Dar: Wanawake wa Kinyerezi wazindua jukwaa lenye lengo la kumuinua Mwanamke kiuchumi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Wanawake wa Kata ya Kinyerezi Jijini Dar es Salaam wamezindua rasmi Jukwaa la Wanawake ikiwa ni hatua ya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kumuinua Mwanamke kiuchumi.

Jukwaa hilo limezinduliwa na Lutta Rucharaba ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli, jana ya Agosti mosi, 2023.

Akizungumza katika uzinduzi huo amesema uzinduzi wa jukwaa hilo ni muendelezo wa kuzinduliwa kwa majukwaa ya Wanawake kupitia ngazi mbalimbali kuanzia mitaa, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa kama lilivyo kusudio la Rais Samia la kumsogezea mwanamke maendeleo.

Amesema “Majukwaa kama haya yalikuwepo tangu zamani lakini yalikufa, kupitia uongozi wa Rais Samia sasa yanafufuliwa, hii ni ishara kwamba Rais wetu ana lengo la kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa akinamama.”

Ametaka Wanawake wa Kinyerezi na nchini kwa jumla kutomuangusha Rais na kujiunga kwa wingi kwenye majukwaa hayo ambayo yanatoa fursa mbalimbali ikiwemo kutetea haki za Wanawake, kuwaunganisha na fursa za kiuchumi na kisiasa.

Amesisitiza “Nawaomba Wanawake mpende kuwania nafasi za uongozi zinapojitokeza. Msijiweke nyuma, ikitokea nafasi ya mwenyekiti wa Mtaa, Diwani, Mbunge na nyinginezo jitokezeni kwa wingi ili mnapokuwa kwenye majukwaa kama haya inakuwa rahisi mambo yenu kutekelezeka.”

Mwenyekiti wa Jukwaa hilo la Wanawake, Kata ya Kinyerezi Mwamini Mkule amesema kata hiyo imeamua kuzindua jukwaa hilo litakalowawezesha kupata fursa za kiuchumi na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.

“Wapo Wanawake wanafanyiwa ukatili wa kijinsia wanapigwa na wanabakwa kupitia jukwaa hili watapata fursa ya kutetewa na kupata haki zao, ninawatahadharisha Mwanamke yeyote atakayefanyiwa ukatili wa kijinsia halafu aliyemfanyie aletwe kwenye jukwaa hili kwa kweli atajuta,” amesema Mkule.

Amesema kupitia jukwaa hilo la Kata ya Kinyerezi Wanawake wa Kata hiyo wataunganishwa pia na wajasiriamali wadogo, watapatiwa mitaji na fursa za masoko, watajengewa uwezo katika maeneo ya ujasiriamali kama vile namna ya kutunza kumbukumbu, elimu ya kodi, ufungashaji bidhaa na kuhamasishwa kuanzisha vikundi vya kiuchumi vya wanawake.

Tayari jukwaa hilo limeanzisha mradi wa kutengeneza batiki unaotarajiwa kuzalisha ajira kwa Wanawake na kuwawezesha kukopeshana na hivyo kujiinua kiuchumi.

Mwenyekiti wa wenyeviti wa Kata katika eneo la Tabata Shamte Mkali amewataka Wanawake hao kutumia jukwaa hilo kujenga umoja na mshikamano kwa kuwa ndio litakuwa sauti yao.

Septemba 15, 2021 katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Demokrasia Duniani yaliyofanyika Dar es salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Rais Samia alihidi kufufua majukwaa yote ya Wanawake nchini.

Aliahidi kukuza uchumi wa wanawake na kusema anajipanga kuyalea majukwaa ya wanawake na kuwasihi wanawake kuyaendeleza majukwaa hayo na kufufua yale yaliyokufa.
 
Mtoto wa kiume ana kazi sana naona anasahaurika sana. Kampeni zimekuwa ni nyingi sana za kufanya empowerment ya mtoto wa kike mwisho wa siku fursa zote wanapewa wao kwa kigezo cha haki sawa ila mwisho wa siku bado wanataka mtoto wa kiume awe provider.
 
Halafu watu wameungana mradi mkubwa ni batiki hivi huko sokoni batiki inaenda kweli kuwezesha hao wamama waendeshe maisha yao ya kila siku.Mi Nadhani tupunguze siasa ningesikia mumewapa eneo la kutosha la kulima na nyezo au mitaji wakalima mazao ya biashara mngekuwa mmewainua sana hao wamama katibu wa mbunge ongea na mmbunge muwatafutie hata trekta kumanisha mnaunga mkono juhudi za Rais wetu
 
Back
Top Bottom