Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Mh. Hii nchi ina matatizo ambayo yana miongo mingi. kuna master plan ilishawahi kutendenezwa nadhnai mwaka 1978 na haikuwahi kufanyiwa kazi na sababu hazijulikani. kariakoo sharia ni kwamba kila jingo lazima liwe na parking na inajulikana, watu wanaenda kuomba permit ilala municipal na michoro inayokidhi sharia lakini nakuhakikishia hakuna jingo lililofuata sharia ya usanifu. majengo yote chini (ground floor ni maduka). na hii ya kigamboni kila mara inabadilika hatujui plan ni nini hasa, wakiwekeza na ataishi humo??!!! wao na nyinyi au sisi sote, sidhani. nadhani ni kuangalia mambo mengi na muwe wawazi kabisa tangu awali. Mikataba ya uwekezaji hapa nchini si unaijua?? hii itakuwa tofauti?? kivipi
 
Mimi nilishagawahi kuuliza kazi ya wizara ya ardhi na makazi ni ipi kama tuna slums kama Mwananyamala Kisiwani na sehemu zingine kama hizo ambako watu wanaishi kwenye vijumba vya udongo.
Yaani ni watu wa ajabu sana hawa wajamaa mji wa dar wameuaribu vyakutosha pengine si chini ya huyu mama lakini kwakweli kero ni kila mahala sijui ni nani ambae yupo responsible kwenye mgao wa ardhi na kutoa vibali vya majengo.

Maana wao wanajenga tu bila ya kujali residential areas ambazo zinaweza ku-support family lives for those who reside on those parts hata kwanini sielewi sehemu zingine ni popular apart from being near to the city but the rent doesn't justify living there considering the quality of life is very poor.

kwa mfano barabara ambazo utotoni wengine tulikuwa tunathubutu kucheza hata mpira kwa uoga uoga na sehemu ambayo tayari ilikuwa populated leo uthubutu kumwona mwanao wa miaka mitano yupo karibu na geti ni traffic kwenda mbele sasa sijui watoto especially vijana watachezea wapi maana viwanja vya mipira leo vyote kuna magorofa.

Worst of jamaa wa NHC washatoa na ma barua watu wahame hayo majengo wanataka kuongeza more towers hili waongeze mapato ya shirika kisa eti rent zake ni kubwa kwenye hiyo sehemu. Wakati unajiuliza hayo magorofa ya zaidi nyumba mia mia yakijaa si traffic zitaanzia mitaani tena asubuhi maana sasa hivi tu kero, ukichanganya na madaladala yanayokatiza anga hizo lo salale usisikie kero yake na vumbi zinazomiminika huko masebuleni.

Mi mwenyewe masikio yangu kuna siku nipo kwenye ofisi zao (NHC) namsikia huyo afisa mmoja bwana mdogo tu anamwambia kadada kengine kadogo tu wewe nenda mitaa ya garden (upanga) kaangalie potential investment i was dum founded. Yaani hawa ndio chanzo cha kero huko mitaani, ni watu wasiojua umuhimu wa community ambazo zipo kwa muda mrefu na umuhimu wake, let alone understanding the complexity of city planning.

Kwakweli the current leadership is a disgrace.
 
Mimi mawazo na maoni yangu ni

1. Endelezeni huo mji wa Dar es Salaam kwanza uwe wa kisasa kwani unatia aibu hasa mvua ikinyesha.

2. Tumieni huo msaada kuendeleza miji mingine mipya kwani kigammboni tayari mna kila kitu in place.

Mengine naona ni siasa na ufujaji wa pesa tu hapo tutakuwa na mi masterplan kibao kwenye makabati.

Mji wa Dar es Salaam hauendelezeki, ulishaharibiwa na kuvunja nyumba ni kutakana ubaya. Ulimwenguni mwote miji ya zamani inaachwa kama ilivyo, kinachofanyika ni kujenga miji mipya. Wazo la kujenga mji mpya wa Kigamboni ni ni jambo jema, lakini tatizo ni ufisadi. Kuna watu pale watataka kujenga nyumba wanavyoona vema wao, na kwa sababu ya nguvu ya pesa, hawatafanywa lolote. Chezea hela wewe kwa viongozi wetu
 
Mama piga kazi,kuna mabadiliko mengi tumeona chini yako,endelea na mikakati yako mama,wanao kukwamisha wachukulie hatua kali,usitumie sana diplomasia kama ulivyokuwa unafanya kwa UN,hii ni bongoland tumia makufuli style.tuko nyuma yako.
 
Pole na kazi mama Tiba, lakini pia si vibaya ukajibu tuhuma zifuatazo kuondoa wingu juu ya mradi huu, Mnamo tarehe 7/December 2012 inasadikika wewe mheshimiwa waziri ulisafiri kwenda nchini Thailand ambako ulikutana na wakuu wa kampuni kutoka China kusaini mkataba wa ujenzi wa mji kisasa wa Kigamboni. Mheshimiwa kwa mujibu wa vyanzo mhimu wewe utapata 3% kama aksante kutoka kwenye kampuni hii kutoka nchini china?

Pia kuna lawama kutoka kwa wadau wakuu ikiwemo wabunge na madiwani ambao ni wawakirishi wa wananchi hukuwashirikisha katika maamuzi juu ya mkataba huu na mradi kwa ujumla.

Mwisho tungependa kujua ni lini zabuni ya ujenzi wa mji wa kigamboni ilitangazwa kwa mujibu wa Public Procurement Regularity Authority-PPRA, ni kwa kupitia mtandao gani au gazeti gani la hapa nchini au nje ya nchi ilitangazwa (International Competitive Procurement-ICP) ili tujirishe kuwa kulikuwa na uwazi katika diri hili. kwa mujibu wa PPRA thamani ya mradi huo hauwezi kuwa Single source au International shoping. Tunaomba kujua sisi wananchi wa kawaida.

Kama atakujibu hizi nondo nitaomba nipigwe ban ya 24 hours
 
Mheshimiwa Mbunge ...mimi nna swali moja tu...

Kwa nini usijenge mji mpya kati ya Dar es salaam na Kibaha ?Kuna eno la wazi kubwa tu..
Jengai mji pale..hamtasumbua mtu...kisha watu wa kigamboni wakiona mji mzuri watakuita wenyewe uwajengee na kigamboni
 
Mhe. Prof. Mama Tibaijuka,
Ahsante kwa picha nzuri ya Singapore. Pengine ni muhimu ukakumbuka kuwa, siku ukistaafu wadhifa ulionao sasa, halafu mji hata mmoja wa Tanzania usiwe na mwonekano huo wa 'kisingapore' tutakukumbuka (pengine kwa masikitiko) kwamba ulituletea picha.
 
Japo unaleta riziki lakini mji wa Dar uko hovyo sana kimpangilio.
Na kama kuna hasira nilizipata kuhusu Wizara hii ni pale walipouza eneo la Uwanja wa mpira mtaani
kwetu. Sasa hivi vijana wanashinda kwenye Pool na kwenye viroba inapofika jioni! Ngoja niishie hapa.
 
Tatizo moja kubwa la hawa viongozi wetu wakienda nje ya nchi wanakuwa kama watoto wadogo! Wameona mji wa Singapore ulivyojengeka wameupenda. Badala ya kukaa chini na kujiuliza ni nini haswa siri ya hayo maendeleo? Wanakimbilia kusema na sisi tunataka mtutengenezee master plan. Hawajajiuliza hawa tu wana taratibu au sheria gani zinazofanya miji yao ikue kwa mpangilio. Kusema ukweli, kitu anachopendekeza Mheshimiwa wetu ni tusi kubwa kwa wasomi wetu wa pale Ardhi. Kwani, huitaji watu wa Singapore wakutengenezee master plan. Na wakati mwingine watu local wanaweza kuwa wazuri zaidi kwa kazi hiyo kwani wanaijua culture yetu kwa undani.

Mwalimu Nyerere, aliwahi kusema ya kuwa maendeleo sio lele mama bali ni mapambano. Ni lazima viongozi wetu wajue ya kuwa maendeleo sio kitu cha siku moja, na kinahitaji mipango madhubuti ili kukifanikisha. Na wakati mwingine Kiongozi husika anaweza hasifaidike au kupata sifa kwa kile alichokianzisha. Kama kweli Mama Tibaigana anataka akukumbukwe basi inabidi afanye mabadiliko ya kweli katika wizara ya Ardhi. Kama watu na wafanyakazi wa wizara walidharau master plan ya Mbezi Beach na kuichakachua, nini kinachomfanya afikiri ya kuwa awataichakua ya Kivukoni?

Niliwahi kuongea na rafiki yangu mmoja ambaye nu muhandisi wa maji taka kwenye mji mmoja mkubwa huko Marekani. Aliwahi kuniambia kuhusu gharama za kujenga mabomba ya maji machafu (drainage system) zilivyo juu. Nilimwuliza kwa nini gharama zinakuwa juu kiasi hicho? Aliniambia wanapo-design ukubwa wa pipe wanajaribu kukadiria population ya hiyo sehemu miaka hamsini ijayo. Nikamwuliza kwa nini mnafanya hivyo? Alisema ni kweli gharama zinaweza kuonekana kubwa lakini ni rahisi kufanya hivyo kuliko kubadilisha hayo mabomba baada ya miaka kumi. Na huu ni mmoja wa mfano mdogo wa jinsi wenzetu wanavyofikiria mbali. Ni maswali kama haya inabidi tujiulize kabla ya kuomba master plan.
 
Ni matumaini yangu kuwa huyu Mama atarudi hapa kufafanua masuala mbalimbali yaliyotokana na hoja aliyoileta hapa jukwaani. Vinginevyo, atakuwa hana tofauti na kina Mwigulu Nchemba na Juma Nkamia.
 
Hongera mama, kazi ya mikono yako tunaiona.! Jitahidi kwa nafasi yako watanzania wote tuko nyuma yako..!
 
Mji wa Dar es Salaam hauendelezeki, ulishaharibiwa na kuvunja nyumba ni kutakana ubaya. Ulimwenguni mwote miji ya zamani inaachwa kama ilivyo, kinachofanyika ni kujenga miji mipya. Wazo la kujenga mji mpya wa Kigamboni ni ni jambo jema, lakini tatizo ni ufisadi. Kuna watu pale watataka kujenga nyumba wanavyoona vema wao, na kwa sababu ya nguvu ya pesa, hawatafanywa lolote. Chezea hela wewe kwa viongozi wetu

Basi kama hawawezi kuendeleza Mji wa Dar es Salaam kama unavyosema hata kuboresha miundombinu hawawezi???
 
Ni matumaini yangu kuwa huyu Mama atarudi hapa kufafanua masuala mbalimbali yaliyotokana na hoja aliyoileta hapa jukwaani. Vinginevyo, atakuwa hana tofauti na kina Mwigulu Nchemba na Juma Nkamia.

Nitashangaa sana akirudi kujadili na kujibu hoja za wadau humu.
 
Mheshimiwa ni jambo jema kuwa kiongozi mkuu namna hiyo unatushirikisha jinsi nchi nyingine kama Singapore ambayo miaka si mingi ilikuwa kama sisi lakini sasa wamepiga hatua si tu katika mipango miji bali hata mifukoni mwa raia wao. Ushauri wangu kwa wizara yako ni kwanza kukubali kuwa nchi hii imekuwa na uholela mwingi katika mambo mbalimbali hata elimu yenyewe na sasa TUFUTE UHOLELA HUO. Kumbuka ujenzi wa barabara ya Ubungo - Kigogo Mheshimiwa Magufuli aliposimamia vema ili watu wafuate sheria, sintaona aibu kueleza kauli ya mkuu wa nchi kuwa tunahitaji kujenga barabara lakini tuwe na utu pia...kana kwamba sheria si utu. Tuateni sheria na la pili epukeni 'double standards' katika kugawa na kumilkisha ardhi. Huyu anaambiwa ni barabarani na mwingine anabomolewa (Kesi ya Mbilinyi barabara ya Morogoro) vyote hivi ni kero kwa wananchi wa kawaida.
 
Madam Prof, tatizo la Nchi yetu wataalam tumewaweka pembeni badala yake wanasiasa ndo wanafanya kazi zote. Mf. Wizara ya yako inaandaa mchoro wa mipango miji (TP Drawing) na kupitishwa na Kurugenzi ya Mipango Miji kisha unapimwa na kupata Survey Plan, lakini inakuja Wizara ya barabara inaweka alama 'X' kwa wananchi ambao walimilikishwa kihalali bila hata kupewa taarifa yoyote huku wengine wakinyimwa mikopo benki kwasababu mali zao zimetiwa alama ya 'X' na wakati huo huo hawajui kama fidia watalipwa ama la. Lifanyie kazi maana sisi wananchi tumeonewa sana na hii Wizara ya Ujenzi/Mabarabara.

Samahani kwa kuchepuka kidogo nje ya mada.
 
Tatizo moja kubwa la hawa viongozi wetu wakienda nje ya nchi wanakuwa kama watoto wadogo! Wameona mji wa Singapore ulivyojengeka wameupenda. Badala ya kukaa chini na kujiuliza ni nini haswa siri ya hayo maendeleo? Wanakimbilia kusema na sisi tunataka mtutengenezee master plan. Hawajajiuliza hawa tu wana taratibu au sheria gani zinazofanya miji yao ikue kwa mpangilio. Kusema ukweli, kitu anachopendekeza Mheshimiwa wetu ni tusi kubwa kwa wasomi wetu wa pale Ardhi. Kwani, huitaji watu wa Singapore wakutengenezee master plan. Na wakati mwingine watu local wanaweza kuwa wazuri zaidi kwa kazi hiyo kwani wanaijua culture yetu kwa undani.

Mwalimu Nyerere, aliwahi kusema ya kuwa maendeleo sio lele mama bali ni mapambano. Ni lazima viongozi wetu wajue ya kuwa maendeleo sio kitu cha siku moja, na kinahitaji mipango madhubuti ili kukifanikisha. Na wakati mwingine Kiongozi husika anaweza hasifaidike au kupata sifa kwa kile alichokianzisha. Kama kweli Mama Tibaigana anataka akukumbukwe basi inabidi afanye mabadiliko ya kweli katika wizara ya Ardhi. Kama watu na wafanyakazi wa wizara walidharau master plan ya Mbezi Beach na kuichakachua, nini kinachomfanya afikiri ya kuwa awataichakua ya Kivukoni?

Niliwahi kuongea na rafiki yangu mmoja ambaye nu muhandisi wa maji taka kwenye mji mmoja mkubwa huko Marekani. Aliwahi kuniambia kuhusu gharama za kujenga mabomba ya maji machafu (drainage system) zilivyo juu. Nilimwuliza kwa nini gharama zinakuwa juu kiasi hicho? Aliniambia wanapo-design ukubwa wa pipe wanajaribu kukadiria population ya hiyo sehemu miaka hamsini ijayo. Nikamwuliza kwa nini mnafanya hivyo? Alisema ni kweli gharama zinaweza kuonekana kubwa lakini ni rahisi kufanya hivyo kuliko kubadilisha hayo mabomba baada ya miaka kumi. Na huu ni mmoja wa mfano mdogo wa jinsi wenzetu wanavyofikiria mbali. Ni maswali kama haya inabidi tujiulize kabla ya kuomba master plan.

Mkuu usishangae na wao wakitaka kufanya land reclamation Kigamboni.
 
Mheshimiwa, tatizo kwa Tanzamia sio master plan. Shida yetu kubwa ni nidhamu ya utekelezaji. Labda vaada ya kuanzishwa kwa Pemandu tutaona mabadiliko. We dont need more plans at the moment,..... We need to implement!
 
Ninakerwaa sana kuomba kusaidiwa saidiwa, eti tumewaomba Singapore waje kutusaidia kujenga mji mpya wa Kigamboni !!!! ni kipi sis tunaweza kufanya wenyewe nasi waje wageni waseme ni watanzania wamejenga! Mjinga mkubwa sana we mama inamaana tumeshindwa kujenga huo mji mpaka waje wageni watusaide?? na wataalamu wote waliomaliza ARDHI university??
 
Back
Top Bottom