Nashauri kwenye majanga viongozi wa serikali wafike mwisho; wataalam wapewe vipaumbele kwanza

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Wakati wa majanga kumekuwepo na kasumba viongozi kutangulia na makamera yao wakielekeza wataalam namna ya kufanya uokoaji!

Hii haina afya kabisa!

Kwa waliosomea elimu ya majanga watanielewa!

Wakati wa majanga ingekuwa vyema zaidi wataalam wetu wangepewa nafasi ya kuonesha utaalam wao!

Viongozi kuanzia DC, RC, Mawaziri na waziri mkuu wangekuwa wanakaa nyuma kusubiri wataalam wafanye kazi yao!

Nguvu ya kuwalinda viongozi, na misafara ya viongozi wakati wa majanga, tungeipeleka kwenye kuongeza vikosi kazi kutoka mikoa mbali mbali ili kuja kuongeza nguvu!

Natamani kuona punde baada ya majanga elikopita na ndege zisafirishe nguvu kazi inayookoa kuliko kupeleka viongozi ambao huongeza mzigo wa kuwapokea na kuwalinda wakati zoezi likiendelea!

Haiwezekana nchi inawataalam ambao ndiyo haswa wanatakiwa kuongea/kuelekeza lakini kwenye ajabu wanaozungumza ni viongozi!

Wanasiasa msiwe vimbelembele acheni wataalam watuambie kitaalam!
Baada ya reportv ya wataalam ndipo mje mseme nyie mwishoni!

Tuheshimu taaluma kwa vitendo! Vinginevyo mtachangia sana kuuwa professionalism katika taifa hili!.

Kuwa mwanasiasa haina maana mnajua kila kitu!
 
Back
Top Bottom