Matajiri 270 wanaohudhuria mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani waomba kuongezewa kodi

Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
348
462
Matajiri 270 wanaohudhuria mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) wanawasilisha kwa mara nyingine tena ombi lao la kutaka kukatwa kodi zaidi kwenye utajiri wao uliokithiri.

Kwa pamoja matajiri hao wamesema kumekuwa na gap kubwa kati ya maskini na matajiri na hivyo kuwafanya maskini wawe katika changamoto nyingi za kimaisha ikiwamo matatizo ya kisaikolojia.

Katika barua yao hiyo wamesema kuwa kufanya hivyo hakutowafanya wao maisha yao na watu wao wa karibu kuathirika bali ni katika harakati za kumuinua mtu maskini.

Wameomba pia watu wengine wenye utajiri ulikithiri na viongozi wa serikali waige mfano wao ili kupambana na athari za umaskini.

My take:
Ombi hili liwe chachu ya kuleta mabadiriko katika sheria zetu zinazowafanya baadhi ya viongozi kutokulipa kodi kutokana na nyazifa zao.

Badala ya kukwepa kodi, ni vyema kila mwananchi aone ni jukumu lake kulipa kodi halali ili zitusaidie kuijenga nchi yetu.

Vile vile wale waliopewa nafasi ya kukusanya na kusimamia matumizi ya kodi zetu basi wafanye hivyo kwa moyo wa uzalendo.
View attachment 2876928
 
Hawa sio waongezewe kodi hela ziwe zinachukuliwa zinapelekwa kwenye matumizi ya kawaida tu
 
Back
Top Bottom