Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mhe. Dk Shukuru Kawambwa akifafanua jambo wakati akizindua wa utekelezaji wa mikakati ya "Matokeo makubwa Sasa" ambapo kwa kingereza unaitwa "Big Result now" katika sekta ya elimu.
Mwaka 2012 watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha sita walikuwa ni 46,658. Mwaka 2013 watahiniwa 50,611 walifanya mtihani huo na kati yao 44,366 walifaulu. Mwaka 2014 watahiniwa 40,695 walifanya mtihani ambapo watahiniwa 38,905 walifaulu.
Matokeo ya mwaka 2013 yanaonyesha kuwa watahiniwa 325 waliofanya mtihani wa kidato cha sita walipata Division I. Matokeo ya mwaka 2014 yanaonyesha kuwa watahiniwa 4,365 wamepata Division I. Ukilinganisha na mwaka jana hapa kuna ongezeko la watahiniwa 4,040 ambayo ni sawa na 1243% waliopata Division I mwaka huu. Niwape pongezi akina
Mamndenyi na wengine wooote ambao watoto wao wamepata Division I.
Waliopata Division II mwaka jana walikuwa 5,372 na mwaka huu ni zaidi ya watahiniwa 9,631, ongezeko la karibu mara mbili au zaidi. Waliopata Division III mwaka jana ni 30,183 na mwana huu ni 16,821. Watahiniwa waliopata Division IV ni 4,362 na mwaka huu ni 4,420. Waliotaka yai mwaka jana ni 2,604 na mwaka huu ni 612 tuu ambapo ni tofauti ya watahiniwa 1992, sawa na 325%!
Kutoka watahiniwa 325 waliopata Division I mwaka 2013 hadi watahiniwa 4,365 siyo mchezo. Waingereza/Wamarekani watakuambia this is extraordinary. Pia kutoka zero zaidi ya 2000 mwaka jana hadi kufikia zero 600 mwaka huu ni maajabu ya karne. Natumaini mwaka huu hakutakuwa na vilio na malalamiko mengi kutoka kwa wazazi juu ya watoto wao kutaga mayai. Hao 600 waliotaga mayai must be very unlucky indeed.
Matokeo haya ni mafanikio makubwa sana ukizingatia kuwa shule ni zile zile na walimu ni wale wale, changamoto kwenye sekta ya elimu ni zile zile, bado kuna uhaba wa mahabara na vitabu, walimu wanalalamika mishahara midogo (nasikia wengine wanataka kugoma), uhaba wa walimu, n.k. Lakini pamoja na hayo yote bado wanafunzi wameweza kupasua ile mbaya. Who knows may be maombi ya akina
Kaunga nayo yamesaidia na Mungu akaamua kufanya miujiza hii ya karne.
But whether amkawewe calls this "genetically modified results" or CHUAKACHARA "politically modified results", I say this is BIG RESULTS NOW, MENGINE TUTAJIJU HUKO MBELE.
Ndiyo maana vyombo vingi vya habari vimenywea kuchanganua haya matokeo.
Pia poleni Alumni wooooote wa Tambaza.