Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Haya mkuu. Ila inasemekana the next (baada ya Bagamoyo), ni kwetu Chalinze...

Kwani hawajipendi? Lindi nako kuna gas. Kama wanataka na Lindi waseme haitoki wajaribu kufanya hivyo
 
Watawala wa tanzania kwa ahadi na write up nzuri hatujambo ila utekelezaji hakuna!!!mama endeleza mradi wa Mama Sijaona wa kupima viwanja maeneo mbali mbali kisha wananchi wanunue,huyu mama alikua mbunifu na mchapa kazi,kosa kutaka kugombea ubunge huko kwa Sitta akatupwa ubalozini Japan kufichwa!!mbona utaratibu ho inalipa sana?Mradi wa sattelite city Kibamba umeishia wapi?wanachi wamenunua maeneo hakuna miundombinu mpaka leo.Hapo wizarani ardhi tatizo lipo wapi kuto a hati za wananchi?mbona zoezi hilo hufanyioka kwa kificho kikubwa?halafu hakuna target kwa watendaji wako ndiyo maana wanakalia mafaili kusubiri rushwa

Nipo pamoja nawe, Mradi wa Mama Sijaona maarufu kama 20,000 plots project ulitakiwa uendelezewe na uwe wa kudumu chini ya Wizara ya Ardhi. Kosa lililofanyika ni kuuamishia kwenye Municipal za Kinondoni, Temeke na Ilala ambazo wameshindwa kuuendeleza huo mradi na viwanja vyao ni ghari mno kwa mwananchi wa kawaida. Kigamboni project inatakiwa kwenda sambamba na project niliyoitaja hapo juu ili kutoa alternative kwa wananchi watakaoshindwa kumiliki plots kigamboni na pia sio wote wanapenda kuishi huko.je wanajua wananchi wa kigamboni sasa wanaelekea wapi kuanzisha makazi mapya yasiopimwa? So wakati mama anakomalia kigamboni ajue sehemu nyingine Squatter zinaota.

Pili ujenzi holela Tanzania hausababaishwi na wananchi bali ni udhahifu mkubwa wa serikali na viongozi wake, mfano asilimia kubwa ya maeneo ya wazi Sinza, kinondoni etc wameuzwa na madiwani na maafisa wa ardhi na wamiliki wake wa sasa ni viongozi wa serikali na wengine kutoka kwenye taasisi za fedha(TRA,BOT,etc) (Mama sijui ile project yako ya kurejesha maeneo ya wazi imeishia wapi??). Tatu Wizara ya Ardhi wanakosa "continuity" kwenye project zao nyingi, matokeo yake wanawaacha wananchi kwenye dilemma matokeo yake wanajenga popote wanapopata plots. Mfano kipindi cha Mkapa tulikua na 20,000 project,Kibamba satellite city etc. Kikwete period-Kigamboni city, Next president atakuja completely new project. Huku nje anakosema Mama Tibaijuka serikali zao ziko makini na upimaji wa ardhi uliwatangulia wananchi, pia kuna mwendelezo ktk project zao,so ujenzi holela na mikataba ya siri aina nafasi. Mwisho,kuuendeleza mji wa kigamboni pekee haitasaidia kama Squatter zinaendelea kuota sehemu nyingine za Dar. Ili kupunguza makazi holela wizara iakikishe inapima viwanja vingi kadri itakavyowezekana maeneo mengine.
 
mheshimiwa mama! hivi umejiandb vipi ku survey japo extension za miji tuu? tunaambiwa nchi nzima ya kenya ilisha surveiwa yote kitamboo! huku kwetu kikwazo ni nini pamoja na technology mpya za gps e.t.c?

huwezi jenga mji wa kisasa kwenye squater, haiwezekani hata siku moja, dawa ya miji ya kisasa ni mipango endelevu ambayo surveying ni sehemu muhimu!
 
Hili nalo ni la msingi, anataka kupata nini kwa sred hii. Na kitu kidogo kama jengo limemsumbua kusimamia utekelezaji, vipi kuhusu mpango/project kubwa kama hii yenye wadau wengi zaidi?


Lakini mie bado najiuliza, kwa nini walienda kujifunza hii reclamation?

Suala la msingi ni Waziri anakusudia kupata nini kutokana na hiki alichokiandika?

Yeye ndiye msimamizi wa ardhi yote ya Tanzania. Kama sheria hazifuatwi, hakuna nidhamu, kuna matani na mchezo ndio maana miji yetu iko chaotic, anataka sisi tufanyaje wakati yeye mwenye madaraka makubwa zaidi kwenye suala hilo ukiacha rais ameshindwa kuonyesha lolote?

Kwa nini anataka kutubebesha lawama Watanzania na anaacha kuchukua yeye lawama ya kushindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi stahiki?
 
Mawazo yako mama ni mazuri tatizo ni usimamizi. Kwa utawala uliopo kila mtanzania ni mvunja sheria kwani hakuna anayewajibika ipasavyo! Kupindisha mambo ni kila wizara, idara na taasisi.

Hakuna mtu asiyependa kitu kizuri sasa inakuja uwezo huna unaishia kuvunja sheria kujenga holela na hakuna anayekuzuia so life goes on.

WaSingapore wanakuja kutusaidiaje ktk ujenzi wa mji wa Kigamboni? Au wanakuja kuwekeza?
 
Mama Anna Tibaijuka,

Nakushauri kuwa Serikali ijitowe katika huu mradi na iwawachie "real estate developers" wa Kimataifa, wenye uzoefu wa hizi kazi.

Serikali yetu haina uzoefu wa hizi kazi na historia inatuonesha Serikali imeshindwa ku-manage mradi wowote wa maana wa kibiashara. Hata NHC inawashinda ni uozo mtupu, ilhali majumba yalikuwa ya kudhulumiwa watu.

Ikiwa Serikali imeshindwa kuendesha viwanda vya umma, leo itaweza kuendesha project ya "magnitude" ya jiji? Jiulize.

Tusipoteze wakati, tuwawachie wenye utaalaam, na uzoefu wafanye haya mambo, wazo ni zuri, watendaji hatuna, tuna wizi tu Tanzania.

Leo ni zaidi ya miaka 6 tunasikia hii lelemama ikiimbwa tu, hebu ondoeni ukiritimba muwape wenye uwezo, kama hamjui pa kuwapata mnaweza wasiliana na mimi kwa PM.

Ndugu ZOMBA.

Ingawa mama hajaja na sijui atakuja lini kujibu, naomba nitofautiane na wewe kwa baadhi ya muono wako, wa kuhusu makazi. Nitaeleza kwa ujumla kwa sababu ya muda, na kusubiri majibu ya profesa Tibaijuka!

Kwanza naomba tuelewe serikali inauzoefu mkubwa sana, katika mambo mengi sana kuliko mtu/kampuni. Sababu serikali inaweza kuajiri mtaalam, kuandaa, kumsomesha na kumpatia exposure ( mfano ndo hata mama na uprof serikali imempeleka kujionea mambo Singapore) mtaalam yeyote mahili, kama itahitaji kufanya hivyo, Serikali imekuwepo kwa muda wa miaka 50 ( baada ya uhuru) hivyo hatuna mtu amefanya kazi 50 Years, ila kabati la wizara limekuwepo na nina amini uzoefu upo kabatini.

Kuhusu kamapuni binafsi, hapana sababu makazi ni mahitaji muhimu sana kwa binadamu. nakumbuka ni moja ya mambo ambao serikali duniani zinafanyia kazi kila siku. Ukisikia mtikisiko wa uchumi mojawapo ya sababu ni hayo mambo ya makazi. Hivyo ili kila mtu aweze kupata makazi stahili na bora serikali lazima ifanye kazi.

Real estate inahitaji mtaji mkubwa, siyo lelemama, ndo maana nilishauri baadala ya kuanzisha benki 3 kwa mwaka huu wa fedha wangeweza kuanzisha Real estate company, kama vipi NHC ijiunge stock market ipate mtaji mkubwa, then isiuze nyumba bali ipangishe na iboreshwe.

Siyo sehemu zote sekta binfsi imefanikiwa, mifano hai ipo siyo tanzania bali hata nchi jirani. Serikali itoe makazi kwa kupangisha, hapo itapanga mji (miji) na kulinda ukuaji wa uchumi wake. Serikali itumie watalaam wake waliopo, ipange, isimamie mambo yataenda, sekta binafsi ije kujazilizia pale serikali inaona itahitajika na kufanya bei iwe ya kuangalia gharama halisi.

Hapo mwisho (rangi ya blue) mkuu tayari umeona hapo kuna deal, umejipigia pass mwenyewe, yaani wewe unaweza zaidi kuliko serikali? kazi ipo!!!!
0.5 cts
SP
 
mheshimiwa mama! hivi umejiandb vipi ku survey japo extension za miji tuu? tunaambiwa nchi nzima ya kenya ilisha surveiwa yote kitamboo! huku kwetu kikwazo ni nini pamoja na technology mpya za gps e.t.c?

huwezi jenga mji wa kisasa kwenye squater, haiwezekani hata siku moja, dawa ya miji ya kisasa ni mipango endelevu ambayo surveying ni sehemu muhimu!

Mkuu Kasimba

unazungumzia survey ya namna gani? ya viwanja na mashamba (cadastral). haya ni maneno ya mtaani kwamba Kenya yote ipo surveyed. Ni vyema kufuatilia hizi taarifa kabla ya ku comment. Kule Kenya kuna squatter pia na kuna maeneo mengi ya nchi (55%) ambayo ni ya wafugaji na eneo lingine ni kavu. Suryeying kama Cadastral Surveying ni kwa ajiri ya land registration inakuwepo maeneo machache yenye umuhimu fulani.

unaweza kusoma hapa http://www.lands.go.ke/index.php?option=com_content&task=view&id=15&Itemid=30

kuna paragraph hii kwenye hiyo website ya Kenya
Achievements of Land Adjudication Surveys

Currently, land parcel boundaries are determined, marked on the ground then photo identified and plotted on enlarged aerial photographs at scales 1 : 2,500 or 1 : 5,000 from which maps are traced off at the same scale to support land registration.

The Land Adjudication and Registration Programme has been completed in Central , Western and Nairobi Provinces . Substantial amount of work still remains to be done in Nyanza, Coast, Rift Valley and Eastern Provinces.


Since its inception, 8.0 million hectares comprising 1.5 million parcels and 338 ranches covering 3.0 million hectares of Trust lands have been finalised and brought onto the Land Registers (registered). The Programme is yet to start in North Eastern Province .


Eneo lote la nchi ya Kenya ni 581,309 km[SUP]2[/SUP] au 58,130,900 ha
 
tatizo kila siku zinakuja master plans ila utekelezaji ndo hamnaaaa

mkuu soma vizuri nadhani hujaelewa hapa "WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni"
siyo kuchora master plan, sasa ni kuanza ujenzi
 
Tunashukuru kwa hizo plans kwa huko Singapore, Mama ningeomba uweze kutuambatanishia na city plan zetu za hapa TZ ili tuweze kujua na uweze kupata mawazo mazuri zaidi, hapo umejikita kwa upande mmoja pekee, ingependeza ungeliweka na upande wa pili huku TZ.

Huko mlienda kujifunza mambo ya land reclamation, kwetu sisi huku Bongo sidhani kama tunahitaji mradi kama huo sababu aridhi bado tunayo ya kutosha, sasa nashindwa ku connect dot kwenye hii thread.
 
Tulikuwa pamoja , tupo pamoja na tutakuwa pamoja hadi mwisho... Lakini malizeni ya mwanzo na ahadi itimizwe.
 
Wewe uliyeelewa hebu nieleweshe?

Uvivu wa kusoma na kuelewa, naombeni watanzania tuwe tunasoma kila neno aliloandika mtu halafu unalichambua na ku-comment sio kukurupuka tu kama wewe mada hii ni muhimu sana, unatia aibu.
 
Ni vema kuangalia mfano au mifano ya waliondelea ili kujifunza na hatimae kufanya kama hao au kufanya zaidi ya hao. Lakini kwa nchi hii; ubinafsi wa viongozi wetu, uvivu wa kufikiri zaidi ya macho yanapoona na siasa zilizotawala kila kona, kamwe hatutoweza kufikia mji kama wa Singapore. Plan zetu nyingi ni za kipindi cha miaka 5 na ikizidi 10, na serikali iliyopanga inapotoka madarakani, licha ya kuwa yenyewe haikutekeleza plan hizo, basi yule anaekuja madarakani anakuja na yake mapya.

Kabla hatujaanza kuota kuwa kama Singapore, ni lazima tuanze chini kabisa na kupanga miji yetu, kitu ambacho kinaonekana kushinda serikali miaka hadi miaka. Mipango ya miji huanza na mipangilio ya miaka mingi na kuwahi kabla watu hawajajaa kwenye maeneo husika, jambo ambalo kwa nchi yetu ni kitendawili. Serikali imekuwa nyuma ya kasi ya ukuaji na kuhamia watu katika maeneo mapya, hili ndo tatizo la miaka na halihitaji hata elimu ya darasa la saba kuliona, licha ya kulishughulikia. Pale wanapowahi kabla ya watu inaonekana ni kwaajili ya mapato zaidi na sio kwa madhumuni ya kuplan, mfano hapa ni vile viwanja vilivyopimwa kule Gezaulole, toka watu wamekamilisha malipo ya viwanja hivyo na Halmashauri husika kukusanya mamilioni ya pesa, mpaka sasa hakuna kilichofanywa kule, hakuna bara bara, wala dalili ya bara bara. Kwa namna hii, hatuwezi kufikia planning goals zozote na zitakuwa ni ndoto za mchana tena tukiwa macho. Nadhani, kabla ya kuanza hata kuwaza mambo ya Singapore, tuondoe madimbwi na mabwawa yanayojaa maji kila kona ya jiji la Dar mvua inaponyesha, japo kidogo tu, bahari ya Hindi ipo karibu sana na kutoa maji hayo ilibidi iwe ni kazi rahisi sana. Hatuwezi kufikia Singapore iwapo mji kama wa Dar es Salaam asilimia kubwa ya wakazi hawana hata maji ya bomba, Singapore wanateka bombani na kunywa, kila nyumba.

Licha ya kwamba ni kisiwa, wana barabara za hali ya juu sana, treni za umeme chini ya ardhi na watu wamefundishwa na kuhimizwa kuwa na nidhanmu ya hali ya juu, hairuhusiwi kula hata chewing gum ukiwa barabarani.

Safari yako iwe ni changamoto, hasa kwa wizara yako, ambayo inahusika zaidi kwenye suala la planning. Na tusiangalie Dar peke yake, kuna miji mingi inakua kwa kasi kubwa na tusipoanza planning mapema tutaishia kuwa na mji kama wa Dar ambao sehemu nyingi hazieleweki, hakuna maji, hakuna vyoo, hakuna acces roads, zilipo basi ni mabonde na huaribu vyombo vya usafiri kila siku.

Yapo mengi ya kusema mengi, hii forum haitoshi kuyamaliza. Ninaweka baadhi ya picha nilizopiga Singapore, mwanzoni mwa mwaka huu. Utaona kabisa hawa ni watu waliopo serious na wan plans za miaka mingi ijayo.
 

Attachments

  • IMG-20130303-00565.jpg
    IMG-20130303-00565.jpg
    419.1 KB · Views: 63
  • IMG-20130308-00603.jpg
    IMG-20130308-00603.jpg
    459.2 KB · Views: 60
  • IMG-20130308-01416.jpg
    IMG-20130308-01416.jpg
    302.7 KB · Views: 60
  • IMG-20130308-01422.jpg
    IMG-20130308-01422.jpg
    255.8 KB · Views: 59
  • IMG-20130308-01436.jpg
    IMG-20130308-01436.jpg
    178.8 KB · Views: 60
  • Singapore-20130308-00606.jpg
    Singapore-20130308-00606.jpg
    341.6 KB · Views: 64
  • Singapore-20130308-00605.jpg
    Singapore-20130308-00605.jpg
    554.6 KB · Views: 56
  • Singapore-20130305-00586.jpg
    Singapore-20130305-00586.jpg
    119.8 KB · Views: 61
  • Singapore-20130305-00582.jpg
    Singapore-20130305-00582.jpg
    754.9 KB · Views: 59
  • Singapore-20130304-00576.jpg
    Singapore-20130304-00576.jpg
    93.9 KB · Views: 55
hii master plan ya Dar es Salaam imefikia wapi?

Dar city master plan underway
By Devota Mwachang`a|4th February 2013

Dar es Salaam residents have been advised to suspend the construction of residential and commercial buildings until the new Dar es Salaam City Master Plan is out next month. The Master plan is meant to provide development programmes for Dar es Salaam City to guide and control its spatial development for a period of 20 years to come.

Currently, the meetings to discuss the First Draft Master Plan report for the city are proceeding whereas the comments and recommendations will be necessary to the consultant in refining the Final Draft plan report. Speaking to The Guardian shortly after the presentation of the Final Draft report for Dar es Salaam City Master Plan (2012-2032) Principal Town Planner Secretary, Tommy Kapinga said the new Master plan might affect some buildings and development.

"It's better for those who have started construction to be patient and wait until the project of the knew master plan complete in between one month from now, this will avoid unnecessary demolition of their buildings and enable them to know the proper areas for the construction as located in the master plan…" he said.

Musa Naty, one of the public stakeholders at the presentation of the report said the existing Master Plan of the city was found to be overtaken by physical development events and therefore called for review of 1979 Master Plan were change as which have taken place since then.

"Among the changes rapid and uncontrolled physical development which has not always been in line with the proposals indicated in the previous Master Plans, frequent national changes in administrative policies, the increase in the rate of industries more than it was planned for, rapid increase of population and the growth of unplanned settlements…" he said.

Naty noted that has been growing into a big Metropolitan City with modern institutions, industries and accommodating an ever increasing population, this growth has resulted into migration of people from rural areas and the consequent population growth have had tremendous demand upon land uses and supporting facilities like transportation, foul and storm water and electricity supply, education and health as well as housing.

Additionally, he said the vision is to build Dar to be a city with sustainable development, managed on the principles of good governance, where residents do not live in poverty and have decent standards of living and a city with a competitive environment which attracts investors.
 
Dada Anna tunashukuru, lakini unatakiwa uelewe Tanzania tatizo sio master plan , tatizo ni akili ndogo kutawala akili kubwa, na watu wenye akili kubwa kukubali kutawaliwa na akili ndogo, hatutofika kokote na hizo master plan, kwani sinza ilikuwaje master plan, mwenge kijijini, reserve land ngapi za barabara zimeliwa, hote lngapi zimejengwa within 200 meters from the ocean, maghorofa mangapi yamejengwa kuliko urefu unao ruhusiwa sehemu hizo, play ground ngapi zimefanywa viwanja vya makazi au biashara.

Mkiacha kutawaliwa na akili ndogo ndiponitaanza kuamini hizi master plan zenu, na mnatakiwa muanzie kwenye chama kutawaliwa na akili kubwa, china na hata Singapore wao hawatawaliwi na akili ndogo, bali akili kubwa. sasa hivi mnatoa viwanja nk, lakini miundo mbini ya maji na maji taka hakuna, matokeo yake mtu moja inabidi uvute maji toka mile kadha ili uweke maji kwenye kiwanja chako, na uweke cesspit tank kwa ajili ya maji taka, wakati hayo maji tak au takataka Prof Mwandosya angetengenezea umeme au mbolea, mpaka najiuliza hivi huko kwenye baraza la mawaziri hua mna jadiliana nini?

Na suala madeski mpaka leo hii bado kulitatua kweli nalo mnashindwa kusema kila mzazi amnunulie mwanae desk na liwemali ya huyo motto mpaka ana maliza darasa la saba, basi kila mtu ataangalia kilio chake, akimaliza la saba, ampe mdogo wake au atoe sadaka hapo shuleni. uwanja wa ndege wa bukoba atreast uwe wa lami sio mvua ikinyesha ndege haiwezi kutua kwa sababu ya utelezi, na msisubiri mpaka Kagasheki atumie u alwatana wake ndio mfanikiwe hilo, wana bukop mkichanga fedha na halmashauri haliwezekani hilo? na subiri utekelezaji mimi hizo master plan zime nichosha.
 
Habari njema hii Prof. sawa huko Kingamboni tupaendeleze kwa kiwango cha juu kama ilivyopangwa, ila kuweni makini na mikataba mnayoingia na hao watu, maana Ufisadi na uingiaji wa mikataba mibovu imekuwa ni tatizo, serikali yetu ni kama imeweka pamba masikioni.
 
Mama Tibaijuka, Nadhani ww unaupeo mkubwa sana lkn hii uliyoleta ni mpya. Ningependa kujua miaka yako takriban 10 umesaidia nini Tanzania yako? Ulikuwa UN Habitant hukufanya lolote sasa waziri wa Ardhi hata manzese umeshindwa kuibadilisha. Viongozi wote kazi yenu kusifia wengine Singapore bwana kumejengwa vizuri sana, badala ya kusema muleba nimeongoza vizuri kwa kuhamasisha master plan. Ninyi wote ni viongozi wa kuchumia matumbo yenu. Kwenu uongozi ni Ajira na sio wito kuijenga nchi. Kuwa na aibu, hayo ungemwambia Mhe rais na sio kutusanifu. Kigamboni tu inakutoa jasho.
 
Mimi si ungi mkono wazo la kung'ang'ania Dar kwa kila kitu. Dar iachwe na bandari pamoja na biashara. Shughuli za utawala (kitaifa) ziende rasimi Dom na Ikulu ya Dar iwe nyumba ya sanaa/makumbusho. Sasa kila kitu Dar majengo mapya ya Wizara yanajengwa Dar na huku tanadanganya eti makao makuu ni Dom.
 
niongeze na kuhusu usafi wa beach zetu iwe baharini au maziwani, halafu tuje kwenye mifereji inayo pita katika mitaa yetu
 
Mwisho,kuuendeleza mji wa kigamboni pekee haitasaidia kama Squatter zinaendelea kuota sehemu nyingine za Dar. Ili kupunguza makazi holela wizara iakikishe inapima viwanja vingi kadri itakavyowezekana maeneo mengine.

Sio Dar peke yake... Squatters zimejaa na zinaongezeka miji yote Tanzania...
We need a "Powerful person" kwenye hiyo wizara...
 
samahani mama hivi ule mji wa kigamboni mmefikia hatua gani? hizi ni kati ya sababu zinazofanya project nyingi zisifanikiwe unawaza ya mbele sana
 
Back
Top Bottom