Mswada mpya uliowasilishwa Bungeni unapendekeza kuondolewa kwa matakwa ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutangaza matokeo ya uchaguzi moja kwa moja (livestream) kutoka vituo vya kujumlisha kura.
Wanaounga mkono pendekezo hilo wanasema hatua hiyo inalenga kuboresha usimamizi wa uchaguzi na kuondoa changamoto za kiufundi ambazo zimekuwa zikijitokeza wakati wa utangazaji wa matokeo. Hata hivyo, wakosoaji wanaonya kuwa kuondoa matangazo ya moja kwa moja kunaweza kupunguza uwazi na kuathiri imani ya wananchi katika mchakato wa uchaguzi.
Iwapo mswada huo utapitishwa, IEBC haitakuwa na wajibu wa kisheria wa kuonyesha mchakato wa kujumlisha na kutangaza matokeo mubashara, jambo ambalo limekuwa likitazamwa na wengi kama njia ya kuimarisha uwajibikaji na kuruhusu wananchi kufuatilia uchaguzi kwa wakati halisi.
Pendekezo hilo limezua mjadala mkali miongoni mwa viongozi wa kisiasa, wanaharakati wa demokrasia na wananchi, huku wengi wakitaka kuhakikisha kuwa mabadiliko yoyote ya sheria hayaathiri uadilifu, uwazi na uaminifu wa uchaguzi mkuu wa 2027.
Ikiwa uchaguzi unapaswa kuwa wa haki na uwazi, kwa nini kuondoa utangazaji wa matokeo mubashara? Je, hatua hiyo itajenga imani ya wananchi au itaibua hofu ya uwezekano wa wizi wa kura?