Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

kuna kipindi alipoteza familia nzima kumbe ilikuwa mwendelezo wa utajiri uliotukuka.usimsahau James Oraa HUYU NASIKIA ALIHASIWA.
James Oraa wa majengo kwa mtei, alikuwa don sana, comoan moja na sawaya hiyo pamoja na patel
 
Hata kama....bado naamini hata hao tembo wanaowindwa nao hupenda waishi maisha marefu!

Sisi binadamu ni wabinafsi sana.

Mtu unaenda kumwinda tembo ili iweje? Ukatishe maisha yake kwa manufaa yako?

Inasikitisha.
Ni kweli, binadamu sie wabinafsi sana..

Kuna wengine wanatoka Marekani na vijiviwalo lakini hata kuachia ndugu zake hapa bongo pindi anarudi hawezi, anarudi nazo zote Marekani..
 
SIJUAGI JINA LAKE ILA NAMJUA KWA JINA LA SHAYO WAKATI NAONDOKA NILIMWACHA AKIUZA DUKA LAKE MOJA RAU MADUKANI AKIWA NA MABUCHA KADHAA KIPINDI HATA MFUNGOMALI ALIKUWEPO.

Inasemekana mwenye mawe zaidi ni yeye sema sababu dogo ni maarufu zaidi na basi watu wanachukulia ibra ndio ana mawe zaidi
 
Kama vile nnakuona yan mlivyokua mkirudi old na mabox yamejaa pilau zilizobakia kwenye masufuria na pombe za kuficha kwenye makoti na kuringe hall
Hahahahaha acha tuu Mkuu,kipindi hicho ikifika Jumatano unafua kabisa suruali yako,shati na tai yako na viatu unapeleka shoe shine then Alhamis saa9 unaenda kutega pale keep left cha YMCA unasoma ramani then saa 12 kasoro unawahi kuingia ukumbuni kabla watu hawajaanza kuingia. Na sisi wazee wa lager tulikuwa tunakaa meza iliyokuwa karibu na vinywaji.
 
Recently kabla ya kupata ajali. Alikuwa anakopesha watu pesa, lakini collateral ilikuwa tittle ya kiwanja ama nyumba.(Hii biashara walianza na Alex Massawe na walikuwa very close). Kwa taarifa ni kwamba wengi sana walishindwa kulipa. Na kwahiyo wakapoteza nyumba zao na viwanja vyao. Sometimes magari. Recently kabla ya ajali pia alikuwa mtu wa karibu sana na Vincent Laswai mwenye Kibo Palace besti yake Uhuru Kenyatta!

Ni ukweli mtupu kuwa kuna watu wanaomchukia sana Babu Sambeke.
Laswai na Uhuru ni good friends kabla hata Uhuru hajawa rais
 
Yesu alipolinganisha ufalme wa mbingu na tundu la sindano hamkumwelewa? Siyo matajiri wa Moshi tuu. Hata matajiri wengi wakubwa Duniani nao wamezulumu Sana tuu.
Mwarabu alikuwa anatupa shanga sie twampa dhahabu..

Mzungu nae akaja akatuibia sana tu..

Utajiri sio lelemama..
 
Sio Babu anaitwa "Bob Sambeke" Huyu Jamaa nilifahamiana nae Mwaka 2012 Nakumbuka nilikuwa Kidato cha Nne, Nilifahamiana nae Baada ya Kukatiza uwanja Mdogo wa Ndege wa soweto (Nikiwa natoka TPC,Kupitia Dar es Salaam Street), Kukatiza Pale tukakamatwa na walinzi wa Airport pale, wakatuonesha Sheria na ibara kibao za Uchukuzi wa Anga wakidai tulipe Dola 200 wakati ule kama 400K, tulikuwa wanne.. Ndipo akatokea Huyo mtu anaitwa Bob Sambeke Wakati ule Bob alikuwa mtu wa makamo na alikuwa akimiliki ndege Mbili zilizokuwa zikipaki Pale uwanja wa Ndege SOweto.. Bob alikuwa mtu Mkorofi.. Katika Hali yake akaanza kutupigisha story (Bob Hadi walinzi walikuwa Wakimwogopa).. Kilatini kuna Msemo unasema "In Vino Veritas" yaani katika Pombe/Kilevi kuna ukweli..Muhusika lazima Aongee ukweli Fulani!
Bob akasema yeye hawezi kufa kwa ugonjwa, Kifo chake kinatakiwa kiwe cha Risasi au Ajali ya Ndege!
Baada ya Bob kuondoka Ndipo Yule Mlinzi akafunguka kuwa Bob alishawahi kuwa Jambazi na Mali zake alizichuma kwa Njia hiyo hasa hasa, pia ikumbukwe Bob alishawahi Kuwa Mwanajeshi...Alikuwa Tajiri Mkubwa Mno!
Muda Mchache Baadaye Nahani 2012/2013 Bob alipata crash ya Ndege Uwanja wa Ndege Arusha Pale..Bob Alifariki (Mungu Amrehemu)
Alikuja Kuzikwa Pale Parokia ya Karanga Moshi..Kanisa lililokuwa karibu sana na Bweni letu... Sikuhudhuria Misa ila niliona Barabara yote inayoelekea Kanisani kama 1 KM ilijazwa na Magari... Nasikia Kanisani hawakuficha kusema Kuwa Bob aliwahi kuwa Jambazi!

Kwako Mtoa Mada!
Eti kwako mleta Mada. Nimecheka mno. JF idumu.
 
Back
Top Bottom