Matatizo matatu makubwa kwenye Dira ya Taifa 2050

Matatizo matatu makubwa kwenye Dira ya Taifa 2050

Mchele unauzwa amcos gani?
Mchelle pia unauzwa Amcos it's just haufuatiliwi sana sababu una matumizi makubwa nchini na wengi wanalima kama Subsistence farming na Smallholder farmers.

Mfano hai ni Sakama Amcos ya Geita ni Amcoss ya mchele wanafanya packaging wenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mazao makubwa yanauzwa kwenye Amcos so hakuna udalali unless mkulima mwenyewe a opt kuyauza kwa njia za magendo.
Mnasoma makaratasi na kusikiliza hotuba za wanasiasa ambazo hazina uhalisia

Mimi nalima pamba, nalima pia tumbaku. Toa neno Amcos, weka neno vyama vya msingi(primary societies). Hapo utakua unazungumzia jumla.

Mkulima anakopeshwa pembejeo na bank kupitia chama alichopo, bank inaweka mzigo kwenye chama, mwenyekiti anashirikiana na wabadhilifu fulani fulani anapiga ile pesa, haifiki yote kwa mkulima. Mkulima anapa. Anapambana anavyojua, anazalisha, anashindwa kufikia malengo waliyokubaliana na chama pamoja na mnunuzi(malengo nazungumzia kiasi atachotakiwa kuzalisha)

Chama kinakuwa deni kubwa bank tofauti na uzalishaji kupitia wakulima, hivyo wakulima wakouza tu wanakutana na rundo la makato ikiwemo mkopo wa bank kupitia chama, hivyo wanakosa kabisa faida. Kinachofanyika ni kuuza kimagendo bila kupeleka chamani, hii nayo ni mbaya sababu wanauza kwa hasara, lakini wanaona bora kupata cash kuliko kusubiri kuuza kwenye kampuni kupitia chama
 
Mchelle pia unauzwa Amcos it's just haufuatiliwi sana sababu una matumizi makubwa nchini na wengi wanalima kama Subsistence farming na Smallholder farmers.

Mfano hai ni Sakama Amcos ya Geita ni Amcoss ya mchele wanafanya packaging wenyewe.
Mazao ya chakula hubanwi kuuza kwenye amcos/chama. Ni uamuzi wako, wengi hawauzii kupitia amcos/chama

Mazao ya biashara unabanwa lazima kuuza kupitia amcos/chama. Zamani kulikua na independent farmers(sio lazima uwe contracted na kampuni zinazonunua kupitia vyama) Ila huu utaratibu wa independent farmers uliondolewa
 
Mchelle pia unauzwa Amcos it's just haufuatiliwi sana sababu una matumizi makubwa nchini na wengi wanalima kama Subsistence farming na Smallholder farmers.

Mfano hai ni Sakama Amcos ya Geita ni Amcoss ya mchele wanafanya packaging wenyewe.
Sikuwa nafahamu mkuu, shukran
 
Ni kweli wanaibiana ila haya mazao makubwa wengi wanatoboa, ni rahisi mkulima kupata Attention kwenye kitu ambacho Serikali pia wanafaidika.
Mi nipo ukanda wa pwani huku wakulima wanayalaani sana mazao haya ya stakabadhi -- hii nadhani sababu kubwa ni mavuno hafifu
 
Ni kweli wanaibiana ila haya mazao makubwa wengi wanatoboa, ni rahisi mkulima kupata Attention kwenye kitu ambacho Serikali pia wanafaidika.
Hayo mazao makubwa ambayo wakulima wanatoboa ni yapi? Mm nimelima karibu yote, kote pangu pakavu. Umaskini mtupu

Anayepata pesa ni mwenyekiti wa chama/amcos, na mtu wa kati(wanasiasa wanaonunua juu kwa juu)
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mi nipo ukanda wa pwani huku wakulima wanayalaani sana mazao haya ya stakabadhi -- hii nadhani sababu kubwa ni mavuno hafifu
Anakuongopea, Hakuna mazao yoyote makubwa ambayo wakulima wanatoboa. Kote ni umaskini mkubwa. Mimi nimelima na bado nalima mazao yote makubwa kwa zaidi ya miaka 10
Kote pangu pakavu tu. Wakulima ni maskini
 
  • Kicheko

Hoja hiyo nimempa akaleta takwimu ikabidi nitulie tu, mkulima kutoboa inabidi awe na mazao ya kimkakati na mipango haswa
 
Hoja hiyo nimempa akaleta takwimu ikabidi nitulie tu, mkulima kutoboa inabidi awe na mazao ya kimkakati na mipango haswa
Hajui kitu, aje hapa tujadiliane mimi na yeye.

Hata uwe na mpango mkakati, Kama wewe ni mkulima basi jiandae kufa kwa presha. Ukitaka upate pesa ya kilimo, kuwa mtu wa kati au juana na wanasiasa wakubwa wenye nguvu ili usipate usumbufu ukiwa mtu wa kati, option nyingine ni uwe mnunuzi(ununue kutoka kwa wakulima na ukauze huko nje ya nchi)

Kuna watu hawajui hata mche unafananaje, lakini wakati wa mauzo kwenye mnada ndio huwa wanaondoka na pesa nyingi
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
1. Malengo yasiyo na uhalisia
Nimemsikiliza Rostam Aziz anasema tume ya kutengeneza dira walikuwa wanalenga Tanzania iwe na ukubwa wa uchumi(GDP) kati ya $bilion 500-700, wao sekta binafsi wakina Rostam wakapendekeza malengo iwe GDP $Trilion 1 ! Haya ni malengo yasiyo na uhalisia, kwa miaka 25 ijayo uchumi wa Tanzania kukua mara 12 zaidi ya sasa unahitaji miujiza au akili kama za Wazungu na Tiger economies. Uchumi wa $Trilioni 1 unazungumzia uchumi kama wa Saudi Arabia na Netherlands.

2. Kutoweka kipaumbele katika kupunguza masikini
Inaonekana walioitengeneza hii dira ni wale watu walioganda na wanaoamini zaidi katika "trickle down economics" , mkakati wa uchumi unaoamini zaidi kwamba ukuaji mkubwa wa uchumi siku zote utajitafsiri katika maisha mazuri kwa raia wengi. Huu ni mkakati ambao kwa sasa unaonekana kufeli vibaya sana katika nchi kadhaa zenye uchumi mkubwa . Ukuaji mkubwa wa uchumi hauna maana sana kama sio jumuishi na wenye kuleta nafuu ya maisha kwa raia wengi. Nchi nyingi duniani zenye uchumi mkubwa hadi za ulimwengu wa kwanza kwa sasa nyingi raia wanapoteza imani juu ya serikali zao kwa sababu uchumi unamilikiwa na watu wachache sana huku mamilioni wakiishi maisha ya kuteseka.

3. Utengenezaji wa Dira kuongozwa na mwalimu wa saikolojia na elimu.
Dira ya Taifa ilitakiwa iongozwe na mwanauchumi nguli, hili halitakiwi kuwa suala la mjadala au kubishaniwa.
Waziri wa fedha, Waziri wa Mipango, ni kutoka Mkoa mmoja masikini sana usio na dira. Wangesaidia kutoa dira ktk Mkoa wao ikatiki,wengi tungeamini hii dira iliyoletwa. Kuna mjanja mmoja kaniambia hiyo dira ni " cut & paste" ya nchi moja hivi huko Asia.
 
Back
Top Bottom