Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

Habari za mida wana jf

Kipindi nakuwa moshi town pale wenyewe wanapaita mji wa wagumu, kulikuwa na matajiri wanajulikana na kusifika sana.
Walikuwa maarufu sana hadi makanisani.Ukienda kanisani ukimwona hata mke wake unabaki waooo
Walikuwa hadi na siti zao kristu mfalme pale.waliishi uzungun,wengine njia ya old moshi.

Kuna siku tumeenda nyumbani kwa rafiki yetu mmoja tulikuwa tunasomanaye mafundisho kanisan maeneo ya uzunguni kule,huo mjumba looh tulibak mdomo wazi.Na ilikuwa first time naona swimming pool nyumban.

Anyway zama zimepita, wengi wameaga dunia,wengine wapo ila umaarufu sio kama zamani.Nilikuwa natoka familia ya kikapuku kabisa so nilitaman siku moja at least na sisi family yetu iweze kuwa na jina kama family zile ama hata visenti tu.

Kuna mzee mmoja alikuwa maarufu sana hapo moshi town,alikuwa na maduka,garages,mabar,mabasi na biashara kibao.Alikuwa anaheshimika kama mfanyabiashara mkubwa moshi.Na wengi tuliamini hivyo.Bwana weeh siku moja katika harakati zake,akapatwa na majanga kwenye mbuga za Kenya, akapigwa risasi akafa,wenzie walifanikiwa kukimbia.Ikaja fahamika mzee alikuwa mwindaji haramu kwenye mbuga ya tsavo,alikuwa anawinda tembo na kuuza pembe na ndio ulikuwa siri ya utajiri wake.

Alirudishwa moshi akaenda zikwa kwao migombani ,after wards Mali zile zikayeyuka kama barafu. Since then nikajifunza kutokutamani cha mtu kwani hujui kakipataje. Utajiri una siri kubwa so vijana wenzangu tufanye kazi.Usiamini story za nilianza na kushona viatu stend,huwa hawasemi ukweli.
Kwa africa especially Tanzania si jambo rahisi kumpata Billionaire aliyepita mfumo usio na ujanja ujanja kufikia mafanikio yake
 
Buffalo ya wapare flani sina uhakika kama wana uhusiano na Mberesero, ana kijana wake mmoja mwenye ile Kindoroko hotel.

Buffalo hawana undugu na Mberesero!! Mberesero ndiye mmiliki wa Ngorika na Kindoroko Hotel.

Ana undugu na Hatco au Zebra Hotel, mabasi ya Ndoika kama unayakumbuka na kuna kampuni ya basi nimeisahau ila ilikuwa inatoka Ar to Mwanza.

Pengine anaweza kuwa na undugu na kina Osaka coz wanatumia facilities za pamoja mfano petrol stations.
 
Hapana alipoteza familia nzima kwenye ajali iliyomuhusisha na yeye mwenyewe. Ilikua almanusura nayeye arudishe namba

Alikaa muda mrefu KCMC akipata matibabu wakati huo hoteli yake ya New Castle ikiwa mpyaa

Kwahiyo siamini kama ajali ile ilikua ni makafara ya kishirikina
Newcastle tumeruka disco Sana pale tukiwa manyokaa aisee
 
Hapana alipoteza familia nzima kwenye ajali iliyomuhusisha na yeye mwenyewe. Ilikua almanusura nayeye arudishe namba

Alikaa muda mrefu KCMC akipata matibabu wakati huo hoteli yake ya New Castle ikiwa mpyaa

Kwahiyo siamini kama ajali ile ilikua ni makafara ya kishirikina
maneno mkuu maneno,ila ni kweli aliponea sindano walikuwa wanatoka arusha nadhani.
 
Maisha yamebadilika sana, na kila zama na wakati wake...

Zamani baadhi ya wafanya biashara walikuwa wana roho ngumu sana, kuna jamaa mmoja ni jirani yangu alikuwa ni mwizi balaa wa magari, alishirikiana na askari wa kenya, huyu jamaa biashara ya wizi kaachana nayo, sasa hvi ana maduka ya kuuza bia za jumla na migahawa..

Nawafahamu vijana wengi sana moshi na arusha wamefungwa magereza ya kenya kwa uwindaji haramu, kuna mtanzania mmoja alidakwa anawinda tembo alinyofolewa kidevu na sime askari wa kenya wanaroho ngumu
sio askari wa kenya mzee usiombe kukutana na askari wa wanyamapori popote na yeyote,ni vita ya kufa na kupona.
 
sio askari wa kenya mzee usiombe kukutana na askari wa wanyamapori popote na yeyote,ni vita ya kufa na kupona.
Ni kweli ila mbona wa kwetu hawaui majangili hivo? Manake tumemalizia tembo zetu na majangil ila sio wengi waliouawa
Wakenya wana roho katili sana
Walikuwa hawawakamati wao ni kuwalamba shaba tu
Aliyebahatika kukamatwa na kuwekwa gerezan Mungu wake ni mkubwa sana
Wengi walimalizwa on the spot
 
Saivi jimbo limesonga kimtindo kuna jengo la ghorofa zisizo pungua 5,ukijumlisha na bank ya mkombozi na makolokolo mengine kristu mfalme panabadilika
Ok ila yule amani wa mwanzo aliyekuwa paroko mnene mrefu mweusi alitafuna sana sadaka za wana mo town hahahah
Baadaye nadhan alipelekwa rombo huko
 
Back
Top Bottom