Maswali tata kifo cha Mchungaji Mtikila

Maswali tata kifo cha Mchungaji Mtikila

ALWATAN KIZIGO

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
542
Reaction score
648
1. Gari yake haijaharibika kabisa na tunaaambiwa iliacha njia na kupinduka tunajua sababu kubwa ya magari kuacha njia ni kupasuka kwa matairi lakini hili gari la Mchungaji Mtikila hakuna tairi liliposuka. Sasa tuambiwe sababu ya kuacha njia na kupinduka ni nini?

2. Mchungaji Mtikila hana alipoumia au kubleed damu.(Labda iwe kafa kwa mshtuko wa moyo au internal wounds. Kwenye picha anaoekana hajaumia hata kidogo hata nguo alivozavaa zikiwa hazijachanika hata kidogo.Sasa tuambiwe sababu gani nyingine iliyopelekea kifo chake?

3.Tunaambiwa ajali alipata SAA 11 alfajiri Chalinze kwaa asili ya eneo la Chalinze ni eneo bize sana kwanini picha iliyosambaa inaonesha ni asubuhi kabisa kumekucha ina maana ajali yake haikushtukiwa na watumiaji wengine wa Barabara mpaka asubuhi.

Angalizo sijamlaumu mtu yeyote kwenye hii ajali ila ni maswali ambayo nilikuwa najiulza binafsi sasa nawaomba msichafue hali ya hewa.

Mazingira ya kifo cha Mchungaji Mtikila bado kinatia shaka kuu mbele ya jamii na nachelea kusema huyu Mzee ameuawa na genge la mafisadi ili wafanikiwe kisiasa kwani Mtikila alikuwa ameshakusanya vielelezo vyote vya kuwashughulikia.


1. Jeshi la Polisi Watanzania tunaomba mtusaidie kumuhoji kwa kina huyu mtu anaeitwa Mchungaji Patrick Mgaya. Huyu alikuwa ni mmoja wa waliopata ajali pamoja na marehemu Mtikila. Ikumbukwe kuwa Magaya ni mmoja wa mashabiki muhimu sana wa Mgombea Urais kupitia Ukawa ndg Edward Lowassa.Taarifa za siri zinasema kuwa Mchungaji Mgaya na Mchungaji Mtikila walikutana takribani mwezi mmoja uliopita tu na kwamba kuna wasiwasi kuwa alipewa kazi maaluum ya kuhahakisha amamuua Mtikila.


Taarifa kutoka nyumbani kwa marehemu zinasema kuwa Mchungaji Mtikila akiwa na Mchungaji Patrick Mgaya walianza safari siku ya Ijumaa jioni kwenda mkoani Njombe ambapo waliambatana na madereva wawili ambao Mchungaji Mtikila hakuwafahamu. Aliewafahamu watu hawa wote ni Mchungaji Magaya ambae ndie aliekodisha gari waliokwenda nayo Njombe kupitia kwa Ndg Victor James Manyii ambaye mbali ya kutoa gari aliyokodisha pia alitoa madereva wawili ambao pamoja na Mchungaji Mgaya wao hawakufa isipokuwa Mchungaji Mtikila pekee.


Ajali hii imeacha maswali mengi kuliko majibu. Kwa mfano ukiangalia shingo ya marehemu Mtikila utaona kuna kitu kama kamba ambayo inaweza kuleta tafsiri kuwa ilitumika kumnyonga marehemu. Pili, kwanini mwili wa marehemu hauna hata kovu wala mchirizi wowote wa damu? Je, ni nani alimpiga picha Marehemu Mtikila? Je, Patrick Mgaya ni nani? Kabla kuwa mchungaji alikuwa anafanyakazi gani? Je gari lile lilipinduka lenyewe au liligongwa? Na kama lilipinduka ni kwanini liharibike eneo la mbele pekee?Je Ni chombo gani kilikuwa cha kwanza kumpiga picha na kusambaza kwenye mitandao?


Patrick Mgaya alipopiga simu nyumbani kwa marehemu alisema wamepata ajali na kwamba kulikuwa na majeruhi wengi sana akamaliza kwa kusema mtuombee kisha akakata simu, je, hao majeruhi wengi ni akina nani? Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama muhojini Mchungaji Patrick Mgaya maana zipo dalili kuwa kuna mengi anayoyafahamu kuhusu tukio hili. Pia fuatilieni uhusiano uliopo kati ya Rais Paul Kagame, Patrick Mgaya na EADWARD LOWASSA. Pia nashauri Jeshi la Polisi kumuhoji mtu anaeitwa Dr. Jean Bosco Ngendahimana ambae anaishi nyumbani kwa marehemu pale Mikocheni.

Wale wote wenye misimo thabiti juu ya kuchukia Rushwa na Ufisadi wachukue tahadhari. Nasema hivyo sababu Humphrey Polepole alivamiwa nyumbani kwake Mbezi na Dkt. SLAA anapokea sms za vitisho. Vyombo vya dola viwe macho.

Mch Mtikila.jpg
 
kuna msemo unasema"you see what you want to see",means unakiona unachopenda kukiona,na wewe umeleta mada ukiwa na majibu yako yaliyo egemea upande fulani,kueni jamani,mungu hadhihakiwi,tumuombee mchungaji huko aendako,na tusiwe wepesi wa kufanya shiriki kwani humchukiza sana mungu,nakuombea mleta mada ubadilishe mawazo yako ya kishirikina katika hili....R.I.P Mchungaji wangu Mtikila!
 
Kwani abiria wengine wanaendeleaje?
 
Wewe si mtaalam wa mambo ya ajali,msitake kuwagawa watanzania kwa kila mtu kuja na mawazo ya chama chake,ajali ni ajali Mohamed Mtoi mbona kafa majuzi haukuoji chanzo cha kifo chake Acheni ktmka kwa tamaa za wanadamu mnaleta mada chonganishi kwa wananchi .
 
maswali yote sijaona logic ya kuoanisha Na unachokiwaza. kama Mwalimu wako wa driving school alikuambia gari kuacha njia lazima tyre lipasuke naomba urudi chuo kingine ukalisiti driving. muda wa ajali na picha nalo sio ksb kama ajali imetokea saa kumi na moja unataka kutuambia kuwa ilikuwa lazima kuwa watu wa kwanza kufika eneo la tukio wasisaidie majeruhi wapige picha kwanza na kuzituma kwenye mitandao na hata kama hawakuwa na camera. mwisho daktari wako alikuambia kuwa kifo cha ajali ya gari lazima uwe na external wound na nguo zichanikane kana kwamba ilikuwa vita . ya mungu mengi .
 
ALWATAN KIZIGO

Muuaji wake anajulikana, hivi karibuni amemshambulia sana na akasema hafai kwenda Ikulu. Huyo huyo muuaji ndiye aliyetuma watu kumvamia Humphrey Polepole nyumbani kwake Mbezi beach.
 
Last edited by a moderator:
Mbona pichani hakuna watu. Lakin Kuna picha za selilate zinawrza saidia upelelezi
 
Back
Top Bottom