Matokeo Kidato cha sita: Lengo limetimia!

Matokeo Kidato cha sita: Lengo limetimia!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,143
Wahusika wa mitaala na mitihani ya kidato cha nne na sita,kuanzia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi hadi Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA),wanapaswa kujipongeza. Lengo limetimia. Katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa leo, asilimia zaidi ya 90 ya watahiniwa wamefaulu. Matokeo makubwa sasa!

Daraja la kwanza ingawa limepunguzwa kutoka 3-9 hadi 3-7 limesheheni;daraja la pili lipo la kutosha;daraja la tatu limejaa;la nne lina watu bwerere na sifuri zimepungua mno (si zaidi ya 650). Jipongezeni kwa matokeo haya kwakuwa mmetimiza lengo. Hongereni!

Furahini mkijua kuwa elimu yetu ndiyo inazidi kuvurugika. Kuanzia wanafunzi wenyewe,wazazi/walezi na washika dau wengine hawajui hata kukokotoa madaraja na hata alama. Hawajui kwanini daraja la kwanza limeishia alama 7 na si 9.Hawajui kwanini kuna A-D za General Studies. Hawajui kama kwenye daraja husika kama kumehesabiwa General Studies na BAM au la.Lakini,wanasheherekea matokeo.

Vyuo navyo vitawekwa njia panda. Itabidi uundwe utaratibu mpya wa 'cut-off points' ili kuendana na matokeo haya. Yote haya yanafanyika ili ionekane kuwa elimu yetu inapaa kwa kuwa na ufaulu wa juu: zaidi ya asilimia 90. Lengo kubwa ni kuonyesha umma wa watanzania na dunia kwa ujumla kuwa elimu yetu na watahiniwa wetu sasa ni moto wa kuotea mbali. Safari hii hamtapigiwa kelele wala kuundwa Kamati. Mmefaulisha vyema sasa.

Lakini,mambo ni tofauti. Wahusika mjipongeze huku mkijiuliza kama kweli mko sahihi kuichora elimu ya nchi hii hivi mnavyofanya.....
 
Namkumbuka dada Joyce Ndalichako, sijui alienda wapi yule dada? Ana msimamo wa viwango kumzidi hata kaka Mukandala.

Mmmmh mkuu mbona wakati ule wanampiga madogo mdada wa watu hukumtetea au ndo ile nyimbo "alipofika yerusalem walimwita mbarikiwa.........."
 
Mmmmh mkuu mbona wakati ule wanampiga madogo mdada wa watu hukumtetea au ndo ile nyimbo "alipofika yerusalem walimwita mbarikiwa.........."

Mkuu sikumbuki kama nimewahi kumponda dada Joyce Ndalichako, nakumbuka kipindi kile cha uchakachuzi wadau wengi tulipinga hatua hiyo nikiwemo na mimi. Kweli dada Joyce namkubali sana kuliko unavyodhani.
 
Mkuu sikumbuki kama nimewahi kumponda dada Joyce Ndalichako, nakumbuka kipindi kile cha uchakachuzi wadau wengi tulipinga hatua hiyo nikiwemo na mimi. Kweli dada Joyce namkubali sana kuliko unavyodhani.

Mkuu ila sikukuona ukimkubali. Anyway kila Nabii na zama zake kipindi kile alisema atarudi mwaka huu mwezi wa kumi chunga mshumaa wako usizime ili akija akukute ukiwa macho mkuu
 
Mkuu ila sikukuona ukimkubali. Anyway kila Nabii na zama zake kipindi kile alisema atarudi mwaka huu mwezi wa kumi chunga mshumaa wako usizime ili akija akukute ukiwa macho mkuu

Nitafurahi sana kama atarudi mapema iwezekanavyo, ona sasa NECTA wanadai ufaulu umepanda wakati TCU wamesimamia palepale kwenye alama za zamani. Nchi hii bwana aagh!
 
Sijaona hata makosa hapo;
Nilitegemea big results kuliko hata hapo alipofikia binti yangu.

Ninaona shule zetu za kidumu na mfagio wamejitahidi sana;

HONGERA SANA WAALIMU WOTE WA "A" LEVEL KWA SHULE ZA SERIKALI.
 
Asante BRN ila huko vyuoni hizo disco sijui tu???? yaani kweli ni watu 600+ ndio waliopata zero???? ina maana zamani watu walikua hawasomi??? kweli kizazi hiki cha kiduku na model wote wafaulu??? masikini Tanzania yangu!!!! yaani kwa mfumo huu wote tuliosoma zamani tungekua vyuoni au maprofesa
 
mwaka huu vyuoni ni mafuliko
wa div 3 hatarin kukosa vyuo
 
Na ndivyo akili zetu zilivyo,vivyo hivyo kwa mawazo yetu,lakini vichwani mwetu wachache tunaelewa nini watawala wanataka,matokeo makubwa sasa.Haijalishi ni matokeo gani ,lakini yawe ni makubwa,haijalishi mfumo upi umetumika lakini yawe makubwa. Ni sawa na kufananisha tajiri mkubwa wa Marekani na tajiri mkubwa wa Swaziland!
 
Malengo yao yametimia lakini ninachoamini siku zote "Ujinga hautaondoshwa kwa upumbavu na ujinga mwingi mbele ni mauti......"WATANZANIA TUJITAFAKARI:israel::israel:
 
Tutawakamata kwenye kazi.
Kama wale 10000 sasa tutachukua 23 kati ya 50000
 
kwan jaman mnacholalamika nn? kwan div 4 nao mnawahesabu kwenda vyuo vikuu? kama sikosei vyuo vikuu mwisho div 3 ya point 15
 
Mimi nakwambia hawa ngoja wajitape hawapati kazi nggoooooo
 
Back
Top Bottom