Maswali tata kifo cha Mchungaji Mtikila

Maswali tata kifo cha Mchungaji Mtikila

We acha uongo..nimepita na Machame inayoelekea Kondoa asubuhi wakati askari wanapima hata kabla mwili haujaondolewa.majeraha anayo kichwani na gari kwa mbele hasa upande wa kulia iko nyan'ga so tumia akili kujiuliza hayo maswali na si kutumia unazi wa chama unachoshabikia.

Acha uchapati ndugu..tujiepushe na uzushi wa hisia zitakazoathiri amani ya Taifa.Bw alitoa na ametwaa, Inalilah wa inalilah rajuim.

Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake na kumpa pumziko la kheri huko aliko.
 
Du tunapoelekea ni kubaya sana,sasa kama MTU kapata ajali na kufa ni kipi cha kushangaza hapo?au yeye ndio Wa kwanza kupata ajali na kufa?mawazo ya kishirikina mlio nayo hayatawasaidia chochote Watu mmegeuka kuwa mashahidi Wa kitu ambacho hamjakishuhudia,kuweni wastaarabu Mungu hadhihakiwi
 
Mazingira ya kifo cha Mchungaji Mtikila bado kinatia shaka kuu mbele ya jamii na nachelea kusema huyu Mzee ameuawa na genge la mafisadi ili wafanikiwe kisiasa kwani Mtikila alikuwa ameshakusanya vielelezo vyote vya kuwashughulikia.


1. Jeshi la Polisi Watanzania tunaomba mtusaidie kumuhoji kwa kina huyu mtu anaeitwa Mchungaji Patrick Mgaya. Huyu alikuwa ni mmoja wa waliopata ajali pamoja na marehemu Mtikila. Ikumbukwe kuwa Magaya ni mmoja wa mashabiki muhimu sana wa Mgombea Urais kupitia Ukawa ndg Edward Lowassa.Taarifa za siri zinasema kuwa Mchungaji Mgaya na Mchungaji Mtikila walikutana takribani mwezi mmoja uliopita tu na kwamba kuna wasiwasi kuwa alipewa kazi maaluum ya kuhahakisha amamuua Mtikila.


Taarifa kutoka nyumbani kwa marehemu zinasema kuwa Mchungaji Mtikila akiwa na Mchungaji Patrick Mgaya walianza safari siku ya Ijumaa jioni kwenda mkoani Njombe ambapo waliambatana na madereva wawili ambao Mchungaji Mtikila hakuwafahamu. Aliewafahamu watu hawa wote ni Mchungaji Magaya ambae ndie aliekodisha gari waliokwenda nayo Njombe kupitia kwa Ndg Victor James Manyii ambaye mbali ya kutoa gari aliyokodisha pia alitoa madereva wawili ambao pamoja na Mchungaji Mgaya wao hawakufa isipokuwa Mchungaji Mtikila pekee.


Ajali hii imeacha maswali mengi kuliko majibu. Kwa mfano ukiangalia shingo ya marehemu Mtikila utaona kuna kitu kama kamba ambayo inaweza kuleta tafsiri kuwa ilitumika kumnyonga marehemu. Pili, kwanini mwili wa marehemu hauna hata kovu wala mchirizi wowote wa damu? Je, ni nani alimpiga picha Marehemu Mtikila? Je, Patrick Mgaya ni nani? Kabla kuwa mchungaji alikuwa anafanyakazi gani? Je gari lile lilipinduka lenyewe au liligongwa? Na kama lilipinduka ni kwanini liharibike eneo la mbele pekee?Je Ni chombo gani kilikuwa cha kwanza kumpiga picha na kusambaza kwenye mitandao?


Patrick Mgaya alipopiga simu nyumbani kwa marehemu alisema wamepata ajali na kwamba kulikuwa na majeruhi wengi sana akamaliza kwa kusema mtuombee kisha akakata simu, je, hao majeruhi wengi ni akina nani? Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama muhojini Mchungaji Patrick Mgaya maana zipo dalili kuwa kuna mengi anayoyafahamu kuhusu tukio hili. Pia fuatilieni uhusiano uliopo kati ya Rais Paul Kagame, Patrick Mgaya na EADWARD LOWASSA. Pia nashauri Jeshi la Polisi kumuhoji mtu anaeitwa Dr. Jean Bosco Ngendahimana ambae anaishi nyumbani kwa marehemu pale Mikocheni.

Wale wote wenye misimo thabiti juu ya kuchukia Rushwa na Ufisadi wachukue tahadhari. Nasema hivyo sababu Humphrey Polepole alivamiwa nyumbani kwake Mbezi na Dkt. SLAA anapokea sms za vitisho. Vyombo vya dola viwe macho.
 
KATIKA SOMO LA MANTIKI...LOGIG!! Waafrika wanaishia kuwa wachawi kwa sababu ya kutengeneze hitimisho kwa vigezo (premises) moja tu, au kuunganisha matukio yasiyo na uhusiano katika kufikia sababu ya tukio

Mfano: MAMA MJA MZITO ASILE MAYAI... ATAZAA MTOTO HANA NYWELE!!
Mfano: MTIKILA ALIMSEMA .. KUWA MGONJWA... MTIKILA KAFA KWA AJALI... KWA HIYO KASABABISHA...

Huu ndio ushirikina wa fikra!!!! subiri wataalam watoe maelezo ya kitaalam. picha tu inakufanya kuandika haya yote!!!
 
Majibu rahisi,

1. Sio lazima gari ilopinduka ipasue tairi. Ninahakika ww sio dereva mzoefu.

2. Kuumia ndani ni hatari kuliko kidonda nje. Biology yako naona ndogo tu, autopsy itajibu zaidi.

3. Chalinze mida hio ni bize maroli ya mkoa nani anamuda wa kutumbua macho asiangalie usalama wake? Jee marehemu alitoa tangazo kwamba wajiandae anataka kupata ajari? Ajali ni nusu ya sekunde tu sio slow motion za transporter.

4. Usianzishe utata.

Pangu Pakavu
 
Assumption zako ndizo zinazua hayo maswali.

Gari kupinduka si lazima lipasuke tairi, yaweza mwendo mkali na dereva kutokuwa makini ikasababisha. Kumbuka ilikuwa alfajiri na sijui walitokea wapi lakini kuna uwezekano kabisa dereva alikuwa amelala au kachoka.

Kwamba hana jeraha siyo sababu ya msingi kwa hakika mtu anayepata ajari na kuonekana hakuumia (kwa maana yamajeraha dhairi) huyo ndiyo anakuwa kwenye hatari zaidi.

Msianze kueneza uzushi na kuutumia kisiasa.
 
Harafu mleta bandiko unasema "tuambiwe"muambiwe na nani sasa?
 
Kupuuzia haya au kuchukulia serious both have same magnitude but in different directions!
 
Mtikila alikuwa mbioni kuwaburuza Edward Lowassa na Freeman Mbowe mahakamani. Likiwemo suala la mauaji ya Chacha Wangwe. Mtakumbuka Wangwe naye alikufa kwa staili hiyo hiyo pale alipopingana na Mbowe

Kwa akili yako unataka kutuambia nini...tanzania tumepata vi techno kila mtu anazoza tu
 
Yule mzee wa kujinyea ni mshirikina sana, huyo mzee wa kunya kwenye nguo ndio amefanya haya yote na kumuua Mtikila. Mara nyingi sana ajali kama hizi huwa ni za kishirikina tu. Mzee wa kujinyea ni hatari sana, lakini mimi simuogopi ng'ooo wala siogopi kufa. Inasemekana hata watu wanaomshabikia wamepumbazwa akili kishirikina.

Haya maelezo yako utaenda kuyathibitisha polisi soon, just wait..!
 
Ni kweli ameuwawa! Na matamshi ya kinywa chake, kuwakejeli wanadamu wenzie kuwa ni wagonjwa hivyo hawawezi kitu, sasa ametangulia yeye akawaacha wale aliowadhania kuwa ni wagonjwa hawawezi kitu!

Mtikila died natural death, Karma did it!
 
Mleta mada inaonekana na wewe unacho kitu cha kuisaidia Polisi, nawe ukamatwe uisaidie Polisi.
 
Ile ilokuwa shingoni kwanza siyo Kamba ni TIE ya Marehemu,,walimfunga ili kumstri mdomo wake ulokuwa wazi,, Halafu unaposema mafisadi wamemuua,,sababu alikuwa na ushahidi wa kwenda kuwafungulia kesi mahakamani,,HIVI SERKALI ILISHINDWA KUWAFUNGULIA KESI HAO MAFISADI MPAKA IKASUBRI MTIKILA? PILI MAREHEMU MTIKILA KESI NI KAWAIDA YAKE,,ALIPENDA SANA KUFUNGUA FUNGUA KESI MAHAKAMANI ENZI ZA UHAI WAKE..SO SI AJABU ALIPOSEMA ATAFUNGUA KESI MAHAKAMANI..ACheni Mungu afanye kazi yake ,,mnaweweseka na nini?
 
Back
Top Bottom