Matokeo Kidato cha sita: Lengo limetimia!

Matokeo Kidato cha sita: Lengo limetimia!

Grades zilizotumika miaka ya nyuma..

75 -100 A
65-74 B
55-64 C
45-54 D
35-44 E
25- 34 S
0- 24 F..

Grades za sasa hivi.. (BRN)

75 -100 A
60-74 B+
50-59 B
40- 49 C
30- 39 D
20-29 E
0-19 F..

Ukijarib ku compare hzo grades.. Tofauti iliyopo sio kubwa sana kama wengi wanavyodhani.. Ahsanteni..
 
Fowarded as received


Unajua maana ya BIG RESULTS NOW?? Fuatilia matokeo haya ya kidato cha sita.

Division zero mwaka jana 2604, mwaka huu 612. Tofauti watu 1992, sawa na asilimia 325%.

Division one, mwaka jana 325, mwaka huu 4,365. Tofauti 4040, sawa na asilimia 1243%. Haya ni maajabu ya karne.

Walitanua ukubwa wa goli ili iwe rahisi kufunga... Kutoka zero zaidi ya 2000 mwaka jana hadi zero 600 tu mwaka huu. Kutoka div.one 300 tu mwaka jana hadi one zaidi ya 4,000 mwaka huu.

Hivi waalimu walewale wa shule zilezile zilizotoa one 300 mwaka jana ndo wametoa one 4,000 mwaka huu??

Changamoto zao zimetatuliwa? Maabara zimejengwa? Vitabu vimeongezwa? Madai ya walimu yamelipwa? Waalimu wa Kiswahili wameacha kufundisha Hesabu kutokana na ukosefu wa waalimu wa hesabu?

Kama changamoto hizo zote hazijatatuliwa mabadiliko haya ya ghafla kutoka div.one 300 hadi div.one zaidi ya 4,000 yametoka wapi? Kweli tumeamua kutanua goli tufunge kirahisi. Karibu Tanzania, hii ndiyo BRN bhana.!

Wanasema BRN means Big Results Now, mimi namwambia Waziri Kawambwa BRN, yani he should "Better Resign Now" maana watoto wetu wanapata BRN = Brain Receive Nothing.!
Aisee,hili tatizo ni kubwa sana kuliko unavyoweza kulifikiria,hii nchi haina dira ya aina gani ya wataalam na wasomi inaowataka,inafuatilisha mfumo ule ule tulioachiwa na wakoloni kutengeneza watendaji wa ngazi za chini na watumwa,ngoja niwape mfano kidogo,nilisoma kitabu kinaitwa THE AIMS OF EDUCATION,muandishi ni lecturer nimemsahau lakin ni wa harvard,alielezea vizuri tangu elementary schools up to university level,elimu inaenda ikbadilika kulingana na mahitaji ya muda mrefu na mfupi,elimu ya chuo kikuu hapa Tanzania nadhani na nchi nyingi za kiafrica ndiyo ya ovyo kabisa kulingana na maelezo ya muandishi na uhalisia ninao ona hapa nyumbani,mwanafunzi mpaka anafika form six,anakuwa ameshasoma mambo mengi saana,anapoingia chuo nyongeza ya theories sio kubwa sana na wengi mnaweza lishuhudia hilo,vyuo kiuhalisia ni sehemu za kufanyia tafiti na majaribo ya mambo mbali mbali ili kuboresha yale ambayo tunayajua na kwenda deep kwenye yale tusiyoyajua ndio maana hospitali bora kabisa America na ulaya ni zile ambazo ziko chini ya vyuo,taasis nyingi za engineering zinafadhili research kwa ajili ya mambo fulani fulan na huo ndio uhalisia wa chuo,embu tuongee ukweli,hizi field wanachuo wanazoenda,field reports asilimia 80 wana pika,kuna ugumu gani wa kuandika report kama kweli ulifanya field?..tumelemazwa!..tunapenda na tumezoea mteremko..hili ni tatizo,angalia sasa kulingana na mahitaji ya wasomi sophiscated kwenya almost every field,hatujajiandaa,mwishowe tuna import labour,vijana wanalalamika mbona wanapewa kazi watu wa nje?ukweli ni kwamba wenzetu wanapofanya investment kubwa huwa wanaangalia vitu vngi ikiwa ni pamoja na ubora wa waajiriwa wao,just imagine,Dangote anaweka kiwanda pale mtwara,unajiua thamani yake?unadhani kwenye sekta nyeti kama za fedha,uhandisi,usafirishaji na masoko ataweka mbulula kisa ni mzawa?...kazi itatangazwa na wata apply wengi...wenye elimu bora na inayokidhi mahitaji ya sasa ndiye atayeipata hiyo kazi,...hivi mwenye ACCA au CIMA ataachwa abebwe mwenye CPA(T),wengi mtabisha lakin matokeo ya interview utayaona mwenyewe,tatizo ni hatui tunapotaka kufika hivyo njia yoyote itatupeleka popote,embu leo tuangalie ubora wa graduates wetu hata kwenye kujieleza tu...sipondi..kujieleza hata kwa kiswahili ni tatizo,fanya dialogue uone mawazo yao,wengine wanaendelea kungeza idadi kwasababu za kisiasa,maji na mafuta kamwe hayachanganyikani!
 
magumash tupu, any way ndo uongoz uliopitishwa cjui kama tutabadirika next year
 
RIP elimu ya Tanzania best wishes BRN and big congrats for big achievement
 
hahaaa,sicheki kwa mazuri bali nahuzunika na huu mfumo ambao ni dhoofu ini khali,kwa taifa la hawa watarajiwa wa nchi hii miaka michache ijayo...lol!
 
Tunatengeneza taifa mbumbumbu kwa lengo la kuwafurahisha wazazi na wadau.
 
0011.jpg


Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mhe. Dk Shukuru Kawambwa akifafanua jambo wakati akizindua wa utekelezaji wa mikakati ya "Matokeo makubwa Sasa" ambapo kwa kingereza unaitwa "Big Result now" katika sekta ya elimu.

Mwaka 2012 watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha sita walikuwa ni 46,658. Mwaka 2013 watahiniwa 50,611 walifanya mtihani huo na kati yao 44,366 walifaulu. Mwaka 2014 watahiniwa 40,695 walifanya mtihani ambapo watahiniwa 38,905 walifaulu.

Matokeo ya mwaka 2013 yanaonyesha kuwa watahiniwa 325 waliofanya mtihani wa kidato cha sita walipata Division I. Matokeo ya mwaka 2014 yanaonyesha kuwa watahiniwa 4,365 wamepata Division I. Ukilinganisha na mwaka jana hapa kuna ongezeko la watahiniwa 4,040 ambayo ni sawa na 1243% waliopata Division I mwaka huu. Niwape pongezi akina Mamndenyi na wengine wooote ambao watoto wao wamepata Division I.

Waliopata Division II mwaka jana walikuwa 5,372 na mwaka huu ni zaidi ya watahiniwa 9,631, ongezeko la karibu mara mbili au zaidi. Waliopata Division III mwaka jana ni 30,183 na mwana huu ni 16,821. Watahiniwa waliopata Division IV ni 4,362 na mwaka huu ni 4,420. Waliotaka yai mwaka jana ni 2,604 na mwaka huu ni 612 tuu ambapo ni tofauti ya watahiniwa 1992, sawa na 325%!

Kutoka watahiniwa 325 waliopata Division I mwaka 2013 hadi watahiniwa 4,365 siyo mchezo. Waingereza/Wamarekani watakuambia this is extraordinary. Pia kutoka zero zaidi ya 2000 mwaka jana hadi kufikia zero 600 mwaka huu ni maajabu ya karne. Natumaini mwaka huu hakutakuwa na vilio na malalamiko mengi kutoka kwa wazazi juu ya watoto wao kutaga mayai. Hao 600 waliotaga mayai must be very unlucky indeed.

Matokeo haya ni mafanikio makubwa sana ukizingatia kuwa shule ni zile zile na walimu ni wale wale, changamoto kwenye sekta ya elimu ni zile zile, bado kuna uhaba wa mahabara na vitabu, walimu wanalalamika mishahara midogo (nasikia wengine wanataka kugoma), uhaba wa walimu, n.k. Lakini pamoja na hayo yote bado wanafunzi wameweza kupasua ile mbaya. Who knows may be maombi ya akina Kaunga nayo yamesaidia na Mungu akaamua kufanya miujiza hii ya karne.

But whether amkawewe calls this "genetically modified results" or CHUAKACHARA "politically modified results", I say this is BIG RESULTS NOW, MENGINE TUTAJIJU HUKO MBELE.

Ndiyo maana vyombo vingi vya habari vimenywea kuchanganua haya matokeo.

Pia poleni Alumni wooooote wa Tambaza.

No thank you! These are politically modifies results. There is at all no Big Results Now. If the world cup matches are faced with scarcity of goals, what do we do. Should we widen the goal post dimension (width and if possible length) so as to incerease the chances of teams scoring? Ndicho walichofanya hawa wa BRN! Nakupa homework, though ni ngumu kuifanya, if possible, let the NECTA use the old grading system and see if the the current passes will stand.
Nawasilisha.
 
Hivi unaposema "Kawambwa he should" unamaanisha nini? Tujadili nini kama title yenyewe inakushinda...? Najua kuchambua wamekuchambulia wengine...wewe kichwa chenyewe cha habari huwezi.
 
Mamndenyi si jambo la kushangilia hata kidogo,mimi kama mwalimu inanisikitisha sana Elimu inavurugwa, kwa wenye ufahamu ndo wataweza kung'amua nini kinaendelea kwenye hii Elimu.Nenda vyuoni kajionee mwanachuo hajui kuandika essay ili mradi siku zinasonga huko vyuoni ni aibu huku ngazi ya chini ndio kilio, mitihani imevuja kuanzia kuanzia necta mwaka jana siye tunajionea mengi nyie endeleeni kushangilia uozo.

Asante The secretary inaniuma sana hali hii sio ya kushabikia hata kidogo!
 
Last edited by a moderator:
Ipo siku mtakumbuka nayo ni baada ya miaka minne ijayo, kazi hakuna na elimu yenu haiwasaidii
 
Kila mtu anatamani kweli wanafunzi wafaulu na wamefaulu ni jambo jema. Swali la kujiuliza ni kwamba je tokea BRN ianze kufanyiwa kazi kwenye sector ya elimu ni mda gani umepita? Ina maana kwa mda huu usiozidi miaka miwili zile changamoto zinazoikabili sector ya elimu zimetatuliwa? Je shulen maabara zimejengwa? Mazingira ya kufanyia kazi waalim pamoja na madai yao tayari suala hili limetatuliwa na kwa sasa wanafunza kwa bidii? Je shule zimepata vitabu vya kutosha kiasi cha kufanya ufundishaji na kusoma kuwe rahisi kiasi cha kupata matokeo hayo kwa mda wa chini ya mwaka au mwaka? Shule zmepata maktaba za kutosha na za kisasa? Vifaa vya maabara vimepatikana vya kutosha kwenye shule zetu? Na mengine mengi. Kama maswali haya na mengine yamepatiwa majib kwa mda huu mfupi wa mwaka mmoja basi ni sawa kabisa ufaulu kufikia 95.98% ila kama majib ya hizo changamoto hayapatikana na bado hali iko vilevile tujiulize kuwa ni nn maana ya matokeo haya.
 
mim nashauri kama ujui ktu kaa kimya au uliza mbona cjasikia mkiongelea wanafunzi waliochaguliwa kwenda 4m 5?una 1/2
 
nadhani vyuo sasa vita-opt kuchukua watu wa diploma na cheti wakasome bachelor kuliko kuchukua hawa wa kisiasa mwisho wa siku waje kutupasua vichwa badala ya miguu. Hii nchi ina watu wa ajabu sana...ila kizazi cha poor planners kinaelekea mwisho...
 
Huenda mtihani wa Marticulation ukarudi kwenye vyuo vikuu
nadhani vyuo sasa vita-opt kuchukua watu wa diploma na cheti wakasome bachelor kuliko kuchukua hawa wa kisiasa mwisho wa siku waje kutupasua vichwa badala ya miguu. Hii nchi ina watu wa ajabu sana...ila kizazi cha poor planners kinaelekea mwisho...
 
Back
Top Bottom