Matani ya nilipokuwa mdogo

Kwenye rede (ready) sasa utasikia ....foo foo foo..............kumbe ndo foul. Foo kwisha.
 
Mmenikumbusha mbali kweli.
Kwa sisi wengine hatima yake ilikuwa ni kuchora mstari chini,"kama wewe ni mwanamume kweli vuka"
.......hii zaidi ilikuwa kwa wale ambao hawawezi utani lakini ni mabaunsa!
 
Nimecheka kweli, mmenikumbusha baada ya matani mnaanza kucheza mchezo wa 'kombolela' na kucheza 'kimama mama" baadaye 'rede ya chupa'
 
Twende, Twende; miguu ka mishikaki ya bibi zena'
Twende, twende; macho ka gololi
Twende, twende; pua ndefu ka fimbo ya mchunga ng'ombe
 
Katuni za enzi hizo zilikuwa ni za Chakubanga.
Ilikuwa raha sana.
Magazeti yalikuwa Mfanyakazi, Mzalendo na Uhuru.
Mwaka 1988 likatoka gazeti la Motomoto ndio lilikuwa linaandika habari za kina Fundikira na Mapalala
 
Bai shoo i love you baby, the baby to the son, the son to the owner the owner to the man,
the man to the put there, there one two three four.


Mkuu ladba we ulisoma st marys. Si tulikua tunayabangaiza hayo kwa kiswahili.
 
Twende twende.. miguu ka Kifimbo cheza...
twende twende.. tumbo kama lodi lofa....
Twende twende.. masikio kama sungura!!..!!
 
unaikumbuka wantu taima shuu freefoo shatedo faiv siks kauntesti sevenei kip ze stret nine ten ebi fat hen

hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa uwiiiiiii am dying here!!!
aiseee wewe umeua hapo duh!!!

kumbe ndo.........'one, two tie my shoes. three four shut the door........lol!!!

thanks Mikela you have made my friday!!!
 
Karudi Baba Mmoja
Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
wakataka na kauli, iwafae maishani.

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
roho naona yachinjwa, kifo kina nikabili,
kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
kama tunataka mali, tutapataje shambani?

Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
kama mnataka mali mtayapata shambani.

Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
kama mnataka mali, tutayapata shambani.

Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
wote wakashangilia, usemi wakakubali,
"KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".
 
hahahaha! lol! umenikumbusha mbali kweli!
nakumbuka wimbo wa baisho i love you baby, mwisho kumbe ni thre one, two, sisi tulikuwa tunasema "tarawan, tu, srii kata kona tara one, tu, sirii......."
unaikumbuka wantu taima shuu freefoo shatedo faiv siks kauntesti sevenei kip ze stret nine ten ebi fat hen
 
Halafu mnakata kona ya kwenda wapi?
hahahaha! lol! umenikumbusha mbali kweli!
nakumbuka wimbo wa baisho i love you baby, mwisho kumbe ni thre one, two, sisi tulikuwa tunasema "tarawan, tu, srii kata kona tara one, tu, sirii......."
 
Twende twende......... masikio kama ungo..........
twende twende ........ mweupe kama mzungu koko........
twende twende mweusi kama mkaa...........
 
Halafu ule mchezo wa KUfumba macho kisha unaruka masanduku yaliyochorwa Chini huku ukisema MA RAITI mwenzako anaitika yes MA RAITI mwenzako anitika yes au no! Maskini kumbe ilikuwa inamaanisha I'm Right? yaani nimepatia au nipo sawa?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom