Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Mbona mlishafanya huo mpango angalia hapa kwenye link (Kigamboni New City) au mnataka kupiga hela nyingine za ili mtutengenezee video nyingine?

...Post of the day!!

Watawala wanaona wadanganyika ni wajinga!
 
Mkuu Anna Tibaijuka nasapoti hoja yako ila kwa mawazo tofauti!

Suala la masterplan ni suala la serikali inajenga ama property developer? Ukiangalia picha hapo chini ni mji wa mwanza, watu wanakimbilia milimani na matokeo yake miundombinu inakuwa shida kuwafikia na kuongeza makazi holela.

Ninachoomba suala la upimaji wa ardhi ipewe sekta binafsi na serikali ibaki kuwa wasimamizi wa zoning. Sababu kubwa ni urasimu uliopo serikalini..viwanja vikipimwa mwaka huu mnaweza kukaa hadi miaka 3 hamjui nini hatma yenu nami ni mmoja wa wahusika coz toka mwaka 2010 kuna viwanja vilipimwa mpaka leo jiji wapo kimya.

Mimi nashauri hiyo kazi wapewe property developers

Mkuu Halmashauri zimeshindwa kusimamia ukuaji wa miji.Yaani Dodoma isingekuwa na chombo kilichoundwa kusimamia mji,Dodoma isingepangika vile.

Serikali pia iongeze fedha katika miji mingine na ikiwezekana iundwe Mamlaka ambayo haitakuwa inaingiliwa na Madiwani,kwani wao wanachangia usimamizi mbovu wa miji.

Wavamizi wa maeneo ya wazi wakitaka kuvunjiwa,wanasiasa wamekuwa wanatetea kwa sabubu za kulinda kura zao wakati wa uchaguzi.
 
Watawala wa tanzania kwa ahadi na write up nzuri hatujambo ila utekelezaji hakuna!!!mama endeleza mradi wa Mama Sijaona wa kupima viwanja maeneo mbali mbali kisha wananchi wanunue,huyu mama alikua mbunifu na mchapa kazi,kosa kutaka kugombea ubunge huko kwa Sitta akatupwa ubalozini Japan kufichwa!!mbona utaratibu ho inalipa sana?Mradi wa sattelite city Kibamba umeishia wapi?wanachi wamenunua maeneo hakuna miundombinu mpaka leo.Hapo wizarani ardhi tatizo lipo wapi kuto a hati za wananchi?mbona zoezi hilo hufanyioka kwa kificho kikubwa?halafu hakuna target kwa watendaji wako ndiyo maana wanakalia mafaili kusubiri rushwa
 
Tanzania tutafanikiwa tu endapo viongozi wa Tanzania mtaacha usanii,maana kinachoendelea Kigamboni kwa sasa ni usanii mtupu
 
Tunakupongeza Mama kwa jitihada zako za dhati. Kujenga miji mipya kunajumuisha mambo mengi sana hivyo kuna hitaji umakini wa hali ya juu. Nilipita pale Gezaurole walipogawiwa watu awamu ya kwanza nikaona tayari mitaa na barabara zinachongwa kwa kweli kunapendeza ila watu wameanza kujenga kwenye viwanja vyao kila mtu na ramani yake anavyojua yeye! niliona hii ni changamoto kuweza kufikia malengo, mitaa haipendezi kama tulivyotegemea. USHAURI ni kuwa wizara muandae ramani (house plans) nzuri na za kisasa kabisa na m-recommend kuwa kama mtu anataka kujenga eneo fulani achague moja ya ramani na alipie, hata kama atarekebisha iwe ni kidogo. Hapa tutapata mji mpya wa kupendeza kama tulivyoona kwenye Master plan.

Mama Tibaijuka[/QUOTE]
 
Sioni jipya kutoka kwa maneno ya waziri,hata kama watkenda mwezini kujifunza. Ruraland Urban planing serikali hii ya CCM haitaweza kuleta mabadiliko, Tibaijuka tuliambiwa Dodoma itakuwa mji wa kisasa uliopangwa kukawa na CDA, leo nenda Dodoma uone uozo,tulikuwa na Oysterbay na Masaki ulipangwa vizuri na wakoloni, leo tunaona kuwa ni crime kuwa na spacious residence watu wanajenga hadi barabarani angalia Chole rd na Haile selasi baa ni kila kona kama umefika ukanda wa gaza (sinza) enzi zile, wakuu wa nchi waliuziwa nyumba za serikali maeneo haya badala ya kuwa mifano ya kuigwa imekuwa kinyume katika kuyaendeleza, hao hao watu ndo wenye elimu kubwa na wanazijua sheria lakini wapi, Msigwa alisema you can't solve the problems you created them
Mheshimiwa waziri walete wasingapore watusaidie kutupangia masaki na oysterbay ni aibu yanayo fanyika huku
 
Mbona mlishafanya huo mpango angalia hapa kwenye link (Kigamboni New City) au mnataka kupiga hela nyingine za ili mtutengenezee video nyingine?

Hawa wasanii wa hii serikali unafikiri wanaeleweka basi,tatizo lao kubwa ni ubinafsi kinachoendelea hakuna
halafu wanakuja na Master plan za wenzao yao yamewashinda,kila siku story zisizoeleweka'
 
Mimi nashauri Mjenge makao makuu ya Tanzania inakuwaje nchi haina mji mkuu Mnazidi kujibana Dar??Jengeni Dodoma fumueni miundo mbinu ya CDA anzisheni miundombinu mipya!!Kigamboni nisawa kwa swala la ustawi wa nchi lakini kwa heshima ya nchi Makao makuu yanahitaji kujengwa pia!!

... Kaka umenena' mimi siwaelewi viongozi wa nchi hii! Tangia enzi hizo za Mwl Nyerere wanahubiri kuhusu ujenzi wa Makao Mkuu Dodoma. Wazazi wetu walikuwa wanakatwa fedha kwenye kila kilo ya mazao wanayouza, lakini walivyokuja awa viongozi wa kizazi kipya wametupilia mbali mpango wa Ujenzi wa Dodoma.
...inavyooneka viongozi wetu wanatafuta miradi mpya ili kuweza kufuja kodi za walala hoi na masikini wa nchi hii...
"mama Tibaijika - jengeni Dodoma kwanza, Kigamboni na mji mpya mingine baadaye"
'... MTAKA YOTE KWA PUPA, HUKOSA YOTE'
 
Hata sielewi kilichowavutia ktk master plan ya Singapore kwasababu kwenye dunia ya kwanza hicho ni kitu cha kawaida yaani safari zote mnazochoma pesa za walala hoi kwa kutembea kundi kubwa mmejifunza master plan! Hivi hatuna architecture engineer tanzania? Nafikiri tatizo ni serikali isiyokuwa na mipango, ufisadi na uvivu wa kujituma, nchi inazalisha wasomi kibao kwenye kilimo Lakini watu wanakufa njaa hili nalo tunataka watu waje kutufundisha kulima! Ni kitu gani tunachoweza Kama watanzania? Gossip na ngonjera, tanzania itajengwa na sisi watanzania, Hakuna nchi duniani iliyojengwa na wageni.
 
Mama Tibaijuka ...Mji wa Dar ni mchafuu!!!

Mama tunahitaji mawazo ya kuondokana na uchafu wa Kutisha wa Jiji hili!!

Tumalize uchafu kwanza ndo tuendelee na mji mpya!
 
Labda swali la Msingi, tunahitaji kufanya Land reclamation Tanzania?

Kwa nini wameenda kujifunza reclamation kama hatuihitaji?

Hata sielewi kilichowavutia ktk master plan ya Singapore kwasababu kwenye dunia ya kwanza hicho ni kitu cha kawaida yaani safari zote mnazochoma pesa za walala hoi kwa kutembea kundi kubwa mmejifunza master plan! Hivi hatuna architecture engineer tanzania? Nafikiri tatizo ni serikali isiyokuwa na mipango, ufisadi na uvivu wa kujituma, nchi inazalisha wasomi kibao kwenye kilimo Lakini watu wanakufa njaa hili nalo tunataka watu waje kutufundisha kulima! Ni kitu gani tunachoweza Kama watanzania? Gossip na ngonjera, tanzania itajengwa na sisi watanzania, Hakuna nchi duniani iliyojengwa na wageni.
 
WanaJF

Nilikuwa mmojawapo wa viongozi tulioandamana na Mhe Rais katika ziara yake ya majuzi nchini Singapore. Ninawaletea sehemu ya Master Plan ya mji wao mpya unaojengwa kutokana na kuokoa ardhi baharini (reclamation). Unaona kila kipande cha ardhi mpya kimeshapangiwa matumizi yake na kuwekewa malengo ya majengo yanayotakiwa.

Kupanga ni kuchagua. Kunahitaji nidhamu na hakuna mchezo wala utani. Huwezi kuwa na mji uliopangwa kama unapenda na kuendekeza uholela na vurugu (chaos). Kinachotakiwa ni kushirikisha wadau wote kupanga malengo na viwango baada ya kupata maoni ya wataalam. Wanaoarithirika na kulazimisha kuhama kupisha maendelezo mapya wanalipw fidia stahiki na endelevu.

Anayedai vinginevyo si msema kweli. WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni. Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.


Mama Tibaijuka

Mama Tibaijuka mimi nadhani hapo nilipo bold ndio kwenye mzizi wa fitna nchi hii. Kukosekana kwa nidhamu ya kusimamia mipango miji na uholela na vurugu (chaos) vimechangia kwa kiwango kikubwa kuharibu miji yetu.

Kuhusu ramani ya mji mpya wa Singapore mimi nadhani ule mji wa Kigamboni tuliouona kwenye video unatosha. Kinachotakiwa ni nidhamu ya kuusimamia ili ujengwe kweli. Tusije kuwa na CDA nyingine ikatuchukua miaka hamsini kujenga kijiji kama cha Dodoma.

Kuhusu ahadi ya wasingapore, hakuna kitu kinachonikera dunia hii kama hii "beggar mentality". Hivi ni lini watanzania tutasimama kwa miguu yetu wenyewe tu-design miji yetu ya kisasa na kusimamia ujenzi wake bila kipitisha bakuli la kuomba misaada bila hata kujishughulisha kwanza?

Mwisho naomba kuuliza swali moja zaidi. Ni lini upimaji wa miji na viwanja utakuwa kazi ya kudumu ya wafanyakazi wa ardhi badala ya mtindo wa sasa ambapo upimaji miji wa viwanja umegeuzwa kuwa miradi ya wakurugenzi wa miji/majiji na maafisa wa ardhi wanaoishia kujilimbikizia viwanja visivyoendelezwa? Hamuoni kuwa mnachochea makazi holela kwa kitendo chenu cha kugeuza upimaji wa miji na viwanja kuwa miradi ya muda mfupi yenye idadi chache za viwanja badala ya kuwa ni shighuli endelevu na ya kudumu?
 
Professor - mada uliyotoa ni nzuri

mimi kama mpima ardhi ningeshauri tuanze na kubadilisha taratibu na miundombinu ya upimaji.

1. Tuamue kuwa na "system" moja ya "reference" iwe Arc1960 au WGS84 au yoyote bora kama ipo na kujenga upya monuments (trig points) katika system mpya.

2. kukamilisha mradi ulioanza wa (Continuously Operating Reference Stations CORS) ili kurahisisha upimaji kwa kutumia "GPS receivers". mradi huu ni muhimu sana na unaweza kuona nchi nyingi duniani (EUROPE, USA nk) wana huu utaratibu ambao unasaidia kupunguza gharama katika miradi ya viwanja, barabara, maji, umeme nk.

3. kuanzisha haraka mradi wa SPATIAL DATA INFRASTRUCTURE (SDI) ambao umeshajadiliwa sana katika wizara yako ya Ardhi pamoja na National Bureau of Statistics NBS na chuo kikuu cha Ardhi. awali ilionekana kwamba NBS wangesimamia lakini tangu 2003 hakuna kilichofanyika.
Mradi huu ni muhimu sana kwani data/information zote za upimaji katika nyanja zote zinahifadhiwa katika mfumo mmoja ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa hizo. katika mfumo huu data zitawekwa katika mfumo mmoja (standards) hivyo zitaboreshwa. Pia kupunguza hali iliyo sasa ya kurudia kupima kila wakati na kuhifadhi data inayofanana (duplication) hivyo kuokoa gharama za serikali. Unaweza kuomba maelezo zaidi ya National Spatial Data Infrastructure (NSDI)

aksante nakutakia afya njema
 
Prof ili nikuamini upo makini vunja kwanza lile ghorofa pacha lililobaki baada ya lile jingine kuanguka huwezi nionesha una mipango mikubwa kama hiyo wakati ili dogo umeshindwa kulitekeleza.
 
Labda swali la Msingi, tunahitaji kufanya Land reclamation Tanzania?

Kwa nini wameenda kujifunza reclamation kama hatuihitaji?

Suala la msingi ni Waziri anakusudia kupata nini kutokana na hiki alichokiandika?

Yeye ndiye msimamizi wa ardhi yote ya Tanzania. Kama sheria hazifuatwi, hakuna nidhamu, kuna matani na mchezo ndio maana miji yetu iko chaotic, anataka sisi tufanyaje wakati yeye mwenye madaraka makubwa zaidi kwenye suala hilo ukiacha rais ameshindwa kuonyesha lolote?

Kwa nini anataka kutubebesha lawama Watanzania na anaacha kuchukua yeye lawama ya kushindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi stahiki?
 
Lakini mh. Kwanini mumeshindwa kuboresha huu mji tulionao sasa hivi na munaanza kutafuta mpya wakati bado hamjachelewa? Tunahitaji tuone mabadiliko hapa tulipo sasa, Hizi sheria ndogondogo za miji zinafanya kazi?

Mtu kuweka maeneo ya mjini vibanda, parking ziko ndani ya barabara ukipita maeneo yote ya mjini sehemu za kupita watu na magari zimepakiwa gari na barabara inakua finyu. Majumba mjini yamekua kama magovu je hakuna sheria ya kuwaagiza wamiliki kuyarekebisha kila kipindi inapofika?

Tatizo la nchi yetu ni kuwa viongozi hawako serious. Hata kama wanatembelea majiji mengine wakirudi hakuna utekelezaji. Chukua mfano huu, miaka michache iliyopita walikuja na concept ya kujenga satellite city maeneo ya nje ya jiji kama Kibamba. Tunaoishi Mbezi na Kibamba tuliitwa kwenye mkutano na tuliambiwa tusimamishe ujenzi kwa miezi mitatu hadi hapo ramani mpya itakapopatolewa. Tulikubali kwa nia njema kabisa ili tuwe na mji uliopangika. Lakini hakuna chochote kilitokea hadi leo. Wananchi wameendelea kujenga kiholele kuliko Manzese. Sasa hapa wa kulaumiwa ni nani? Mhe. viongozi wetu hampo serious mambo yafanyika kufuata upepo wa kisiasa.
 
Mama,

Nasukuru kwa leo kuona thread hii. Me nashauri Tanzania tuache siasa twende kwenye sayansi. Hatutafika bila kutanguliza ushauri wa kitalaamu na kutengemea watalaamu wa ndani kwa angalau 70%. Kuna vitu ambavyo naona:

Je kuna uwezekano wa Tanzania kuzuia mapema ujenzi holera (nyumba binafsi) katika miji inayokuwa hara kama Arusha,Dar, Mwanza, Mbeya ili kuwa na mpango mzuri wa maendeleo?


Nyumba zinazo jengwa na NHC inaonyesha bei yake ni kubwa sana, kwa nini zisiwe za kupangisha tu hasa mkizuia kujenga nyumba binafsi

Najua kupanga ni kuchagua, yote yanawezekana. Tujaribu katika mji mmoja tunaweza pata majibu. Sasa hivi DSM hatuwezi kujenga hata barabara zuri tena.Pengine tufanye Dar ya sasa iwe Old Dar, Tujenge nyinigine. Kama Cairo kuna Old Cairo halafu unaona New Giza ambaoni mji wa kisasa.

 
Mheshimiwa waziri kwanini siku zote nyie serikali mnachelewa mnafika sehemu mnakuta wananchi wameshajenga holela!!

Kwanini msitafute pesa mkapima ardhi ili watu wakae sawa, barabara ziwepo na huduma za jamii?
 
Mama, Mhe. Tibaijuka kwanza nikupongeze kwa kuwa mshiriki mzuri wa mitandao ya kijamii tena kwa kutumia jina lako halisi. Hii inaonyesha dhamira na nia yako ya dhati ya kupata maoni halisi na shirikishi kutoka kwa watanzania wenzanko wenye uendelevu wa fikra na maono ya kufikia Tanzania tuitakayo.

Angalizo, hatuwezi kufikia ndoto hizo kama mawazo, fikra, mitazamo na nidhamu zetu watanzania hasa viongozi zitabaki kama zilivyo. Lazima uwe na uthubutu wa kufanya maamuzi magumu ili uache legacy kwa kizazi kilichopo na vizazi vingi vijavyo.

NAKUTAKIA KAZI NJEMA.
 
Back
Top Bottom