Habarindiyohiyo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 263
- 13
Date::1/31/2009
Profesa Lipumba amtaka Jaji Makame ajiuzulu
Kizitto Noya
SIKU chache baada ya Chama cha Wananchi (CUF), kushindwa katika uchaguzi wa Mbeya Vijijini, mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, ameibua shutuma nzito dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na kumtaka mwenyekiti wake, Jaji Lewis Makame, ajiuzulu.
Profesa Lipumba aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, akiwa Mtendaji wa tume,Jaji Makame, anapaswa kujiuzulu na tume hiyo kuvunjwa na kuundwa upya, kwa sababu imeshindwa
kusimamia chaguzi huru na haki.
Alisema kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi wa Mbeya Vijijini na wapigakura wengi kutojitokeza kupiga kura, kumetokana na udhaifu wa tume hiyo, katika kusimamia uhuru na haki katika chaguzi.
"Kampeni zilitawaliwa na vituko vya mashabiki kupigwa, bendera za CUF kuchanwa, masunduku ya kura kukutwa kwa watendaji wa CCM, FFU kuwatisha wananchi na kasoro nyingine nyingi ambazo CUF imeziripoti kwa msimamizi wa uchaguzi na polisi," alisema Profesa Lipumba.
Akitoa mfano wa tukio moja baada ya jingine, Profesa Lipumba alisema, katika kata ya Ikukwa, CCM iliingilia kampeni za CUF, kubandua mabango ya mgombea wa chama hicho na kuchana bendera zake huku baadhi ya makada wake, wakinunua kadi za wapigakura kwa fedha taslimu.
Kwa mujibu wa Profesa Lipumba, Daftari la wapigakura lilikuwa na udhaifu mkubwa uliojitokeza kwa majina ya watu waliofariki dunia kuendelea kuwepo na wengine kujiandikisha zaidi ya mara moja.
Akizungumzia suala hilo, Jaji Makame alimpuuza Profesa Lipumba akisema, anongea asichokijua.
Jaji Makame aliliambia gazeti hili jana kuwa tume yake haihusiki na matukio yote aliyoyaeleza Profesa Lipumba na kwamba uchaguzi huo ulifanyika chini ya msimamizi maalum.
"Hivi ni kweli Lipumba hajui kama kama tume imeshatoa masanduku, anayepaswa kuyatunza ni msamamizi wa uchaguzi," alihoji na kuendelea " Hata kama masanduku yalikutwa kwa balozi, baada ya kuyakagua polisi walikuta nini ndani yake."
Kwa mujibu wa Jaji Makame, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ilijitahidi kadiri ilivyoweza kufanya uchaguzi wa Mbeya Vijijini, kuwa huru na wa haki, lakini kilichovuruga ni kuondolewa kwa mgombea wa Chadema katika suala la kisheria.
"Sababu za matatizo hayo sio tume kwani imefanya kila liwezalo ikiwamo kutoa elimu ya uchaguzi katika vijiji vyote vya Mbeya ambako huenda Lipumba hakufika. Hapa kuna sababu nyingine, na sisi tunaungana na watu wanaosema kuwa uchache wa wapigakura umetokana na Chadema kuenguliwa kwenye uchaguzi huo," alisema.
Alisema ingawa hiyo ndiyo sababu ya msingi, halalamiki kwani Chadema iliondolewa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi na wala isingekuwa vyema tume kukiuka sheria hiyo kwa sababu ya kuuhamasisha uchaguzi huo.
Uchaguzi mdogo wa ubunge Mbeya Vijijini ulifanyika Januari 25 mwaka huu ambapo watu waliopiga kura walikuwa 44,855 kati ya 127780 waliojiandikisha.
Kura halali zilikuwa 4394, na kura zilizokataliwa zilikuwa 914.
Mgombea wa CCM Mchungaji Lackson Mwanjali alishinda kwa kura 32867 sawa na asilimia 73, CUF ilipata kura 10,578 ambazo ni asilimia 23 na Chama Cha Sauti ya Umma (Sau) kiliambulia kura 496 sawa na asilimia moja hivyo kura zote zilizopigwa ni sawa na asilimia 35.
Siku moja baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo hayo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejigamba kwamba asilimia 65 ya watu ambao hawakujitokeza kupiga kura, ni watu waliotaka kikipigia kura chama hicho.
Naibu katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe aliliambia gazeti hili jana kuwa watu hao ni wapenzi na wanachama wake ambao wameamua kutojitokeza kwa sababu ya chama hicho kuenguliwa.
Kabwe alitoa kauli hiyo baada ya Mwananchi kumtaka asema endapo anadhani kuwa idadi ya wapigakura ambao hawakujitokeza, ni wapenzi na wanachama wa Chadema.
"Unachosema ni kweli ni hii ni kwa sababu Tume imemwengua mgombea wetu ambaye alikuwa chaguo la wengi," alijibu kwa ufupi Kabwe na kuongeza:
Alisema wapiga kura hao waligoma kupiga kura kwa sababu walimkosa yule waliyetarajia kumchagua ambaye ni mgombea wa chama hicho alienguliwa katika kinyang'anyiro hicho Sambwee Shitambala.
Chanzo: Mwananchi