Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Ili tuondokane na miji holela
lazima kuwepo na nyumba za bei nafuu
watu wawe discouraged kujenga wawe encouraged kununua au kukopeshwa cheap houses..

na serikali iache kupimia watu viwanja,badala yake ipimie makampuni maeneo yajenge nyumba kwa wingi...

Mtu mzima, kwani umesahau kuwa hizi nyumba za Mchechu za milioni sitini za saiv ndo hizo tunaambiwa za bei nafuu....
 
Mama Prof.Tibaijuka,
Waziri jasiri,zimetolewa hoja nzito hapa jukwaani ni wakati wa wewe kuja kufanya majumuisho sasa,.ila nilichokipata toka kwa wadau ni kwamba siku nyingine ukija humu jukwaani hasa kuhusu mradi wa Kigamboni,njoo na implementation plan maana ipo na sio haya madesa maana hata sisi tukigoogle tunayapata,tuambia changamoto unazozihisi na solns ni nini,nasi tuchangie...LINDA HESHIMA YAKO KWA KUYAWEKA HAYO YALIYO KWENYE MAKATARASI,ARDHINI ILI UKUMBUKWE NA VIZAZI KWA VIZAZI!
 
Tatizo mama si mji mpya mumewakataza watu kujenga kigamboni toka 2008 mmewakaza hadi sasa haijulikani lini mtawalipa mbona hili Jambo limekuwa Siri?
 
Mama yetu Tibaijuka tunakuheshimu sana lakini wanaochelewesha maendeleo ya nchi hii si wananchi. Unawajua; ni hao mafisadi mnaowalea, Au mnawaogopa nchi itatikisika mkiwagusa?
Nchi hii mkiondoa ufisadi tutapata maendeleo. Wala hatutakuwa na haja ya kuomba misaada, Tutashirikiana nao tu kiutaalamu.
 
Kweli Mh. Tibaijuka unachapa Kazi .
Hadí umekuja huku.
Kua na masterplan ya Miji ni jambo jema kabisa, lakini ugumu unakuja kwenye utekelezaji maana ktk nchi yetu hakuna ' NIDHAMU' ya utendaji ktk maeneo Yote . Sijui kama dar es salama ilivyo ndivyo ilivyopangwa kuwa? Nadhani serekáli ingeimarisha vyombo vya kusimamia nidhamu ili kila Mtendaji serekalini atimize wajibu wake kikamílifu na Kufikia malengo yaliyowekwa. Unaona katika Miji yetu watu wanabomolewa Nyumba zilizojengwa ktk maeneo yasiyoruhusiwa ,lkn waliokua na wajibu wakuhakikisha kua pale hapajengwi hawachukuliwi hatua.
Hata Dodoma mamlaka ipo lkn haikuweza kusimamia na leo watu wanabomolewa, waliouza maeneo wanaendelea kua salama huku pengine walishahamiswa hivyo kuendelea pia kuharibu na pengine wataingizwa kwenye mamlaka ya mji wa kigamboni ! huku wananchi wanaathika.
ktk plan yako mahakama ikihusika utakua na miaka mitano kusubiri kesi iishe na hapo uombe Mungu isiwepo rufaa! Maana tuna 'Uhuru wa Mahakama'
Ili kufanikisha Mipango Yako mizuri uanzie kwenye Baraza La mawaziri ili serekali isimamie tu nidhamu yaani sheria na kanuni zilizowekwa Kwa usawa. Nimegundua kua watanzania hawana tatizo na sheria kama inatekelezwa kwa usawa na haki.
Mahakama , polisi wataalam wa ardhi halmashauri nk watimize wajibu bila kuweka malengo ya maslahi binafsi kwenye mipango mbalimbali ya serekali .
Wataalam wa wizara Yako Ndio watumishi wa ajabu zaidi Tanzania , lkn wamekua hivyo Kwa miaka mingi , inahitajika nguvu kubwa sana kurejesha nidhamu.
Nina chotaka kusema ni kua ni sekta nyingi sana zinahusika ili kutekeleza Mipango mbalimbali uone hili na ujue jinsi ya kupambana na changamoto zake .
..naomba nizungumzie Kariakoo , mpango wa pale ukoje hasa maana Biashara zote zinafanyika pale!
Kuanzia mchicha hadí Magari!
Kila Mtu anafungua Biashara Kariakoo !
Na wanunuzi wote watanzania na kutoka nje ya Tanzania kama Kongo , Burundi , Rwanda , Zambia , Zimbabwe nk wanaelekea Kariakoo Kununua . Kwani pale pana ukubwa gani ?
Hali hii imesababisha bei ya 'frem' Kupanda sana na wenye Nyumba kubana sana ukubwa wa fremu na hivyo kudumaza Biashara lkn kusababisha Ujenzi mkubwa kuelekezwa tu Kariakoo sababu ya faida kubwa Kwa Nyumba ambazo ziko Kariakoo .
Wataalam wangeamua Kwa mfano Kariakoo pawe ni vyakula Nguo viatu na serekali ikaweka viwango (ubora) vya frem. Spare za Magari Temeke , Vifaa vya Ujenzi Buguruni nk (hapa nazungumzia maduka Ya jumla) nadhani ikiwa hivi hata usafi ungewezekana na mji wote wa Dar es salaǎ ungejengwa sawia.
Mwisho mimi nakutia Moyo sana mama Tibaijuka huwa ninavutiwa sana na utendaji wako.
Asante sana.
 
Labda swali la Msingi, tunahitaji kufanya Land reclamation Tanzania?

Kwa nini wameenda kujifunza reclamation kama hatuihitaji?

Land reclamation ni kwa wale wasio na ardhi kama hao Singapore na Uholanzi, sijui ina apply vipi kwa nchi kama Tanzania ambapo Makazi na Kilimo havifiki hata 30% ya nchi nzima!!
 
Anna Tibaijuka mbona uko kimya kuhusu mpango wako wa kuiendeleza Kigamboni?
Una lipi la kutuambia sisi wakazi wa Kigamboni, maana kimya kimetanda sasa na hatujui kinachoendelea.

Buji, Mama Anna amesema Wasingapore watasaidia katika mpango mji wa Kigamboni.

Inawezekana ni huo usanii wa kuandaa mpango mji mpya baada ya kugundua ile michoro ya mwanzo na video walizotoa ilikuwa ni kwa ajili ya kampeni na uchaguzi.

Inawezekana pia ni njia ya kutafuna "vijisenti" kwa kushirikisha wadau"wataalamu" wa mipango miji wa Singapore.

Tanzania na kutafuta ufadhili na misaada ndio sera ya kuleta maendeleo. Lakini pia unaelewa UDSM na Chuo cha ardhi havina wataalamu wenye uwezo wa kuchora michoro ya kupanga miji yetu.

Mama Anna hivi mnawashirikisha na wataalamu wazawa katika kuandaa master plans ya miji yetu au wadhungu na wachina tu ndio wataalamu?
 
WanaJF

... WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni. ......

View attachment 97055

Mama Tibaijuka

Mama Tibaijuka

Wasingapore wanakuja kutusaidia katika ujenzi mpya wa Kigamboni.

Ni msaada gani huo watakaokuja nao?

Je wao tutawalipa nini? Watataka mawe na udongo ili wapeleka kwao kwa ajili ya kufukia hiyo bahari ili wapate ardhi ya kujenga na kuutanua mji wao?

Na mna mipango ipi kuendeleza vijiji ambako watanzania wengi ndio wanakoishi viwe vya kisasa na kupunguza kasi ya vijana kukimbilia mijini kuja kuzurura (kutafuta maisha)?
 
Hongera sana mama prof. Tiba, nafurahia utendaji kazi wako. Sasa basi agiza wasaidizi wako kwa kushirikiriana na ofisi ya waziri mkuu - TAMISEMI, halmashauri zote nchini ziandae master plan za wilaya zao na wasimamishe ujenzi holela holela. Ujenzi holela hautokani na usimamizi duni wa sheria peke yake bali pia wananchi kukosa uelewa. Mipango miji katika kila wilaya wafanye kazi ya kuelimisha umma ili sheria zitakapokuwa implemented waelewe kuwa ni wao walikaidi taratibu. Elekeza nguvu katika hilo kama ambavyo umezielekeza kuhakikisha jiji jipya la Kigamboni linafanikiwa. Mungu akulinde, akupiganie na akufanikishe katika yote!
 
Mhe,
Naumia sana napoona uwezo wako wa utendaji,matarajio yangu yamekuwa tofauti.

Ipo kazi kubwa ya mipango mji inayotakiwa kufanyika Tanzania,wewe umeona hilo tu,ili mradi upate kibali cha mji mpya kigamboni.

Tafadhali nitakuona wa maana japo ukizungumzia master plan ya mwabupande

Tengeneza City in the forest,academic city,tourist city na kadhalika......

Acha ushabiki wa kisiasa,kuwa mtendaji wa fani yako.
 
BADO NASUBIRI MAJIBU KUTOKA KWAKO.

Pole na kazi mama Tiba, lakini pia si vibaya ukajibu tuhuma zifuatazo kuondoa wingu juu ya mradi huu, Mnamo tarehe 7/December 2012 inasadikika wewe mheshimiwa waziri ulisafiri kwenda nchini Thailand ambako ulikutana na wakuu wa kampuni kutoka China kusaini mkataba wa ujenzi wa mji kisasa wa Kigamboni. Mheshimiwa kwa mujibu wa vyanzo mhimu wewe utapata 3% kama aksante kutoka kwenye kampuni hii kutoka nchini china?


Pia kuna lawama kutoka kwa wadau wakuu ikiwemo wabunge na madiwani ambao ni wawakirishi wa wananchi hukuwashirikisha katika maamuzi juu ya mkataba huu na mradi kwa ujumla.

Mwisho tungependa kujua ni lini zabuni ya ujenzi wa mji wa kigamboni ilitangazwa kwa mujibu wa Public Procurement Regularity Authority-PPRA, ni kwa kupitia mtandao gani au gazeti gani la hapa nchini au nje ya nchi ilitangazwa (International Competitive Procurement-ICP) ili tujirishe kuwa kulikuwa na uwazi katika diri hili. kwa mujibu wa PPRA thamani ya mradi huo hauwezi kuwa Single source au International shoping. Tunaomba kujua sisi wananchi wa kawaida.
 
Mhe,
Naumia sana napoona uwezo wako wa utendaji,matarajio yangu yamekuwa tofauti.

Ipo kazi kubwa ya mipango mji inayotakiwa kufanyika Tanzania,wewe umeona hilo tu,ili mradi upate kibali cha mji mpya kigamboni.

Tafadhali nitakuona wa maana japo ukizungumzia master plan ya mwabupande

Tengeneza City in the forest,academic city,tourist city na kadhalika......

Acha ushabiki wa kisiasa,kuwa mtendaji wa fani yako.

Fani ya huyo mama ni UCHUMI
 
Mi naona kuliko kuongeza plans nyingine zikawa nyingi alafu zikashindwa kutekelezwa,
Kwa nini tusianze na miji iliyopo kwanza angalau hata moja? Dar fly over zinawekwa sawa, lakini zile kwa jinsi zilivoandaliwa hata kama ni kupunguza tatizo la traffic jam itakua ni kidogo sana, na kumbuka kila siku idadi ya watu yazidi kuongezeka pale, ni kama vile Tanzania nzima inahamia dar, Sijawahi sikia plan ya Tanzania kujenga Underground Subways? Maana nchi za nje hichi ni kitu ambacho kinasaidia sana wasafiri, kuliko kukaa kupangana muda wote huku juu, mtu unaingia underground unatokea unapotaka bila kuinterfere na magari huku juu, hata hii train ambayo mmeweka sasa magari yasimame ipite alafu ndiyo yaende mbona ni jambo la ajabu? traffic jam inatakiwa kupunguzwa ila mbona kama inaongezwa? Miji mingi pia ni michafu mno, kama barabara tu zimebomokabomoka za majiji makuu Tanzania, iweje kuweka plan ya mji mpya huku iliyopo tu iko ovyo? hakuna hata moja wa afadhali au ndio huo mpya mnataka uwe na uafadhali? sasa si watu wote watajaa au ndio ile kila tajiri anawahi plot yake afu wengine wa ngazi ya kati na chini itabaki ndoto kwao. Ukweli Kingamboni wameipamba kweli lakini transport system yake haina utofauti na transport system za miji mingine, Transport ni kitu muhimu sana ili mji uonekane uko safi maana muda wote watu wako safarini tu... My take narudia kitu Tanzania ingeanza nacho ni kushughulikia transport systems kwanza kufanya underground plan na wapi subway stations ziwekwe, na majengo vilevile ya majiji yaliyopo kuliko kuanza na kitu kipya
 
Hongera mama, kazi ya mikono yako tunaiona.! Jitahidi kwa nafasi yako watanzania wote tuko nyuma yako..!

Kazi ya mikono yake ipi ya usanii? Ameshafanya nini toka amepewa hiyo wizara zaidi ya usanii mtupu?!!!
 
Halafu mama Tiba JF siyo ya watu wa hivyo unaowafikiria ni ya maGT,umeleta post yako isiyo husiana na
sisi watanzania juu ya Singapore ambayo haina ardhi wakati sisi tuna ardhi kibao tatizo hatuna viongozi
wenye roho za uzalendo,halafu unaishia kuingia humu kama guest hujibu hoja'
 
kutoa maoni yako kwa serikali hii ni kutwanga maji kwe kinu. mh wewe labla unajiona tofaut lakin kwakua umo humo mimi nakuona walewale tu. mangap ya wataalam yameshauriwa hamtekelez?
kimsingi serikali hii haina nidham inayohitajika kufanya hao wa-nje wanayofanya. labla kama linahusu tu kuandika au kusema bt likifika kwe pesa/ utendaji mmmh. mifano ni mingi chagua mwenyewe.
 
WanaJF

Nilikuwa mmojawapo wa viongozi tulioandamana na Mhe Rais katika ziara yake ya majuzi nchini Singapore. Ninawaletea sehemu ya Master Plan ya mji wao mpya unaojengwa kutokana na kuokoa ardhi baharini (reclamation). Unaona kila kipande cha ardhi mpya kimeshapangiwa matumizi yake na kuwekewa malengo ya majengo yanayotakiwa.

Kupanga ni kuchagua. Kunahitaji nidhamu na hakuna mchezo wala utani. Huwezi kuwa na mji uliopangwa kama unapenda na kuendekeza uholela na vurugu (chaos). Kinachotakiwa ni kushirikisha wadau wote kupanga malengo na viwango baada ya kupata maoni ya wataalam. Wanaoarithirika na kulazimisha kuhama kupisha maendelezo mapya wanalipw fidia stahiki na endelevu.

Anayedai vinginevyo si msema kweli. WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni. Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.

View attachment 97055

Mama Tibaijuka

69177_157820217583469_4081295_n.jpg
na hii ndio plani ya miji ya Tanzania, sasa mama kwa nini angalau usiunde vikosi jamii kwenye kila kata kama mfano inavyoanzishwa vikundi vya polisi jamii vitavyohakikisha kuwa kila kiwanja kina access the barabara na kuweka kipimo cha chini cha kiwanja. hamuwezi kukaa mnajivunia miji ya wenzenu huku yakwetu inazidi kuhabirika

Serikali ya CCM ni ""Makini Sana"" hizi picha ni za enzi kabla ya Uhuru 1961 Sasa hivi Maisha ya kila Mtanzania yamekuwa bora kama tulivyowaahidi. Mkakatiwetu ni kuboresha miji kama Kigamboni na mingine nchi nzima.
 
Ndio maana nashangaa, why land reclamation in Tanzania ambapo tuna ardhi ambayo wala hatujai-utilise kabisa?

Kama hii ilitokea kama 'by the way', kwa nini aripoti by 'the ways' aache ya msingi yaliyowapeleka?

Ageleta taarifa ya kilichowapeleka na walicho-achieve ningeona mantiki labda.

Land reclamation ni kwa wale wasio na ardhi kama hao Singapore na Uholanzi, sijui ina apply vipi kwa nchi kama Tanzania ambapo Makazi na Kilimo havifiki hata 30% ya nchi nzima!!
 
Back
Top Bottom