Matokeo Kidato cha sita: Lengo limetimia!

Matokeo Kidato cha sita: Lengo limetimia!

Critical analysis.....,, Behaviour and academic performance are twin sisters..... How come a deteriorated society leads in academic matters..... God bless Tanzania......
Asante BRN ila huko vyuoni hizo disco sijui tu???? yaani kweli ni watu 600+ ndio waliopata zero???? ina maana zamani watu walikua hawasomi??? kweli kizazi hiki cha kiduku na model wote wafaulu??? masikini Tanzania yangu!!!! yaani kwa mfumo huu wote tuliosoma zamani tungekua vyuoni au maprofesa
 
Magumash matokeo kidato cha sita 2014.div 0 mwaka jana zilikua 2604 mwaka huu 612 tofaut ni asilimia 325% div 1 mwaka jana zlikua 325 mwaka huu 4365 sawa na ongezeko la asilimia 1243% haya ni maajabu ya karne. Swali hivi ni walimu walewale wa shule zilezle zilizotoa one 300 mwaka jana ndo wametoa one 4000 mwaka huu? Vipi kuhusu

changamoto zao zimetatuliwa? Maabala zimejengwa madai ya walimu yamelipwa.kama jibu ni hapana mabadiliko ya ghafla yametoka wapi? Kweli tumeamua kutanua goli tufunge kilahisi. Karibu tanzania hii ndio big results nw bwana.mchana mwema
 
Ndicho walichofanya hawa wa BRN! Nakupa homework, though ni ngumu kuifanya, if possible, let the NECTA use the old grading system and see if the the current passes will stand.Nawasilisha.

Definitely Division I zaidi ya 4,000 hazitapatikana.

Lakini wazazi wengi niliongea nao seem to be pleased with these results.

Kuliko mwanae apate Division III kwa grade ya zamani ni heri eti apate Division I kwa grade ya sasa.

BTW vyuo vyetu vikuu vinaweza kuchukua wanafunzi zaidi ya 4,000 kwa mkupuo?

If not, then kupata Division II siyo guarantee ya kwenda Chuo.

Kama vinaweza then, vyuo vitakuwa vinanamwaga kama shule za kata unless ma-lecturers wafelishe nusu.
 
Fowarded as received

Unajua maana ya BIG RESULTS NOW?? Fuatilia matokeo haya ya kidato cha sita.

Division zero mwaka jana 2604, mwaka huu 612. Tofauti watu 1992, sawa na asilimia 325%.

Division one, mwaka jana 325, mwaka huu 4,365. Tofauti 4040, sawa na asilimia 1243%. Haya ni maajabu ya karne.

Walitanua ukubwa wa goli ili iwe rahisi kufunga... Kutoka zero zaidi ya 2000 mwaka jana hadi zero 600 tu mwaka huu. Kutoka div.one 300 tu mwaka jana hadi one zaidi ya 4,000 mwaka huu.

Hivi waalimu walewale wa shule zilezile zilizotoa one 300 mwaka jana ndo wametoa one 4,000 mwaka huu??

Changamoto zao zimetatuliwa? Maabara zimejengwa? Vitabu vimeongezwa? Madai ya walimu yamelipwa? Waalimu wa Kiswahili wameacha kufundisha Hesabu kutokana na ukosefu wa waalimu wa hesabu?

Kama changamoto hizo zote hazijatatuliwa mabadiliko haya ya ghafla kutoka div.one 300 hadi div.one zaidi ya 4,000 yametoka wapi? Kweli tumeamua kutanua goli tufunge kirahisi. Karibu Tanzania, hii ndiyo BRN bhana.!

Wanasema BRN means Big Results Now, mimi namwambia Waziri Kawambwa BRN, yani he should "Better Resign Now" maana watoto wetu wanapata BRN = Brain Receive Nothing.!

Kwa kweli hata mimi nilijiuliza mara mbili shule kama Tambaza, Mtwara Tech na Ifunda Tech ziwe kumi bora za Mwisho Kitaifa. Hata taarifa ya habari saa2 usiku( 18.07.2014) Star Tv wananchi wameshangazwa sana!
 
Fowarded as received

Unajua maana ya BIG RESULTS NOW?? Fuatilia matokeo haya ya kidato cha sita.

Division zero mwaka jana 2604, mwaka huu 612. Tofauti watu 1992, sawa na asilimia 325%.

Division one, mwaka jana 325, mwaka huu 4,365. Tofauti 4040, sawa na asilimia 1243%. Haya ni maajabu ya karne.

Walitanua ukubwa wa goli ili iwe rahisi kufunga... Kutoka zero zaidi ya 2000 mwaka jana hadi zero 600 tu mwaka huu. Kutoka div.one 300 tu mwaka jana hadi one zaidi ya 4,000 mwaka huu.

Hivi waalimu walewale wa shule zilezile zilizotoa one 300 mwaka jana ndo wametoa one 4,000 mwaka huu??

Changamoto zao zimetatuliwa? Maabara zimejengwa? Vitabu vimeongezwa? Madai ya walimu yamelipwa? Waalimu wa Kiswahili wameacha kufundisha Hesabu kutokana na ukosefu wa waalimu wa hesabu?

Kama changamoto hizo zote hazijatatuliwa mabadiliko haya ya ghafla kutoka div.one 300 hadi div.one zaidi ya 4,000 yametoka wapi? Kweli tumeamua kutanua goli tufunge kirahisi. Karibu Tanzania, hii ndiyo BRN bhana.!

Wanasema BRN means Big Results Now, mimi namwambia Waziri Kawambwa BRN, yani he should "Better Resign Now" maana watoto wetu wanapata BRN = Brain Receive Nothing.!

Elimu kuchakachuliwa ilianza toka enzi za mwalimu baada ya kuanza mpango wa walimu waupe yaani darasa la saba kumfundisha la saba mwenzie!mimi shule ya msingi niliyosomea mwalim wetu wa hesabu alikuwa hajui hata hesabu ndogo za maumbo! kwakuwa wengine tulikuwa tukifundishwa na kaka zetu waliokuwa vyuoni tulikuwa tunabaki kumtizama tu anavyochemka! hivyo km serikali ilifanya uchunguz kipindi cha matokeo yakiwa mabaya na sasa hv wanatakiwa kufanya uchunguz kwa matokeo haya tena washirikishe wataalam waliopo nje ya system ili uchunguz uwe huru!shenz gete
 
Grades zilizotumika miaka ya nyuma..

75 -100 A
65-74 B
55-64 C
45-54 D
35-44 E
25- 34 S
0- 24 F..

Grades za sasa hivi.. (BRN)

75 -100 A
60-74 B+
50-59 B
40- 49 C
30- 39 D
20-29 E
0-19 F..

Ukijarib ku compare hzo grades.. Tofauti iliyopo sio kubwa sana kama wengi wanavyodhani.. Ahsanteni..

Hivi boss unatumia akili utasemaje tofaut ni ndogo km mfano E ya 40 ya zaman ni sawa na C ya 40 ya sasa hv ambayo inaonyesha mwanafunz amefanya vizur kumbe kafeli
 
Grades zilizotumika miaka ya nyuma..

75 -100 A
65-74 B
55-64 C
45-54 D
35-44 E
25- 34 S
0- 24 F..

Grades za sasa hivi.. (BRN)

75 -100 A
60-74 B+
50-59 B
40- 49 C
30- 39 D
20-29 E
0-19 F..

Ukijarib ku compare hzo grades.. Tofauti iliyopo sio kubwa sana kama wengi wanavyodhani.. Ahsanteni..

Mkuu ningependa kujua ulimaliza mwaka gani. form six na pia ulipata division gani ndipo uendelee kukoment ili usiendelee kuwa potosha wengine!!
 
polen sana kama mlikosa bahat ya kupendwa na serikal,ila wenzenu 2mepata bahati hyo achen tuitumie BRN
 
Last edited by a moderator:
hivi div ii pts 11 (Economics c, geography d na mathematics d) ya 1990 leo ingefair vipi?
 
Wahusika wa mitaala na mitihani ya kidato cha
nne na sita,kuanzia Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi hadi Baraza la Mitihani la Taifa
(NECTA),wanapaswa kujipongeza. Lengo
limetimia. Katika matokeo ya kidato cha sita
yaliyotangazwa leo, asilimia zaidi ya 90 ya
watahiniwa wamefaulu. Matokeo makubwa sasa!
Daraja la kwanza ingawa limepunguzwa kutoka
3-9 hadi 3-7 limesheheni;daraja la pili lipo la
kutosha;daraja la tatu limejaa;la nne lina watu
bwerere na sifuri zimepungua mno (si zaidi ya
650). Jipongezeni kwa matokeo haya kwakuwa
mmetimiza lengo. Hongereni!
Furahini mkijua kuwa elimu yetu ndiyo inazidi
kuvurugika. Kuanzia wanafunzi wenyewe,wazazi/
walezi na washika dau wengine hawajui hata
kukokotoa madaraja na hata alama. Hawajui
kwanini daraja la kwanza limeishia alama 7 na si
9.Hawajui kwanini kuna A-D za General Studies.
Hawajui kama kwenye daraja husika kama
kumehesabiwa General Studies na BAM au
la.Lakini,wanasheherekea matokeo.
Vyuo navyo vitawekwa njia panda. Itabidi uundwe
utaratibu mpya wa 'cut-off points' ili kuendana na
matokeo haya. Yote haya yanafanyika ili ionekane
kuwa elimu yetu inapaa kwa kuwa na ufaulu wa
juu: zaidi ya asilimia 90. Lengo kubwa ni
kuonyesha umma wa watanzania na dunia kwa
ujumla kuwa elimu yetu na watahiniwa wetu sasa
ni moto wa kuotea mbali. Safari hii hamtapigiwa
kelele wala kuundwa Kamati. Mmefaulisha vyema
sasa.
Lakini,mambo ni tofauti. Wahusika mjipongeze
huku mkijiuliza kama kweli mko sahihi kuichora
elimu ya nchi hii hivi mnavyofanya....
 
Asante BRN ila huko vyuoni hizo disco sijui tu???? yaani kweli ni watu 600+ ndio waliopata zero???? ina maana zamani watu walikua hawasomi??? kweli kizazi hiki cha kiduku na model wote wafaulu??? masikini Tanzania yangu!!!! yaani kwa mfumo huu wote tuliosoma zamani tungekua vyuoni au maprofesa

disco zitoke wapi vyuoni .... watu wamejipanga kuchakachua mpaka vyuo .... subiri uone! .... ma engineers fake, madaktari fake ili mradi ilani ya chama itimizwe kwa 110%!
 
HAKUNA ENEO LA BRN ambalo litafanikiwa kiualisia kama si means justify the aim, BRN ni upuuzi mwingine. ELIMU INASHUKA!!
 
HAKUNA ENEO LA BRN ambalo litafanikiwa kiualisia kama si means justify the aim, BRN ni upuuzi mwingine. ELIMU INASHUKA!!
 
Back
Top Bottom