Matani ya nilipokuwa mdogo

MMMMMMMMmmmm haahahahaaaaa ila uzuri ilikuwa mwiko kutukana ........mamako,sio kama siku hizi neno moja matusi matano tena ya wazeee wako aaaa dunia kwishnei
 
Penye red pamekuwa ni kiungo cha sentesi.
Yaani zis bongo flavor generation ni hatari na aibu tupu.
Ndio maana wamekulia kwenye video game na kuku wao wa broliler.
mmmmmmmmmmmm haahahahaaaaa ila uzuri ilikuwa mwiko kutukana ........mamako,sio kama siku hizi neno moja matusi matano tena ya wazeee wako aaaa dunia kwishnei
 
hahahaha, mmenichekesha kweli, nipo ofisini hapa mbavu sina, kazi haiendi, nasubiri kufunga ofisi lol! kwa kweli Old is Gold.
 
Twende! twende!! Masikio ka Popo!!
Twende!! twende!! Pua ka tonge la ugali!!
Twende!! twende!! Macho ka gololi!!!
Twende!! twende!! Meno ka ya ngiri!!! Fantastic!!!
Twende! twende!! Ndevu ka Misumari!!
Twende!! Twende!!..............!!
Twende!! Twende!!..............!!
Twende!! Twende!!..............!!
Twende!! Twende!!..............!!
Twende!! Twende!! Tumbo ka Muwakilishi wa wananchi mjengoni!!!

Mkuu Sisi haya tulikuwa tunayapiga kwa kilugha - sasa nikiyarudia kimoyomoyo kweli yananifurahisha sana -- of couse hizo zilikuwa happy days bwana na haziwezi kurudi tena.

kuye vava kuye - nyindo kate itonge lya ugale
kuye vava kuye - minso gako kate ntulantu....
Kuye vava kuye - mino gako kate gi gere....
Kuye vava kuye - migulu zyako kati myanzi
Kuye vava kuye - kilezu kati walumaga ka titi...
etc.....

Tatizo unayemtania akiwa baunsa - utasitukia kichapo cha mbwa mwizi...
ha haha --- those days...
 
mi nilikuwa sijui malani basi siku moja nikajifanya kupambana na mtaalam wa malani mwishi nikabaki kusema "twend twende chungwa kama embe....." watu walicheka hadi wakakaa chini.

hahahahahahahahh!umenifurahisha sana...sasa hapo ukute kuna bingwa wa kucheka pembeni au wewe unatoa yako watu hawacheki lazima ikuume.

twende twende.....sura mbaya ukiangalia mboga inachacha!!
twende twende......domo kubwa chapati haukunji!!!
twende twende.....meno ya njano kama shabiki wa yanga!!
twende twende.....sura kama unasubiri chenji!!!!
 
Haha haaaaaaaaa...

Nimemaliza siku yangu ofisin vizuri kwa kucheka kwa nguvu dah, mkuu mikela nimegonga senks hapo juu kama kawa... dah ya kale dhahabu isee...
 
Kudos mtoa maada na wachangiaji mliotukumbusha enzi zile haki ya nani nikimwangalia junior hivi sasa namhurumia kuwa uttoto wake unajengwa na vitu ambavyo si asilia na sijui tunajenga kizazi gani?cha watoto waliolelewa na video games!
 
.....Watu mna vituko humu si mchezo, nafuu siku inaishia kwa kucheka hadi basi.
 
kwa kweli nimekumbuka mbali sana, kwa bahati mbaya hatuwezi kurudi huko. mi ningerudi
 
Ha ha haaa those days ukinunua ashikirimu marafiki wanakuzunguka nawe bila hiana unawamegea nao bila kujali mate wanakula kwa furaha...tatizo mwalimu akikupa kumuuzia kashata halafu watu hawanunui........
aaaaah kwa HIV iliyopo sasa na fangasi za midomo sijui madogo wanafanyaje huko!!!

mix with yours
 
Kuna dogo alikuwa akifika anasema "nitanie". Kama hufahamu basi Yesaya wetu anakuambia "niambie mimi mweusi kama chungu cha makande".... Na jamaa kweli alikuwa mweusiiiiiiiiiii....... Ukifanya kosa ukasema .....

Twende Twende, ukiona Chura anaruka unasema baba anafanya mazoezi.
Twende Twende, macho pima kama mama Muuza (pombe).
Twende Twende, ............

Nyingine nakumbuka kwa mbali ni za Kinyamwezi kwa ajili ya Elnino na wanaoinyaka External. Ntakuja zimalizia baadaye.....

"..... Llilinge, nyindo kiti Ntensu i wa-Mayeyu.........." Elnino, asante kwa Pua kama tunguja....hahahahaaaaa. Hivi Elnino, kwa nini ule wimbo ni maarufu na una tusi moja baaya sana " Nguluve ikulyanga twingi vayaya, kamna mna nguluve. Nani wamleta ****** Nina kumle masumle...." Hebu niandikie kwenye PM wimbo wote maana nshausahau na kuuliza vijana Noma.
 
Mkuu Sisi haya tulikuwa tunayapiga kwa kilugha - sasa nikiyarudia kimoyomoyo kweli yananifurahisha sana -- of couse hizo zilikuwa happy days bwana na haziwezi kurudi tena.

kuye vava kuye - nyindo kate itonge lya ugale
kuye vava kuye - minso gako kate ntulantu....
Kuye vava kuye - mino gako kate gi gere....
Kuye vava kuye - migulu zyako kati myanzi
Kuye vava kuye - kilezu kati walumaga ka titi...
etc.....

Tatizo unayemtania akiwa baunsa - utasitukia kichapo cha mbwa mwizi...
ha haha --- those days...


HII KALI!
Tafsiri tafadhali lol
 
kuye vava kuye - nyindo kate itonge lya ugale
Twende baba twende, pua kama tonge la ugali.

kuye vava kuye - minso gako kate ntulantu....
Twende baba twende, macho yako kama tunguja.

Kuye vava kuye - mino gako kate gi gere....
Twende baba twende, meno yako kama hayana ......... (hapa naona sikumuelewa)

Kuye vava kuye - migulu zyako kati myanzi
Twende baba twende, miguu yako kama Mianzi.

Kuye vava kuye - kilezu kati walumaga ka titi...
Twende baba twende, kidevu kama umeuma ka kurumbiza (Thrush Nightingale) ndege.

Titi aka Thrush Nightingale aka kurumbiza
PO07-TN-05-07.JPG


Kwa Wanyamwezi: Huyu ndege huwa mwimbaji sana mwakumbuka wimbo wake? Hebu ondoeni watoto karibu.
"Titi, wampota mpota, kwikala mkalambo lufindo fyetete, mtweeee pono.
Mtaka kwa Mponda kusema lakini limvwa ihhhhhh kusata".
Mdogo wake aliupenda sana huu wimbo na mwisho tukamwita Tiiti.

Kwenye picha naona kititi kimetulia juu ya mti wa Mponda..... heheheeeeeeee.....
HII KALI!
Tafsiri tafadhali lol
 
............miguu kama LMG!!
............sura kama mwenye tumbo la kuhara
 
Twende! twende!! Ndevu ka Misumari!!
Twende!! Twende!!..............!!
Twende!! Twende!!..............!!
Twende!! Twende!!..............!!
Twende!! Twende!!..............!!
Twende!! Twende!! Tumbo ka Muwakilishi wa wananchi mjengoni!!!

Inaonekana nyie mlikua mnataniana mkiwa watu wazima ....Koz mtaniwa alikua na ndevu...si mtoto huyo tena..au vp mazee???
 
Twende twende "Tumbo ka Mimba ya Panya"
Twende twende "Macho ka Gololi"
Twende twende "Sura Mbaya ka Mandemla"
Twende twende "Miguu ka Nche ya Bamia"
Twende twende "Miguu ka Ngadu"
Twende twende "Uso ka Mboga ya Juzi"
Twende twende "Masikio ka Sungura"
Twende twende "Mweusi ka Mpingo"
Twende twende "Chogo ka Madenge"
Twende twende "Macho ka ya Panzi"
Twende twende "Mfupi ka Pimbi"
 
Nimekumbuka zamani sana.
Ukizidiwa malani unasubiri muda wa kurudi nyumbani ili uanzishe vagi.
Ukiwa na bahati mbaya unazidiwa malani na kichapo unakula kama kawa.
najua badhi yenu ntakuwa nimewakumbusha kitu.
Twende twende kichwa kama boga.
Twende twende ukomaa hadi ukitema mate yanadunda
twende twende mikono kama mchimba makaburi

haha haha haha zama hizo mambo yalikuwa shwari kwelikweli
 
Back
Top Bottom