BAK,Wapinzani hawatapata mafanikio yoyote katika chaguzi za Tanzania bila ya kuungana. Watanzania tumewapigia kelele juu ya umuhimu wa kuungana ili kuunda chama kimoja chenye nguvu. Hata Waziri Mkuu wa Kenya Odinga alipitembelea Tanzania ili wapate mafanikio ya kuing'oa CCM madarakani inabidi waungane, lakini wapi.
Kama wameshindwa huku Mbeya vijijini hakuna wa kulaumiwa bali ni wao wenyewe wapinzani. Hii danganya toto ya vyama vya upinzani 'vina ushirikiano' haitawafikisha kokote bila kuvunja vyama vilivyopo na kuunda chama kimoja chenye nguvu.
2010 inakaribia na dalili si nzuri maana bado kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwa Wapinzani. CCM haistahili kuendelea kuwa madarakani kutokana na matatizo mbali mbali yakiwemo ya mafisadi, lakini Wapinzani kwa kutotaka kuungana wanaisadia sana CCM kuendelea kubaki mdarakani kwa kuyaweka mbele maslahi yao badala ya yale ya Taifa. Enyi wapinzani sikilizeni vilio na ushauri wa Watanzania ili muungane kabla ya uchaguzi wa 2010 kwani bado kuna muda wa kutosha kabisa kuweza kufanya hivyo.
Zaidi ya nusu ya tunaochangia humu tunaonekana ni WAPINZANI. Viongozi wa upinzani huko waliko wanatusikiliza na kutusoma sana.Tumewasaidiaje/Tunawasaidiaje ili WAUNGANE/WAELEWANE?