Matamko ya (baadhi) waislam (Dar na Mwanza)

Matamko ya (baadhi) waislam (Dar na Mwanza)

Status
Not open for further replies.
:smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big: you really made my night!! yaani nimecheka , na mbavu sina hapa.
 
kama unataka kujua kama watu hawa walioandika hiyo article wamekosa shule, angalia tu mwenyewe hicho wanachokisema hapo...ni utumbo huwezi amini hawa ndo wanaswalisha watu. sasa wanataka nini? unajua, mimi nafikiri ifikie kipindi selikali ijitoe kabisa, iondoe misamaha ya kodi, irudishe hospitali zote za kidini na shule zote za kidini, halafu ituache sisi wakristo tujiendeshe wenyewe, kwasababu kinachoonekana hapa ni WIVU na si sababu yoyote, wivu tu. jamani, sisi tunajenga mashule na hospitali kwa sadaka zetu, tunajenga pia kwa misaada toka ulaya....ninyi mbona hamuwezi?
Wakipewa misaada, eti wanapewa tende. Alafu wanaona wamepata kitu cha maana sana?!! Shhuuuuuuuuuuuuuuuuuiiiiiiiiii
 
Ningewaona watu wa maana Kama

1: Mngetangaza Kuwaachisha Shule Watoto wenu Wanaosoma katika Shule zinazomilikiwa na Mashirika Ya Kikristo

2: Mngeacha Kwenda Katika Hospitali zinazomilikiwa na Masharika ya kikristo

Vinginevyo mtaendelea Kulalamika Wakati sisi tuko Bize Kujenga Shule, Vyuo na Mahospitali
 
Jamani , kulalamikaaaaa kutwa, ingekua Rais Mkristo wangesema wanaonewa, adui wetu waislamu ni waislamu wenyewe, Tunajilaum kwa mambo yaliyo ndani yetu. TUNAOGOPA VISIVYO OGOPESHA.

UKITAKA KUJUA SISI NA MASHEHE WETU TUNAJIDHALILISHA ANGALIA MATAMKO YETU, Yamepwaya, hayana uzito wala mantiki, Maaskofu wakikemea Jambo, Mashehe wanakuja kujibu, ahaaaah kinyaa kabisa, Maaskofu wanawapuuza mashehe, kwakua wanaonekana ni watu wasio na ufahamu, uelewa na wala elimu katika maisha ya kawaida.

Soma hiyo thread juu, ni ujinga unaoweza kuukuta ndani ya Gazeti la Annuur na redio Imani sijui ya kule Morogoro.

tunajidhalilisha sana.


My friend you are not a MUSLIM. it did not work. Big lie!
 
Basi Nadhani kwenye katiba mpya tuombe nafasi maalumu za upendeleo bungeni kwa waislamu na nafasi maalum za upendeleo kwa waislamu za Ukuu wa wilaya, ukuu wa mkoa etc.

Kwa maana kama Muislamu mwenzetu JK anateua wakuu wa wilaya ambao ni nyumba ndogo tu! na kuacha waislamu wenzake then tunawatupia lawama maaskofu na wakristo then tunasafari ndefu ya kujikomboa kifikra!
 
Basi Nadhani kwenye katiba mpya tuombe nafasi maalumu za upendeleo bungeni kwa waislamu na nafasi maalum za upendeleo kwa waislamu za Ukuu wa wilaya, ukuu wa mkoa etc. Kwa maana kama Muislamu mwenzetu JK anateua wakuu wa wilaya ambao ni nyumba ndogo tu! na kuacha waislamu wenzake then tunawatupia lawama maaskofu na wakristo then tunasafari ndefu ya kujikomboa kifikra!

JK+AONGOZA+KIKAO.JPG


Nafasi kuu za uongozi wa nchi wamekamata wao, angalia hawa viongozi wa kamati kuu ya ccm
 
Kisha niende dini gani? upagani? acha kudharau imani ya mtu kaka hapa tunafahamishana kwa lugha nyepesi kuwa wapo waislam wa kweli ila waliowekwa mfano "bakwatwa" wapo kimaslahi zaidi sijaamanisha kuwa uislam unaniboa hutaniboa na nitakufa nikiwa Muislamu Insha'Allah.

Ndugu yangu kama BAKWATA iliyoanzishwa na serikari ya mzee wetu Ali Hassan Mwinya (Mzee Ruksa) haina uhalali mbele ya waislamu kwa sababu tu ni chombo kilicho anzishwa kwa usimamizi wa serikali, Je mnapata wapi ujasiri na imani kuwa mahakama ya kadhi itakayoanzishwa na serikari haitakuwa kama BAKWATA? mbona jamani mnakuwa too contraversial and double standard kiasi hicho?

Waislamu wanaita BAKWATA ni wasaliti kwa sababu wako pro government na wanalipwa pesa na serikali za kuanzisha BAKWATA, hiyo imani yenu kwa serikari kuanzisha na kumlipa kadhi mkuu inatoka wapi, Je maaskofu hawawezi kuchangia fedha za kuanzisha kadhi na kuwalipa kama ilivyokuwa kwa BAKWATA. I am just trying to think jamani!
 
I will feel so low to discuss this.......
 
Topical,

Hiv wewe, hujishangai kila mtu anakupinga hapa Jamvini, hata waislam wenzako tunakupinga kwa hoja zako dhaifu,zilizojaa Fitna,uhasidi,uchochezi,zina expose jinsi brain yako ilivyo shallow sawa na hao mashekh waliotoa huo waraka, hebu hiv mtu kama Prof Abdalah Safari anaweza ku support upuuzi unaoulte hapa ambao ni tamko la VILAZA wachache wanaojiita viongozi wa dini yetu tukufu.

Sikiliza Kaka, uislam sio ujinga kama unayvo ji express wewe, sisi wengine ni waislam,tumesoma, tuna Degree zetu (Mimi ni Engineer),tunafanya kazi zetu,tunapata kipato na tunaendesha Familia zetu,suala la ugumu wa Maisha ya Mtanzania sio la Tatizo letu pekee, ni Tatizo la hata pia wenzetu wa kristo, hebu jiulize,R OSTAM ni muislam safi (anajiita hivyo), lakini unaona matatizo karibu yote tuliyo nayo chanzo ni yeye,hatuwezi kumtetea eti kwa sababu ni muislam mwenzetu.

Kusema kuwa hatuwezi kujadili katiba mpya hadi tupewe haki zetu ni upuuzi kubwa sana,hiyo ni Janja ya CCM kukutumia (Upumbafu wa viongozi wetu) kuuwa moto uliowashwa na Wa Tanzania juu ya kupata katiba mpya..
 
waliowaletea hizi dini wenyewe wako kimya wanawaza maendeleo,nyinyi mnawaza kubaguana, kama sio akili mbovu ni nini?
miafirika bwana tuko hovyo!

Sasa serikali ni ya JK muslimu mwenzenu, madai yenu serikali inawaonea, sasa uhusiano wa kuwa-attack maaaskofu inakujaje hapa? Mbona sielewi hata nini hasa watu hawa wanataka? Jamani tupeni atleast kwa kifupi...what exaclty these people wants......hakuna wasomi ndani ya jamii ya Kiislamu kuweza kuwasaidia kuelewa mambo?
 
Aliyecompose hii habari ni mchakachuaji wa dini

Ndugu zangu waislamu, hakuna dhuluma au mikakati ya kuwakandamiza waislamu ila tu Waislamu wenyewe wafunguke akili na kutambua kwamba elimu ndio njia mahsusi ya kujikomboa. Hutakabidhiwa kuendesha ndege kama we hujahitimu urubani. Huwezi kabidhiwa utunzaji wa daftari za hesabu kama hujasomea maarifa ya utunzaji pesa la sivyo utavuruga uchumi. Huwezi fanyia ukarabati gari kama we hujui mfumo wa gari upoje. Huwezi shiriki mbio za maratoni kama hujafanya mazoezi ya kutosha vinginevyo moyo utasimama kabla hujahitimisha mbio hizo.

Serikali tangu utawala wa Nyerere imefanya jitihada kubwa mno kuinua elimu na kufungua milango kwa waislamu wasome. Sababu mojawapo ya Nyerere kuanya elimu ya msingi hadi vyuo vikuu iwe bure ilikuwa kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wote ambao uwezo wa kulipia ada hawana. Na wengi wa viongozi wetu wa sasa wamepitia katika mfumo huo wa elimu bure kwa kila mtanzania. Madrasa ni elimu ya dini ya kiislamu lakini si elimu endelevu ya maisha ya ajira ya kiuchumi na maendeleo. Sawa na wakristo kama wanaamua kusoma biblia tu kama ndo elimu imekamilika, la hasha.

Mkombozi wa umaskini, haki na maradhi ni elimu.
 
Dears,

Ifahamike wazi kabisa, serikali ya CCM haiko tayari kufanya mabadiliko ambayo wa Tanzania tunayahitaji kwa Sasa, kati ya Mabadiliko hayo ni Suala la Kuundwa kwa Katiba mpya, Kuanzishwa kwa Tume huru ya Uchaguzi, kutokuilipa Kampuni ya Kitapeli ya Dowans jumla ya THS 94 Bilions na mambo mengi ambayao mnawezakunikumbusha.

Inatupasa tuwe makini sana na mwenendo wa mambo yanayotokea hivi sasa ambayo ukifikirisha sana ubongo wako unaweza kuya relate na njama chafu za serkali ya CCM kutaka kuyazima,kuyadhoofisha na kuyapotezea kabisa madai ya Watanzania tulio wengi ambayo nimejaribu kuyaorodhesha hapo juu.

Tamko la waislam:

Katika hali ya kushangaza, kusikitisha,kufedhehesha na kukatisha tamaa ni tamko la viongozi wa dini ya Kiislam ambayo ukuyachunguza na ukafikirisha ubongo kidogo utagundua kuwa yana Mkono wa CCM.

Sina haja ya kujadili tamko lao la kuwajibu Maaskofu kwa sababu tumeshalijadili sana.
Tamko walilotoa juzi nita summarize baadhi ya mambo waliyoyasema:

(2) Kwa kuwa kila wanchosema Maaskofu ndicho kinachofuatwa na serikali, na kwa kuwa Maaskofu wamekwishatamka hadharani na kwa sauti kali kuwa katika nchi yetu hakuna kabisa udini na atakayesema kuna udini basi ni yeye ndiye anayetaka kuleta udini, na kauli hiyo kudakwa na mawakala wa Maaskofu katika serikali, ni dhahiri kuwa dhulma za udini zinazoendelea kuwakandamiza Waislamu miaka 50 baada ya Uhuru hazitaondoshwa na Katiba mpya. Hivyo wajibu wetu mwingine ni kupigania ukombozi wa Waislamu ili washiriki katika kuandaa katiba mpya wakiwa ni raia huru na sawa na wenzao. Waislamu popote tulipo tunao wajibu wa kuorodhesha dhulma zote za udini tunazofanyiwa na kupigania ziondolewe kwanza na kulipwa fidia."

Hiki ni kiashirio tosha kuwa Serikali ya CCM haitaki katiba mpya,inachofanya ni kuwachochea ndugu zetu waislam waone kuwa kudai haki zao (Sijui ni zipi kwa kweli) ni bora zaid kabla ya kudai katiba mpya, eti waislam hawako huru ilhal Rais,Makamu wa Rais,Katibu Mkuu wa chama n.k ni Waislam,naomba tuchukue fursa hii kwa wale wenye mapenzi mema na nchi yetu,kuwaelimisha Ndugu zetu wasiingizwe kwenye Mkumbo ambao unafanywa na Viongozi wao bila kujijua kwa hila za CCM.

"(1) Maadam Mfumo Kristo umeimarika kiasi cha kuweza kuitisha serikali na viongozi wake na wakatishika, na maadam Mfumo huo Kristo una nguvu za kuweza hata kuvitisha na kuvikemea vyombo vya dola na vikasalimu amri, Waislamu tutake tusitake, kama alivyohadharisha Mh. Membe, ukweli unabaki kuwa hautapita muda mrefu, dhulma hii ya udini italisambaratisha Taifa letu, kama udini ulivyoisambaratisha Ivory Coast ambayo katika miaka ya 1960 na 1970 ilikuwa mfano wa kuigwa.

Hivyo basi wajibu wetu wa mwanzo ni kuufikisha ujumbe huu kwa Waislamu wote nchini, na kuwataka wazingatie kuwa kwa kuwa wanabaguliwa na kudhalilishwa katika nchi hii kwa sababu ya Uislamu wao, basi ni wajibu wao na wao kushikamana kama Waislamu."

Hii ni trick ya CCM kujaribu kupoteza malengo yetu wapenda mabailiko kwa kupoteza hoja amabazo kimsingi zinichachafya CCM na serlikali yake, wanataka kutupoteza tusijadili DOWANS, tusijadili Mauaji waliyoyafanya Arusha, Tusijadili Katiba Mpya, tusihoji nia na uwezo wa Muungwana katika vita Dhidi ya Rushwa na ufisadi kama alivyodokeza Edward Hoseah.

Sisi Wapenda mabadiliko hatutyumbishwa na haya na Mapambano yataendelea kama kawaida, Waislam ni watu wastaraabu, ni marafiki zetu, tumesoma nao,ni Wa Tanzania wenzetu, ni majirani zetu, wengine tumeoa huko.

Regardless, the strugle shall continue "Matola's Signature"
 
Ukisoma article kuna sehem wanadai kuwa 75% ya wakuu wa wilaya ni wakristo, Hivi anaeteua wakuu wa wilaya ni nani? Si Raisi wa nchi ambae ni Muislam? Hivi sasa mnalaum nini? Angekuwa Rais Mkristo mngelalamika kwa hoja kuwa ni anaeteua ni mkristo.

Kwa sasa Ukiangalia Top leaders wengi waislam. Mfano, Rais, Makamu wake, Jaji mkuu, IGP, Mkuu wa tume ya haki za binadam, Mbaneni JK alete mabadiliko kwenu kwa sababu ndio ameshika lungu, lakini mnapolaum wakristo tu sio vizuri.
 
Wanachofanya CCM ni kama kawaida yao kutumia udhaifu wa Masheikh, ambao ni njaa ili kuwatumia kama ule mpira wa kujikinga na ukimwi halafu 2015 kama wakiweka mgombea mkristo kibao kinageuka.

We umesoma elimu ahera halafu unataka kujifanya mahiri ktk mambo ya kidunia? Lazima CCM watakuzidi akili tu na kukutumia kwa manufaa yao
 
Niambie ni halali kuchota pesa na kupeleka kwenye miradi ya kanisa? pesa za umma through MoU? kama huo ni wivu mkuu basi sijakusoma!

Hiyo Mou ilikuwa inahusu kanisa kubeba jukumu lililoishinda serkali. Kwa vile kanisa linaamini kuwa ibada ya kweli ni kuwasaidia wahitaji (wajane na yatima). Hivyo kanisa likatumia resources zake za kifedha na talents kuanzisha huduma mbali mbali za kusaidia jamii. Serkali kwa kuona wanasaaidiwa kubeba mzigo wake na kanisa waka pledge kutoa mchango fulani katika baadhi ya huduma hizo za jamii zizazoendeshwa na kanisa.

Mfano mahospitali, vituo vya watoto walemavu, yatima n.k Na hii ilifanywa kusudi serkali isije kujisahau kuwa hili ni jukumu la kanisa wakati ki ukweli ni jukumu la serkali maana ndiyo inayotoza wananchi kodi. Na hata hivyo kwa sehemu kubwa serkali haitimizi ahadi zake. Mfano serkali inapaswa kutoa kiasi fulani cha fedha kila mwezi kwa kila mtoto yatima anayelelewa makao ya watoto yatima lakini muda mrefu hawatoi.

Hivyo kama serkali ingetumia kodi kutoa huduma za jamii na si kuzila kwa ufisadi kanisa lingebaki kuendesha shughuli zake za ki ibada. Kamwe kodi za serkali haziwahi kutumika kuendesha makanisa kama kulipia mishahara ya maaskofu na wachungaji. Pia hawatoi ruzuku kuendesha ibada. Misamaha ya kodi inayosemwa iko katika huduma hizo za jamii. Pia kuna misamaha katika vifaa vinavyoingia nchini kwa ajili ya ibada kwa dini zote hata na waislamu. Kama ukiagiza konteina la koran leo hutalipa ushuru bandarini leo. Ni vile vile kwa biblia na vifaa vingine vya ibada.
 
Wanachofanya CCM ni kama kawaida yao kutumia udhaifu wa Masheikh, ambao ni njaa ili kuwatumia kama ule mpira wa kujikinga na ukimwi halafu 2015 kama wakiweka mgombea mkristo kibao kinageuka.

We umesoma elimu ahera halafu unataka kujifanya mahiri ktk mambo ya kidunia? Lazima CCM watakuzidi akili tu na kukutumia kwa manufaa yao

CCM wanatumia Ignorance na njaa za ndugu zetu (Though wapo wa kristo ignorance na njaa kwa sana tu pia), sijui kwa nini CCM wame opt kuwatumia Waislam nao kuingia Mkenge kiasi cha kutoa matamko shallow na hatari kama wanavyofanya na ninaamini wataendelea kufanya (kwa kutumiwa na CCM)
 
JK+AONGOZA+KIKAO.JPG


Nafasi kuu za uongozi wa nchi wamekamata wao, angalia hawa viongozi wa kamati kuu ya ccm

Siku zote nilikuwa naliangalia suala la udini kwa kulipuuza. Sijawahi kuamini kwamba ni kitu cha kuangalia kwa makini. Mimi ni mkristo, sijawahi kufundishwa kumchukia muislamu, kuchukia uislamu wala kuupenda ukristo zaidi ya dini nyingine yoyote. Nimeshtuka sana niliposoma hilo tamko. Siamini kwamba tamko kama hilo linaweza kutolewa halafu hakuna kiongozi yeyote wa serikali aliyelizungumzia.

Nataabika na mawazo. Nashindwa kuelewa kwamba tamko hilo halina maana yoyote hivyo limepuuziwa au yaliyosemwa yamekubaliwa.

Vyovyote itakavyokuwa huu udini na dhana ya waislamu kuonewa itatuharibia nchi. Itatuharibia sana. Nimetafakari maneno kama wakristo wamestarehe kwa miaka 50 nikalazimika kumfikiria mama yangu mzazi kule kijijini. Nikafikiria ni starehe gani amepata. Nikajifikiria mwenyewe nikajilinganisha na watoto wa kina Idrissa Rashid, Rashid Kawawa, Jakaya Kikwete, Julius Nyerere, Edward Lowassa, Alihassan Mwinyi, Abeid Karume na wengineo wengi......nikaangalia nafasi ya ukristo wangu sikuiona! Natambua suala hili kuna watu wanaliangalia kwa ujumla na si kwa mmoja mmoja. Lakini bado nabaki kushangaa.

Huo upendeleo uko kwenye nini? Na wakati unafanyika viongozi waislamu wako wapi? Sasa hivi wako wapi kutetea waislamu wenzao? Zimewekwa picha za kamati kuu, hakuna aliyebisha! Mkuu wa usalama wa Taifa ni muislamu, haoni haya manyanyaso? Raisi je? Makamu wa Raisi haoni? Aliyepita haoni? Hawana upeo walio nao hao waliotoa tamko?

Nasita kulichambua tamko. Lakini kwa yeyote aliyeandika hakuwa na nia njema. Tamko hilo haliwakilishi mawazo ya waislamu hata robo! Ni tamko lililoandaliwa na watu wenye maslahi yao binafsi au watu wasio na uelewa mkubwa.

Hizo haki wanazozungumzia wameshindwa kupata wakati huu ambao Raisi, Makamu wa Raisi, Jaji Mkuu, Raisi wa Zanzibar, Makamu wa Raisi wote wawili wa Zanzibar, Waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Katibu Mkuu wa CCM Taifa ni waislamu zitapatikana vipi ikiwa tofauti? Kama sio kuandaa mazingira ya baadae kuleta vurugu kwa kisingizio cha kuonewa?

Wote walioandaa tamko hilo si watu wenye kututakia mema. Mawazo na mapendekezo waliyotoa ni kuudhalilisha uislamu na viongozi wake. Naamini kabisa kwamba uislamu ni dini bora na ina mafundisho mazuri lakini wachache kwa maslahi yao binafsi au kwa uelewa wao finyu wanaamua kupotosha. Hawatafanikiwa kamwe. JK tafadhali, tuondolee hii balaa inayotunyemelea. Tafadhali sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom