Matajiri wakubwa Tanzania si wafanya biashara bali ni wanasiasa, viongozi wa serikali na ndugu zao, kuonyesha kwamba kuna kitu hakipo sawa

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Ni kawaida kwamba katika nchi nyingi matajiri wakubwa utakuta ni wafanya biashara, lakini sio Tanzania. Kwa sasa wanaoongoza kwa kuwa matajiri wakubwa Tanzania ni wanasiasa waliopo madarakani au waliokuwa madarakani huko nyuma. Halafu wanafuatiwa na viongozi wa serikali, pamoja na ndugu zao.

Imefikia kwamba hata ukiwa mfanya biashara, ili utajirike kwa haraka lazima uwe na connection na wanasiasa na viongozi wa serikali, kuanzia connection za ofisi ya raisi, makamu wake au mawaziri. Hata vjana wadogo kabisa wenye hizi connections sasa wanaibukia kuwa na fedha nyingi sana za kufuja na kuishi maisha ya anasa sana.

Inatokea pia kwamba kikundi hiki cha matajiri wa kisiasa uongozi wanalinda sana himaya yao, mara nyingi kwa kutumia vyombo vya dola kama polisi, na sasa hata wanajaribu kutumia jeshi la ulinzi, JW. Hawataki watu wengine wa "kawaida" wawe kama wao. Kwa hiyo wanajaribu kuendelea umiliki wa himaya zao kwa kuwekeza katika watoto wao ili kuja kuwarithisha kuwa "wenye nchi" pamoja na utajiri wao. Hii ni kutia ndani kuendelea kufanya ufisadi mkubwa ili hata vizazi vyao vya baade viendelee kuwa katika neema ya kuwa tofauti na Watanzania wa kawaida.

Wengi wasichojua ni kwamba tatizo kubwa la serikali kukataa uraia pacha sio suala la "usalama wa nchi", bali ni usalama wa hiki kikundi kuona Watanzania walioko nje wana uhuru wa mawazo na upeo wa kuona wanachokifanya. Ndio maana hawataki watu wa diaspora wapewe nafasi ya kuja kuwa tishio kwa himaya yao. Wanawaogopa sana watu wa diaspora na wanaona kuwapa uraia pacha ni kuleta hatari ya kuondolewa katika "ufalme wao". Hawa "wenye nchi" wanajua watu wa diaspora hawana "political illiteracy" ambayo wameijenga katika Watanzania wanaoishi nchini. Wanadiaspora wana macho na wanaona, na wanaogopwa.

Lakini nataka nitoe tahadhari kwa watu hawa, kwamba katika jamii yoyote ile, hali kama hii iliyopo Tanzania huwa haidumu. Kuna wakati itafikia critical point, na kutakuwa na mlipuko mkubwa ambao ni namna fulani ya mapinduzi, ili kuliondoa tabaka hili la "wenye nchi" katika hii himaya yao ambayo kwa sasa wanaifurahia sana na kujaribu kuilinda kwa kila namna. Hili ndilo lililotokea nchi kama Tunisia na Misri, na si muda mrefu litatokea Tanzania, hali ikiendelea hivi.
 
Ni kawaida kwamba katika nchi nyingi matajiri wakubwa utakuta ni wafanya biashara, lakini sio Tanzania. Kwa sasa wanaoongoza kwa kuwa matajiri wakubwa Tanzania ni wanasiasa waliopo madarakani au waliokuwa madarakani huko ny lilotokea nchi kama Tunisia na Misri, na si muda mrefu litatokea Tanzania, hali ikiendelea hivi.
Nimekuja kugundua upinzani nao ni wanachama wa chama tawala waiowekwa huko kimkakati
 
Wataje hao wanasiasa wenye hela kumzidi Bakhresa, Mount Meru, Mo au Lake group,

Sometimes tusidanganyane sana, wanasiasa wana hela ila usiseme ndio wenye hela nying nchini, matajiri hii nchi ni wahindi na waarabu
Tanznia kuna kina Bakhresa wangapi? Kwanza Lake Oil ni connection ya wanasiasa, kwa taarifa yako tu.

Na labda nilipaswa kusema matajiri wengi Tanzania ni wanasiasa na viongozi, yaani more than 70% ya matajiri wa Tanzania
 
Hili lipo hivyo kwa nchi nyingi za Africa.

Biashara nyingi ni za viongozi, mara kadhaa imefanyika kwa kificho kupitia Wafanyabiashara wengine ambao sio viongozi wa serikali.
Kama kiongozi sio mfanyabiashara wa moja kwa moja basi jua anatumika na wafanyabiashara kutengeneza mazingira mazuri kwa wafanyabiashara ikiwemo kukwepa kodi na kuwapa dili za serikali.
Ndio sababu hakuna kiongozi anajali kuhusiana na mfumuko wa bei kwa kuwa hizo ni biashara zao ama wana hisa kwenye hizo kampuni.
Jambo baya ni kuwa kadiri miaka inavyokwenda tunatengeza tabaka la watu wenye nacho na mafukara wa kutupwa.

Viongozi wa serikali wana mikono yao katika biashara za usafirishaji( hapa ni mabasi na malori), sekta ya madini (kumiliki vitalu na kuuza madini), sekta ya nishati ( hapa ni uagizwaji wa petrol, disel na kerosene) na kwenye kumiliki vituo vya mafuta(petrol station).
Kwenye sekta ya Ujenzi huku kazi wanayofanya ni ''lobbying'' ya nani apewe mradi upi, halafu yeye anakula tender ya ku-supply kama sio cement basi ni nondo au kupewa sub-contract ya baadhi ya kazi (haswa umeme, plumbing, fire fighting na ICT).

Huwezi kuona majina yao kwa kuwa hizi kampuni zimesajiliwa kwa majina tofauti na wamefanya hivyo makusudi ili waendelee kupiga hela bila bugudha.
 
Tanznia kuna kina Bakhresa wangapi? Kwanza Lake Oil ni connection ya wanasiasa, kwa taarifa yako tu.

Na labda nilipaswa kusema matajiri wengi Tanzania ni wanasiasa na viongozi, yaani more than 70% ya matajiri wa Tanzania
Wataje kwa majina, mbna unazunguka ? Wataje fulani anamiliki nin na nini, usiwe mwongo,

And mind u kuna wengine wana pesa chafu kabla ya kuingia kwenye siasa, kina Msukuma, Mbowe, yule jamaa wa CRDB,

Haya tuambie tajiri gani anamiliki nini na ni mwanasiasa?
 
Wataje hao wanasiasa wenye hela kumzidi Bakhresa, Mount Meru, Mo au Lake group,

Sometimes tusidanganyane sana, wanasiasa wana hela ila usiseme ndio wenye hela nying nchini, matajiri hii nchi ni wahindi na waarabu
Nyie ndio mnaamini Bakhresa aliuza kahawa pale msikitini akaanzisha kiwanda cha kusaga nafaka taratibu hivyo hadi akawa bilionea. Upewe mashine ya kusaga tuone kama utapata hata utajiri wa milioni 50. SAS anawatazama uko.

Au mnakuja kwa mzee Gulam Dewji na mwanae Mo mnasema walipambana, ni sawa walipambana. Ila hata wewe tukikupa vile viwanda vya nguo bure kwenye ubinafsihaji, na ukavitumia kama dhamana kukopea mabilioni nje, na tukakupa mashamba ya mkonge sawa na bure miaka 20 baadae huwezi shindwa kuwa bilionea mkubwa.
Huwezi nipa klabu kubwa kwa hela za "maandishi" billioni 20, alafu nikiulizwa nimeziweka akaunti gani na zimetumikaje nafoka nakulalamika ninavyopata hasara. Baadae ukarudi ukakuta sipo bilionea.

Sasa hayo yote huwezi yapata bila mkono wa kisiasa au kuwa na wanasiasa nyuma. Katafute mmiliki wa Kagera kiwanda cha sukari nani, mmiliki wa Mtibwa nani alafu ujue kwanini sukari Tanzania haitoshelezi kwa uzalishaji ila serikali haitaki kuagiza nje tena kwa bei nafuu.

Nilishtuka baada ya serikali ya Magufuli kukisumbua kiwanda cha Dangote kuhusu either makaa ya mawe au clinker (sikumbuki ni kipi hapo) ghafla Rais mstaafu wa Nigeria, Olisegun Obasanjo akafanya ziara binafsi kwa private jet kuonana na Magufuli. Baada siku chache mambo ya Dangote cement yakatulia. Nikaenda kufuatilia kwanini suala linamhusu Dangote alafu Olisegun ndio aje binafsi wakati ana tiketi ya kidiplomasia anaweza kuja kitaifa.

Kiufupi iko hivi, Dangote alitokea familia ya uwezo ila akaongezea kuwa na political and military connection, Nigeria ilitawaliwa na military rulers. Akafanya awe na haki ya kuagiza mchele na sukari nje na kuuza kwa faida kubwa (sababu kwa kutumia siasa aliua ushindani). Baadae Nigeria ikafanya uchaguzi kutafuta kiongozi wa kiraia iachane na utawala wa kijeshi, Dangote akafadhili uchaguzi mkuu wa Olisegun Obasanjo na akashinda.
Obasanjo akaleta sera ya viwanda kwa kiqsi fulani, ghafla Dangote akaanza kujenga viwanda na ghafla akawa bilionea maradufu. Ukifuatilia biashara za Dangote huwa zinapewa subsidiaries, exclusive rights, mara ndio zinakuwa kipaumbele na sera kuu ya serikali. Kwa sasa ana refinery, ni usanii mtupu unaendelea. Dangote ni GSM wa Obasanjo. Na Marais wa Nigeria huwa wanaachiana na kulindana, mnyororo unaendelea na ukitaka kuingia hapo kati wanufaika wako tiyari muingie vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Biashara za Afrika zina mkono mkubwa wa kisiasa. Hata pale Misri ni hivihivi, Sudan ni hivi, Somalia baada ya kuharibika ile miaka ya 90 waliokuwa wanahamia Nairobi na Dar kujenga mahoteli na kuanzisha biashara kubwa ni wanasiasa wao waliotoroka. South Africa pale hao ndio kabisa wanafanya biashara ikulu.
Biashara ambayo haina innovation nyuma ni vigumu itengeneze utajiri wa haraka. Biashara za kawaida kama unga na simenti inataka uwekezaji mkubwa (sijui hela utapata wapi), sera rafiki kwako mfanyabiashara hiyo (nani ataweka sera za kuku-favour) na ulinzi (dhidi ya sheria, kesi, upinzani, ushindani). Hivyo vyote vinapatikana kwenye siasa za Kiafrika.

Hao wote uwezo mkubwa kibiashara wanao, kisha tag ya kisiasa ndio inakuja.
 
Sasa ngoja nikuambie kitu,
Biashara popote pale duniani, na wafanyabiashara wakubwa popote duniani wanaitumia sana serikali either kuwadhamin au kulinda mitaji yao, refer Apple Vs Huawei case, saizi inaenda kuibuka nyingine ya BYD Vs Tesla tayari marekani ametangaza kuingilia kati,
Hio ni kawaida, huko china sitaki hata kukuambia jinsi makampuni yao yalivyobebwa na serikali zao, kina BYD, Huawei, Alibaba, Tencent na wengine,

Cha kujiuliza ni je una hizo sifa za kubebwa? Juzi hapa bongo Magu kampa Bakhresa eka 10K, unadhani kwann kapewa yeye, lazima uonyeshe potential kisha serikali inakuja kati, ipo hivyo dunia nzima,

Nenda India uone kina Ambani na Tata walivyokuwa connected na serikali, ndio mfumo wa uchumi duniani, kuwa mfanyabiashara lazima ujue kucheza na wanasiasa,

Ila back to your point, ni wanasiasa gani matajiri hapa bongo?
 
Sasa mkuu mtu kudhamin kampen za uraisi unadhani alikuwa hana hela?
Halafu hio ya kudhamin vyama au kampen ipo dunia nzima, kuanzia USA hadi andora, ni kawaida, usishangae kaka, dunia sio fair play ground, lazima kuna kuviziana kwa hapa na pale,
 
Ni kawaida kwamba katika nchi nyingi matajiri wakubwa utakuta ni wafanya biashara, lakini sio Tanzania. Kwa sasa wanaoongoza kwa kuwa matajiri wakubwa Tanzania ni wanasiasa waliopo madarakani au waliokuwa madarakani huko nyuma. Halafu wanafuatiwa na viongozi wa serikali, pamoja na ndugu zao.

Imefikia kwamba hata ukiwa mfanya biashara, ili utajirike kwa haraka lazima uwe na connection na wanasiasa na viongozi wa serikali, kuanzia connection za ofisi ya raisi, makamu wake au mawaziri. Hata vjana wadogo kabisa wenye hizi connections sasa wanaibukia kuwa na fedha nyingi sana za kufuja na kuishi maisha ya anasa sana.

Inatokea pia kwamba kikundi hiki cha matajiri wa kisiasa uongozi wanalinda sana himaya yao, mara nyingi kwa kutumia vyombo vya dola kama polisi, na sasa hata wanajaribu kutumia jeshi la ulinzi, JW. Hawataki watu wengine wa "kawaida" wawe kama wao. Kwa hiyo wanajaribu kuendelea umiliki wa himaya zao kwa kuwekeza katika watoto wao ili kuja kuwarithisha kuwa "wenye nchi" pamoja na utajiri wao. Hii ni kutia ndani kuendelea kufanya ufisadi mkubwa ili hata vizazi vyao vya baade viendelee kuwa katika neema ya kuwa tofauti na Watanzania wa kawaida.

Wengi wasichojua ni kwamba tatizo kubwa la serikali kukataa uraia pacha sio suala la "usalama wa nchi", bali ni usalama wa hiki kikundi kuona Watanzania walioko nje wana uhuru wa mawazo na upeo wa kuona wanachokifanya. Ndio maana hawataki watu wa diaspora wapewe nafasi ya kuja kuwa tishio kwa himaya yao. Wanawaogopa sana watu wa diaspora na wanaona kuwapa uraia pacha ni kuleta hatari ya kuondolewa katika "ufalme wao". Hawa "wenye nchi" wanajua watu wa diaspora hawana "political illiteracy" ambayo wameijenga katika Watanzania wanaoishi nchini. Wanadiaspora wana macho na wanaona, na wanaogopwa.

Lakini nataka nitoe tahadhari kwa watu hawa, kwamba katika jamii yoyote ile, hali kama hii iliyopo Tanzania huwa haidumu. Kuna wakati itafikia critical point, na kutakuwa na mlipuko mkubwa ambao ni namna fulani ya mapinduzi, ili kuliondoa tabaka hili la "wenye nchi" katika hii himaya yao ambayo kwa sasa wanaifurahia sana na kujaribu kuilinda kwa kila namna. Hili ndilo lililotokea nchi kama Tunisia na Misri, na si muda mrefu litatokea Tanzania, hali ikiendelea hivi.

Maskini ni maskini tuu Mkuu.
Kama Ulaya tuu kuna maskini na mifumo yote iko sawa kwa kiwango kizuri sidhani kama kuna namna ya kumuokoa Maskini
 
Tanznia kuna kina Bakhresa wangapi? Kwanza Lake Oil ni connection ya wanasiasa, kwa taarifa yako tu.

Na labda nilipaswa kusema matajiri wengi Tanzania ni wanasiasa na viongozi, yaani more than 70% ya matajiri wa Tanzania
Wewe unajua kuwa bakhresa utajiri wake umetokana na maamuzi ya siasa mbovu Na hata Mo wameweka upenyo wajajikwapulia asset za nchi. Niambie National milling ilimezwa na Nani na ufuatilie asset za makapuku zilizomezwa na Mo
 
Sasa ngoja nikuambie kitu,
Biashara popote pale duniani, na wafanyabiashara wakubwa popote duniani wanaitumia sana serikali either kuwadhamin au kulinda mitaji yao, refer Apple Vs Huawei case, saizi inaenda kuibuka nyingine ya BYD Vs Tesla tayari marekani ametangaza kuingilia kati,
Hio ni kawaida, huko china sitaki hata kukuambia jinsi makampuni yao yalivyobebwa na serikali zao, kina BYD, Huawei, Alibaba, Tencent na wengine,

Cha kujiuliza ni je una hizo sifa za kubebwa? Juzi hapa bongo Magu kampa Bakhresa eka 10K, unadhani kwann kapewa yeye, lazima uonyeshe potential kisha serikali inakuja kati, ipo hivyo dunia nzima,

Nenda India uone kina Ambani na Tata walivyokuwa connected na serikali, ndio mfumo wa uchumi duniani, kuwa mfanyabiashara lazima ujue kucheza na wanasiasa,

Ila back to your point, ni wanasiasa gani matajiri hapa bongo?
Hapo unashindwa kutofautisha sera za kiuchumi za serikali na uamuzi binafsi wa kisiasa kwa biashara.

Hao Huawei vs Apple ni sera za kiuchumi za nchi zao kulinda data na kubaki na teknolojia muhimu ya mawasiliano. Hao kina Ambani na Tata Group ni sera za nchi India wana Make in India Initiative, mwanasiasa hafanyi single picking ya mtu na kumpendelea. Hao Tata waliisaidia India kwenye teknolojia ya nyuklia na kuunda silaha nyingi za kijeshi, sio ajabu wao kulindwa sababu hata upinzani wa maana pale India haina, ikipotea ni hasara kwa nchi. Ila ni ajabu kwa serikali kuchagua muuza mchele mmoja kati ya 20 na kumpa haki ya kuagiza kutoka nje yeye tu.

Bakhresa kupewa eka zote hizo sio shida. Kama aliweza kupewa kiwanda cha National Milling kuzalisha unga anashindwaje kupewa eneo azalishe sukari. Ndio siasa zenyewe ninazosema.
 
Wewe unajua kuwa bakhresa utajiri wake umetokana na maamuzi ya siasa mbovu Na hata Mo wameweka upenyo wajajikwapulia asset za nchi. Niambie National milling ilimezwa na Nani na ufuatilie asset za makapuku zilizomezwa na Mo
Mkuu, utajiri sio kuangalia source,
Kina Abood walimeza viwanda vingap leo iko wapi, baba na babu zetu walikuwa wapi wakati hao wanameza viwanda,

Hayo yote ndio yanayotutofautisha, hakuna utajiri wa bahati, ni kutumia fursa zilizo mbele yetu, wazee wetu nao walikuwepo kipindi hicho cha ubinafsishaji, je walifanya nini? Kama hawakufanya kitu bas they don't deserve wealth, hizo sera mbovu zipo kwa wote, wazungu na sisi, tupambane tuache sababu nyingi, hakuna nchi perfect, hakuna nchi isio na maskini, kikubwa kwenye mazingira haya haya jua unachomokaje na unapataje pesa nying
 
Back
Top Bottom