Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
KILICHOTOKEA KWENYE HII AJALI
Hilo eneo lina makunyanzi ya kufa mtu barabarani kwa zaidi ya kilometa kadhaa. Ilikuwa ni alfajiri yenye giza na gari lilikuwa mwendo kasi kwa zaidi ya km 120 kwa saa. Ile gari ni saloon ya kawaida 'small size' na suspension system yake ni kwa barabara za Tokyo sio hiyo iliyodidimia kwa 'axe load inbalance' na low quality bedding.
Walikuwa wanapishana na Lorry, Lorry lilikuwa likiyumbishwa na hayo makunyanzi, dereva hakuona vizuri kwa kuwa Lorry lilikuwa limewasha full light. Na dereva wa ki saloon hakutumia tahadhari ya kupunguza mwendo akaja hivyo hivyo na spidi zake. Kashaambiwa tunawahi ibada na lazima tufike saa by saa mbili jeshi la wokovu.
Aliposhtukia Lorry hili hapa linahama 'lane' kwa kuyumbishwa na hayo makunyanzi ya barabarani akajaribu kukata kushoto ili kukwepa, tairi za kushoto zikapanda kunyanzi mstari( gema) gari ikaserereka na ikatoka mshazari hadi nje na kupinduka.
Dereva wa Lorry kaendelea na safari zake na hata hajui nini kimetokea nyuma yake japo vishindo vingeweza kumshtua.
Kufa ajalini kuna mengi, zile pilika pilika za kupinduka kuna mshtuko, majeraha, umri, mambo ya ufahamu hasa kama ulikuwa usingizini na 'mind' yako ilihama, kuna maamuzi ya Mola n.k, n.k
Onyo;
Hizo ni hisia zangu tu.
Ufafanuzi mzuri sana.
Mwakajuzi nikiwa likizoni homeland Tanzania, nilikuwa na safari ya dharura toka Dar kwenda Morogoro na kurudi siku hiyo hiyo kuwahi jioni yake kupanda ndege kurudi ninakoishi.
Niliondoka Alfajiri sana Dar kama saa kumi na moja, ukweli usumbufu wa kipekee niliopata ni yale makunyazi na mibonyeo ya low quality ya barabara alizosimamia Mafuguli.
Kuna sehemu nilipishana na basi la abiria wa mikoani HOOD LIMITED baada ya kuvuka tu lile daraja la Reli baada ya Mto Ruvu kuelekea Morogoro alimanusura nipinduke na kagari nilikoendesha, nilichepuka kulipa site bus nikafikiri barabara za Obama, oh my goodness, niliyumba na bahati nilipunguza speed.
Ajali nyingi huchangiwa na quality mbaya ya barabara anazojisifia Magufuli.