Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Mama hii ndo nini? zawadi kwa watanzania kutoka Singapore? master plan ya mji na tena wamekuahidi kusaidia ujenzi? kwa interest zipi? kwa hiyo hii ndo habari umealetea watanzania kutoka Singapore,master plan ya mji wa kigamboni!? na unaamini Watanzania wamefurahi na wamekupongeza?! Mama kuwa makini. wanakijiji wa jimboni kwako watanufaikaje na master plan ya mji wa Kigamboni? vitu vingine vya kwenu m'bakinavyo,mara Wamarekani mara Singapore! hopeless
 
Hivi mama Tiba si ninasikia Dar ilikuwa na master plan yake iliyotengenezwa na wakoloni na ambayo ilizingatia ukuaji wa jiji hili tangu enzi hizo hadi miaka mingi ijayo lakini kwa ukaidi wa wanasiasa hawakujali hiyo kitu ambayo leo inatusumbua?iko wapi hiyo kitu?tusifanye makosa kwa miji midogo inayokua muwe tayari mmeipangilia.msiwaze Dar tu.ni uzuri wa miji hiyo utakaopunguza ongezeko kubwa la watu kwenye mji kama Dar.Kuhusu Dar yenyewe,mie nadhani kuna umuhimu wa kuupanga mpya mji wote huu na si Kigamboni tu.na katika kufanya hivyo msitumie nguvu bali akili huku utendaji na kauli zenu vikionyesha kuwa nyinyi mpo kwa ajili ya wananchi na si watu wachache.natanguliza hili kutokana na uzoefu wetu wabongo wa kuingiza siasa na ufisadi hata ktk very technical and sensitive issues.nasisitiza kama hamtaweza kuwa na discipline ktk kusimamia na kutekeleza project hii ni heri muiache tu hadi kutakapotokea viongozi disciplined.Dar inaweza kupangiliwa kwa serikali na makampuni binafsi kukabidhiwa utaratibu wa kujenga mji kulingana na master plan iliyoko.master plan hiyo izingatie utaratibu halisi wa maisha na mazingira ya wabongo nchini mwao mf.wabongo wengi hupendelea nyumba za nafasi kwa ajili ya makazi na si sana maghorofa na ardhi yetu inaruhusu ujenzi kama huo.wapo wengi ambao wana uwezo wa kupanga zile nyumba za ghorofani NSSF lakini hawapendi maisha yale ya kulundikana kwenye jengo moja.wapo wenye system hizo lakini wengi wetu hatupendi.sasa mkishaleta plan sahihi kwa mazingira yetu,how do you implement?mie nadhani mortgage inaweza kusaidia sana.cha msingi shusha bei za kupanga na kununua majengo na nyumba za serikali ili kuvutia watu kwenye utaratibu huo huku nyumba na majengo hayo yakijengwa na makampuni ambayo yanakuwa monitored kufuata plan iliyopo.gradually mnabadilisha mji na watu wakishakolea baadae,hata mkija kuweka sheria ya kupiga marufuku ujenzi bila kibali maalum cha manispaa hadi kwa watu wanaojenga nyumba ndogo tu za kuishi,watu hawataona mzigo.tena nyumba zenu zikijaa maji na umeme wa uhakika na mitaa mpangilio mzuri watu hawataona umuhimu wa kujenga wenyewe.ushauri wangu binafsi,ni muhimu kujenga upya miji yetu kwa kuzingatia SECURITY ya watu ktk disasters na hasa zile za asili.kiwango cha majanga ya asili duniani kinaongezeka sana na huko mbele hata miji kama Dar haitaachwa kukumbwa nayo.Dar nimeona assembling place moja tu pale Mlimani city,sijui ziko ngapi na zimejengwa vipi kwa kuzingatia emergency situation?this is my take,msipuuzie hili,jiandaeni na majanga mengi sana miaka ijayo,wala huu sio ushirikina,ni fact!
 
Hongera Mh.
Nafurahi kwamba ni mwana JF, nafikiri pia hii ndiyo njia sahihi ya kufikisha ujumbe kwa Critical thikers wenzako.
Kuhusiana na MADA, tumeona wenzetu walivyo serious hasa ukizingatia reclamation investment yahitaji fikra peve na endelevu.

Tatizo kubwa ninaloliona kuhusu kigamboni yetu;
1. Hatujafahamu hakika nania anayeendeleza mji huo na kwa faida ya nani? Je ni serikali kuu? Ni mwekezaji? Ni halmashauri ya Temeke ama ni jiji la Dar es Salaam?.
2. Nini hasa sababu ya kuchagua Kigamboni penye wa kazi tayari na kuacha maeneo km Kibaha, Kisarawe au hata Bagamoyo?
3. Nini faida hasa ya uwekezaji huo kwa Mtanzania?
 
Ndugu Tibaijuka,

Pamoja na kuja na hii master plan ya Singapore, je kuna vitu vingine ulivyojifunza :
1. Ukiwa UN Habitat
2.Ukiwa Waziri wa Makazi, na ukatembelea nchi nyingi tu.....kwa mfano, umewahi kufuatilia wenzetu wanalipaje kodi za nyumba nchini mwao? Au hili halikusumbui? Huku mtaani Mama, tunalipa kodi ya nyumba kwa Mwaka mzima....hili unalionaje Mheshimiwa sana? Kwamba mimi ni mfanyakazi wa kuajiriwa au kujiajiri, napata kipato changu kwa mwezi, nalipia karo watoto wangu kwa Mwaka, nalipa kodi kwa mwaka, hili halikusumbui Mheshimiwa?
Umebakiza miaka miwili kwenye serikali hii katika wadhifsa huu ulio nao, TUKUKUMBUKE KWA LIPI? kwa mji wa Kigamboni ? Kwa new satelite cities nchi nzima? Vipi hili la kodi ni lini utatoa waraka na KUUSIMAMIA kwamba ni marufuku kumdai mtu kodi kwa mwaka mzima wakati kipato chake ni cha mwezi? U wapi ubunifu wa makazi ya watu wa hali ya chini Mheshimiwa, ambayo umekuwa msimamizi wa makazi duniani?

Mheshimiwa, ulipoteuliwa kushika wizara hii tulishangilia sana kwamba hatimaye tumepata mtu ambaye anajua hasa tatizo la makzi duniani.......ila kadiri siku zinavyoenda, napoteza matumaini kwamba umeisahaingia kwnye "inner circle" ya kupiga dili kama kawaida ya vigogo wetu humu ncini, maana hatuoni ni vipi umejiandaa kusaidia watu wa kipato cha chini......Mheshimiwa naomba kuto hoja!
 
WanaJF

Nilikuwa mmojawapo wa viongozi tulioandamana na Mhe Rais katika ziara yake ya majuzi nchini Singapore. Ninawaletea sehemu ya Master Plan ya mji wao mpya unaojengwa kutokana na kuokoa ardhi baharini (reclamation). Unaona kila kipande cha ardhi mpya kimeshapangiwa matumizi yake na kuwekewa malengo ya majengo yanayotakiwa.

Kupanga ni kuchagua. Kunahitaji nidhamu na hakuna mchezo wala utani. Huwezi kuwa na mji uliopangwa kama unapenda na kuendekeza uholela na vurugu (chaos). Kinachotakiwa ni kushirikisha wadau wote kupanga malengo na viwango baada ya kupata maoni ya wataalam. Wanaoarithirika na kulazimisha kuhama kupisha maendelezo mapya wanalipw fidia stahiki na endelevu.

Anayedai vinginevyo si msema kweli. WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni. Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.

View attachment 97055

Mama Tibaijuka

Hongera kwa kutaka kujua maoni ya watanzania tofautitofauti kutoka sehemu tofautitofauti, viongozi wetu wengi hawafanyi hivi.
 
Mama kwanza shikamoo

Pili nimefarijika sana kwamba nawewe ni mwanachama mwenzetu wa JF

Tatu ni kwa wewe kutambua kwamba ndani ya JF utapata elimu, maarifa, maoni na mengi mengineyo

Nne na mwisho ni masikitiko yangu kwamba umeitupa hii post yako, nimesoma ukurasa kwa ukurasa, post kwa post lakini sijaona majibu yako. Au pengine nia yako hasa ilikuwa ni kupata maoni tuu?

Nikutakie siku njema mama yetu

Respect !!!
 
mkuu soma vizuri nadhani hujaelewa hapa "WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni"
siyo kuchora master plan, sasa ni kuanza ujenzi

mmmh kwahiyo na wao wanasaidia sasa hivi katika huo ujenzi sio.....si nilisikia mara wachina mara wamarekani full vurugu.....
 
Ndio maana nashangaa, why land reclamation in Tanzania ambapo tuna ardhi ambayo wala hatujai-utilise kabisa?

Kama hii ilitokea kama 'by the way', kwa nini aripoti by 'the ways' aache ya msingi yaliyowapeleka?

Ageleta taarifa ya kilichowapeleka na walicho-achieve ningeona mantiki labda.

Land reclamation inafanyika kwenye Maji (Bahari/Ziwa), that obviously kwa DSM inaweza ikawa Posta to Osterbay labda mpaka Kunduchi au Ununio. Nina uhakika hapa wame-target zaidi Posta, na ni kulekule kuendekeza ulimbukeni kwamba majengo marefu lazima yakae Posta.

Kama ndivyo basi tumekwisha maana kama kwa majengo yaliyopo Posta sasa, watu wanaamka saa 10 alfajiri na kufika ofisini Saa 3 asubuhi basi wakifanya hiyo reclamation yao watu watakua wanafika saa tano ofisini.

E mungu tunusuru!!
 
Wanasiasa wanakwamisha kila kitu kwa sababu ya kutaka umaarufu. Mfano katika mji wa Moshi unaosifika kwa usafi kwa muda mrefu, sasa huenda ukawa miongoni mwa miji michafu Tanzania. Ile sheria iliyokuwa inawabana wachafuzi wa mazingira kwa kutumia wazabuni wa kuwakamata wachafuzi wa mazingira sasa imezuiliwa na madiwani wa H/shauri ya Manispaa inayoongozwa na Chadema. Walichofanya ni kuwaondoa wazabuni na kuacha kazi hiyo ifanywe na watumishi wa H/mashauri ambao hawatoshi na hawako. Sasa hivi watu wanatupa taka watakavyo hata wewe njoo Moshi halafu utupe chupa yako ya maji hovyo, hakuna atakaye kugusa. Na kama si uumini wa usafi alionao mkurugenzi wa Manispaa, hali sasa hivi ingekuwa mbaya sana. MAMA TIBAIJUKA, SIASA ZA KUTAFUTA UMAARUFU ZINAANGAMIZA TAIFA HILI.
 
Jamani, sisi ardhi tunayo kwa nini posta tu?

Hivi gharama ni sh. ngapi kwanza ya miradi kama hii?
Okay, miundombinu yenyewe kama barabara na mengine haisapoti saana hili.

Hivi hawezi kuja kutufafanulia huyu Mkuu?

Land reclamation inafanyika kwenye Maji (Bahari/Ziwa), that obviously kwa DSM inaweza ikawa Posta to Osterbay labda mpaka Kunduchi au Ununio. Nina uhakika hapa wame-target zaidi Posta, na ni kulekule kuendekeza ulimbukeni kwamba majengo marefu lazima yakae Posta.

Kama ndivyo basi tumekwisha maana kama kwa majengo yaliyopo Posta sasa, watu wanaamka saa 10 alfajiri na kufika ofisini Saa 3 asubuhi basi wakifanya hiyo reclamation yao watu watakua wanafika saa tano ofisini.

E mungu tunusuru!!
 
Mama yangu Tiba

Kwanza nakusihi sana uache uongo. Umesema uongo mwingi sana Bungeni kuhusu mchakato ya mji mpya Kigamboni. Hasa swala la kushirikiksha wananchi. Unaufahamu ukweli na unajua kwamba tunaufahamu ukweli kwa sababu siku hizi teknolojia inatufanya tuyajue mambo pindi yanapotokea siyo ile zamani waziri ndiye pekee alikuwa anajua jambo

Pili, nakutaka uje kufanya mikutano na wananchi ujibu maswali. Mwaka juzi ulitengeneza ratiba ya kufanya mikutano kila kata. Ukafanya kata mbili maswali yakawa magumu ukaingia mitini

Baada ya hapo umekuwa ukiwahonga madiwani ili wakupe sapoti. Majuzi ukaanza tena kuwahonga wenyeviti wa mitaa ili waitishe mikutano wananchi waridhie mradi. Wananchi tulikataa. Lakini wewe umekwenda kuliambia bunge na watanzania kwamba sisi tumeridhia mradi na tunakupa sapoti sana. Wakazi wa Kigamboni ni wasomi na wanajua haki zao

Sasa unatundika hapa master plan ya Singapo uliyookota huko barabarani ulikokuwa unatembea. Ulipokuwa UN ulifundishwa kwamba mipango hufanywa hivyo? Ulipokakamaa Bungeni kila mwaka unadai mradi uko tayari na lazima uanze kumbe ulikuwa hata plan huna? Na sasa unasema Wasingapo wako tayari kusaidia kujenga, sisi wakazi wa Kigamboni tulikutuma hilo?
 
Mama kwanza shikamoo

Pili nimefarijika sana kwamba nawewe ni mwanachama mwenzetu wa JF

Tatu ni kwa wewe kutambua kwamba ndani ya JF utapata elimu, maarifa, maoni na mengi mengineyo

Nne na mwisho ni masikitiko yangu kwamba umeitupa hii post yako, nimesoma ukurasa kwa ukurasa, post kwa post lakini sijaona majibu yako. Au pengine nia yako hasa ilikuwa ni kupata maoni tuu?

Nikutakie siku njema mama yetu

Respect !!!

Anaisoma kimya kimya. Watoto wake na wasaidizi wake pia. Hakutarajia haya kwa sababu huwa hawa watu hawakutani na jamii. Hukutana na viongozi wenzao hasa wa ccm ambao huwadanganya na kuwakuza kiasi cha kujiona miungu watu
 
...atajibu lini hizi hoja jamani? maana kila muda najaribu kuchungulia kama ameshaanza kujibu baadhi ya hoja za wanaJF lakini naona kimya.
 
Mh Mama Tibaijuka,

Kwanza nikupongeze kwa mara yakwanza kujitokeza katika jukwaa letu tukufu na imara kwa fikra za mswahili kamili.

Juu ya andiko lako ambalo mimi naliona kama chagizo la kile serikali ilichokifanya hasa Kigamboni na kwingine, ambalo linapingana na utendaji na maamuzi ya serikali yako,

Mimi nimkazi wa Kigamboni, ninasema wazi kuwa wananchi HAWAKUASHIRIKISHWA katika mradi wa mji mpya wa Kigamboni
 
Mama Tibaijuka, hongera kwa kujianika jamvini. Kwa uzoefu wako, ukiwa chuoni, WAMATA, Habitat na sasa Waziri, nilitegemea kabla ya kuwakilisha hoja yako basi ungewatumia wasaidizi wako na kujiridhisha kwa sana kabla ya kupost. Hiyo post yako ni sawa sawa na kuweka chumvi kwenye kidonda. Nikuambie kati ya wizara mbovu kiutendaji, kukosa weledi, uzalendo, kujawa na ubinafsi, na kuchangia kuiangusha kwa kila hali nchi yetu ni wizara yako. Sikutegemea kweli ungeweza kuibuka na kusingle out ka issue kadogo kwa taifa ukitegemea sympathy. Forget. Nikuambie, mimi ni mtumishi wa serikali ambaye karibu naelekea kustaafu maeneo ya Arusha. Nikuambie sasa nimeanza kuomba kupata kiwanja ili nijenge makazi yangu tangia 1996. Sijawahi kupata. Utasikia vimepimwa tena kidogo, lakini unakuja ona majina au kuambiwa wakubwa wamegawana or zoezi la upimaji limesimamishwa. Ni migogoro juu ya migogoro or ulipie mara mia. Huwezi kuniletea hadithi zako leo nikusifie wakati vitu vidogo na vya msingi kabisa katika mipango miji ni kugawa surveyed lands vinawashinda. Siwezi.
Sasa niseme, unaweza kuwa unania njema, lakini haitatekelezeka kwa sababu UWEZO HUNA. Serikali yako inayoongozwa na chama chako hawana uwezo huo kwa sababu. 1. Nyie nyote hamna vipa umbele. 2, Hamsimamii sheria zilizopo ambazo ni nzuri tuu. 3. Hamna mipango endelevu. 4. Suala lote la ardhi limezingirwa na Rushwa, Ubinafsi, Kujuana na akili ndogo isiyo na uzalendo kusimamia. Aliingiaga Magufuli wakati Fulani. Kulikuwa na impact japo naye hakukaaa. Sijui aligusa pabaya! Angalau alijaribu kutaka kurudisha nidhamu, kusimamia taratibu zilizopo, uwajibikaji nk.
Matatizo yote haya yamefanya serikali na nyie kina Tibaijuka kufikia mahali mnakuwa na narrow vision badala ya kuwa pana, mnafocus kwenye vitu vidogo, badala ya kitaifa, Waziri huwezi kujitapa na Kigamboni, wakati kila dakika li-squatter linazaliwa kwenye miji yetu. Mmegota, ni kama engine inayosumbua kila mara. Ukienda kwa fundi atakushauri very simple kuwa inahitaji overhaul. Ndicho kilichobaki. Muondoke waje wengine, or nchi ipate RAIS DIKTETA MZALENDO ambaye atakuwa anauliza maswali kama UTARATIBU UNASEMAJE? KWA NINI HAUKUFUATWA? BASI UFUATWE NA NIPEWE RIPORT YA UTEKELEZAJI BAADA YA SIKU SABA.
Mmetuharibia sana nchi yetu.
 
Ukishakuwa na Ardhi unahitaji sambaza watu nchini watu wapate hewa, na mazingira safi....Australia hadi leo wengi hawajui magurufa marefu sana...wengi wanashaaa wakienda hong kong, dubai, south Korea etc..ila maisha yao mazuri sana..hadi wafanyakazi wa level za office assistants wana holidays za kutosha,watoto wao wan aoutdoor activties za kutosha, kwa kiasi cha kuwafanya wawe na sekata ya michezo iliyokomaa sana na inayobeba ajira kubwa.

Mama kwa mpango huu,inabidi dar iwe na barabara 16 za kutoka na kuingia Dar kuanzia mlandizi...otherwise ipo siku panatokea mashambulizi au hata tsunami na evacuation time ikawa mwezi......Siku moja mnahitaji fanya simulation test halaf muangalie results....Pia mfikirie watu wa mbezi,kunduchi etc, watakimbiaje bila kupitia bagamoyo road ambayo bado inakwenda na bahari.

Tunajua mawaziri wa Tanzania kw akuiga kila kitu kulivyo ktk damu,ila kwa hili tutawakumbusha tuu....Tunakumbuka,enzi za kuigana kufuga kuku, ikaja chai maharage, hiace, ..ktk ujenzi ..watu wameboa nyumba mara nyingi kwa vile kila dirisha walionalo kwa mtu wanataka liwe ktk nyumba zao..
 
zomba kama huyu mama yupo serious ahakikishe NHC wanauza hisa DSE
wakusanye mtaji wa kufa mtu wajenge nyumba za kuuza na kupangisha tele

NHC hawatoweza kusimamia, ingekuwa ni shirika binafsi, hizo kodi wanazokusanya na assets za majumba waliokuwa nayo hawana hata sababu ya kukusanya mtaji, wana mtaji tosha kabisa. Lakini wamekalia pale kujineemesha wao tu.
 
Mama Tibaijuka, hongera kwa kujianika jamvini. Kwa uzoefu wako, ukiwa chuoni, WAMATA, Habitat na sasa Waziri, nilitegemea kabla ya kuwakilisha hoja yako basi ungewatumia wasaidizi wako na kujiridhisha kwa sana kabla ya kupost. Hiyo post yako ni sawa sawa na kuweka chumvi kwenye kidonda. Nikuambie kati ya wizara mbovu kiutendaji, kukosa weledi, uzalendo, kujawa na ubinafsi, na kuchangia kuiangusha kwa kila hali nchi yetu ni wizara yako. Sikutegemea kweli ungeweza kuibuka na kusingle out ka issue kadogo kwa taifa ukitegemea sympathy. Forget. Nikuambie, mimi ni mtumishi wa serikali ambaye karibu naelekea kustaafu maeneo ya Arusha. Nikuambie sasa nimeanza kuomba kupata kiwanja ili nijenge makazi yangu tangia 1996. Sijawahi kupata. Utasikia vimepimwa tena kidogo, lakini unakuja ona majina au kuambiwa wakubwa wamegawana or zoezi la upimaji limesimamishwa. Ni migogoro juu ya migogoro or ulipie mara mia. Huwezi kuniletea hadithi zako leo nikusifie wakati vitu vidogo na vya msingi kabisa katika mipango miji ni kugawa surveyed lands vinawashinda. Siwezi.
Sasa niseme, unaweza kuwa unania njema, lakini haitatekelezeka kwa sababu UWEZO HUNA. Serikali yako inayoongozwa na chama chako hawana uwezo huo kwa sababu. 1. Nyie nyote hamna vipa umbele. 2, Hamsimamii sheria zilizopo ambazo ni nzuri tuu. 3. Hamna mipango endelevu. 4. Suala lote la ardhi limezingirwa na Rushwa, Ubinafsi, Kujuana na akili ndogo isiyo na uzalendo kusimamia. Aliingiaga Magufuli wakati Fulani. Kulikuwa na impact japo naye hakukaaa. Sijui aligusa pabaya! Angalau alijaribu kutaka kurudisha nidhamu, kusimamia taratibu zilizopo, uwajibikaji nk.
Matatizo yote haya yamefanya serikali na nyie kina Tibaijuka kufikia mahali mnakuwa na narrow vision badala ya kuwa pana, mnafocus kwenye vitu vidogo, badala ya kitaifa, Waziri huwezi kujitapa na Kigamboni, wakati kila dakika li-squatter linazaliwa kwenye miji yetu. Mmegota, ni kama engine inayosumbua kila mara. Ukienda kwa fundi atakushauri very simple kuwa inahitaji overhaul. Ndicho kilichobaki. Muondoke waje wengine, or nchi ipate RAIS DIKTETA MZALENDO ambaye atakuwa anauliza maswali kama UTARATIBU UNASEMAJE? KWA NINI HAUKUFUATWA? BASI UFUATWE NA NIPEWE RIPORT YA UTEKELEZAJI BAADA YA SIKU SABA.
Mmetuharibia sana nchi yetu.
...Tukishindwa kuwaondoa 2015 hivi hatuwezi kumuazima Kagame kwa miaka michache tu? mbona makocha tunawanunua kwa gharama yoyote wakati tatizo letu kubwa nchini ni uongozi wa juu - Rais na mawaziri?
 
NHC hawatoweza kusimamia, ingekuwa ni shirika binafsi, hizo kodi wanazokusanya na assets za majumba waliokuwa nayo hawana hata sababu ya kukusanya mtaji, wana mtaji tosha kabisa. Lakini wamekalia pale kujineemesha wao tu.
...Mkuu Zomba kumbe na ninyi huwa mnafikiria kama sisi wa CHADEMA? yaani nimeshangaa!
 
Back
Top Bottom