Matokeo ya Uchaguzi Mbeya

- Mkuu Asha ahsante kwa majibu yako, nilifkiri na nyinyi mnahusika na hizi nyepesi nyepesi za CUF huko, lakini nimekusikia mkuu.
 
Ukweli ni kwamba CCM watashinda, hawakuwa na upinzani, CUF haina ngome hapa Mbeya, kina Lipumba wanaudanganya umma, wameshiriki kuipa CCM ushindi kwa kumwekea pingamizi Mgombea wa chadema aliyekuwa akitakiwa na wapiga kura.

CUF walirubuniwa na CCM kutangulia kumwekea pingamizi Shitambala, wasingeweka wao CCM isingethubutu kumwekea kwani walijua watu hawataamini watajua ni njama za CCM, ndio maana mara baada ya CUF kumweka pingamizi nao CCM wakafuata.

Mwakani CCM hawana chao iwapo Shitambala atagombea, huyo mchungaji hana mvuto kabisa, CUF wakipata basi ni kutokana na hasira ya wananchi na msaada walioupata toka kwa Mrema ambaye bado anakubalika na watu wengi.
 
Hadi saa saba mchana ni watu wachache sana waliojitokeza kwa eneo la Mbalizi.

CUF wamepeleka Blue guard, wamewakamata makada wa CCM wakiwa na masanduku majumbani, mwanafunzi shule ya msingi kakamatwa na sanduku begani, waelekezaji wameteuliwa na maafisa watendaji badala ya Msimamizi ambaye ni DED, mawakala wa SAU wamegoma na kuchana kadi zao za uanachama zaidi ya 100.

CUF walia na mchezo mchafu wa CCM
 
Heading yako inatuambia matokea ya uchaguzi Mbeya, hayo matokeo yako wapi?

sasa ndugu huoni kama CCM imeshashinda hata uchaguzi bado,Kiravu anasema daftari limeboreshwa-- hivi ni nini maana ya kuboreshwa ,natumai daftari lingekuwa safi na marehemu wote wasingekuwemo ,hapo ndio tungekubali kuwa limeboreshwa ,japo ajali za mabasi kwa upande wa Mbeya ni nyingi watu zaidi ya mia tatu sidhani kama wangefikia tokea liboreshwe,na iweje wawemo ndani ya watakaoruhusika kupiga kura,maana kama wangekuwemo kwenye daftari la kudumu sawa lakini lililohakikiwa ni daftari ambalo ndio litumikalo leo.
Na hii ni dalili mbaya kwa uchaguzi mkuu ujao,sijui ni lini tutakuwa na ID ili kila atakaekufa Tanzania nzima itajua kuwa fulani amekwisha kufa na ni v itu ambavyo vinakuwa automatic ikiwa teknolojia itapata wajuzi wa kuifanyia kazi.
Ila mpaka hivi sasa Mbeya ni shwari na CCM wanaonekana wanyonge sijui kama wameshapenyezewa vikaratasi kuwa jamaa ameonekana kuanguka na mapema.
 
Opaque,
Huyu anayelialia kutaka aachiwe jimbo kwa kuwa hana mbunge hata mmoja ana sifa ya kuitwa mpambanaji? Anatakiwa apambane apate wabunge ndipo tumpe hiyo sifa ya upambanaji na si kusubiri kubebwa.
 
- The dataz huko ni kwamba so far ni aibu kubwa sana, yaani kati ya vituo vya kura 70 vya kata 17 za mjini, tayari CCM imezoa kura nyingi mno hata ni inasikitisha kusema, I mean we are talking about kura 100 against 0, ni kata zisizozidi 5 tu so far ndio CUF wamepata angalau hata kura 20 katika kushindwa, kama kulikuwa na mategemeo ilikuwa mjini na matokeo ndio haya, yaani huko vijijini itakuwa tsunami, inategemewa CCM kushinda kwa at least 98% ya kura zote,

- According to the dataz, CUF did everything they could ikiwa ni pamoja na kupeleka wabunge wake karibu wote huko Mbeya na Lipumba mwenyewe, lakini waliposhitukia kua hakuna uwezekano wakaanza filimbi za kawaida kwamba mabox yameibiwa na CCM na the rest of the story, hivi ninapoandika mabalozi wa nje waliokuwepo kuangalia uchaguzi wanakutana kwa faragha na kiongozi wa CCM katika uchaguzi huu.

- Anyways, by saaa mbili usiku tutakua na matokeo kamili.
 
Kwi kwi kwi kwi!!! siasa za TZ zinachosha kweli kweli. Kuna haja ya kupumzika na kukusanya nguvu ya 2010 maana najua wakati huo JF patafurika.
 
........................................After all vitambulisho vyote vinapicha kama mtu atatumia kitambulisho cha mtu mwingine atajulukana.Wasiwasi wa CUF ........QUOTE]

Message ya kwanza toka kwa mama imeingia JF kama 'fragment' natafuta chanzo sikioni lakini hata hivyo;

SaidSabke, suala la kuhakiki vitambulisho vyenye picha na kulinganisha na sura halisi huwa lina uzito sawa na lile la kujua kusoma na kuandika.
Kuna illiteracy ya kusoma picha. Enzi hizi tunaruhusiwa kutumia picha zilizoziba masikio na nywele na kuacha uso tu, hapo ndo kabisa!
 
Kwanza subirini naona mnasema mambo ya ajabu ajabu,hivi huyu mgombea wa CHADEMA aliyeenguliwa,Je kuenguliwa kwake ni sawa au amedhulumiwa,maana tupange na kuyatazama mambo yanavyokwenda kwa vile sisi sote ni wadau tusiwe na jazba kwa kuwa tu CUF imemwangua na wenyewe wa CHADEMA ni lazima wautazame ukweli kama walivyofanya CUF ni sawa basi hakuna haja ya kupiga makelele na kununa au kuona CUF ni wabaya kwani watu husoma kutokana na makosa na hivyo kwa kuwa haya ni makosa basi lawama zote ziwaendee wahusika wa Chama cha Mgombea ambao walitakiwa kuona wanamkinga mgombea wao na kila uwezekano wa kukosa kugombea,sioni sababu za wapenzi wa CHADEMA kuwavamia wanachama wa Chama kingine kwa mujibu wa kosa lililotokea ,wanachama na wapenzi hawana budi kuwalaumu wanaohusika na jukumu au hata wenye viti wao kwa kukosa uangalifu.
Ila hadi sasa matokeo bado kutokana na sababu za kuzimika umeme wakati kura zikianza kuhesabiwa.
 
Wapinzani hawatapata mafanikio yoyote katika chaguzi za Tanzania bila ya kuungana. Watanzania tumewapigia kelele juu ya umuhimu wa kuungana ili kuunda chama kimoja chenye nguvu. Hata Waziri Mkuu wa Kenya Odinga alipitembelea Tanzania ili wapate mafanikio ya kuing'oa CCM madarakani inabidi waungane, lakini wapi.

Kama wameshindwa huku Mbeya vijijini hakuna wa kulaumiwa bali ni wao wenyewe wapinzani. Hii danganya toto ya vyama vya upinzani 'vina ushirikiano' haitawafikisha kokote bila kuvunja vyama vilivyopo na kuunda chama kimoja chenye nguvu.

2010 inakaribia na dalili si nzuri maana bado kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwa Wapinzani. CCM haistahili kuendelea kuwa madarakani kutokana na matatizo mbali mbali yakiwemo ya mafisadi, lakini Wapinzani kwa kutotaka kuungana wanaisadia sana CCM kuendelea kubaki mdarakani kwa kuyaweka mbele maslahi yao badala ya yale ya Taifa. Enyi wapinzani sikilizeni vilio na ushauri wa Watanzania ili muungane kabla ya uchaguzi wa 2010 kwani bado kuna muda wa kutosha kabisa kuweza kufanya hivyo.
 
FMES,
Kama CUF walitegemea kushinda Mbeya vijijini wana wazimu, na hata Chadema kufikiria kwamba mgombea wao angeweza kuuzika Mbeya vijijini ni hadithi za Alinacha!..Walichouza kwa wananchi ni kuonyesha nani anayefaa kupokea ruzuku kati ya CUF na Chadema kwani yalikuwa majungu matupu!
Hivi vyama vyote vinatakiwa kuondoa different zao na kuunda umoja wa nguvu na sio kukimbilia ruzuku inapohitajika.. Chadema kabla ya Uchaguzi wa mwaka 2005, hakuna hata mmoja wetu aliyefikira wangeondoka na wabunge watano tu hasa nikitazama mikutano ya Mbowe..
Uchaguzi wa mwaka 2005 utumike kama fundisho na kama wataendelea kujenga matumaini ya uwezo wao pekee chini ya tawala ya dola CCM basi hizi ni njozi mpya kabisa!...
Namshukuru sana Mbowe kwa hotuba yake aliyoitoa Arusha na hakika matokeo ya Kiteto, Tukuyu na Mbeya vijijini yatumike kama funzo la kutazama wapi wamekosea...wajipange upya waondoe tofauti zao hasa ktk kugombea ruzuku badala ya maslahi ya Taifa..
 
FMES,
Kama CUF walitegemea kushinda Mbeya vijijini wana wazimu, na hata Chadema kufikiria kwamba mgombea wao angeweza kuuzika Mbeya vijijini ni hadithi za Alinacha!..Walichouza kwa wananchi ni kuonyesha nani anayefaa kupokea ruzuku kati ya CUF na Chadema kwani yalikuwa majungu matupu!
Hivi vyama vyote vinatakiwa kuondoa different zao na kuunda umoja wa nguvu na sio kukimbilia ruzuku inapohitajika.. Chadema kabla ya Uchaguzi wa mwaka 2005, hakuna hata mmoja wetu aliyefikira wangeondoka na wabunge watano tu hasa nikitazama mikutano ya Mbowe..
Uchaguzi wa mwaka 2005 utumike kama fundisho na kama wataendelea kujenga matumaini ya uwezo wao pekee chini ya tawala ya dola CCM basi hizi ni njozi mpya kabisa!...
Namshukuru sana Mbowe kwa hotuba yake aliyoitoa Arusha na hakika matokeo ya Kiteto, Tukuyu na Mbeya vijijini yatumike kama funzo la kutazama wapi wamekosea...wajipange upya waondoe tofauti zao hasa ktk kugombea ruzuku badala ya maslahi ya Taifa..

Nyie vijana mnaojifanya sijui mko marekani sijui wapi mnatumika vibaya sana. Laiti kama mngekuwapo hapa na kuonja hii joto ya jiwe msinge kuwa mnaropoka hayo maneno ya kukatisha tamaa kila kukicha. Mshindwe na mlegee kwa........................
 
Nyie vijana mnaojifanya sijui mko marekani sijui wapi mnatumika vibaya sana. Laiti kama mngekuwapo hapa na kuonja hii joto ya jiwe msinge kuwa mnaropoka hayo maneno ya kukatisha tamaa kila kukicha. Mshindwe na mlegee kwa........................
Tulia... nani anakudanganya kama kuishi Tz ni sawa na kuishi jehanamu?
 
CCM imeshinda uchaguzi wa Mbeya Vijijini. Kutokana na matokeo ambayo nimeyaona hapa kwenye kata mbalimbali mpaka sasa CCM inaongoza. Hata hivyo, idadi ya wapiga kura imekuwa ndogo sana. Katika kata za mjini kama utengule usongwe ambayo ina mji wa Mbalizi, wapiga kura waliojitokeza katika vituo vingi hawafiki hata asilimia 10. Wakati kwenye kata ya Ilembo waliojitokeza ni asilimia 15 tu ya wapiga kura wote. Kwenye kata nyingi zilizobaki wapiga kura waliojitokeza ni wastani wa asilimia 25, kati kata za Santilya, Iwiji, Iyunga Mapinduzi, Iwindi, Ikukwa nk. Mpaka ilipofika mchana hapakuwa na foleni za wapiga kura, watu wengi walikuwa makanisani, wengine majumbani na baadhi mashambani. Watu wengi walieleza dhamira ya kutokupiga kura kutokana na kampeni kupoteza mvuto baada ya mgombea wa CHADEMA kuenguliwa. Wananchi hao walikuwa wakielezea kwamba wanasubiri kupiga kura mwaka 2010 kukiwa na ushindani kati ya Shitambala na mgombea wa CCM. Nawapongeza timu yetu, hususani Mzee Malecela, kwani mbinu iliyotumika mchana ya kutuma mabalozi kwenye kila kaya kuhimiza watu kwenda kupiga kura ilifanya jioni ya kati ya saa 9 na 11 wapiga kura kujitokeza kiasi ambao kwa kweli wamechangia ushindi wa CCM. Nitawaletea matokeo kamili lakini katika vituo vingi CCM imeshinda kati ya asilimia 70 na 80 ya kura zilizopigwa. Nasubiri ya kata chache zilizobaki ili kupata matokeo kamili. Bado naendelea kujiuliza sababu ya watu kujitokeza chini ya asilimia 20 kupiga kura kama ni hiyo inayosemwa tu ya watu kususa baada ya CHADEMA kuondolewa au kuna sababu nyingine ya siri. CUF imeanza kulalamika kwamba imeshindwa kwa sababu ya hujuma za CCM na CHADEMA. Kwamba CCM imechukua kadi za kura kwa kubadilishana na mbolea na kwamba CHADEMA imechochea wananchi wasione umuhimu wa kupiga kura kwa kuwa wagombea wa CCM na CUF wameshirikiana kumwondoa mgombea aliyekuwa chaguo la wananchi wengi. Mrema naye ametoa lawama kwa CHADEMA kwamba ndio chanzo cha kuvurugika kwa uchaguzi huo.

…….ndiyohiyo
 
Chifu ataka CCM isichaguliwe Mbeya
Na Brandy Nelson, Mbeya

CHIFU mkuu wa kabila la Wamalila, lililo katika tarafa ya Isangati wilayani Mbeya Vijijini, Golian Mpoli, 90, amewataka wananchi wake kutokichagua chama

ambacho kinawanyima maendeleo na badala yake wamsubiri mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sambwee Shitambala, katika uchaguzi wa mwaka 2010.


Mgombea huyo alienguliwa kwenye kinyang'anyiro cha kiti cha ubunge cha jimbo la Mbeya Vijijini baada ya kugundulika kwa kasoro kwenye kiapo chake. Vyama vya CCM na CUF vilibaini kasoro hizo na kuweka pingamizi ambalo lilikubaliwa na Tume ya Uchaguzi.


Lakini chifu huyo wa kabila la Wamalila anaona kuwa bado kuna haja ya kumsubiri mgombea huyo katika uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa hawana la kufanya kwa sasa.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, Chifu Mpoli, akiwa na mkalimani kutokana na kutojua vizuri lugha ya Kiswahili, alisema kuwa toka uhuru wamekuwa wakitawaliwa na viongozi wa CCM, lakini hakuna maendeleo yoyote ambayo chama hicho kimewapa zaidi ya kuendelea kuwanyonya.


Alipoulizwa kuwa ni kwanini anamtaka Sambwee Shitambala kuwa mbunge wa jimbo la Mbeya Vijijini wakati hajawahi hata kuwaongoza na pia si mzaliwa wa tarafa hiyo ya Isangati, Chifu Mpoli alisema kuwa kutokana na jinsi alivyomuona na kutafakari anaamini anaweza kuwasaidia wananchi wake.


"Tangu afariki mbunge wetu Edward Shiwa aliyetuongoza kipindi cha mwaka 1995 hadi 2000, tulikuwa hatuna shida yoyote kwa kuwa alikuwa anatusikiliza na kutatua shida zetu na alianza harakati za kuleta umeme. Alifikia hatua ya kuwekwa nguzo na bahati mbaya akafariki dunia kabla ya kulimalizia," alisema.


Alisema tangu alipoondoka mbunge huyo bado nguzo hizo zimelazwa chini na

nyingine zimechimbiwa, lakini hakuna maendeleo yoyote ya suala la kupata umeme kwa wananchi wa tarafa hiyo.


Chifu huyo alisema kuwa Mbunge Shiwa ndiye aliwaletea wazo la kujenga Shule ya Sekondari ya Ilembo na kwamba baada ya hapo tangu mwaka juzi wamekuwa wakichangishwa fedha kila mara kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, lakini hakuna kinachoendelea.


"Baada ya kuondoka Mbunge Shiwa, kuna wabunge wa CCM walikuwepo lakini hakuna walilotufanyia kama huyu wa mwisho... pamoja na kuwa mimi ni chifu mkuu nilikuwa simfahamu... nilikuwa nasikia jina tu mpaka alipofariki dunia. Hivyo kwa niaba ya machifu wenzangu na wananchi, hatuitaki CCM... tunamsubiria Sambwee Shitambala mwaka ujao, ndiyo maana nimeamu kuja huku kuwaeleza," alisema.


Alipoulizwa sababu za kutoitaka CCM, chifu huyo alijibu kuwa viongozi wake wanawanyonya wananchi na wamekuwa na matatizo mengi katika eneo hilo lakini viongozi wa CCM wanashindwa kutatua na kwamba tayari kikao cha machifu kimefanyika katika kujadili suala hilo na kwamba wamekubalina wamsubiri Shitambala mwaka 2010 ili aweze kuwasaidia katika kusukuma gurudumu la maendeleo.


Wakiongea na Mwananchi, baadhi ya wananchi wa kata ya Ilembo walisema kuwa kitendo cha kuondolewa mgombea wa Chadema ni sawa na kunyang`anywa tonge la ugali mdomoni kwa kuwa hali hiyo imewasikitisha sana.


Walisema kuwa kati ya wabunge watatu waliowahi kuongoza jimbo la Mbeya Vijijini, ni Shiwa (CCM) ndiye aliyeweza kuwaletea maendeleo hivyo bado anahitaji mabadiliko na kwamba msimamo wao ni kuchagua chama pinzani.


"Kama Mbunge Yete Mwaliyego ambaye alichaguliwa mwaka 2000 huyo ndiyo hatusemi kwani alikuwa anaomba kura kwa mabavu na alifikia hata kutuambia kuwa mnichague msinichague mimi ni mbunge wenu tu na alipochaguliwa hakuonekana tena hadi naye alipofariki dunia," alisema Sipiti Solomoni wa Kijiji cha Ilembo.


Alisema kuwa wao ni wanachama wa CCM na wana kadi za CCM, lakini dhamira yao ilikuwa ni kumchagua mgombea wa Chadema kwa kuwa ndiye alikuwa chaguo lao hivyo kwa sasa hawana la kufanya.


"Kweli suala la mgombea wa Chaema kuondolewa limetuumiza sana tulikuwa tunampenda na bado tunampenda na tunamuhitaji awe mbunge wetu kwani ndiye tuliyemdhania kuwa angeleta mabadiliko katika jimbo hili... labda kama anaweza kupita huyo wa CCM wakimchagua kwani anasema kwa yeye katumwa na Mungu aje kuwa mbunge," alisema.


Walisema kuwa wanahitaji mabadiliko kwani CCM imekuwa ikiwahaidi lakini hakuna mafanikio yoyote na kwamba wamechoka na chama hicho ambcho wamekuwa wasikilza kiula mara sera zake lakini hakuna zinazotekelezwa katika eneo hilo.


"Msimamo wetu ni ule ule wa kutaka mbunge kutoka katika chama cha upinzani. CUF wamekuja hapa tumewasikiliza sera zao na tunawasubiri kuona sera zao ni nini kama tunaona nao hawaturidhishi, basi tutajua la kufanya," alisema mmoja wao.


Wananchi hao ambao walikuta wamesimama katika vikundi vikundi maeneo ya klabu cha pombe na sokoni katika kijiji hicho cha Ilembo ambacho rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi alizindua kampeni za CCM.


Walipohojiwa kama wangeenda kwenye mkutano huo wa uzinduzi, walisema kuwa wangeenda kwa ajili kumfahamu rais huyo mstaafu kwa kuwa hawajawahi kumuona.

Leo ni leo Mbeya Vijijini

Habari Zinazoshabihiana
• CCM: CHADEMA msijisumbue Mbeya Vijijini 09.12.2008 [Soma]
• Ajali yaua 4 papo hapo 05.07.2006 [Soma]
• Atangaza kumrithi Nyaulawa jimboni 15.11.2008 [Soma]

*Askari wajipanga, kuimarisha ulinzi
*Vigogo, CCM, CUF wajazana Mbeya
*Watu 126,780 kupiga kura


Rashid Mkwinda na Peter Twite, Mbeya

UCHAGUZI mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini unafanyika leo ambapo jana wagombea na wafuasi wa vyama vinavyoshiriki uchaguziu huo walifanya kampeni za lala salama katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

Majira Jumapili ilishuhudia askari wakiwa wanavinjari maeneo kadhaa wakiwa kwenye magari ya landrover 110 huku yakiwa yamewasha taa kuashiria kwamba hali ya ulinzi itaimarishwa wakati wa uchaguzi utakapokuwa unafanyika leo.

Msimamizi wa uchaguzo huo Bibi Juliana Malange alisema jana kwamba kuna jumla ya vituo 395 vya kupigia kura na jumla ya wapiga kura 126,780 kutoka kata 17 wanatarajiwa kupiga kura leo katika uchaguzi ambao hata hivyo hauna ushindani mkubwa kutokana na mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuenguliwa wiki chache zilizopita.

Ili kujiweka sawa katika kampeni za mwisho jana, Chama cha Wananchi (CUF) kilialika baadhi ya wabunge kutoka Tanzania Visiwani huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiwa kinapigiwa debe na wabunge wote wa chama hicho mkoani Mbeya ambao jana walikiuwa wametawanyika katika maeneo mbalimbali kuhakikisha chama chao kinaibuka kidedea kwenye uchaguzi huo.

Wagombea watakaopigiwa kura leo ni Mchungaji Luckson Mwanjale wa CCM ambaye kwa mujibu wa taaluma yake kama alivyojieleza katika kampeni za uchaguzi jimboni humo ana uzoefu na stashahada yaufundi ambaye hadi anagombea kiti hicho alikuwa ni Katibu mkuu wa Kanisa la Uinjilisti lenye makao yake makuu mkoani Mbeya.

Mgombea mwingine ni Bw. Daud Mponzi mwenye shahada ya uhandisi ambaye kwa mtazamo wa maelezo yake katika kampeni za uchaguzi atatumia utaalamu wake na uzoefu wake wazaidi ya miaka 30 akiwa mtumishi wa Shirika la Posta na simu kuhamasisha na kuboresha mahitaji muhimu ya wakazi wa jimbo hilo ambao wanahitaji maendeleo ya kisiasa kiuchumi na kijamii.

Mwingine ni Mgombea pekee mwanamke katika kinyang'anyiro hicho kutoka chama cha Sauti ya Umma SAU, Bibi Subi Mwakapiki ambaye kwa mtazamo wake kama mwanamke amejitoa mhanga katikati ya kundi la wanaume wenye mbinu mbalimbali za kampeni ambaye kwa mtazamo wake atatumia fursa yeye kama mjasiriamali kuwainua akina mama wenzie ambao anaamini wako nyuma kimaendeleo kutokana na mfumo dume uliopo katika wakati huu ambao kila mtu anahitaji maendeleo.

Aidha kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu jimbo hilo lilianza kuonekana kuwepo katika matumaini kwa juhudi binafsi za aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Richard Nyaulawa ambaye kwa hatua za awali aliweka mikakati ya kuanzisha kiwanda cha mbolea, Pembejeo za kilimo Company Limited.

Hata kabla ya kuhitimisha ndoto yake kwa wapiga kura wa jimbo lake Mwenyezi Mungu alimuita kwake huku akiacha fikra zake zikielea hewani ambapo kwa sasa wamejitokeza wagombea kwa tiketi ya vyama vitatu ambao kila mmoja anaangalia ni yupi ambaye anaweza kulivusha jahazi hili ng’ambo ya mto.

Chanzo: MAJIRA

CCM, CUF vitani Mbeya leo



na Christopher Nyenyembe, Mbeya




UCHAGUZI mdogo wa ubunge katika Jimbo la Mbeya Vijijini unafanyika leo ukivishirikisha vyama vitatu, Sauti ya Umma (SAU), Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), huku upinzani mkubwa ukitarajiwa kuwa baina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Wananchi (CUF).

Uchaguzi huo unafanyika leo baada ya kampeni kuhitimishwa jana huku zikikosa msisimko uliotarajiwa baada ya mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maaendeleo (CHADEMA) kuenguliwa kwenye kinyang’anyiro hicho, baada ya mgombea wake, Sambwee Shitambala kuwekewa pingamizi na vyama vya CCM na CUF.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 CCM iliibuka na ushindi kwa kupata asilimia 80 ya kura zote zilizopigwa.

Ni ukweli usiopingika kuenguliwa kwa mgombea wa CHADEMA, Sambwee Shitambala, kumeonyesha wazi kuipa mwanya CCM kuibuka na ushindi.

Katika uchaguzi huo, jumla ya wapiga kura 127,780 ikiwa ni ongezeko la wapiga kura 10,539 ikilinganishwa na wananchi 117,241 waliopiga katika uchaguzi mwaka 2005.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, Juliana Malange, wapiga kura 127,780 wanatoka kata 17 za jimbo hilo lenye vijiji 89 huku vituo 395 vimetengwa kwa ajili ya kupigia kura.

Ongezeko la wapiga kura zaidi ya 10,000 ndani ya kipindi cha miaka mitatu tangu uchaguzi mkuu ulipofanyika mwaka 2005 kunatia shaka na tayari yapo malalamiko kadhaa kutoka kwa viongozi wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo.

Kasoro zilizoainishwa na kulalamikiwa zinahusu Daftari la Kudumu la Wapiga Kura baadhi ya wapiga kura kuonekana na picha zao wamejiandikisha zaidi ya mara mbili, picha zikifanana huku majina yakibadilishwa.

Kasoro nyingine zilizojitokeza ni kuwepo kwa majina ya wapiga kura wa jimbo hilo waliokufa lakini majina yao hayajafutwa kwenye daftari hilo.

Katika uchaguzi wa 2005 uliomweka madarakani marehemu, Richard Nyaulawa alipata kura 65,109, huku CUF ikiambulia kura 6,833, ambazo zilikuwa sawa na asilimia 8.

Katika kampeni zilizomalizika jana, CUF ilijikita zaidi katika miji maarufu jimboni humo ya Mbalizi, Ilembo, Igoma, Iyunga Mapinduzi na Santilya wakati CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanya kampeni karibu vijiji vyote 89, huku ikiwa imepanga safu kubwa ya viongozi wake kutoka ngazi ya kitaifa hadi wabunge wote wa Mkoa wa Mbeya.

Chama cha Sauti ya Umma (SAU) kupitia mgombea wake, Subi Mwakapiki, hakikuweza kufanya kampeni za kutosha huku kikiwa kinaitupia lawama CCM iliyoongozwa na wapiga kampeni wake wakidaiwa kumkashifu mgombea huyo, mwanamke pekee katika uchaguzi huo.

Mazingira ya lugha chafu na uchochezi yalisababisha Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, katika dakika za lala salama awaonye viongozi wanaotumia lugha chafu na kukashifu wenzao huku akisisitiza kuwa mgombea wa SAU ana haki ya kulifikisha suala hilo kwenye vyombo vya sheria.

Katika madai yake alisema kuwa kata za Santilya na Ilembo majina ya watu wengi waliokufa yamebainika kuwepo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura wa jimbo hilo na wengine kadhaa kujiandikisha zaidi ya mara mbili.


Chanzo: Tanzania Daima
 
1. Wapinzani hawatapata mafanikio yoyote katika chaguzi za Tanzania bila ya kuungana.

2. Watanzania tumewapigia kelele juu ya umuhimu wa kuungana ili kuunda chama kimoja chenye nguvu.

3. Hata Waziri Mkuu wa Kenya Odinga alipitembelea Tanzania ili wapate mafanikio ya kuing'oa CCM madarakani inabidi waungane, lakini wapi.

4. Kama wameshindwa huku Mbeya vijijini hakuna wa kulaumiwa bali ni wao wenyewe wapinzani.

5. Hii danganya toto ya vyama vya upinzani 'vina ushirikiano' haitawafikisha kokote bila kuvunja vyama vilivyopo na kuunda chama kimoja chenye nguvu.

6. 2010 inakaribia na dalili si nzuri maana bado kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwa Wapinzani.

- Maneno mazito sana haya, mwenye masikio na asikie, ubarikiwe tu mkuu!
 
Muungano wa vyama vya Upinzani kweli ni Muhimu. Lakini kweli kuna haja ya Chadema kuungana na Chama kama TLP, UDP na sijui nini tena? maana hapo hujiungi na chama bali unajiunga na Mrema au Cheyo. Hivyo sio vyama bali Taasisi zao binafsi ndio maana hakuna mabadiliko yeyote ndani yake. CUF na NCCR navyo ni yaleyale, unafiki na undumila kuwili tu. Hivyo ni jambo gumu sana kumshawishi Mtu makini kujiunga na watu wa aina hiyo. Mpaka viongozi wababaishaji watakapotolewa katika vyama hivyo pengine ndio huo muungano utawezekana, vinginevyo tunajidanganya.
 
Matokeo rasmi yanakaribia kutangazwa. Sasa tume inamalizia kuweka pamoja matokeo ya kata mbalimbali. Uchambuzi wa matokeo unaonyesha kwamba CUF haikuwa na nguvu kabisa maeneo mengi ya ya vijijini. Viongozi wa CCM wanaeleza kwamba ilikuwa kazi rahisi sana kushindana na CUF kwa kuwa haikuwepo kwenye kata hizo. Wanasema kila kijiji walichokwenda walikutana tu na wanachama wa CHADEMA, hivyo mkakati ulikuwa ni kuwaeleza tu wananchi kuhusu kilichomwengua Shitambala. Wanasema hata TLP ilikuwa inaizidi CUF kwa mtandao wa chama kwa kiasi kikubwa sana katika jimbo la Mbeya Vijijini. Hawa wapinzani wameshazidiwa. CUF wanaendelea kulia kuwa wamefanyiwa hujuma, sasa wanalia zaidi na CHADEMA. Mchana wamepanga kufanya press conference


.........ndiyohiyo
 
Back
Top Bottom