Baba Levo ashinda kesi ya uchaguzi.

Baba Levo ashinda kesi ya uchaguzi.

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,423
Reaction score
46,140
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Kigoma, leo Alhamisi Julai 16, 2026, imeifuta kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Mjini yaliyompa ushindi Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CCM, Levocatus Chipando maarufu Baba Levo.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Victoria Nongwa anayesikiliza shauri hilo amesema ushahidi uliowasilishwa na walalamikaji haukufikia kiwango cha kuwalazimisha wajibu maombi kuanza kujitetea mbele ya Mahakama.

Kesi hiyo ya uchaguzi namba 28949 ya mwaka 2025, iliyotokana na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, ilifunguliwa na wananchi wanne waliodai kuwa ni wapiga kura wa Jimbo la Kigoma Mjini ambao ni Johary Kabourou, Luma Akilimali, Pendo Kombolela na Lumu Mwitu.

Walalamikaji walikuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi huo wakidai kuwepo kwa ukiukwaji wa sheria za uchaguzi na kuiomba Mahakama ibatilishe ushindi wa Baba Levo.

Hata hivyo, baada ya kupitia ushahidi uliowasilishwa, Mahakama imeamua kuifuta kesi hiyo hatua inayomaanisha kuwa ushindi wa Levocatus Chipando unaendelea kusimama.
 
The expected from shyster Judges. Nimesema hapa hakuna.mahakama kuna takataka
 
"NJOENI KUTAMBUA MAITI KUMBE NI MKUTANO WA CCM"
Viongozi wa serikali kupitia chama cha mapinduzi CCM Mbeya wametumia mbinu ya kusema kuna maiti zipo watu waje kuzitambua maiti hizo kumbe hakuna maiti wanataka watu waende mkutanoni hii Ina maana gani?
Hii ni mbinu ya kuwakusanya watu wanaojiandaa Kwa msiba ndo waende kwenye mkutano?

Najiuliza hii inaonyesha uzima wa CCM au umaiti wa CCM je Kwa mantiki hii CCM Imekufa au IPO hai?

Eheeeeeeh nimewashtukia Kama mkutano wa CCM unaitishwa Kwa jina la kutambua MAITI basi ni wazi CCM ndio maiti yenyewe wananchi ee twendeni tukaizike hiyo maiti tumeitambua ni CCM ndo Imekufa na ndo maiti yenyewe hapa tusishtuke kama una D Mbili ushaelewa kaburi linachimbwa wapi
 
Kuna kipindi Zitto akiwa CHADEMA alipigwa kelele za kuutaka urais. Ila cha kushangaza alipoanzisha chama chake akawa hataki urais ila ubunge pekee yake. Zitto ni mnafiki sana. Bora ashinde huyo chawa kuliko mnafiki Zitto.
 
Back
Top Bottom