa kupambana na ufisadi, Jusa aliwabeza viongozi hao na kutaka waeleze historia zao katika kipindi chote walichokaa bungeni kwa nyakati tofauti.

  “Mbowe anajidai yeye ni bingwa wa kupambana na mafisadi, sasa atuambie katika kipindi chote alichokuwa Mbunge alifanya nini na pia Dk. Slaa aseme alikuwa wapi kusema anayosema sasa kabla hajashinda tena kiti cha ubunge wa Karatu mwaka 2005,” alihoji Jusa .

  Awali, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho, Abdul Kambaya, alisema baada ya Chadema kuonyesha kuwa hawataki siasa za kweli, hivi sasa chama chake kinawahesabu kuwa ndiyo maadui zao namba moja pamoja na CCM.
   
 20. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu FMES

  Mbona viongozi wa CHADEMA hawajasema chochote hivi karibuni kuhusu Mbeya Vijijini toka waondolewe wakati ule? Naona ni CUF, TLP na NCCR ndio wanasema sema tu mambo mengi kuhusu CHADEMA.. Viongozi wa CHADEMA si wako kwenye Sangara yao wanazungumzia ufisadi tu katika taifa na sera za chama?

  Asha
   
Loading...