Binti apotea baada ya matokeo ya kidato cha sita

Binti apotea baada ya matokeo ya kidato cha sita

Best home tutor

Senior Member
Joined
May 8, 2026
Posts
194
Reaction score
265
Binti mwenye umri wa miaka 19, Neema Phinias Eric (maarufu kama Anifa), mkazi wa Tarime Sirari, anadaiwa kutoweka nyumbani kwa dada yake alipokuwa amekwenda mapumzikoni tangu Siku ya Jumatatu, Julai 6, 2026, kufuatia kutoka kwa matokeo ya Kidato cha Sita.

Neema, ambaye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Robanda iliyopo Wilayani Serengeti, mkoani Mara, alikuwa amesafiri kuelekea Kata ya Nyakato, Wilayani Musoma, kupumzika nyumbani kwa dada yake mkubwa, Happiness Rhobi, baada ya kumaliza mitihani yake.

Kwa mujibu wa maelezo ya dada yake, mara baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kutangaza matokeo na Neema kubaini kuwa amepata Daraja la Tatu (Division 3), aliaga kwenda kwenye duka la uchapaji (stationery) ili kujiridhisha zaidi na matokeo hayo, lakini hakurejea tena nyumbani mpaka sasa.

Taarifa za kupotea kwa binti huyo tayari zimewasilishwa na kuripotiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya ya Musoma na kupewa namba ya jalada MUS/RB/4686/2026.

Ndugu, wazazi na familia wanaomba msaada wa umma: Mtu yeyote atakayemuona Neema/Anifa anaombwa kutoa taarifa mara moja katika kituo chochote cha Polisi au kanisa lililokaribu, au kupiga simu moja kwa moja kupitia namba: 0623907117 au 0624166420.

Msaada wako ni wa muhimu sana kuokoa maisha. Tafadhali sambaza taarifa hii au toa maoni yako kupitia ukurasa huu ili kuisaidia familia ya Neema kumpata binti yao.
 
1000003132.jpg
 
Jiandaeni kuja wajitambulishe kwamba mstafute yupo pahala anachezea zeze
 
Huyo yuko anachezea ukuni tu hapo mwigobelo..
 
Back
Top Bottom