Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Master PLan ya Mji mpya wa Singapore


Serikali ya CCM ni ""Makini Sana"" hizi picha ni za enzi kabla ya Uhuru 1961 Sasa hivi Maisha ya kila Mtanzania yamekuwa bora kama tulivyowaahidi. Mkakatiwetu ni kuboresha miji kama Kigamboni na mingine nchi nzima.
kama unaongea na watanzania wanaoishi ngambo mda mrefu labda watakusikiliza lakini kama unaongea na watanzania wanaoishi Tanzania nakushauri tena acha kutaja chama chako maana unakiabisha. waulize serikali wenyewe kwa nini mfumo wa anwani za makazi umekwama kama sio makazi holela yanakwamisha. Tena mtu kama wewe hufai uongozi kabisa maana tunapaaza sauti ili serikali itekeleze wewe unawapaka watu mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
WanaJF

Nilikuwa mmojawapo wa viongozi tulioandamana na Mhe Rais katika ziara yake ya majuzi nchini Singapore. Ninawaletea sehemu ya Master Plan ya mji wao mpya unaojengwa kutokana na kuokoa ardhi baharini (reclamation). Unaona kila kipande cha ardhi mpya kimeshapangiwa matumizi yake na kuwekewa malengo ya majengo yanayotakiwa.

Kupanga ni kuchagua. Kunahitaji nidhamu na hakuna mchezo wala utani. Huwezi kuwa na mji uliopangwa kama unapenda na kuendekeza uholela na vurugu (chaos). Kinachotakiwa ni kushirikisha wadau wote kupanga malengo na viwango baada ya kupata maoni ya wataalam. Wanaoarithirika na kulazimisha kuhama kupisha maendelezo mapya wanalipw fidia stahiki na endelevu.

Anayedai vinginevyo si msema kweli. WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni. Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.

View attachment 97055

Mama Tibaijuka

Ndugu Waziri,

Walioko nje hawatakusaidia sana kwa kuwa na hata wewe ulikuwa nje na umesaidia sana kupanga maeneo mengi tu nadhani.

Tulioko ndani ambao hatuwezi kufikiwa na huduma za maji, zimamoto, na hata magari ya kwenda hospitali ndio tunaweza kukusaidia.

Tatizo liko Wizarani kwako. Wizara haina mkakati wa kupima viwanja na kuwapa wananchi. Viwanja imekuwa kama lulu vikitangazwa watu wanaenda kukesha kwenye foleni kuchukua form. watumishi wa wizara wanajilimbikizia viwanja na kuviuza kwa bei ya kuruka kwa wananchi wenye uwezo wananchi masikini wakiendelea kujaza mabanda mijini.

Wizara inafanya supply ya viwanja iwe scarce ili demand iwe kubwa na watumishi wake walijilimbikizia hivyo viwanja vichache waweze kuviuza kwa bei ya juu. Rushwa ndio inajaza mabanda mijini. Safisha nyumba yako kuna siku tutakuwa kama Singapore na wala hatuwahitaji kuja kutusaidia. Kama wewe ulikuwa mkuu wa Makazi wa UN unatafuta Waindonesia waje kukusaidia kitu gani tena. Tulitegemea utusaidie Watanzania baada ya kutoka UN lakini sasa tena unaenda kuomba usaidizi Indonesia!

Pima viwanja mama vimwage miji itajipanga.
 
Mh..Pole na safari...Ulikuwa mkuu wa UN Habitat...tunajua unajua mengi..Ila sisi mazoba wa Tanzania ambao Keko magurumbasi na Tandale kwa Mtogole Jiko na choo vinapeana mgongo?
unataka kutuambia nini kwa picha yako na mtu wa Makete anayeingia hapa mtandaoni au mtu wa Old Moshi , hata Iramba kule kwa Mwigulu na Shinyanga huko, Njombe na pengine.
Wanaona ufahari gani kwa hiyo new plan wakati shule mashaka, Afya ni mashaka?
Sipingi hoja yako..ni nzuri ila where to deliver your idea and expect reputation is a problem. Mimi ni maoni yangu tu..Hoja umeleta nimesema langu...
Itoe na bakiza hii topic na wenye viwanja kigamboni pamoja na Ikulu mtende kazi..Msetegemee jibu zuri kwa watu wa Galapo Babati au sehemu za kuleeee jimboni kwako kuwa za kukusaidia sana
 
Uholela una athari nyingi sana ambazo hata ukurasa huu hauwezi kutosha kuzieleza. mama fanya kazi yako, wewe ni jembe isipokuwa madiwani wamekushindaje??? mji huo wa Kigamoni ulitakiwa kuwa na tume maalumu ya kuuendesha mpaka utakaposimama (kama ilivyokuwa tume ya jiji chini ya Keenja). Hao jamaa wataleta siasa mpaka mipango yako itavurugika na wewe ndiyo utaonekana umefeli sio wao. HONGERA SANA MAMA.
 
WanaJF

Nilikuwa mmojawapo wa viongozi tulioandamana na Mhe Rais katika ziara yake ya majuzi nchini Singapore. Ninawaletea sehemu ya Master Plan ya mji wao mpya unaojengwa kutokana na kuokoa ardhi baharini (reclamation). Unaona kila kipande cha ardhi mpya kimeshapangiwa matumizi yake na kuwekewa malengo ya majengo yanayotakiwa.

Kupanga ni kuchagua. Kunahitaji nidhamu na hakuna mchezo wala utani. Huwezi kuwa na mji uliopangwa kama unapenda na kuendekeza uholela na vurugu (chaos). Kinachotakiwa ni kushirikisha wadau wote kupanga malengo na viwango baada ya kupata maoni ya wataalam. Wanaoarithirika na kulazimisha kuhama kupisha maendelezo mapya wanalipw fidia stahiki na endelevu.

Anayedai vinginevyo si msema kweli. WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni. Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.

View attachment 97055

Mama Tibaijuka

Mama naona unataka kushusha heshima yako.Ni bora kukaa kimya kulikoni kuja na hoja hizi.Picha haziwasaidii watu.

Kwa hoja hiyo hapo juu inaonekana unataka kuwashawishi watu /Wana Jf kuwa Watu wa Kigamboni hawautaki mradi siyo?

Kitu hicho si kweli na umekutana na Kamati ya Wanakigamboni mara kadhaa kuhusu jambo hili.

Utasababisha watu waje humu na makabrasha yote uliyoyakalia Ofisini na kwingineko ambayo yana lundo la mapendekezo ya wadau/waathirika wa Mji Mpya wa Kigamboni na namna bora yakufanikisha mradi huu na ambazo kimsingi Wizara yako haitaki kuyafanyia kazi na badala yake wanazunguka mitaani kuwa laghai watu wasiojua kusoma na kuandika.
 
NHC hawatoweza kusimamia, ingekuwa ni shirika binafsi, hizo kodi wanazokusanya na assets za majumba waliokuwa nayo hawana hata sababu ya kukusanya mtaji, wana mtaji tosha kabisa. Lakini wamekalia pale kujineemesha wao tu.

waliuza hisa watabadilika
 
Mama Tibaijuka hawezi kujibu mpaka atoke kwao kunywa rubisi. Akija amelewa hamtaamini kama ni majibu yanatoka kwa Profuessa!
 
waliuza hisa watabadilika

mkuu hapo kwenye red nadhani, panahitaji rekebisho!!
Bajeti mpya, TIB, ime megwa kuwa benki 2, na pia kuna benki ya Kilimo TADB (ADB) hiyo inaanza na mtaji wa shs.100b toka serkalini. Hivi kwani haukuwa wakati wa kuweza kuipatia fedha NHC? au kuiruhusu NHC baada ya kuifanyia mabadiliko ( moja ni kuacha kuuza nyumba bali kupangisha) hii ni kwa muda angalau 15-20 year ili kumantain consistance ya cash flow. Kuipeleka public NHC ni muhimu kuliko jambo jingine kama anataka makazi bora na kuondoa makazi holela.
Hivi ile TBA (Tanzania Building Authority) inafanya nini hasa, mipango yake na mafanikio yake yamekaaje kwa sasa.
SP
 
Mheshimiwa Profesa,mipango miji na makazi ni tatizo kubwa kwa serikali yako wakati ni chanzo endelevu cha MAPATO YA SERIKALI.Mkiacha siasa pimeni basi maeneo yote na maeneo ya akiba yaeleweke.Pia sisi tuna ardhi nyingi kuliko hao wenye kuhitaji reclamation lakini bado serikali ni dhaifu mno.Iwapo DAR kuna makazi holela zaidi ya 70% ya makazi,TANDAHIMBA,ROMBO,NGARA NA KWINGINEKO?
 
Kutuletea hiyo plan yako toka Singapore ni muendelezo wa fikra zenu za kutaka kupata 10% yenu huku mnashindwa kutatua matatizo yaliyopo kwenye miji yetu kwa muda mrefu!! Hapa Dar watu wamelalamika mara ngapi kuhusu hii idara ya mipango miji kugawa viwanja hovyo mpaka wanaziba barabara na kusababisha maffriko ya maji wakati wa masika kwenye makazi ya watu; Tibaijuka anza kusahihisha uozo huu kwenye majiji ndio baadae utilie mkazo huko Kigamboni!!! Tunajua wewe na bosi wako muda wenu ndio unakaribia kufika ukingoni na ndio maana mnakazania miradi mipya ,lakini mkumbuke kuwa nyie mtatoweka lakini Tanganyika itabakia baada ya nyie kwenda mbele ya haki; hivyo mnapaswa kuweka uzalendo mbele ya maslahi yenu binafsi!!
 
attachment.php
 
Mipango si matumizi,, hii nchi ina mipango mingi sana, lakini mpaka sasa haijatekelezwa na mingine haitekelezeki,,, mngetumia akili zenu na shule zenu kwenye miaka hii 10 ya the utawala wa huyu le'profeseri basi kuna mambo mawili au matatu yangekuwa yameshatekelezwa, mfano unaweka plan wakati miundombinu mibovu, huna umeme... Hizi plan zitafanikiwa tu kama siku tutapata uongozi bora..
hela za utekelezaji wa hiyo plan bila shaka hazitoki mfukoni kwako na kwa sasa haupo kwenye wizara na nchi haina policy, 2015 uchaguzi unategemea nani atatoa hiyo fund,,
huo mji utasaidia nini katika taifa hili masikini, je ni muhimu kwa sasa??? Wananchi wa hali ya chini kama waalimu na madaktari Itawasaidiaje??? Nini manufaa ya miradi iliyopo kwa mtanzania???
 
Back
Top Bottom