Historia ipo ili watu wajifunze kwayo, kila tukio linalotekea ni funzo kwa mwenye akili
Mwaka 1985 tarehe 7 April, Afisa mstaafu, Mwanasheria na Mwanaharakati maarufu nchini Uingereza mwenye asili ya usikochi Willie MacRae ambaye alikuwa Makamu mwenyekiti wa SNP, aliyekuwa akipambana na Unyonyaji wa waskochi masikini na makundi ya mafia yenye kumiliki makampuni makubwa nchini humo alipata ajali ya gari na kufariki katika milima ya Scot.
Ajali yake ilizua mjadala mkubwa kuwahi kutokea nchini humo kutokana na mambo yafuatayo;
1.Wajihi wa Willie na vita yake dhidi ya MAFISADI.
2.Utata wa Ajali yake.
3.Ripoti ya Polisi.
WAJIHI WA WILLIE NA VITA YA UFISADI.
Willie kama walivyo wanaharakati wengi duniani alikuwa ni sauti ya wasio na sauti, wanyonge wa nchi ambae alitangaza wazi wazi vita dhidi ya Wanyonyaji na Mafisadi nchini mwake, akiwa kama Mpinzani ambaye aliweza kuwashambulia na hata kufungua kesi mara kadhaa mahakamani kupinga operation za makampuni makubwa ya Nuclear yanayomilikiwa na Mafia wenye mikono mirefu Serikalini ambao walinunua vyama vya siasa ambavyo vilikuwa vikipambana kwenye kampeni ili kuchukua Serikali.
Willie akiwa mstari wa mbele kupinga Kitendo cha Kampuni ya Dounrey Nuclear Power Development kumwaga takataka baharini, alifungua kesi na kuandaa vidhibiti vya kisheria kuthibitisha kuwa jambo hilo lina athari kubwa kwa wananchi, na kutokana na vitisho na sensitivity ya vidhibiti hivyo ilimbidi awe anatembea navyo kila wakati na kila anapokwenda hakuwahi kuziacha sehemu hata ofisini kwake ingawa baada ya kifo chake haikujulikana Document hizo zilipotelea wapi.
UTATA WA AJALI.
Watalii wawili watalii wa Ki-australia waliona gari aina ya Volvo katika bonde la Glenmoriston, na watalii wale walisogelea na kukuta mwili wa mtu kwenye gari hiyo ukiwa umejaa damu kuanzia kichwani na mwili mzima, mikono ikiwa imeshika usukani wa gari, kichwa kimelalia bega moja na hakuwa amevaa mkanda wa gari (seatbelt)
Wakasogea barabarani na kusimamisha gari ambayo ndani yake kulikuwa na Diwani wa Chama Cha SNP ambaye alimtambua WILLIE na kutambua pia kuwa alikuwa HAJAFA bado, wakamuwaisha Hospitali Aberdeen Royal infirmary ambapo alifariki na hospitali hapo iligundulika alipigwa risasi kichwani, kabla ya gari yake kutumbukia kwenye korongo hilo.
RIPOTI ZA POLISI
Ilikuwa kitendawili kikubwa kwa kuwa ripoti ya kwanza ilisema kuwa alitumbukia bondeni kwa kukosa kulimiliki gari kutokana na spidi, lakini ripoti ya hospitali inasema alipigwa risasi ya kichwa kabla ya kutumbukia kwenye korongo na kwa kuwa kioo cha gari hiyo hakikuwa na tundu la risasi ikabainika kuwa mpigaji wa risasi hiyo alikuwa ndani ya Gari hiyo kisha akashuka na kulisukuma gari kwenye Korongo.
Uchunguzi pia ulibaini kuwa bastola aina ya Wesson 45 Calibre ilipatikana mita chache kutoka ilipookotwa gari ya Willie, lakini hakukuwa na alama zozote za vidole kwenye bastola hiyo jambo lililofanya isitumike kama ushahidi katika upelelezi wa kesi hiyo.
TUKIO SIKU YA KIFO CHA WILLIE.
Siku ya Kifo cha Willie ambacho kilikuwa ni gumzo kilifuatiwa na tukio la Wanasiasa wawili maarufu na wabunge wa Chama Cha Ulster Unionist kujiuzulu, Ulster ni Chama ambacho kilikuwa kinapingana na harakati za WILLIE. Kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa ni Decoy..,kuwaondoa wananchi katika mjadala wa kifo cha WILLIE.
NCHI zingine Duniani Serikali zina Mafia lakini TANZANIA mafia wana Serikali.. Dr Slaa Nov,2009 on response to Richmond Scandals.
R.I.P Mtanganyika Rev. Christopher Mtikila
Hivyo ndivyo ulivyo mwisho wa wanaharakati wa kweli duniani.
Namna hii ndio ulikuwa mwisho wa;
@ Kassi Manlan wa Burundi 2001
@ Clement Oumarou wa Burkinafaso 1991
@ Abdelkader Hachani wa Algeria 1999
@ Rev. Emile Biayenda wa Congo 1977
@ John Kaiser wa Kenya 2000
@ Carlos Cardoso wa Msumbiji 2000
@ Dian Fossey wa Rwanda 1985
Na pia ulitanguliwa na Rev Janani Luwum wa Uganda mwaka 1977...na hakika wapo watakaofuata baada yao