Maswali tata kifo cha Mchungaji Mtikila

Maswali tata kifo cha Mchungaji Mtikila

Taarifa imetoka lakini kwa kuwa kulikua na utata, the report must be informative and descriptive. Mfano Gari lilihusika na ajali Jana njombe na lilikua na uharibifu, state upi? Uharibifu ulioongezeka upi? Gari lilipinduka mara ngapi? That it, a report is meant to inform and resolve doubts
 
AJALI Mambo matano ya kuyafahamu kuhusu Kifo cha Mchungaji Christopher Mtikila .. (RIP)

October 05 2015 ni siku ya pili inaisha tangu litokee tukio la ajali ya gari ndogo katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze Mkoa wa Pwani ambapo ndani yake kulikuwa na watu watatu pamoja na Mwanasiasa Mkongwe Tanzania, Mchungaji Christopher Mtikila-ambaye alifariki kutokana na ajali hiyo.

Tangu kutokea kwa ajali hiyo mambo mengi yameongelewa kuhusu ajali na kifo chake, mazingira ya ajali? Marehemu kutokuwa na jeraha? Mchungaji kufariki na wengine kupona? Ripoti ya Hospitali? Mazishi?

Familia ya Mchungaji Mtikila imeweka kila kitu sawa >>>> “Mchungaji Christopher Mtikila alipata ajali majira ya saa 11 Alfajiri eneo la Msolwa Chalinze, bahati mbaya alikuwa hajafunga mkanda na gari ilikuwa speed… Kulikuwa na gari llilikuwa lime-overtake upande wao, dereva wao akakwepa kwenda kushoto“.–-Victor James Manyai, Msemaji wa Familia.

Victor James Manyai, Msemaji wa Familia.

Hapa Msemaji wa Familia anasimulia mazingira ya ajali ilivyokuwa >>> “Eneo lile barabara imeinuliwa juu zaidi na eneo la pembeni limeshuka chini.. gari lilipaa juu, liliposhuka chini matairi yakapasuka yote, kwa sababu hakuwa amevaa mkanda akatokea mbele ya kioo cha gari.. alipoenda kuangukia, gari likaenda kumfunika upande wa kushoto, akawa hawezi kupumua“.--Victor Manyai.

Watu wengine walitoka na Majeraha kwenye gari, nini kilifanya Mchungaji afariki pekeyake? >>> “Ilichukua muda kwa sababu walikuwa watu wanne, mmoja alikuwa ameumia zaidi, mwingine alitupwa mbali… ilibidi mpaka wasamalia wema waje kusaidia kumuinua… walijaribu kumsaidia lakini hakuweza kupumua tena“.

Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani.

Kuna stori kwenye Mitandao ya Kijamii kuhusu kifo chake huku wengine wakihoji kwa nini mwili wa Mchungaji Mtikila haujaonekana kuwa na majeraha yoyote? >>> “Mimi nilikuwepo katika Kikosi cha watu waliofanya postmortem pale Kibaha, tulikuwa na madaktari wanne, madaktari wawili wa Familia, mmoja wa Polisi na mmoja wa Hospitali ya Kibaha… sio kweli kwamba hana majeraha, alikuwa na majeraha kichwani na miguuni, ila siwezi kutaja siri za Marehemu ni kinyume cha maadili...-Ukweli ni kwamba alikosa hewa, na kama kungekuwa na msaada wa dharura maisha yake yangeokolewa…“>>>

Mke wa Marehemu Mchungaji Mtikila.

Gari alilopata nalo ajali je? >>> “Ukweli ni kwamba gari lilikuwa limekodiwa, Mchungaji alikuwa na magari mawili na yote yalikuwa katika Kampeni Mkoa wa Mara na jingine Wilaya ya Kahama… Mimi ndio nilimkodia gari kwa madereva wa Taxi Mbezi mwisho, ni vijana ambao nawafahamu.” >>>

Hii ndio Taarifa ya Familia kuhusu taratibu za kuaga Mwili wa marehemu na Mazishi >>> “Mwili wa Marehemu kwa sasa upo Hospitali ya Lugalo, Jumatano tutaaga mwili wa Marehemu Karimjee au Leaders Club, baada ya hapo tutasafirisha mwili kwenda Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe” >>> Victor James Manyai, Msemaji wa familia
 
Huyu mtu alichezea moto wa Maziwa Makuu. Usinyooshe kidole popote, maana wale jamaa wanajua sana haya mambo, na kila siku wanabuni mbinu mpya. Wakati mwafaka walijua TISS watakuwa wanashughulika kufukuzana na wapinzani!
 
Mambo ya kimbea achene sikilizeni ukweli ni huu.

[JFMP3]https://www.hulkshare.com/millardayo__/oct-5-2015-link-1-amplifaya-mtikila-family[/JFMP3]
ALWATAN KIZIGO
 
Last edited by a moderator:
1. Gari yake haijaharibika kabisa na tunaaambiwa iliacha njia na kupinduka tunajua sababu kubwa ya magari kuacha njia ni kupasuka kwa matairi lakini hili gari la Mchungaji Mtikila hakuna tairi liliposuka. Sasa tuambiwe sababu ya kuacha njia na kupinduka ni nini?

2. Mchungaji Mtikila hana alipoumia au kubleed damu.(Labda iwe kafa kwa mshtuko wa moyo au internal wounds. Kwenye picha anaoekana hajaumia hata kidogo hata nguo alivozavaa zikiwa hazijachanika hata kidogo.Sasa tuambiwe sababu gani nyingine iliyopelekea kifo chake?

3.Tunaambiwa ajali alipata SAA 11 alfajiri Chalinze kwaa asili ya eneo la Chalinze ni eneo bize sana kwanini picha iliyosambaa inaonesha ni asubuhi kabisa kumekucha ina maana ajali yake haikushtukiwa na watumiaji wengine wa Barabara mpaka asubuhi.

Angalizo sijamlaumu mtu yeyote kwenye hii ajali ila ni maswali ambayo nilikuwa najiulza binafsi sasa nawaomba msichafue hali ya hewa.
1-Kama ilikuwa imara ndo asife,je alimofia hayati Sokoine haikuwa imara kama hii ya jamaaako?
2-Je kwa uelewa wako kinachoua ni ajali au Mungu?
3-Je Dk Omar aliyekuwa makamu wa rais alifariki akiwa kitandani tena usingizini hilo nalo tuliwekeje au uliona kitanda chake hakikuwa imara na alikuwa na michubuko?

Imagine, nyie wanaume kuna mtu anasafiri long trip kavaa suit kwenye gari dogo?

Hard to believe. I have a feeling he was dead before the "accident".
 
Nae mtikila alikuwa hachangii amani ya nchi, mara azushe sijui askofu kamshika nyuma, alijisahau sana.
 
Imagine, nyie wanaume kuna mtu anasafiri long trip kavaa suit kwenye gari dogo?

Hard to believe. I have a feeling he was dead before the "accident".
Faizafoxy
1-ninachojaribu kufikiria mimi je hili gari lilikuwa na hadhi /uimara wa kukodiwa kwenda safari ndefu kiasi hicho kwa mtu wa aina hiyo?
2-Je alifanya hiyo mikutano huko njombe kama inavyoelezwa kwenye sababu ya safari hiyo?Hebu wana Njombe mtuambie.
3-Mbona ni muda mfupi sana kwa kampeni kwa umbali huo ..maana tunaambiwa ni cku moja ya pili kageuza.
4-Je gari iliyosababisha ajali kuyagonga magari mengine huko njombe kesi ilimalizwaje kwa muda mfupi kiasi hicho na dereva akaruhusiwa kuondoka na gari kurudi dar?Dereva alisababish ajali pia leseni yake inaweza kuzuiliwa kwa muda je huyu ilikuwaje?(ref police statements)
 
Kuna siku Lowassa alinyoosha mkono na kusema People's, walianguka na kuzirai Wanachama wetu wa CCM tuliowalepeka kusikiliza na kupiga picha iwapo ataanguka. Jamaa si mtu, amini usiamini.
 
ALWATAN KIZIGO

Muuaji wake anajulikana, hivi karibuni amemshambulia sana na akasema hafai kwenda Ikulu. Huyo huyo muuaji ndiye aliyetuma watu kumvamia Humphrey Polepole nyumbani kwake Mbezi beach.

Hivi huwa unajaribu kushirikisha ubongo wako kabla ya kuchangia?! Mdomo huponza kichwa we jitie uchizi tu.
 
Last edited by a moderator:
Kila ajali ni tofauti... Hazinaga formula maalum..!!

RIP Rev. Mtikila..!
 
1. Gari yake haijaharibika kabisa na tunaaambiwa iliacha njia na kupinduka tunajua sababu kubwa ya magari kuacha njia ni kupasuka kwa matairi lakini hili gari la Mchungaji Mtikila hakuna tairi liliposuka. Sasa tuambiwe sababu ya kuacha njia na kupinduka ni nini?

2. Mchungaji Mtikila hana alipoumia au kubleed damu.(Labda iwe kafa kwa mshtuko wa moyo au internal wounds. Kwenye picha anaoekana hajaumia hata kidogo hata nguo alivozavaa zikiwa hazijachanika hata kidogo.Sasa tuambiwe sababu gani nyingine iliyopelekea kifo chake?

3.Tunaambiwa ajali alipata SAA 11 alfajiri Chalinze kwaa asili ya eneo la Chalinze ni eneo bize sana kwanini picha iliyosambaa inaonesha ni asubuhi kabisa kumekucha ina maana ajali yake haikushtukiwa na watumiaji wengine wa Barabara mpaka asubuhi.

Angalizo sijamlaumu mtu yeyote kwenye hii ajali ila ni maswali ambayo nilikuwa najiulza binafsi sasa nawaomba msichafue hali ya hewa.

View attachment 294725

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
[h=3]Taarifa ya Jeshi la Polisi Kuhusu Kifo cha Mchungaji Mtikila[/h]

Mpekuzi blog

Mnamo tarehe 04/10/2015 majira ya saa 05:45hrs huko Msolwa Kata ya Bwilingu barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro, Wilaya ya Ki-Polisi Chalinze, Mkoa wa Pwani, Gari No. T.189 AGM aina ya Toyota Corolla likiendeshwa na George Steven Ponera miaka 31, mkazi wa Mbezi Mwisho Dar es Salaam liliacha barabara kisha kupinduka na kusababisha kifo cha Christopher Mtikila miaka 62, mpangwa, mchungaji wa Kanisa la Assemblies, na mwenyekiti wa Chama cha siasa DP mkazi wa Kinondoni “B” Dar Salaam.

Katika ajali hiyo, watu watatu waliokuwamo ndani ya gari hilo na marehemu Mchungaji Mtikila walijeruhiwa ambao ni Ally Mohamed miaka 42 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, yeye alipata maumivu shingo, mabegani na kifuani, mwengine ni Patrick Mgaya miaka 37 ambaye ni mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God mkazi wa Mbagala Dar es Salaam ambaye alikuwa na michubuko midogo usoni na kuumia kichwani, pamoja na George Steven miaka 31 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam ambaye alipata michubuko kidogo eneo la mabegani.

Majeruhi wote walipatiwa matibabu katika Kituo cha afya Chalinze na badae wawili kati yao katika Hospitali teule ya Tumbi na waliruhusiwa kutokana na hali zao kuendelea vizuri.

Baada ya kutokea kwa hiyo ajali, timu maalum ilifika katika eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji wa ajali hiyo ikiongozwa na Mkuu wa utawala wa Traffic kuu Dar es Salaam SACP J. Kahatano, pamoja na mimi mwenyewe, Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Pwani na kuwashirikisha wataalamu wa Forensic Makao Makuu ya Polisi ACP Kashindye na Dokta A. Makata.

Uchunguzi wa mwili wa marehemu tayari umefanyika, na taarifa ya Daktari aliyefanya uchunguzi huo katika Hospitali ya Rufaa tumbi Kibaha tarehe 04/10/2015 umeonyesha kuwa, kifo cha marehemu kimesababishwa na kuvunjika kwa mbavu nane (8) upande wa kushoto na kuingia kwa damu kwenye mfumo wa hewa na kusababisha kushindwa kupumua.

Kabla ya ajali hiyo kutokea marehemu na wenzake tarehe 02/10/2015 jioni waliondoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa Njombe na kufika tarehe 03/10/2015 alfajiri kwa ajili ya kampeni za Chama chao cha DP. Wakiwa huko walipata ajali kwa kugonga magari mawili yaliyopata ajali na kusababisha uharibifu wa gari lao.

Kulingana na taarifa ya Mkaguzi wa magari ya tarehe 03/10/2015 huko Njombe walishauriwa walitengeneze kwanza kabla ya kulitumia tena.

Tarehe 03/10/2015 saa 21:30hrs waliondoka Njombe kwenda Dar es Salaam na ilipofika saa 05:45hrs katika eneo la Msolwa ndipo wakapata ajali hii.

Uchunguzi uliofanywa kwa kukagua tukio na kuwahoji majeruhi walionusurika (katika eneo hilo hakuna watu wengine walioshuhudia tukio hilo kwa kuwa si eneo la makazi ya watu, ni mbuga). Ajali hii imeonyesha kuwa imesababishwa na sababu zifuatazo:

  1. Mwendo kasi, dereva mwenyewe anakubali kwamba alikuwa mwendo kasi licha ya kuwepo kwa alama zinazooonyesha kwenda mwendo wa Km 50 kwa saa. Aidha baada ya kuacha barabara kuu, gari hilo lilikwenda umbali wa mita 125 kabla ya kupinduka hali inayoashiria kuwa lilikuwa kwenye mwendo kasi.
  2. Uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu kwa kuendesha gari mchana na usiku kucha kabla ya kuanza safari walikuwa wakishughulikia matengenezo ya gari hilo ambapo hakupata muda wa kupumzika.
  3. Kutofunga mkanda ya usalama. Katika uchunguzi inaonyesha marehemu hakufunga mkanda kwa kuwa alirushwa nje kupitia kioo cha mbele (wind screen).
  4. Ubovu wa gari. Gari hilo lilipata ajali tarehe 03/10/2015 na moja ya sehemu muhimu iliyoharibika ni mfumo wa usukana (steering system) yawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia kutokea kwa ajali hiyo.
Hivyo nitumie fursa hii kuwaomba wananchi kuwafichua maderva wanaokwenda mwendo kasi kupitia namba 08007575 ama 0715 009953 au 0658 376012. Aidha niwatake madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kwa wale watakao kaidi Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani hatutasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengi.

Asanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani

Kamishina Msaidizi Jafari Ibrahim.

Jamani tufike Mahala tuache vyombo husika vitoe majibu ya nini kilichotokea kwenye ajali hii kuliko kuanza kutengeneza majibu yasiyo na ushahidi na yenye lengo la kuleta uchonganishi wa kijamiii. Haya angalieni sasa majibu ya Dakitari na Polisi wenye taaluma zao.
 
AJALI Mambo matano ya kuyafahamu kuhusu Kifo cha Mchungaji Christopher Mtikila .. (RIP)

October 05 2015 ni siku ya pili inaisha tangu litokee tukio la ajali ya gari ndogo katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze Mkoa wa Pwani ambapo ndani yake kulikuwa na watu watatu pamoja na Mwanasiasa Mkongwe Tanzania, Mchungaji Christopher Mtikila-ambaye alifariki kutokana na ajali hiyo.

Tangu kutokea kwa ajali hiyo mambo mengi yameongelewa kuhusu ajali na kifo chake, mazingira ya ajali? Marehemu kutokuwa na jeraha? Mchungaji kufariki na wengine kupona? Ripoti ya Hospitali? Mazishi?

Familia ya Mchungaji Mtikila imeweka kila kitu sawa >>>> “Mchungaji Christopher Mtikila alipata ajali majira ya saa 11 Alfajiri eneo la Msolwa Chalinze, bahati mbaya alikuwa hajafunga mkanda na gari ilikuwa speed… Kulikuwa na gari llilikuwa lime-overtake upande wao, dereva wao akakwepa kwenda kushoto“.–-Victor James Manyai, Msemaji wa Familia.

Victor James Manyai, Msemaji wa Familia.

Hapa Msemaji wa Familia anasimulia mazingira ya ajali ilivyokuwa >>> “Eneo lile barabara imeinuliwa juu zaidi na eneo la pembeni limeshuka chini.. gari lilipaa juu, liliposhuka chini matairi yakapasuka yote, kwa sababu hakuwa amevaa mkanda akatokea mbele ya kioo cha gari.. alipoenda kuangukia, gari likaenda kumfunika upande wa kushoto, akawa hawezi kupumua“.--Victor Manyai.

Watu wengine walitoka na Majeraha kwenye gari, nini kilifanya Mchungaji afariki pekeyake? >>> “Ilichukua muda kwa sababu walikuwa watu wanne, mmoja alikuwa ameumia zaidi, mwingine alitupwa mbali… ilibidi mpaka wasamalia wema waje kusaidia kumuinua… walijaribu kumsaidia lakini hakuweza kupumua tena“.

Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani.

Kuna stori kwenye Mitandao ya Kijamii kuhusu kifo chake huku wengine wakihoji kwa nini mwili wa Mchungaji Mtikila haujaonekana kuwa na majeraha yoyote? >>> “Mimi nilikuwepo katika Kikosi cha watu waliofanya postmortem pale Kibaha, tulikuwa na madaktari wanne, madaktari wawili wa Familia, mmoja wa Polisi na mmoja wa Hospitali ya Kibaha… sio kweli kwamba hana majeraha, alikuwa na majeraha kichwani na miguuni, ila siwezi kutaja siri za Marehemu ni kinyume cha maadili...-Ukweli ni kwamba alikosa hewa, na kama kungekuwa na msaada wa dharura maisha yake yangeokolewa…“>>>

Mke wa Marehemu Mchungaji Mtikila.

Gari alilopata nalo ajali je? >>> “Ukweli ni kwamba gari lilikuwa limekodiwa, Mchungaji alikuwa na magari mawili na yote yalikuwa katika Kampeni Mkoa wa Mara na jingine Wilaya ya Kahama… Mimi ndio nilimkodia gari kwa madereva wa Taxi Mbezi mwisho, ni vijana ambao nawafahamu.” >>>

Hii ndio Taarifa ya Familia kuhusu taratibu za kuaga Mwili wa marehemu na Mazishi >>> “Mwili wa Marehemu kwa sasa upo Hospitali ya Lugalo, Jumatano tutaaga mwili wa Marehemu Karimjee au Leaders Club, baada ya hapo tutasafirisha mwili kwenda Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe” >>> Victor James Manyai, Msemaji wa familia

Taarifa ya familia inakinzana na ya polisi...mfano wamesema kuna wasamalia walikuja kuwasaidia...polisi wanasema eneo la tukio halina makazi ya watu ndio maana wahanga walikutwa peke yao bila mashuhuda.....fuatilieni what opposition parties are saying in Rwanda abt this death...hiyo siyo issue ya tz pekee kwa sasa..ni cross border issue
 
Back
Top Bottom