Matani ya nilipokuwa mdogo

Matani ya nilipokuwa mdogo

Twende twende, nywele kama mkutano wa inzi!
...Twende twende nywele ka machicha ya nazi
Twende twende tumbo ka kibuyu cha madhiwa
Twende twende miguu miembamba ka gia liva ya lelandi
Twende twende macho makubwa ka mjusi kabanwa na mlango
 
KWELI WEWE WA ZAMA ZA KALE ZA MAWE.
HAYA MAGARI WALIKUWA NAYO RAILWAYS ENZI HIZO.
attachment.php


...Twende twende nywele ka machicha ya nazi
Twende twende tumbo ka kibuyu cha madhiwa
Twende twende miguu miembamba ka gia liva ya lelandi
Twende twende macho makubwa ka mjusi kabanwa na mlango
 
twende twende... macho makubwa ka umekabwa tonge la ugali!!
 
Twende... Twende... Shingo feni, macho balbu..
Twende... Twende... Tumbo bibo Kichwa korosho..
Twende...T
 
twende twende.........macho kama maembe ya mama john (kuna mama alikuwa anauza maembe machachu kishenziii) hahaha!
 
Mfupi mpaka mpaka ukikaa chini miguu haifiki kwenye sakafu
 
Hii moja haikuwa very nice na ni ya Long mno....

'twende, twende.. Takataka za #$#%&ni kwenu kisamvu..!
 
Twende twende........
Mashavu kama unapuliza moto

Twende twende........
Sura imekunjamana kama ngozi ya goti

Twende twende .......
Kope za macho zimekomaaa hadi ukifumba zinatoa cheche...

Nakumbuka enzi hizo kuna jamaa alikuwa anaitwa Madeje au Mzee wa Zagafula shule ya Msingi alikuwa balaa kwa matani
 
Halafu ule mchezo wa KUfumba macho kisha unaruka masanduku yaliyochorwa Chini huku ukisema MA RAITI mwenzako anaitika yes MA RAITI mwenzako anitika yes au no! Maskini kumbe ilikuwa inamaanisha I'm Right? yaani nimepatia au nipo sawa?
No inamaanisha Am I right?
 
Wenyewe tulikuwa na staili tunapangiana zamu ya kuwa baba mwenye nyumba,.......Sasa hapo mtu unajifanya kama ratiba umeisahau vile mziki wake asikwambie mtu kila mtu anataka kuwa baba LOL.

Nyingine ilikuwa mnazuga mko kwenye kombolela halafu haooooooo mnapotelea mafichoni huko mnabanjuana tu, yaani mara nyingine watu wanamaliza hadi wanasahau ..... nyie saa hiyo hamna hata habari .......full malavidavi.

Nyingine Namtafuta mke wangu namtafuta mke wangu..........haapa hayupo hapa hayupo.....Huu mti gani wa mchongoma, nikiukata? haukatiki......sijui mbele nini nishasahau long time sana.
 
Twende twende...tumbo kama mkoba wa kinyozi
Twende twende...nywele kama mkutano wa inzi
Twende twende...utangoutango kama gari la jeshi (utangoutango = ugonjwa wa ngozi)
Twende twende..chogo utafikiria ncha ya kisu
Twende twende...masikio kama popo
Twende twende...sura imekomaa kama tacko la bibi kizee
 
Twende twende bichwa ka unaitwa tukale.hapo unakuta msosi tayari sa ukiitwa direct wadowezi watawafata.na dogo anaitikia tumbo ka tangulia naja.duh?kweli watoto wazamani tulikuwa mabriliant.
 
hii ni ya kisasa;
Twende twende twende...eti we ni mjinga badala ya kuweka antivirus kwa comp unaweka miti shamba
 
Hahaha pua ka mkoba wa shetani
Sura ka kona ya kiazi 😬
 
Bai shoo i love you baby, the baby to the son, the son to the owner the owner to the man,
the man to the put there, there one two three four.
Hahaha nilivyokuwa naimba aisee🤣🤣

Baishoo ailavyu bebi, the bebik to ze saa, the saa to the yonaa, the yona to the mee, the me to the puu.. yani ujinga tuu😫
 
Back
Top Bottom