Maswali tata kifo cha Mchungaji Mtikila

Maswali tata kifo cha Mchungaji Mtikila

Historia ipo ili watu wajifunze kwayo, kila tukio linalotekea ni funzo kwa mwenye akili…

Mwaka 1985 tarehe 7 April, Afisa mstaafu, Mwanasheria na Mwanaharakati maarufu nchini Uingereza mwenye asili ya usikochi Willie MacRae ambaye alikuwa Makamu mwenyekiti wa SNP, aliyekuwa akipambana na Unyonyaji wa waskochi masikini na makundi ya mafia yenye kumiliki makampuni makubwa nchini humo alipata ajali ya gari na kufariki katika milima ya Scot.

Ajali yake ilizua mjadala mkubwa kuwahi kutokea nchini humo kutokana na mambo yafuatayo;

1.Wajihi wa Willie na vita yake dhidi ya MAFISADI.
2.Utata wa Ajali yake.
3.Ripoti ya Polisi.

WAJIHI WA WILLIE NA VITA YA UFISADI.

Willie kama walivyo wanaharakati wengi duniani alikuwa ni sauti ya wasio na sauti, wanyonge wa nchi ambae alitangaza wazi wazi vita dhidi ya Wanyonyaji na Mafisadi nchini mwake, akiwa kama Mpinzani ambaye aliweza kuwashambulia na hata kufungua kesi mara kadhaa mahakamani kupinga operation za makampuni makubwa ya Nuclear yanayomilikiwa na Mafia wenye mikono mirefu Serikalini ambao walinunua vyama vya siasa ambavyo vilikuwa vikipambana kwenye kampeni ili kuchukua Serikali.

Willie akiwa mstari wa mbele kupinga Kitendo cha Kampuni ya Dounrey Nuclear Power Development kumwaga takataka baharini, alifungua kesi na kuandaa vidhibiti vya kisheria kuthibitisha kuwa jambo hilo lina athari kubwa kwa wananchi, na kutokana na vitisho na sensitivity ya vidhibiti hivyo ilimbidi awe anatembea navyo kila wakati na kila anapokwenda hakuwahi kuziacha sehemu hata ofisini kwake ingawa baada ya kifo chake haikujulikana Document hizo zilipotelea wapi.


UTATA WA AJALI.

Watalii wawili watalii wa Ki-australia waliona gari aina ya Volvo katika bonde la Glenmoriston, na watalii wale walisogelea na kukuta mwili wa mtu kwenye gari hiyo ukiwa umejaa damu kuanzia kichwani na mwili mzima, mikono ikiwa imeshika usukani wa gari, kichwa kimelalia bega moja na hakuwa amevaa mkanda wa gari (seatbelt)
Wakasogea barabarani na kusimamisha gari ambayo ndani yake kulikuwa na Diwani wa Chama Cha SNP ambaye alimtambua WILLIE na kutambua pia kuwa alikuwa HAJAFA bado, wakamuwaisha Hospitali Aberdeen Royal infirmary ambapo alifariki na hospitali hapo iligundulika alipigwa risasi kichwani, kabla ya gari yake kutumbukia kwenye korongo hilo.


RIPOTI ZA POLISI

Ilikuwa kitendawili kikubwa kwa kuwa ripoti ya kwanza ilisema kuwa alitumbukia bondeni kwa kukosa kulimiliki gari kutokana na spidi, lakini ripoti ya hospitali inasema alipigwa risasi ya kichwa kabla ya kutumbukia kwenye korongo na kwa kuwa kioo cha gari hiyo hakikuwa na tundu la risasi ikabainika kuwa mpigaji wa risasi hiyo alikuwa ndani ya Gari hiyo kisha akashuka na kulisukuma gari kwenye Korongo.

Uchunguzi pia ulibaini kuwa bastola aina ya Wesson 45 Calibre ilipatikana mita chache kutoka ilipookotwa gari ya Willie, lakini hakukuwa na alama zozote za vidole kwenye bastola hiyo jambo lililofanya isitumike kama ushahidi katika upelelezi wa kesi hiyo.

TUKIO SIKU YA KIFO CHA WILLIE.

Siku ya Kifo cha Willie ambacho kilikuwa ni gumzo kilifuatiwa na tukio la Wanasiasa wawili maarufu na wabunge wa Chama Cha Ulster Unionist kujiuzulu, Ulster ni Chama ambacho kilikuwa kinapingana na harakati za WILLIE. Kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa ni Decoy..,kuwaondoa wananchi katika mjadala wa kifo cha WILLIE.

‘’NCHI zingine Duniani Serikali zina Mafia lakini TANZANIA mafia wana Serikali..” Dr Slaa Nov,2009 on response to Richmond Scandal’s.

R.I.P Mtanganyika Rev. Christopher Mtikila…Hivyo ndivyo ulivyo mwisho wa wanaharakati wa kweli duniani.
Namna hii ndio ulikuwa mwisho wa;
@ Kassi Manlan wa Burundi – 2001
@ Clement Oumarou wa Burkinafaso – 1991
@ Abdelkader Hachani wa Algeria – 1999
@ Rev. Emile Biayenda wa Congo – 1977
@ John Kaiser wa Kenya – 2000
@ Carlos Cardoso wa Msumbiji – 2000
@ Dian Fossey wa Rwanda – 1985

Na pia ulitanguliwa na Rev Janani Luwum wa Uganda mwaka 1977...na hakika wapo watakaofuata baada yao…
Mahitaji yaliyopo ni kuondoa Ccm madarakani hayo mengine nenda kwenye msiba wa mtikila nyumbani kwake kamwambie mkewe
 
Ninachojua mimi ni kwamba baada ya kumsaliti yesu na kuchukua mihela ya mafarisayo Yuda Iskariot alijinyonga.
 
Mahitaji yaliyopo ni kuondoa Ccm madarakani hayo mengine nenda kwenye msiba wa mtikila nyumbani kwake kamwambie mkewe
Hata ikiwa kuiondoa CCM ndio Ultimate goal but not on this expenses...KARMA
 
Watanzani wanafki sana. Na mungu atazidi kutugonga kichwani mpaka tukae sawa. Alivyokuaanamwita binadamu mwenzake maiti kanakwamba yeye anamkataba na mungu watu waliona sawa. Ila si sawa kabisa. Kupewa vihela kidogo na ccm tu kajiona mungu mtu. Na hii naina sana kwa ccm wengi na watoto wao.
 
Ukiangalia picha kwa makini unaweza kuona logic ya mleta mada kwa ajali ile sioni kweli gari kubigirika mara kadhaa zaidi kupinduka mara moja tu kwa hivyo siyo ajali ya kuuwa provided wapo kwenye good health labda shocks tu lakini kusema majeraha ndio yamepelekea kifo hizo evidence hazipo.

Watu wafanye kazi zao tupewe majibu lakini sioni motive za Lowassa pia kushiriki kama ni shutuma huyu keshazizoea na azimnyimi usingizi katika safari yake ya kitapeli. However kuna watu ni waoga kwa sasa ni wapambe wa CDM na kuna raisi jirani ni coward asiyependa kupata negative publicity even if it the information is nothing new and unharmful to his status.
 
hivi ajali inapokutokea unaweza kuwa na nafasi ya kuomba ufe kwa style ipi!!!?
jamani tumwogope Mungu. kufa hakuchagui
 
Kutokana na ripoti ya polisi kuhusu kilichosababisha kifo cha mtikila, nimeona ni mkanda tu ndio uliosababisha kifo chake, kama angevaa asingekufa.
Kwa sababu Gari yake haikubonyea body katika picha japo ilikua kasi ikaacha barabara mita 125 na kumtupa nje mtikila kupitia kioo cha mbele, itakua aligonga kichwa. Kuna eneo dogo la pembeni mbele ndio limebanduka rangi na kwa ripoti iliyotolewa, Gari hiyo ilihusika katika ajali ya kugonga magari mawili huko njombe Jana yake na kuambiwa afanye matengenezo ambayo hakufanya. Sijui lilipinduka mara ngapi na uharibifu upi lilitoka nao ajali za njombe na upi ajali ya chalinze, lakini the car was real durable, ndio maana wale wengine walipona na mikanda yao
Source :global publisher
 
Labda alilala halafu mkanda wake ukajichomoa labda? Au sijui ukachomolewa labda sijui na nani sasa? Au naota?
 
Source: global publisher!!! Ndiyo source??!
 
labda alikuwa anawaa kumpeleka lowasa mahakamani akasahau mkanda akafia ndotoni kumzuia lowasa asiapishwe, ameacha ujumbe mzito kwa nape.
 
Labda alilala halafu mkanda wake ukajichomoa labda? Au sijui ukachomolewa labda sijui na nani sasa? Au naota?


Jina lako limetosha kunijibu. Manake unajiuliza mwenyewe unajijibu mwenyewe.
 
Mods bana..... Ile taarifa ya polisi wanaitoa ila hii ya global mpaka sasa bado ipo tu..... Aisee, whats wrong na hawa watu wakuu
 
Kutokana na ripoti ya polisi kuhusu kilichosababisha kifo cha mtikila, nimeona ni mkanda tu ndio uliosababisha kifo chake, kama angevaa asingekufa.
Kwa sababu Gari yake haikubonyea body katika picha japo ilikua kasi ikaacha barabara mita 125 na kumtupa nje mtikila kupitia kioo cha mbele, itakua aligonga kichwa. Kuna eneo dogo la pembeni mbele ndio limebanduka rangi na kwa ripoti iliyotolewa, Gari hiyo ilihusika katika ajali ya kugonga magari mawili huko njombe Jana yake na kuambiwa afanye matengenezo ambayo hakufanya. Sijui lilipinduka mara ngapi na uharibifu upi lilitoka nao ajali za njombe na upi ajali ya chalinze, lakini the car was real durable, ndio maana wale wengine walipona na mikanda yao
Source :global publisher
Inaonekana unajua mengi.!
 
Marehemu alipewa kazi wiki iliyopita na ccm akaifanya mpaka kazi ikamfanyia..ccm sasa wanamfanyizia propagandb.
 
Back
Top Bottom