Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Khaa!! Mama Anna Tibaijuka, mji mpya wa Kibamba umeishia wapi? Mie mnanishangaza kuanzisha mji mpya lazima muanzishe kwenye maeneo ambayo tayari ni makazi ya watu?? Tanzania tumejaaliwa maeneo mengi ambayo kuyaendeleza hayahitaji kiasi kikubwa cha kulipa kama fidia. Tatizo letu kuu ni kwamba Masaveyors wazuri ni wanasiasa, Maplanner wazuri ni wanasiasa hata Maengineers ni wanasiasa. Siasa, Siasa, Siasa kila mahali. Hebu tupumzike kidogo muwasikilize na wataalam nao wanasemaje. Siku hizi hata amri ya kuvunja jengo linalohatarisha maisha ya binadamu lazima itoke kwa Mwanasiasa:heh:
 
Leading from behind.

Waziri badala ya kutuambia mipango yake ni ipi na kashatekeleza ipi na anahitaji maoni wapi, anatupa li post la Singapore lisilo na kichwa wala mguu, full of generalities, no exactitude or specificity.

Sasa mimi nikikwambia New York City kuna underground train (subway) ndo itakusaidiaje wewe bongo ambaye rapid transit lanes na taa za barabarani zinakupiga chenga?

Na huyu ndo Ph.D ya ukwee, hao darasa la saba na Ph.D za kununua wakoje?
 
Plan ya Kigamboni nadhani ilikuwepo nilidhani ni suala la utekelezaji au Donor amebadilika?
Maana izi inchi zetu zinazotegemea misaada huchelewi kuta mwekezaji wa kwanza katutelekeza
 
Mama hongera kwa kutujuza. Napenda kutoa mapendekezo machache kwenu mliopewa dhamana kutuongoza katika kipindi hiki:-
1. Ili kuondoa foleno DSM-jengeni reli kutoka bandarini hadi Chalinze na kuhakikisha kuwa Chalinze mnaweka bandari kavu kwa maana ya kuchambua mizigo inayokwenda Mby, Kigali malori ya kubeba mizigo, mafuta yote yaishie Chalinze wala yasiingie mjini
2. Wataalamu wako wa mipango miji wasikae ofisini huku wamefunga tai na AC wanatakiwa kuzunguka katika maeneo ambayo hayajapimwa wawapimie wenyeji wao uza viwanja na mashamba yao ili wanao nunua angalau wakute viwanja vilivyopimwa,
3. Kwa kweli hatuawaelewi mlioko serikalini mnatunia hekima ipi kuachia raslimali zetu kuondoka na wageni wakati bungeni na kwenye wizara zenu mnalalamikia bajeti ndogo.
4. Huo wimbo wa mji mpya wa Kigamboni ni kipaumbele cha nani,kma huko Manzese, Buguruni na kawe tunashindwa kulipia kodi ya elfu 20 Je ukijenga hayo maghorofa ya mji mpya tutaweza kuishi huko kweli au ndo lugha tunayoisikia kuwa Kigamboni imeuzwa?
5. Mama tutashukuru sana ukifunguka utueleze sawasawa maana humu ndani hatuna kanuni kandamizi na miongozo kama ya zamu ya Ndugai na Mama Makinda.

Tafakari!!!!!!!!!!!!!!!
 
Profesa shida ya nchi yetu ni kutokutii sheria zilizopo na kutojali mipango tuliyojiwekea. Inasikitisha kuona miji mingi nchini ikikua kwa kasi-holela...kila mtu anajenga anavyotaka na hakuna mamlaka inayojishughulisha kuzuia hali hiyo.

Kama ulivyosema kupanga ni kuchagua. Nyie mliopewa nafasi ya kusimamia miji yetu ndiyo mnapaswa kuhakikisha sheria zilizopo zinafuatwa na kila raia. Pia wizara yako na halmashauri au manispaa zijitahidi kupima, kuuza na kusimamia uuzaji ardhi hasa za mijini kwa wananchi kuliko kuachia kila mtu auze kiholela hali inayopelekea ujenzi holela kuendelea kuwa tatizo kwenye miji yetu.

alternative mkuu wanaweza kuwasaidia wale wenye mashamba makubwa kuyagawa kuwa viwanja vya makazi kwa kuwatoza kodi na kuwaacha wauze viwanja vyao wenye, kuliko kuachia halimashauli zenye upendeleo kwenye ugawaji waviwanja, KWASASA INAONEKANA KAMA WANANYANG'ANYA MASIKINI VIWANJA NA KUJIMILIKISHA WANASIASA TUU!
 
Mama hongera kwa kutujuza. Napenda kutoa mapendekezo machache kwenu mliopewa dhamana kutuongoza katika kipindi hiki:-
1. Ili kuondoa foleno DSM-jengeni reli kutoka bandarini hadi Chalinze na kuhakikisha kuwa Chalinze mnaweka bandari kavu kwa maana ya kuchambua mizigo inayokwenda Mby, Kigali malori ya kubeba mizigo, mafuta yote yaishie Chalinze wala yasiingie mjini
2. Wataalamu wako wa mipango miji wasikae ofisini huku wamefunga tai na AC wanatakiwa kuzunguka katika maeneo ambayo hayajapimwa wawapimie wenyeji wao uza viwanja na mashamba yao ili wanao nunua angalau wakute viwanja vilivyopimwa,
3. Kwa kweli hatuawaelewi mlioko serikalini mnatunia hekima ipi kuachia raslimali zetu kuondoka na wageni wakati bungeni na kwenye wizara zenu mnalalamikia bajeti ndogo.
4. Huo wimbo wa mji mpya wa Kigamboni ni kipaumbele cha nani,kma huko Manzese, Buguruni na kawe tunashindwa kulipia kodi ya elfu 20 Je ukijenga hayo maghorofa ya mji mpya tutaweza kuishi huko kweli au ndo lugha tunayoisikia kuwa Kigamboni imeuzwa?
5. Mama tutashukuru sana ukifunguka utueleze sawasawa maana humu ndani hatuna kanuni kandamizi na miongozo kama ya zamu ya Ndugai na Mama Makinda.

Tafakari!!!!!!!!!!!!!!!

mKUU HIYONAMBA MBILI SIJUI NIMWAMBIE VIPI HUYU MAMA AIELEWE!?
NI MUHIMU SANA KWAKUZUIA MAKOSA YALEYALE YA MIAKA YOOTE SI KUKAA NA KULALAMIKA TUUU HUKU WENGINE TUKIJENGA MAENEO AMBAYO HAYAJAPIMWA!
 
Ndugu ZOMBA.
Ingawa mama hajaja na sijui atakuja lini kujibu, naomba nitofautiane na wewe kwa baadhi ya muono wako, wa kuhusu makazi. Nitaeleza kwa ujumla kwa sababu ya muda, na kusubiri majibu ya profesa Tibaijuka!
Kwanza naomba tuelewe serikali inauzoefu mkubwa sana, katika mambo mengi sana kuliko mtu/kampuni. Sababu serikali inaweza kuajiri mtaalam, kuandaa, kumsomesha na kumpatia exposure ( mfano ndo hata mama na uprof serikali imempeleka kujionea mambo Singapore) mtaalam yeyote mahili, kama itahitaji kufanya hivyo, Serikali imekuwepo kwa muda wa miaka 50 ( baada ya uhuru) hivyo hatuna mtu amefanya kazi 50 Years, ila kabati la wizara limekuwepo na nina amini uzoefu upo kabatini.
Kuhusu kamapuni binafsi, hapana sababu makazi ni mahitaji muhimu sana kwa binadamu. nakumbuka ni moja ya mambo ambao serikali duniani zinafanyia kazi kila siku. Ukisikia mtikisiko wa uchumi mojawapo ya sababu ni hayo mambo ya makazi. Hivyo ili kila mtu aweze kupata makazi stahili na bora serikali lazima ifanye kazi.
Real estate inahitaji mtaji mkubwa, siyo lelemama, ndo maana nilishauri baadala ya kuanzisha benki 3 kwa mwaka huu wa fedha wangeweza kuanzisha Real estate company, kama vipi NHC ijiunge stock market ipate mtaji mkubwa, then isiuze nyumba bali ipangishe na iboreshwe.
Siyo sehemu zote sekta binfsi imefanikiwa, mifano hai ipo siyo tanzania bali hata nchi jirani. Serikali itoe makazi kwa kupangisha, hapo itapanga mji (miji) na kulinda ukuaji wa uchumi wake.
Serikali itumie watalaam wake waliopo, ipange, isimamie mambo yataenda, sekta binafsi ije kujazilizia pale serikali inaona itahitajika na kufanya bei iwe ya kuangalia gharama halisi.
Hapo mwisho (rangi ya blue) mkuu tayari umeona hapo kuna deal, umejipigia pass mwenyewe, yaani wewe unaweza zaidi kuliko serikali? kazi ipo!!!!
0.5 cts
SP

Ndugu, amini usiamini Serikali yetu ina uzoefu wa kuharibu na si kutengeneza au kuendeleza biashara. Viwanda vya umma walivyodhulumiwa watu kwa kutaifishwa viko wapi? hali kadhalika mashamba, majumba, mabenki?

Usitake kutetea kilicho wazi. Kwa sasa sisi bado.

Serikali ijitowe kabisa katika hizi biashara, wao wawe policy makers tu na wasimamie na kuhakikisha kuwa raia watafata standard zinazowekwa. Hata kusimamia hizo standard kwa sasa zinatushinda, tazama jiji letu linavyotia kinyaa, wakati wa mkoloni haikuwa hivi, tulikuwa masikini lakini standard tulisimamiwa kuzifata. Fikiri, ikiwa Serikali imeshindwa kusimamia majumba iliyodhulumu watu aka Taifisha na mpaka wanaingia ubia kutafuta watu wayajenge upya, kwa akili yako wataweza kusimamia jiji la kisasa? Maweee!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Leading from behind.

Waziri badala ya kutuambia mipango yake ni ipi na kashatekeleza ipi na anahitaji maoni wapi, anatupa li post la Singapore lisilo na kichwa wala mguu, full of generalities, no exactitude or specificity.

Sasa mimi nikikwambia New York City kuna underground train (subway) ndo itakusaidiaje wewe bongo ambaye rapid transit lanes na taa za barabarani zinakupiga chenga?

Na huyu ndo Ph.D ya ukwee, hao darasa la saba na Ph.D za kununua wakoje?
Tatizo kubwa la Tz ni kujazwa kwa viongozi wasiojua wafanye nini. Kama kiongozi hajui afanye nini ni wazi hakuezi kuako na maendeleo.
 
....another wastage of TZ tax payer's money.....yaani Prof with all your experience working with UN habitat...kweli umeona ulete mchango wako kwa reference ya Singapore??....unataka kuilinganisha Singapore na TZ overnight!!...

.Hivi tatizo (challenges) lililopo TZ na kwenye wizara yako kwa wakati huu ni master plan??kweli??....Hivi tatizo la TZ ni uwepo wa master plans za miji au discipline kwenye implementation za master plans??

...Hata mji wa Dodoma mnapofanyia vikao vyenu vya bunge una master plan nzuri sana (tena nasikia ndio iliyojenga mji wa Abuja)...but what have you done todate(as a Minister)to make Dodoma look like it should in its master plan??...yaani mnajionyesha mnavyotafuna hela za walipa kodi kwenye hizi safari zenu...

Labda nikuulize swali Prof....was your Singapore trip the first of its kind??.....considering that you have had big time international exposure when working with UN habitat!....The problem with TZ is not absence of master plans but lack of good leadership in proper implementation of its plans (all plans....not only master plans).....
 
Tatizo kubwa la Tz ni kujazwa kwa viongozi wasiojua wafanye nini. Kama kiongozi hajui afanye nini ni wazi hakuezi kuako na maendeleo.

Frankly I find the post smacks of underinformed condescension.Which is just a continuation of Madam's original stance that basically gave us the impression that she thought JF is a "kids hangout", she even reminisced about how when in NYC at the UN she used to visit youngsters at MTV. No sense of recognition that her bigwigs do come to draw from this well, and countless Tanzanians, do contribute here.

Kama anasema "Watoto, msifikiri sipo hapa, nipo, haya pigeni kelele kwenye hii post isiyo na mguu wala kichwa, mimi najikata".

Hata kama Waziri anataka maoni ya wananchi, ningetegemea alete kitu kinachoeleweka, kilicho specific, kinachoonyesha plan za Wizara, execution, challenges na kwa nini/ wapi wanahitaji maoni ya wananchi.

Ukitaka maoni hapa yapo lukuki.

Maoni yangu ni kwamba Waziri anatakiwa kujiandaa na kufanya homework yake kabla ya kuja kutaka maoni. It's not like hajui kujiandaa, she is supposed to be a highfalutin Ph.D high roller who has been to Turtle Bay and all.
 
Maswali yamekuwa mengi kuliko majibu......

Kwa sababu post yake inaleta maswali mengi zaidi ya majibu. Waziri ametuletea sehemu ya Master Plan ya mji wao mpya unaojengwa kutokana na kuokoa ardhi baharini (reclamation).

Kwani sisi tuna mpango wowote wa kufanya land reclamation? Tuna uhaba wa ardhi mpaka kufikia stage ya kufanya land reclamation?

Pia kama alivyouliza Mohamed Hussein si tayari
wameshafanya huo mpango mpaka tukapewa na kideo au wanataka kututengenezea kideo ingine?

Master plans tunazo nyingi, lakini hazifanyiwi kazi. Mfano, Master plan ya Mtwara imekuwepo miaka nenda rudi lakini hakuna kinachofanyika.

Mara nyingi tunaongelea kuhusu mji mpya wa Kigamboni, lakini kuna mipango ya kundeleza miji iliyopo sasa tokea kipindi cha ukoloni hadi sasa bado haijatekelezwa.

Instead Rais alisema hivi karibuni kuwa "
Baada ya kutembelea bandari ya Mtwara na Chuo cha VETA, nilikaa na kuzungumza na viongozi wa Serikali na Manispaa ya Mtwara. Katika mazungumzo yangu nao niliwasisitizia umuhimu wa kuwa na mpango kabambe wa kuendeleza mji wa Mtwara – (Mtwara Masterplan) Mpango ambao utawezesha kujengwa mji mkubwa wa kisasa unaokidhi mahitaji ya mji wa uchumi wa gesi. Niliwataka wahakikishe kuwa kuna maeneo ya viwanda, biashara, makazi, mahoteli, huduma za afya, elimu, mapumziko na burudani, viwanja vya michezo na kadhalika. Kazi ya kutayarisha Masterplan hiyo imeanza na Manispaa ya Mtwara inashirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi."

Hii kazi imefikia wapi sasa?

banner14.jpg
 
Master plans tunazo nyingi, lakini hazifanyiwi kazi. Mfano, Master plan ya Mtwara imekuwepo miaka nenda rudi lakini hakuna kinachofanyika.

Mara nyingi tunaongelea kuhusu mji mpya wa Kigamboni, lakini kuna mipango ya kundeleza miji iliyopo sasa tokea kipindi cha ukoloni hadi sasa bado haijatekelezwa.

That's because we talk more than we do!
 
Ama kweli wanayoiaribu nchi yetu ni wasomi, Mama Tiba naomba uirekebishe kwanza Manzese kisha uende kw Mnyamani Buguruni theni ukamalizaie ya kigamboni ndo uje hiyo ya singapore maan inaonekana mkijaenda namtumbo na kibandasamaki mtatuletea nyingine. fnya hivyo kabla ya 2015.
 
Ama kweli wanayoiaribu nchi yetu ni wasomi, Mama Tiba naomba uirekebishe kwanza Manzese kisha uende kw Mnyamani Buguruni theni ukamalizaie ya kigamboni ndo uje hiyo ya singapore maan inaonekana mkijaenda namtumbo na kibandasamaki mtatuletea nyingine. fnya hivyo kabla ya 2015.

Mimi nilishagawahi kuuliza kazi ya wizara ya ardhi na makazi ni ipi kama tuna slums kama Mwananyamala Kisiwani na sehemu zingine kama hizo ambako watu wanaishi kwenye vijumba vya udongo.
 
WanaJF

Nilikuwa mmojawapo wa viongozi tulioandamana na Mhe Rais katika ziara yake ya majuzi nchini Singapore. Ninawaletea sehemu ya Master Plan ya mji wao mpya unaojengwa kutokana na kuokoa ardhi baharini (reclamation). Unaona kila kipande cha ardhi mpya kimeshapangiwa matumizi yake na kuwekewa malengo ya majengo yanayotakiwa.

Kupanga ni kuchagua. Kunahitaji nidhamu na hakuna mchezo wala utani. Huwezi kuwa na mji uliopangwa kama unapenda na kuendekeza uholela na vurugu (chaos). Kinachotakiwa ni kushirikisha wadau wote kupanga malengo na viwango baada ya kupata maoni ya wataalam. Wanaoarithirika na kulazimisha kuhama kupisha maendelezo mapya wanalipw fidia stahiki na endelevu.

Anayedai vinginevyo si msema kweli. WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni. Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.

View attachment 97055

Mama Tibaijuka
Nadahani wewe ndio ulitakiwa kuulizwa haya maswali... '' Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.'' . Inakuwaje watu wanaachiwa kujenga holela na kukaa miaka hata zaidi ya arobaini(kama hamna serikali) halafu mkishaona mambo hayarekebishiki tena ndio mnakurukupa kurekebisha! Kwa mfano ghorofa lililojengwa holela likaporomoka na kuua ni nani aliacha mambo yaende holela?
 
Huyu mama ni chai tupu....hana kitu wakuu msimtilie maanani.....hana power alisema mangapi na wenye nchi wanamuangalia tu......

nakumbuka alipokuja machava kigamboni alivyokuwa na hasira....kuwa kuhama tutahama.....she's playing tu hana lolote....huwa wamama ninao waonea huruma ni huyu na yule aliekuwa gogo UN..nimemsahau jina......

sasa hivi na usomi wao wanaburuzwa,tupwa tupwa kule hapa na wajinga wajinga kama nape na mwigulu...sasa ana sauti huyu?.....
 
ni dhahir dunia mnayoishi nyie inawafanywa msiweze kurelate kabisa na plight ya majority ya wa Tanzania. Prof kabla ya kuiga master plan ya singapore umetembezwa ule mji ukaona kuna sehem zilizochoka kama buguruni manzese e.t.c. Wao hizo hawana lakin ww hujaona ila umeona hio master plan yao. Nikama kutaka kushindana na Ussian Bolt wakati una ulemavu wa miguu.
 
tumekuwa tukiongozwa na viongozi wasiokuwa na hata tone la aibu,nchi wameifikisha pabaya lakini hata hawaoni wala kusikia,nchi inaongozwa bila chembe ya utekelezaji wa dhati wa plan na hata sheria zilizopo, maana embu angalia nchi inakokwenda kila mahali frem za maduka, mitaa ni michafu maplastic yamejaa mitaani,mitaani plani ya miji midogo ni maeneo ya ccm na kata ambapo wanapewa wananchi na kujijengea kiholela,bure sana sijui nchi hii wataifikisha wapi.

hivi kweli mnaotuongoza hamna aibu?ukiritimba kila mahali tu
 
Mh.Mama Tibaijuka, hili suala la ujenzi holela wakati kila eneo la makazi kuna halmashauri ya wilaya, meya, diwani, mwenyekiti wa mtaa na umuhimu wa barabara/majenzi ya mpango/ huduma za kijamii. Structure/mfumo wa kiuongozi/utawala wa kuwa na maeneo yaliyojengwa kwa mpango tayari upo kama nilivyoeleza hapo mwanzo, tatizo ni nini Mh. Mama Prof. Tibaijuka?
 
mama tibaijuka umenikumbusha enzi zile watu walikua wanaenda ng'ambo wanarudi na laizon, kweli ccm huwezi kujua nani maji marefu na ni nani profesa waukweli
 
Back
Top Bottom